SIMULIZI; BALAA
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SEHEMU YA SITINI NA MOJA
Tatu na Nne walibaki pale hospitali, kulinda usalama wa pale, Moja na mbili ndio walienda kuwasaka wakina Dokta Yusha, kuwasaka mahala pasipojulikana.
Ghafla, simu ya Don Genge iliita.
Aliangalia katika kioo cha simu yake, kilisomeka..... Kifo!
Don Genge alipokea ile simu huku akiwa na hofu kuu.
"Hallo Bosi" Don Genge aliita simuni kwa sauti yake yenye hofu.
"Nipe maendeleo ya project yetu Don Genge"
"Mambo yako sawa Boss, ingawa kuna kidudu mtu katuingilia kidogo katika mipango yetu"
"Ni nani huyo Don Genge? na kaiingilia vipi hiyo project?"
"Anaitwa Dokta Yusha, amegundua kila kitu tunachokifanya huyo jamaa ni mjanja sana aisee"
"Na na bado anaendelea kupumua mpaka sasahivi?"
"Ndio Bosi anapumua, ingawa naamini anamalizia pumzi zake za mwisho"
"Six killers wanasemaji?"
"Wanajaribu kupambana vijana, ila bado hali haijakaa sawa mpaka sasa, mmoja ni missing in action, na mmoja ni majeruhi"
"Nani aliyepata majeruhi, na nani missing in action?"
"Majeruhi Tano, missing in action Sita"
"Lazima ufanye kitu Don, usiache hali ikawa namna hiyo, vipi kuhusu mzigo?"
"Mzigo uko wa kutosha, tutausafirisha kesho asubuhi"
"Fanya hivyo Don, mzigo umepungua sana huku, na tuna oda nyingi sana"
"Nitafanya hivyo"
"Sawa jamaa, huyo jamaa sijui Dokta nani anastahili kifo kabla hajatoa taarifa kwa jeshi la polisi au mahala popote ambako itakuwa si salama kwetu"
"Nimekuelewa Bosi, nitahakikisha tunamziba mdomo"
Simu ikakatwa.
Kifo, alikuwa ndio Mkurugenzi mkuu wa mradi huu kitaifa. Mradi wa kutoa mioyo ya maiti. Mioyo ambayo ilikuwa inatumika katika utengenezaji wa sumu kali zaidi duniani, Sumu ya Proxine!
Sumu ambayo, ukiigusa bila ya kuwa na kizuizi chochote kinachofuata ni kifo! Kifo baada ya dakika thelathini. Sumu ambayo ilikuwa inatengenezwa nchini Ujerumani, lakini malighafi za kutengeneza sumu hiyo zilikuwa zinatoka Tanzania. Sumu ya Proxine, sumu hatari iliyopigwa marufuku kutumika dunia mzima.
Hiyo ndio kazi ya mioyo hii ikiyochukuliwa na kundi la Six killers likiongozwa na jasusi Don Genge. Unaweza ukasema utoaji wa mioyo haukuwa na madhara sana kama asemavyo Don Genge, lakini je hivyo ndivyo wanavyopaswa kufanyiwa maiti, na je matumizi ya sumu ya Proxine, yalikuwa hayadhuru watu wasio na hatia?
Dokta Yusha na msafara wake uliingia katika hospitali ya Ndanda, wote wakiwa hoi kwa uchovu wa safari. Moja kwa moja walienda kwenye hospitali hiyo kubwa ya misheni. Wagonjwa walichangamkiwa walipofika nje tu ya hospitali hiyo. Manesi wenye vitoroli waliwapokea haraka haraka na kuwapeleka wodini. Kwa umakini na kasi walipewa huduma zinazojitajika. Huduma zilizomridhisha sana Dokta Yusha. Alikuwa na furaha usoni, ingawa furaha yake ilisinyaa akikumbuka madhila ya watu wale wabaya aliowaacha huko Kilwa.
Ndani ya wiki Moja, Mzee Mpaukha alikuwa mzima kabisa. Nasra na Hasina waliendelea kuwa wafu kitandani. Huku Hasina akifumba na kufumbua macho yake bila ya kuongea lolote. Akiba aliyokuwa anaweka Dokta Yusha ilimsaidia sana katika kipindi kile kigumu kilichohitaji awe na pesa za kutosha...
ITAENDELEA MUNGU AKIPENDA.