mzaramo
JF-Expert Member
- Sep 4, 2006
- 6,371
- 5,174
SIMULIZI: ANTI EZEKIEL
MTUNZI: George Iron Mosenya
SEHEMU YA KWANZA
Marashi yaliyopuliziwa na mtu ambaye nilikuwa sijauona
uso wake wala kujua yu umbali kiasi gani kutoka katika kiti
nilichokuwa nimekaa kwa ajili ya kunyolewa nywele zangu
yalinivutia kiuhakika, nikaamua kumshirikisha yule kinyozi
aliyekuwa ametingwa katika kuninyoa nywele zangu katika
mtindo niliokuwa nimeuchagua.
Kausha . Alinambia na sikuelewa ni kitu gani
anamaanisha. Nikahisi hakuwa akizungumza na mimi.
Marashi yale yakaendelea kutawala na sasa yalisadikika
kuwa karibu kabisa na pua zangu. Hapo nikajikuta
nanyanyua kichwa changu, kwa lengo la kutazama ufundi
ambao kinyozi aliufanya katika kichwa changu.
Badala ya kutazama kichwa changu nikajikuta natazamana
na tabasamu murua la kike. Kichwa chake cha mviringo
kilikuwa kimefunikwa na koti lisilokluwa maalumu kwa ajili
ya kupambana na baridi bali mojawapo ya kivazi
kinachoenda na wakati.
Nilipoendelea kubungaa mara yule mmiliki wa sura ile
ambaye nilikuwa natazamana naye katika kioo alinikonyeza.
Hapo nikakumbwa na aibu na kisha nikajifanya kutazama
pembeni.
Ana aibu mwenyewe looh!! ilimtoka sauti fulani yenye
mchanganyiko wa besi na nyororo. Nikalazimisha tabasamu
lakini sikukitazama kioo.
Hakujishughulisha na mimki tena badala yake aliendelea
kuzungumza na mmiliki wa ile saluni ambaye pia alikuwa
kinyozi mkuu na wakati huo alikuwa katika kuzishughulikia
nywele zangu. Baada ya hapo akatoweka huku nyuma
akiacha harufu kali ya marashi isiyokera pua za mnusaji.
Bwege katoka kwa wanaume yule kinyozi akasema ili
nisikie,
Ndo wasichana wa siku hizi hao niliunga mkono hoja
pasipo kutilia maanani.
Wasichana!!! Bora angekuwa msichana basi .yaani mi
ananikera sana ujue. Kidume kizima kabisa. Akatokwa na
kauli iliyorindima katika mawimbi ya hasira na kupokelewa
na ngoma ya siko langu katika hali ya mshangao na
sintofahamu. Nikaamua kuuliza.
Mwanaume? Mwanaume kivipi sasa ama umbo lake.
Niliuliza na bado sikutilia maanani mazungumzo yale kama
yangeweza kunifikisha popote. Niliamini ni mazungumzo tu
ya hapo saluni na yanaishia hapo hapo.
Shoga huyu!!! Halafu yupo wazi hata aibu haoni, kuna
washkaji wangu washalala naye, mimi siwezi hata kwa
bunduki yaani. Aliongea kwa kunongona. Nikamsikia
vyema.
Sasa niliishughulisha akili yangu kuelewa kile alichokuwa
ananieleza.
Kumbe yule dada aliyenikonyeza na kunisia kuwa
nimependeza si dada ni mwanaume anayeupenda udada?
Niliduwaa hakika. Na hapo nikamuuliza maswali mengi sana
yule kinyozi, naye akafurahia kuyajibu.
Haikuwa mara yangu ya kwanza kusikia kuhusu jina hilo la
shoga la!! Lakini huyu macho yake ni kama yalitangaza kitu
fulani cha ziada, alikuwa kama shoga anayejilazimisha japo
yule kinyozi alidai kuwa yeye mwenyewe anajitangaza
waziwazi kuwa ni shoga.
Nilipozidi kuuliza maswali mengi, kinyozi akarusha kijembe.
Vipi kaka na wewe unataka kukamatilia? sikumjibu badala
yake tukajikuta tunacheka, na hapo alikuwa anamalizia
kunifuta kichwa baada ya kuninyoa.
Vipi na ndevu niondoe.. aliniuliza nikakataa. Nikafanya
malipo na kisha nikajiondokea huku nikijilazimisha yale
mawazo kuhusu yule kijana anayeupenda usichana yanitoke.
Nilipofika nyumbani sikuwa na mawazo hayo tena na
sikutaka hata kumfikiria maana kwa kashfa alizotoa yule
kinyozi basi zilitosha kumaanisha kuwa kijana yule alikuwa
mdhambi tena asiyestahili hata kupewa salamu.
Inakuwaje mwanaume anajigeuza kuwa mwanamke??
Nililala nikiwa na swali hilo kichwani!!!
Asubuhi hapakuwa na lile swali tena na jibu lake pia
halkikufanania kuwepo.
Siku ikaanza nikiwa nimeyasahau ya jana.
*****
SAFARI YA KUKUTANA ANA KWA ANA NA MUHUSIKA.
UCHAGUZI mdogo wa serikali za mitaa kata ya
Makangarawe wilayani Temeke uliambatana na mechi ya
kukata na shoka katika mchezo wa soka.
Timu mbili pinzani zilikuwa zinaumana na mshindi
angejiondokea na kitita cha shilingi laki tano.
Mchezo ule ulivuta mashabiki wengi sana kutokana na
upinzani wa wazi wazi baina ya timu hizo. Nikiwa mmoja
katika ya wapenzi wa mpira wa miguu niliungana na
mashabiki wengine uwanjani.
Hali ya usalama ilikuwa nzuri kuanzia kipindi cha kwanza
hadi ilipokuja kuchafuka kipindi cha pili majira ya saa kumi
na mbili ambapo mwamuzi wa mchezo huo alipokataa goli
la waziwazi. Walianza wachezaji kumzonga mwamuzi mara
mashabiki nao wakaingilia kati, hapo ikazuka vita kubwa ya
mashabiki wa kila upande.
Kikosi cha kutuliza ghasia hakikuwa mbalki, mabomu
yalipopigwa ndipo kikazuka kizaazaa cha aina yake, kila
mmoja akikimbia kuelekea upande wake. Kipigo kilitolewa
haswaa na ungekuwa mwenye mikosi kama ungejikuta
katika mikono ile ya maaskari.
Nilichanja mbuga huku machozi yakinitoka kwa wingi baada
ya kuuvuta ule moshi wa bomu. Niliruka matuta hapa na
pale.
Kakaaa nilisikia sauti ya kike ikiita, sauti iliyotia
simanzi, sijui ilikuwaje lakini licha ya hatari ile ya kuishia
kulala rumande na kipigo kupokea niligeuka kutazama
kulikoni.
Macho yangu yakakutana na macho yaliyonitia mashaka
siku moja nikiwa mahali fulani ambapo sikupakumbuka,
nilitaka kuendelea kukimbia lakini nafsi ikasita. Nikiwa
bado sijapata maamuzi mara kijana mmoja aliyekuwa katika
harakati za kukimbia alipita kwa kasi na kumkanyaga mtu
yule, akatokwa na kilio cha maumivu.
Nikataka kuzuia huruma yangu, lakini nikakumbuka kuwa
nimeajiriwa katika kampuni ya kutetea haki za wanadamu
na mimi mwenyewe ni mwandishi, mara kwa mara naandika
makala zinazosisitiza usawa na pia utu.
Kwa maana hiyo kama ningekimbia basi ninachokiandika
mara kwa mara kisingekuwa na maana. Nisingekuwa na utu.
Haraka nikakimbia mahali alipokuwa, nikamnyanyua,
hakuwa mzito sana nikagundua naweza kumuhimili.
Nikambeba begani! Nikajikokota hadi aliponielekeza kuwa
nyumbani kwake ni jirani tu .nikafuata uelekeo aliokuwa
amenielekeza.
Tukaufikia mlango, nikamshusha. Akajikongoja na
kuufungua mlango baada ya kujipekua na kutoka na
ufunguo.
Niliaga na kutaka kuondoka, akanisihi kuwa niingie ndani
hadi vurugu zipungue. Naam alikuwa amewaza jambo la
maana sana, nikakubaliana naye. Nikaingia ndani.
Nilipoingia ndani nikakuta picha yake, nikatazamana na ile
picha nikakumbuka sasa wapi tulionana.
Ni huyu kijana tulionana saluni, nikaambiwa kuwa ni shoga!!
Damu ikachemka nilipofikiria kuwa nipo katika chumba cha
shoga.
Nilifananisha sebule ile na sebule yangu, hakika alikuwa
ameniacha kwa kila kitu. Hali hii ya kuniacha kwa kila kitu
ikanivuta kuendelea kukaa pale.
Unaitwa nani kakangu. Aliniongelesha kwa sauti ilele ya
mchanganyiko.
Sam!! nilimjibu kwa kifupi.
Mimi naitwa Ezekiel asante sana kwa kuniokoa, sijui kama
ningelala nyumbani kwangu leo. Alinijibu huku akiachia
tabasamu. Sikusema neno nami nikatabasamu huku
nikikwepa kumtazama machoni.
Nyumbani kwako pazuri sana!! nilimsifia.
Ah kawaida tu, lakini asante si unajua tena mwanamk ..si
unajua tena kujipenda jambo la muhimu. Akajibu kwa
kigugumizi.
Unaishi peke yako? nilimuuliza pasipo na wasiwasi
wowote kumtilia.
Yah ni nyumbani kwangu naishi peke yangu khaa!
Nimejichubua jamani kucha zangu. Alijibu kisha
akalalamika akizitazama kucha zake zilizopakwa rangi.
Tofauti na siku niliyomuona pale saluni, siku hii alikuwa
amedhoofu sana. Alikuwa amekonda na uso wake ulikuwa
umebonyea. Hali hii ilinishangaza, lakini nikalazimika
kuuliza baada ya yeye kuanza kukohoa kwa fujo.
Unaumwa
Bora ningekuwa naumwa .mimi naumwa sana. Alinijibu
kwa uchungu. Sasa sauti yake haikuwa mchanganyiko sana,
bali ilisikika kama ya kiume waziwazi. Sauti ilikuwa
inakoroma.
Nini tena maana siku ile tunaonana saluni haukuwa hivi, au
kioo kilikuwa kinanidanganya.
Saluni? Saluni gani? aliniuliza huku akistaajabu.
Nikamkumbusha siku ile ambayo ilikuwa miezi miwili
iliyopita. Hapo chozi likamtoka sikujua kama ni kwa furaha
ama uchungu.
Lazima nife lakini basi tu .basi tu nasema. Ipo siku yao na
wenyewe Alilalamika peke yake na sikujua kama alikuwa
ananishirikisha ama la.
Mbona unasema hivyo bro. nilihoji. Akanyanyua kichwa
akanitazama. Hakusema neno akakohoa tena kikohozi
kikavu ambacho kwa kukisikia tu nilitambua kuwa kilikuwa
kinamuumiza koo.
Wewe ni nani? aliniuliza ..kabla sijajibu akazungumza
tena. Umesema unaitwa Sam lakini bado sijajua wewe ni
nani hadi umeamua kurudi nyuma na kuniokota mimi wakati
mama yangu mzazi alishindwa kuniokota. Alitamka haya
huku akiniazia macho.
Kauli yake ikanitetemesha kidogo, ni kama alikuwa
ananikaripia. Sikushtuka sana nikaendelea kumtazama,
kwani nilishazoea harakati hizi.
Mimi ni Sam, mwanaharakati na pia ni mwajiriwa kwenye
kampuni fulani hivi nilimjibu.
Hivyo tu! aliuliza na sikujua ana maana gani.
Unamaanisha nini.
Ndo hivyo tu kuhusu wewe maana sura yako si ngeni sana
kwakweli, licha ya kukuona siku ile saluni bado kuna mahali
nadhani tumewahi kuonana ama nimekuona.
Labda gazetini, huwa naandika vihadithi hadithi. Nilijibu
bila kutarajia kuwa anaweza kuwa ananifahamu.
Akasimama na kujipigia makofi, lakini kikohozi kikaondoka
na cheko lake akakaza sura na kuugulia maumivu lakini
bado aliweza kuzungumza.
Nimesoma hadithi zako kadhaa, wewe si ndo umeandika
ile ya NISAMEHE KABURI ..na nyingine ile ya dada fulani
hivi chuoni hana miguu wala mikono na anataka kuwa
rubani .yaani napenda hadithi zako hasahasa za kipelelezi,
hivi wewe ni mpelelezi eeh . Alizungumza kwa sauti yake
ya kubana pua, bila shaka alikuwa ameizoea. Alionyesha
kunifahamu vyema.
Baada ya koo kukaa sawa aliendelea kuorodhesha makala
na hadithi zako ambazo amewahi kuzisoma, na hatimaye
tukaagana huku nikiwa sina shauku kubwa sana ya
kuendelea kumsikilia Ezekiel, kwani hakuonyesha kama
anajitambua vyema. Na mbaya zaidi niliamua kuondoka kwa
kuhofia kujitekenezea skendo nikionekana natoka katika
nyumba ya yule shoga.
Mke wangu na wivu wake!! Nilimjua mimi mwenyewe.
Nikamuaga Ezekiel na kuondoka, huku nikijiapia kuwa
hakuna ninalohitaji kujua zaidi kutoka kwa mwanaume
qaliyejigeuza mwanamke.
UTATA MKUU
Siku iliyofuata nilikuwa na safari ya kuelekea mkoani, hivyo
asubuhi na mapema niliwahi kwenda Ubungo. Kiubaridi
kilikuwa kinapuliza na nilikuwa nimejiegesha mahali
nikipuliza hewani moshi wa sigara kupasha mwili wangu
joto.
Nilijitenga eneo la mbali kabisa na abiria wengine ili
nisiweze kuwabughuzi. Mawazo yangu yalikuwa yote juu ya
safari yangu kuelekea Singida, niliwaza kuhusu watu wa
Singida jinsi walivyo wakarimu na hapo nikajengea picha
mara yangu ya mwisho mjini Singida.
Nikiwa bado pale nilipojiegesha mara nilisikia naguswa
begani.
Nilipogeuka nyuma nilikutana na maajabu.
Ana kwa ana na yule shoga!!
Hakuwa anatabasamu ba alionekana kama anayefanya
mambo kwa shinikizo. Alinikazia macho kama anayetaka
nielewe kitu fulani, nilijitahidi kungamua jambo nikasafiri
na macho yake hadi katika mguu wake, akatabasamu na
kisha kutoweka pale katika mguu wake wa kuume akaacha
kifurushi kidogo tu cha nguo. Nikataka kumfuata
anapoelekea lakini akanionya kwa vitendo. Mwendo wake
ulinishangaza sana, alitembea mithili ya ngongoti, alikuwa
amenyooka na ni kama hakutaka kupinda, masikioni alikuwa
ana vifaa vya kusikilizia, sijui alichokuwa anasikiliza lakini
bila shaka walikuwepo watu ambao alikuwa anawasikiliza.
Ezekiel akatoweka na sikumuona tena.
Nikarejea hadi pale nilipokuwa nimesimama mwanzo,
nikaanza kukitafuta kile kifurushi alichokiacha pale lakini
sikukiona, nilihaha sana na kujiuliza nini kimemsibu yule
kijana. Na ni kitu gani alikuwa ameniachia katika fundo lile
la nguo??
Lazima kilikuwa kitu cha msingi maana alionyesha kusihi
sana.
Swali gumu jingine likawa, yule bwana amejuaje kama
nitakuwa stendi asubuhi ile hadi aniletee ujumbe ule.
Nikiwa bado katika mtihani mgumu, mara basi nililotakiwa
kusafiri nalo likapiga honi kuashiria kuwa dakika yoyote ile
linaondoka.
Ule utata ambao huwa naujenga kwa wahusika katika
simulizi sasa ukajijenga katika nafsi yangu na sikujua
nautatua vipi?
Katiba basi tayari begi langu lilikuwa kule, sikukipata
kifundo nilichoachiwa na mtu niliyeamini kuwa ni Anti
Ezekiel.
Na ubaya mwingine sikujua hata kitu kilichokuwa kinamsibu
Ezekiel.
Nikayakumbuka maneno yake usiku uliopita nitakufa
lakini .IPO SIKU YAO NA WENYEWE
Hakumalizia, na sikujua alitaka kusema nini.
Kwanini afe na hao wenyewe ni kina nani??