Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Swali langu mshana!
Umempiga paka kumbe mtu na akafa na ukashuhudia kabisa yule paka kafa, je yule paka mfano umemchukua umemfukia, sasa yule mtu kule atarudije augue na kufa ilihal alikuwa paka na umemuua na kumfukia kabisa.
Paka hafii pale atachechemea mpaka apotee ukimuulia ndani ukaenda kumzika siku ya pili huwezi kukuta mzoga wake kwakuwa hakuwa halisi
 
Mshana JR daah Umenikumbusha Kuna Siku Bhana Paka Aliingia Hostel moja Hivi tuliyokuwa tunaishi kipindi Nipo Chuo . Sasa Cha Ajabu Akaja Mpaka room kwangu Usiku Kwenye Mlango akajisaidia Pale Haja Kubwa kwenye Kapeti la miguu. Nilivyoshtuka Usiku naenda Toilet nikakuta Paka Wengine Wakakimbia ....Sasa Yule Aliyejisaidia Pale kwangu nikamkimbiza Akakimbia Ila Akawa Amejificha Kwenye Kona moja Hivi , nikaona Nisimuue maana Wengine bado wamelala

Nikatoka Nikaenda Kuyamwaga Yale mavi yake Chooni nikaflash..

Nilivyoamka Asubuhi yake Cha Ajabu Yule Paka bado hajatoka Mule Ndani amejibana Pale pale... Nikasema Wewe utakuwa Umetumwa Yaani mpk sasa Hivi Hujatoka Ndani.. nikachukia Fimbo nene Nikaanza Kumpa Kipogo heavy.. Bahat nzuri hakuchukia Muda Nikampiga Kwenye kichwa Akashuka Chini ghafla na Kupoteza Maisha..nikamzika nikasepa chuo

Muda si mrefu Nimerudi Nikasikia Sehemu Fulani Kuna Msiba . Tulio ndani mule tukaanza kusema Itakuwa Yule paka nn. Basi tukapotezea
Ulimmaliza nguvu kwa kwenda kuflash kile kinyesi.. Hicho kilitakiwa kikae mpaka asubuhi
 
Kuna paka alikua anakuja kulia kila siku nyumbani kwetu siku moja mbwa wetu alimuua huyo paka ... Kesho yake tu huyo mbwa akaanza kuumwa na mwishowe kufariki
Duuu walikutana njiapanda hao
 
Kuna paka mmoja ilikuwa jioni tumekaa kibarazani wakati anakuja kudoea doea bi mkubwa alikuwa anapika pika ,akajikuta kamwagia maji ya moto kwnye kiuno...kesho yake asbh akaja mjukuu wake katoto kadogo kakatuambia kunabibiake anumwa kababuka makalio
 
mshana jr
Nilikuwa siamini binadamu aweza kuwa mnyama,

Pale kibo kushuka kule bonde la gide,kuna siku nimeshinda nje akatokea mama mmoja anafoka anadai paka amemfuata alipokuwa anachota maji,na amempa kichapo hivyo tusubiri msiba,

Kama masikhara tukawa tunacheka tukajua ni utani,

Hayakupita masaa tukasikia yowe za msiba mzee mmoja mitaa ile akafariki na aliondoka na mpangaji wake pia.
Hornet ya kweli au umeamua tu tucheke.
 
Yaani mada ya kusisimua halafu baadae kidogo unakuta watu wanapetiana kwa Maneno matamu, sijui ndio kupoozea msisimko? Kama pili pili na maji inapendeza zaidi.
 
Usiombe uwe na jicho la tatu kwani utashindwa kuishi kwa amani. Utaona mambo mengi katika ulimwengu wa roho. Unaweza ukaona mtu yupo uchi huku anauza chakula, unaweza kupanda gari lenye fisi ndani, je utahimili?
 
Back
Top Bottom