Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Swali langu mshana!
Umempiga paka kumbe mtu na akafa na ukashuhudia kabisa yule paka kafa, je yule paka mfano umemchukua umemfukia, sasa yule mtu kule atarudije augue na kufa ilihal alikuwa paka na umemuua na kumfukia kabisa.
 
Hii ni kaliba iliyojaa upweke na mateso japo kuna watu eti wanatamani wanatamani kuwa wachawi...
Mojawapo ya advertise ya kuwa mchawi ni uwezo wa kujigeuza umbo la kibinadamu na kuwa mnyama... Na binadamu wengine wasikujue kabisa kama wewe sio mnyama halisi.. Japo wanyama huwa wana hisia na maranyingi watajitenga na wewe ama kukufukuza...
Unapokutana na kundi la wanyama lakini kuna mmoja kajitenga na wenzake... Tambua tu kwamba huyo si mnyama halisi kwa asilimia kubwa
Kwenye mikusanyiko ya watu ukifanikiwa kuwa na jicho la tatu utaona mengi sana.. Pale kariakoo pale Ilala sokoni, buguruni nknk kuna wanyama wengi sana katikati ya makundi ya watu
Kujigeuza umbo la kibinadamu kuwa mnyama ni uthubutu wa hali ya juu japo ni sifa kwa mtendaji ila anapaswa kuwa na msingi mzuri kwenye taaluma yake kwakuwa akikutana na nguvu kubwa kuliko yeye atapigwa dafrau na kupoteza maisha
Kuna wanga hupenda kujigeuza paka na kuingia kwenye majumba ya watu, sometimes panya au hata nyoka nk.. Sasa hawa ukiwavizia ukawalia timing ukawapa mkong'oto... Asubuhi yake utapata tu habari
Utasikia mzee fulani kaumia bega au kichwa au mkono nknk.. Na ukija kurudisha kumbukumbu nyuma unakuta pale ulipompiga yule mnyama ndio hapo hapo anapoumwa huyo mzee.. Na haendi hospital ataugulia nyumbani mpaka apone...
Risk kubwa ni pale wanapopata kipigo mpaka kupoteza maisha. Siku ya pili mtaani utaona turubai
Mshana JR daah Umenikumbusha Kuna Siku Bhana Paka Aliingia Hostel moja Hivi tuliyokuwa tunaishi kipindi Nipo Chuo . Sasa Cha Ajabu Akaja Mpaka room kwangu Usiku Kwenye Mlango akajisaidia Pale Haja Kubwa kwenye Kapeti la miguu. Nilivyoshtuka Usiku naenda Toilet nikakuta Paka Wengine Wakakimbia ....Sasa Yule Aliyejisaidia Pale kwangu nikamkimbiza Akakimbia Ila Akawa Amejificha Kwenye Kona moja Hivi , nikaona Nisimuue maana Wengine bado wamelala

Nikatoka Nikaenda Kuyamwaga Yale mavi yake Chooni nikaflash..

Nilivyoamka Asubuhi yake Cha Ajabu Yule Paka bado hajatoka Mule Ndani amejibana Pale pale... Nikasema Wewe utakuwa Umetumwa Yaani mpk sasa Hivi Hujatoka Ndani.. nikachukia Fimbo nene Nikaanza Kumpa Kipogo heavy.. Bahat nzuri hakuchukia Muda Nikampiga Kwenye kichwa Akashuka Chini ghafla na Kupoteza Maisha..nikamzika nikasepa chuo

Muda si mrefu Nimerudi Nikasikia Sehemu Fulani Kuna Msiba . Tulio ndani mule tukaanza kusema Itakuwa Yule paka nn. Basi tukapotezea
 
Hahahahahaha kuna mzee mmoja hapa mtaani alikuwa anakuja kuniwangia anajigeuza paka siku nikamtegeshea akapigwa dafrau akaugulia kwake akawa ananiulizia mbona siend kumuona ajab siku nimeenda kumuona asubuh jion akapona hakukoma akaja tena akachezea vitasa sasa anaugulia ndani pamoja na kuniulizia sijaenda kumuona
 
Asante kwa uzi nzuri, ikitokea mchawi kajigeuza mnyama, akatokea mnyama halisi anataka ka mchezo, huyo mchawi na umbo la mnyama yupo tayari kuachia penzi
 
mkuu ushanipa tahadhari, ukizingatia nitakua natembeaa na kipande cha mkaa na chumvi vipi hapo bado naweza kudhurika?

Kitakachokudhuru ni hayo mapicha utakayoona mengine utayakimbia kisha watu watadhani zimekuruka.. Utamuona fisi halafu unajaribu kuwaambia watu huyo ni fisi wao wanaona ni mtu utapelekwa mirembe... Soma hiije vichaa wana jicho la tatu?
 
vipi kuhusu wale wanaolinda nyumba zao au maduka kwa uchawi unakuta wezi wanapoenda kuiba hawaioni nyumba au duka inakuwa imebadirika kuwa kichuguu au bahari
Huko ni kuingia anga za wengine... Kama ni kwa ajili ya self defense usitafute ubaya
 
Back
Top Bottom