Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Risk ya mchawi kujigeuza mnyama...!

Mmh.... Duuu
Baada ya yule mdada wa nyumbani kupandisha na kuzungumza alozungumza, bi mkubwa yalimuingia sasa akilini na kabla ya huyo mdada kuongea kuna siku mama alikuwa anakwenda kwa huyo mganga, kaishika njia ya kwenda kwake akasikia sauti inamuita. Kugeuka akakuta ni kijana alowahi kuishi kwa huyo mganga wakashindwana akafukuzwa, akamuambia achana na huyo mama hakuna mganga hapo na familia yako utaitesa mno!!!

Sasa alipokuja kuunganisha na yale ya majini ya yule dada wa hom akili ikamfunguka
 
Anaekataa uchawi haupo, basi na aendelee kukataa vivyo hivyo. Nakupeni visa kadhaa vilivyowahi kutokea katika maisha yetu(Kifamilia).


Mnamo mwaka 2005 zikiwa zimebaki siku takribani 4 kufika Xmas, kuna mjukuu wa kwanza wa mama, alianza kuwa anaanguka, hapa ndipo nilipochoka. Humuoni akianguka, ila unamuona akijikung'uta tu kutoka chini.
Kile kitu kiliwashinda aliokuwa anacheza nao(wadogo zetu) wakamwambia mama, mama akajifanya mkali, anamwambia aache upumbavu wake wa kujiangusha, atampiga. Dogo akamwambia, bibi miguu haina nguvu na mimi sijiangushi! Mama akamwambia hebu njoo ukae hapa nione kama utaanguka, dogo akaenda kukaa mbele ya mama. Kidogo tukamuona anajikung'uta vumbi kutoka chini, mama akasema umefanyaje!!!? Hapo sasa wote tupo tunamuangalia.

Hatujakaa sawa, tukamuona tena anainuka kutoka chini, mama akasema tuingine ndani, ile kuingia ndani, tukamuona mlangoni anainuka kutoka chini, tukaingia ndani, akawa anaangalia juu pande zote za ndani akiwa amekaa kwenye kiti, mama nikamwambia aache ukali wake kwani hautasaidia chochote kujua ukweli wa unaosumbua.
Usiku ukafika tukalala, hali ikawa ile ile. Mama akanambia hebu mchukue mpeleke kwa fulani(huyo nloagizwa kwake alikuwa ni mganga wa majini alokuwa akitutibia nyumbani). Nikafika, nikamueleza, akachukua vitu vyake akaanza kumkanda miguu, akagunaaa, akasema huyu mbona Miguu imeshakufa! Ni ya baridi kabisa, ila haina shida nitapambana nayo. Akamkanda pale akanambia kaeni mpumzike kidogo, ukiondoka usiage wala kumsemesha yeyote ila ukifika nyumbani umwambie dada(mama sasa) aje jioni nataka aongee na Maimuna. Nikasepa nikafika hom, mama nikampa ujumbe jioni akaenda.

Akaenda kilingeni, yule mganga akapandisha, Maimuna kaja wakaanza kupiga stori hapo akamwambia kuna watu wanataka kumuua huyo mjukuu, asipofanya juhudi basi xmas ya mwaka huo itakuwa na msiba, mama akaelekezwa cha kufanya, akafanya huku dogo akaendelea na maisha fresh mpaka leo na yeye sasa hivi ana mtoto.
Mjukuu wa mama!
Mjukuu huyo wewe hauna nasaba naye? Je ni nani yako? Siyo mwanao huyo!

Ndiyo haya, badala ya kumuita nduguyo wa kiume 'kaka' ama nduguyo wa kike 'dada' yako, badala yake humuita 'mtoto wa baba'!
 
Mkuu hii mada yako imenifanya nianze kufikiri kitu. Kila nikitoka kwenda kwenye kinywaji ninapokua narudi kuna sehemu huwa namkuta mbwa jike ananisindikiza mpaka home. Wife alikua anamwogppa sana Mara ya kwanza lakini kwa sasa anamsifia sana kwamba anatulinda. Na huwa tunamkuta sehemu ile ile moja. Sasa ninawasiwasi asije kuwa ni mchepuko wangu ana fani ya kujibadili. anatusanifu tunavyoongea
😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
giphy.gif


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mjukuu wa mama!
Mjukuu huyo wewe hauna nasaba naye? Je ni nani yako? Siyo mwanao huyo!

Ndiyo haya, badala ya kumuita nduguyo wa kiume 'kaka' ama nduguyo wa kike 'dada' yako, badala yake humuita 'mtoto wa baba'!
Ndiyo haya, badala ya kumuita nduguyo wa kiume 'kaka' ama nduguyo wa kike 'dada' yako, badala yake humuita 'mtoto wa baba'!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahahaha kuna mzee mmoja hapa mtaani alikuwa anakuja kuniwangia anajigeuza paka siku nikamtegeshea akapigwa dafrau akaugulia kwake akawa ananiulizia mbona siend kumuona ajab siku nimeenda kumuona asubuh jion akapona hakukoma akaja tena akachezea vitasa sasa anaugulia ndani pamoja na kuniulizia sijaenda kumuona
Hahahh kumbe ukienda kumuona anapona
 
Ni kweli kabisa... Mimi nasema ni kwa Neema ya Mungu tu wallah maana kwa nguvu na utashi wangu singeweza asilani

Sent using Jamii Forums mobile app
Ashukuriwe Mungu maana kwa tunavyosikia.....

Yuko jamaa yangu mmoja naye aliniambia ALIACHA....alisema yeye alikuwa ni "rubani kabisa"...toka utoto wake....ila alipofika 22yrs akaacha kwa "kupambana" sana na pia kukimbia mji wao....Sasa ukweli anaujua Mungu kwani isije akawa alinifunga "kamba" tu 🤣

All and all nimekupata bingwa👊
 
Simple, chukua mwiko uliosongewa ugali halafu haujaoshwa, lala nao kitandani ukiwa umeukumbatia kichwani. Ila baada ya hapo utakumbuka kila ulichokiona lakini hautaweza kusimulia kamwe wala hata kuandika ulichokiona
Tutaomba mrejesho wa hii theory
 
Hapo kwenye kumkata nakubali kabisa nikiwa mdg kule arusha tulikua na mti wa mchungwa, sasa si unajua mambo ya wamasai hawaogopi chui/ sijui simba silewi sana kama ni kwel hili ila alikuaja chui nyumbani ambao wamasai wanaita (lowaru) sasa sina hakika ni chui wale wa porini au la maana sikumshuhudia huyo chui kwani sisi tulikua ndani babu akaenda kupambana nae huyo chui akarukia juu ya ule mvhungwa babu akafanikiwa kumkata yule chui mguu wa mbele kesho yake kuna babu mtaani hua wanasema ni mwanga nae akawa amekatwa mkono basi toka siku ile mambo ya vitu kutembea juu ya bati yakaisha mpk akampa babu yangu jina nalisahau kwa kimasai linaitwaje ila kwa kiswahili alikua akimaanisha akimuona babu yeye anatetemeka ( lokirikira kama sikosei?
 
Back
Top Bottom