Risiti za efd machines kufutika

kluger

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,093
1,894
Wasalaam wakuu,

Hii nchi tuwe serious kidogo, nashindwa kuelewa kwa nini tunapenda kuishi kwa mazoea?

Yaani watu wamepambana tuwe na Mashine za EFD, nia hasa tulipe kodi na kudai risiti.
Cha ajabu hakuna anayeona umuhimu wa hiyo risiti! Hii ni rekodi ambayo ni kidhobitisho cha umiliki wa mali mbali mbali.

Wenzetu ulaya wana risiti kama hizi na hazifutiki.
Sasa sisi ukitaka kutunza risiti, utoe kopi, hivi Kweli jambo kama hili hakuna mtu anaona umuhimu wa kurekebisha hii kasoro.

Nawakilisha.!!!!
 
Hizi risiti ni kwa ajili ya kukusanya mapato tu ila siyo uthibitisho wa kumiliki mali fulani. Maana huwa zinaadikwa amount na items. Sasa mfano umenunua TV ya Sony kwa 900k utathibitisha vipi kwa kutumia risiti wakati serial number ya item haipo?
 
Zinafutika zote, sio ulaya tu, maana technolojia inayotumika sio ya ink au laser ni mfumo tofauti, na ile ni katika kuifanya mashine isihitaji wino wowote, labda wanaoleta mashine wakafanye utafiti wa mashine mpya zitakazofanya kutoa risiti isiyofutika, maana mi pia nna risiti zina mwezi tu zimeisha hamna hata herufi, na zingine nimezitunza bila kuzigusa bado zipo fresh tuu
 
Wasalaam wakuu,

Hii nchi tuwe serious kidogo, nashindwa kuelewa kwa nini tunapenda kuishi kwa mazoea?

Yaani watu wamepambana tuwe na Mashine za EFD, nia hasa tulipe kodi na kudai risiti.
Cha ajabu hakuna anayeona umuhimu wa hiyo risiti! Hii ni rekodi ambayo ni kidhobitisho cha umiliki wa mali mbali mbali.

Wenzetu ulaya wana risiti kama hizi na hazifutiki.
Sasa sisi ukitaka kutunza risiti, utoe kopi, hivi Kweli jambo kama hili hakuna mtu anaona umuhimu wa kurekebisha hii kasoro.

Nawakilisha.!!!!
Hâta hizo za ulaya zinafutika mkuu, labda zile za kuandika kwenye computer na ku print kwenye printer ..... hizi ni lazma utoe kopi tu hamna ujanja mwengine !!!
 
Hizi risiti ni kwa ajili ya kukusanya mapato tu ila siyo uthibitisho wa kumiliki mali fulani. Maana huwa zinaadikwa amount na items. Sasa mfano umenunua TV ya Sony kwa 900k utathibitisha vipi kwa kutumia risiti wakati serial number ya item haipo?
Pigia mstari. Tena hata uandishi wake ni wa kiujumla.
Nilinunua saruji, bati, misumari na mbao.
Kuja kusoma risiti , imeandikwa "vifaa vya ujenzi" bila kufafanuliaa, mwisho Total na hesabu ikafungwa!
 
Back
Top Bottom