Rished Bade kumsaidia Kitillya TRA

It seems this Gentleman is going to replace H. Kitilya @ TRA ?
 
Katiba mbovu mbovu imemfanya JK (na waliomtangulia pia) kuwa autocratic ruler who assumes sole and absolute power to do anything at his will without questioning. Angalau kungekuwa na ka'mechanism' kupitia wawakilishi wetu bungeni ka kupitia teuzi kama hizi
 

Sio katiba iliowafanya wawe na NGUVU ni KULIVUNJA AZIMIO LA ARUSHA na kupachika AZIMIO LA ZANZIBAR; limeongeza ULAFI; NGUVU ZA

KUTAKA KUTAWALA Sababu wameruhusu VIONGOZI serikalini kuwa na MAKAMPUNI na kubeba wanao sababu ni system ya kulindana...
 
Hivi huyu naye ni wa lile tawi lao la CCM? Just asking,maana Jk hotuba ya kwanza alisema SASA NI ZAMU YETU! Baada ya muda akaanza kuwajaza kila sehemu ukichukulia analindwa na katiba ya kikoloni.
 
Ana CV nzuri ya banking & Finance, nafikiri ni mtu mzuri anaejua kutumia human resources zake ndio maana anaonekana amekuwa na achievement katika sehemu nyingi alizopita, binafsi namtakia kila la kheri katika kazi yake hiyo mpya.

sijakuelewa...barclays tangia ianze biashara haikuwahi ku'break even....hapa alifeli...pia hiyo TMRC bado haijawa na changamoto za kutosha kutumika kumpima mtu....Huyu jamaa mi nna mashaka naye..kwanza naona km si mzawa...pili naona kama anazo za darasani na amewekwa pale kwa manufaa binafsi ya mkulu...na mwisho..hawa jamaa yaan huyu wa TMRC,MD wa stanbic wana kamtandao ka kakutafuna mabinti hapa mjini...no wonder ni washkaji wa mkulu.....

Uteuzi wa ovyo....kwa nn hizi post zisipatikane kwa ushindani???kuliko hii ya blah blah......Naingojea tume ya katiba inifikie...
 


Ha haa huyu ni nani ? du siasa za bongo mchosho hapo anawaza atakachopata tuu haijalishi alipita wapi na alifanya nini.
 
Hongera zake, kiukweli jamaa kichwa inachemka,alitoka Mlimani na 1st Class na kuchukuliwa na BOT moja kwa moja.
 

Kimbunga,

Mpango wa Retail Expansion haukuwa mpango wa Rished Bade.Huo mpango ulikuwa wa Barclays Emerging Markets (Kutoka Dubai makao makuu) , kina Rished waliletewa tu wautekeleze. Sasa tatizo kubwa lilitokea pale ni kwenye Personal Loans maana wabongo kama unavyowajua. Walitaka kuiga Barclays Kenya wakati kule wenzetu wana system nzuri za identification. Nadhani kama ingekuwa ni failure ya Rished kama yeye binafsi wasingempa kazi nyingine kule Nairobi wangemtimua tu!
 
Inatia matumaini tunapokuwa na wateule wenye damu changa na wenye kuthubutu kuliko teuzi za mitumba.

Anaweza kuwa mtendaji mzuri ambaye hajaathiriwa na urasimu uliopo serikalini. Naamini hili linaweza kuwa kundi la kina Mchechu wa NHC. Shida kubwa ni jinsi yake kusimama kwani wimbi la mafisadi na viongozi wengi mafisadi ndio wanaoharibu utendaji wa wateule wazuri.
 

kwa kuongezea tu yeye ni mwanachama wa kila kijiwe cha kina jenerali ulimwengu,balozi ami mpungwe,wendo mwapachu cisco mtiro,jaji mkuu othman na wengine pale mitaa ya kati,nazungumzia british legion club,na huwa anabisha sana na wendo mwapachu,kama namuona wendo atakavyomchachafya pale club
 
Hii inawezekana na hasa kama baada ya hapo alielekea ACB ambayo pia Bw. Rashidi ana stake kubwa.

 
Udini/ukabila utatumaliza Watanzania. Katika yoote umeona dini ndio muhimu? hapa tunaangalia utendaji wa mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…