Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
Kuna taarifa za kuzuka switafahamu katika vituo vya uandikishaji wapiga kura katika DKWK, katika jimbo la uchaguzi la Ole, Wilaya Wete Kisiwani Pemba.
Hali hiyo imepelekea risasi kadhaa kufyetuliwa na kikosi cha wanamaji (KMKM), kutuliza wananchi walioghadhibishwa na mbinu chafu cha za tume ya uchaguzi kukataa kuwaandikisha wapiga kura wapya katika DKWK.
Mwakilishi wa jimbo la Ole Mh. Hamad Masoud ameiambia BBC kuwa mtu mmoja amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa virungu na askari wa majini (KMKM) na hivi sasa anapatiwa matibabu hosipitalini.
Hadi sasa tume ya uchaguzi imesitisha kwa muda zoezi hilo jimboni hapo hadi hapo hali itakapotengemaa.
source: BBC