Ripoti ya Twaweza ya #SautiZaWananchi: Magufuli na CCM wang'ara dhidi ya wapinzani - Sept 22, 2015

Hii ni aibu ya mwaka..taarifa za matokeo zimaanza kuzunguka kwenye magroup ya whatsapp tangu jana na kweli ndo walivyo present...shame on you.....
 
Hata wasemeje hapa.mwendo mdundo tu Lowassa ndio Rais tunaemtambua hizo Tathmini zao za uongo na kweli wazipeleke kule huku tumejipanga kura yangu ni Lowassa tu sitetereki hata kidogo
 
Wakuu,

Twaweza kupitia utafiti wao wa Sauti Za Wananchi wanazindua utafiti kuelekea Uchaguzi mkuu leo hii, saa nne kamili asbuhi hadi saa sita katika ukumbi wa Makumbusho.

Ripoti hiyo ya #SautiZaWananchi inahusisha vyama vyote vitakavyoshiriki #Uchaguzi2015 katika kugombea kiti cha uraisi.JamiiForums kushirikiana na Twaweza inawaletea LIVE updates ya uzinduzi wa ripoti na tafiti za ripoti hiyo.

Wasalaam!

View attachment 289727
Mkurugenzi wa TWAWEZA

Uzinduzi umeanza rasmi saa 4:10 Asubuhi.
=========

2012 Udiwani asilimia 60 wangepigia CCM

2015 kwenye udiwani asilimia 60 CHADEMA 24% CUF 2% ACT 1% UKAWA 3%

Mwaka 2014 Kwenye ubunge 47% 23% 4%

Mwaka 2015 kwenye ubunge asilimia 60 wangepigia CCM, CHADEMA 26%

Kwenye urais mwaka 2014 wangeipigia kura CCM asilimia 51 na CHADEMA asilimia 23

2015 kwenye urais 66% wangepigia kura CCM, 22% CHADEMA, UKAWA 3%

Kama uchaguzi ungefanyika leo asilimia 65% walisema Magufuli, 25% walisema Lowassa.

Magufuli anapendwa zaidi vijijini na Lowassa mijini, japo kote Magufuli anaongoza. Kadri watu wanavyokuwa wazee wanamchagua Magufuli na Lowassa kwa vijana zaidi.

Zaidi ya asilimia 60 ya wasiosoma wako kwa Magufuli, nusu ya wasomi wako kwa Magufuli.

Kwanini utampigia kura mgombea wako? Kwa Magufuli ni kwa sababu ni mchapakazi, karibu wote na kwa Lowassa asilimia kubwa sababu anaweza kuleta mabadiliko.


ukawa sio chama,shame on you,hamjui hata kudanganya!!!
 
Matokeo haya hayaaminiki na kukubali na mtu yeyote including wanaccm wenyewe kwani hayaelezi uhalisia lengo likiwa ni kupotosha umma kutokubalika kwa lowasa. Hii itasababisha watu ukipiga kwa za Hasira kwa lowasa na kuendelea kufanya safari yake ya ikulu kuwa rahisi. Kura ndizo zinazoamua mshindi so Tafiti zisizo na credibility.

adm usiondoe wala kuunganisha Uzi huu plse.!!

Utafiti wowote unatakiwa uoneshe sample size, eneo la tafiti kwa maana ya ukubwa wa eneo vinginevyo ni data za kupikwa tu, mwisho wa siku ballot box ndio itaamua yote.....
 
Msisikie tu wimbo wetu. Msiwaone tu TOT wetu wanaimba na kuchez. Msiwaone tu wananchi wakiimbishwa na kupagawishwa. Tuna maana yetu. Tuna lengo letu. Litatimia tu.

Tafiti za kisiasa za kisasa zitatubeba. Zitatufanya imara kama mnara katika kutetea madaraka ya chama chetu. Baada ya kampeni kutoridhisha na hata kututisha,tafiti ndizo zitakazotuokoa.

Wameanza TWAWEZA. Wameweza kutubeba na kuwaacha wapinzani mbali. Watakuja na REDET na hata SYNOVATE kututetea. Kitaeleweka tu. Tafiti hizi zitatangazwa luningani,redioni,magazetini na mitandaoni hadi mchoke.

Tumejipanga,mwaka huu mtaisoma!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Uongo. Hakuna asiyemfahamu lowassa

Nasema hivi kwa sababu kuna jambo maria sarungi ameliongea kuwa wananchi wasitegemee kukutana na neno ukawa , nccr au cuf ndani ya chumba cha kupigia kura.Elimu ninayomaanisha hapa ni kuwa wale wanachama wa cuf na nccr wasifike mle ndani wakawaanza kutafuta chama chao na badala yake wanatakiwa wawe wameshajulishwa kuwa wanatakiwa waipigie chadema ambayo inawakilisha hivyo vyama vyao. Elimu ni muhimu hasa huko vijijini na ukizingatia muda unaishia sasa.
 
Wasomi mnaharibu taaruma zenu kwakuficha ukweli wamambo haya bhana alibuni kizazi kijacho kwakutoa tathimini isiyokua na haki kwa raia. Ila mkiwa mnafanya hivi mtatuatalishia maisha sisi watu wachini kwasbb nyie mumeshapata mema ya nchi sisi ambao hatujapata mnatudidimiza. Kuweni makini ktk kutumia elimu yenu ili tunufaike nasi kwa elimu yenu. Ili nanyi muandikwe katk kumbkumb kwamazr. Mungu bariki Tanzania mungu mbaliki mpakwa mafuta wako ili ashinde vishawishi anavyokutana navyo.
 
Kumbe wanawapa simu na chaja vijijini ndio wawape majibu ya utafiti.....haaa.....very funny.....! Halafu utegemee majibu ambayo ni independent......!Wajinga ndio waliwao.....!
 
Sasa hasira imehamia mtaani...........sasa ni man to man campaign, hakuna lori, hakuna basi, hakuna posho, hakuna fulana, hakuna kofia, kiu ni mabadiliko, mtanzania changamka hakikisha una watu 50 walioelewa dhana ya mabadiliko na watakaopigia kura mabadiliko, M4C original sio "MforC"

Inachosha na inaboa hii
 
Samahani wadau mimi sijaelewa huu utafiti unahusu tanganyika pekee au hadi zanzibar na kama unahusu Tanzania mbona napata shida kidogo afu wanatenganishaje ukawa na chadema afy watu wanashabikia bora wangekaa kimya wanajidhalilisha mi naona maswali magumu ya aibu kwa wasomi wetu
SAUTI YA WANANCHI ITASIKIKA OCT 25/2015
 
Magufuli anaongoza kwa asilimia 66

Ujue kinachonifanya niwaone malofa na wapumbavu zaidi ni..kuwa, asilimia 70 ya waliojiandikisha kupiga kura ni vijana. Alafu hapohapo mnasema Lowasa anakubalika zaidi na vijana....alafi hapohapo mnasema ana wastana wa asilimia 22?? Holly ----!!! hiivi kwa hesabu za kijinga tu mnashindwa kuona upishi ulioshindwa viungo??
 
Mkuu inabidi kwanza ujue role yake ni ipi. mimi nimeona kwenye bango kuwa ameitwa kama mgeni mwalikwa, sasa sijui kama alishiriki kwenye utafiti au ameingizwa chaka kwa kutumiwa kuung'arisha utafiti!
mkuu maria pale kaongea kuwa naye ni mmoja wa walioshiriki huo utafiti na sio mgeni mwalikwa. Labda ndio maana yule dokta kaona ujinga hakuja
 
na wameenda kuhoji Dodoma ,Tanga na Morogoro

Hapa dodoma ccm watatafuta kura kwa tochi,ukawa inakubalika kuanzia mjini mpaka vijijini,lowasa anakubalika kila kona,hao twaweza warudi tena kwenye field au kwenye makablasha yao walete utafiti wenyewr u walioutengeneza na January makamba ni feki
 
Mgombea wa ccm analalamika kuwa mxhana kunawatu wako nae wakiachana wanaeenda upande mwingine....
Hii maanake nini ameshaona dalili mbaya kuna wanachana kibao wa ccm hawajatoka lakini hawana imani na ccm hii ni hatari kumbuka kuna jamaa kasema hata wakikaa wana ccm watano lazima habari yao inawafikia ulawa..
Jana bukoba wanafunzi kibao wamekuja kuona ccm fiesta nao pia wmejumlishwa kwenye huu utafiti njaa..wenzetu ethiopia wamezindua tren ya ume
d sisi tumekalia ujinga tuuuu na mungu ametupa kila kitu kasoro uongozi hatuna
 
hivi kumbe waliwagawia simu na chaja wanaoulizwa maswali tangu 2012??
au nimesikia vibaya!!! msaada plz......
Tuache kuhangaika na upuuzi huu! Haiwezekani LOWASSA awe mbali kiasi hicho, Hawa Twaweza hatutawaamini tena! Ni wachumia tumbo wakubwa hawana hata haya. Waangalie tafiti walizomfanyia LOWASSA wakati yuko CCM! Alishinda kila utafiti! Mpaka hata CHADEMA wakanunua kampuni imfanyie utafiti LOWASSA wakati yuko CCM lakini akapigwa na butwaa na ushindi wake na ndio Dr Slaa akashauri ahamie Chadema baada ya kukatwa CCM.
 
Back
Top Bottom