Ripoti ya Twaweza ya #SautiZaWananchi: Magufuli na CCM wang'ara dhidi ya wapinzani - Sept 22, 2015

Mods, naomba msiuunganishe uzi huu na uzi mwinginetafadhali!

Wakuu,
Ikumbukwe kwamba wakati CDM inafanya maamuzi ya kubadili gia angani, M/Kitiwake alisema kwamba walikuwa wameshafanya utafiti tena kwa kutumia Wataalamkutoka nje ya nchi. Kwa mujibu wa Mbowe, utafiti huo ulionesha kwamba ni kwakubadili gia tu angani (kwa kumchukua Mhe. ENL) ndipo UKAWA ungeweza kushindaUchaguzi wa Mwaka huu. Ingawa taarifa zaidi kuhusiana na Utafiti huohazikutolewa (ikiwemo vigezo, sampuli, muda na malengo ya Utafiti huo) hatahivyo ni wakati muafaka sasa wa UKAWA kujiuliza endapo kweli ule Utafiti wao waawali bado unaakisi uhalisia wa mazingira ya kisiasa hasa katika kipindi hikikifupi kilichobaki kuelekea Uchaguzi Mkuu. Tayari tafiti mbili zimeshatolewa nazote zinaonyesha kukanusha ule Utafiti wa UKAWA uliopelekea gia kubadilishwa angani!Sasa swali ni je, bado ule Utafiti wa Mbowe unaakisi uhalisia uliopo kwasasa??????


 
Wewe Hauna Macho? Unataka nani akwambie? Fanya Tafiti mwenyewe utajua ukweli wa Swali Lako.

Yaani unataka nifanye Utafiti kujua ulipo ule Utafiti wa Mbowe? Nadhani wewe si mzima kichwani, wahi hospitalini mapema kabla malaria haijapanda kichwani!
 
Muda umefika sasa kwa ripoti ya twaweza kufanyiwa uhakiki na wananchi wenyewe ,na majibu ya uhakika kupatikana .Matokeo yakitoka nitakuwa nayo mezani kulinganisha kila kipengele nitaandika ripoti ya majumuisho na kuchapisha andiko la kitaaluma litakalokuwa na kichwa "Mambo yanayoathiri tafiti za Uchaguzi Tanzania:Case of TWAWEZA 2015
 
".......mtu akikuambia upige kura na ulinde kura ..mwambie mzee njoo tulinde wote..."
Kanali kinana

Jioni njema kwa hisani ya raisi wa awamu ya tano
Dkt john pombe magufuli.
 
Back
Top Bottom