Ripoti ya Twaweza ya #SautiZaWananchi: Magufuli na CCM wang'ara dhidi ya wapinzani - Sept 22, 2015

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,200
4,988
Wakuu,

Twaweza kupitia utafiti wao wa Sauti Za Wananchi wanazindua utafiti kuelekea Uchaguzi mkuu leo hii, saa nne kamili asbuhi hadi saa sita katika ukumbi wa Makumbusho.

Ripoti hiyo ya #SautiZaWananchi inahusisha vyama vyote vitakavyoshiriki #Uchaguzi2015 katika kugombea kiti cha uraisi.JamiiForums kushirikiana na Twaweza inawaletea LIVE updates ya uzinduzi wa ripoti na tafiti za ripoti hiyo.

Wasalaam!

Mkurugenzi wa Twaweza.jpg

Mkurugenzi wa TWAWEZA

Uzinduzi umeanza rasmi saa 4:10 Asubuhi.
=========

2012 Udiwani asilimia 60 wangepigia CCM

2015 kwenye udiwani asilimia 60 CHADEMA 24% CUF 2% ACT 1% UKAWA 3%

Mwaka 2014 Kwenye ubunge CCM 47% CHADEMA 23%, 4%

Mwaka 2015 kwenye ubunge asilimia 60 wangepigia CCM, CHADEMA 26%

Kwenye urais mwaka 2014 wangeipigia kura CCM asilimia 51 na CHADEMA asilimia 23

2015 kwenye urais 66% wangepigia kura CCM, 22% CHADEMA, UKAWA 3%

Kama uchaguzi ungefanyika leo asilimia 65% walisema Magufuli, 25% walisema Lowassa.

Magufuli anapendwa zaidi vijijini na Lowassa mijini, japo kote Magufuli anaongoza. Kadri watu wanavyokuwa wazee wanamchagua Magufuli na Lowassa kwa vijana zaidi.

Zaidi ya asilimia 60 ya wasiosoma wako kwa Magufuli, nusu ya wasomi wako kwa Magufuli.

Kwanini utampigia kura mgombea wako? Kwa Magufuli asilimia 26 ni kwa sababu ni mchapakazi na 2% wanaitoa sababu hio kwa Lowassa, 12% wanasema Lowassa anaweza kuleta mabadiliko ilhali 7% wanasema Magufuli anaweza kuleta mabadiliko, kwenye sera nzuri 5% kwa Magufuli na 3% kwa Lowassa.

Last edited by a moderator:
Huo ni utafiti ambao hautofautiani na utabiri, na unafanywa kwa watu wasio timia o.oooo1% ya idadi ya wapiga kura, ni chombo ambacho hakina uhakika, sidhani it will never make any difference to the actual facts on ground and on 25th October.
 
Wakuu,

Twaweza kupitia utafiti wao wa Sauti Za Wananchi wanazindua utafiti kuelekea Uchaguzi mkuu leo hii, saa nne kamili asbuhi hadi saa sita katika ukumbi wa Makumbusho.

[FONT=Helvetica Neue, Helvetica, Arial, sans-serif]Ripoti hiyo ya #SautiZaWananchi inahusisha vyama vyote vitakavyoshiriki #Uchaguzi2015 katika kugombea kiti cha uraisi.JamiiForums kushirikiana na Twaweza inawaletea LIVE updates ya uzinduzi wa ripoti na tafiti za ripoti hiyo.[/FONT]
[FONT=Helvetica Neue, Helvetica, Arial, sans-serif]
[/FONT]
Wasalaam!

Nasikia kua imetengenezwa... Ata hivyo tafiti nyingi za nchi zq kiafrika asa za kisiasa mara nyingi haziaminiki.. naisi awe lowasa au magufuli muda bado upo kwa raundi nyingn ya kusawazisha mambo..#ukwelihubakimoyoni#
 
Hivi twaweza ni UKAWA ipi tena.NGO hii inatafuta mishiko tu.hawana utaalamu wowote.wao wafuatilie ilani yao
 
Kuchakachua wanaweza lakini,mwisho wa siku LOWASA ndiye rais ajaye,mgonjwa hufarijiwa,hata kama hakuna matumaini ya kupona,usimwambie mgonjwa kuwa hatapona bali mpe faraja na yeye ajisikie!kama vp wawape ccm 100%ili wafarijike,25 oktoba ni LOWASSA IKULU
 
Leo TWAWEZA watatoa utafiti wao.. ambayo inaongozwa na miriam sarungi baada ya hapo siku zijazo REDET watatoa zao lkn nawaombeni mjue ni kwann JANUARY alitangaza asilimia zile,,,ule ulikuwa ni mpango ambao kwss utafuatiwa na TWAWEZA, halafu REDET yote yaki pendelea CCM na kutengeneza mazingira ya kuiba kura maana hawana namna nyingine. Kutokana hali hyo nawaombeni ndugu zangu msiwe na wasiwasi ppt ulipo endelea kupigana
Taarifa za uhakika nilizopata CCM imeandaa utafiti feki kupitia Twaweza....watasema Magufuli ana asilimia 68% na Lowassa 22%

Ripoti halali wanayo ya Lowassa kuongoza lakini watatoa ripoti Feki.

Kwa huu muda wa asubuhi mpaka saa 4 pigeni kelele kupitia njia mbalimbali kulaani ushenzi huu.Tumieni JF,FB,tweeter,Instagram nk...
 
hiyo taarifa alishaitoa msemaji wa ccm wiki jana so sio kitu kipya na ukiangalia hata magazeti yaliyoandika juu ya utafiti huo kwa leo ni yale yale uhuru na mengineyo. nawaonea huruma hao wataalam watakaitumika kuilezea hiyo tafiti.
 
Back
Top Bottom