Ripoti ya mauaji ya raia Dar sasa kesho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya mauaji ya raia Dar sasa kesho

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, May 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.  Ripoti ya timu iliyoundwa na Jeshi la Polisi nchini kuchunguza mauaji ya raia Octavian Kashita, ambaye alipigwa risasi na polisi wa kituo cha Oysterbay, inatarajiwa kuwekwa hadharani kesho.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema taarifa hizo ni pamoja na timu mbalimbali walizowahi kuziunda ambazo zilikuwa zikichunguza matukio ya mauaji ya raia yaliyofanywa na askari wake jijini Dar es Salaam.
  "Ripoti za matukio hayo zilikuwa zimekamilika lakini tulikuwa hatujaziweka wazi kwenye jamii," alifafanua.
  Kamanda Kova alisema kwa sasa timu inayochunguza mauaji ya Kashita inaendelea na kazi ya kuchunguza taarifa mbalimbali walizozipokea kutoka kwa wananchi.
  Aidha, aliwataka mtu yeyote mwenye taarifa, apige simu namba 0715 748333.
  Mauaji ya raia huyo yalitokea Jumapili ya wiki iliyopita baada ya askari watano wa kituo cha polisi Oysterbay kupata taarifa za kuwepo kwa watekaji eneo la Victoria karibu na nyumba za viongozi wa serikali.
  Askari hao ni Koplo Ahmad, Detective Cyprian, PC Kombo, PC Kasa na PC Charles ambao kwa sasa wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Usishangae ukiambiwa Polisi walikuwa wanajilinda!
   
 3. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,814
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  blaaaah,blaaaaaaaaaah,blaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaha,blaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaablllllllllllllllaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.hili zee jitu la wapi hili???natamani ningekua prezidaa nikalikata makofi mawili matatu na hizi taarifa zake za kifala huku linaripoti kifo cha mtu,watu wanasikitika mtu katutoka we unaKUJA NA MLOLONGO WA TAARIFA YA UCHUNGUZI WA POLISI WAKATI POLISI NDIO KAUA?NONSENSE.katika watu watakufa vibaya wewe kova wa kwanza maana una-cover habari ya kifo kama vile unasimulia mwali alivyoolewa kwa mbwembwe.:angry:
   
 4. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wana edit kwanza ripoti ili kuwasafisha polisi wao!
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Wahenga walisema tomorrow never comes, kamanda Kova kesho uliyoisema ni ya terehe 20 may 2010 au ya siku utakayoulizwa, hata kama ni mwaka kesho?????

  Jamani kama hiyo ripoti imetolewa na mtu anayo sio mbaya akiweka jamvini.
   
Loading...