Ripoti ya kumchunguza Jairo imeota mbawa?

Status
Not open for further replies.

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
....Zikiwa zimebakia siku mbili bunge kuharishwa hakuna dalili wala taarifa za lini taarifa ya kuchunguza sakata la Jairo aliyekuwa katibu wa wizara ya nishati na madini itawekwa mezani kwa ajili ya majadiliano na maamuzi...Hii inaanza kutilia shaka dhamira ya bunge hili linaloongozwa na Bi Anne Makinda ambalo linaonekana kuanza kulemewa na hoja ya mswada wa mabadiliko ya katiba..Je,kuna taarifa za kusomwa hoja hii?
 
bunge ni kama kuwadi wa serikali ktk kutetea ufisadi. Na hivi spika mwenyewe kapewa ubunge kwa style ya viti maalum, unadhani kuna kitu tena hapo. acha kabisa huyu mama historia itamnyuka kweli.
 
Tusubiri Ijumaa... lakini nahisi kama tunarudi kule kule wakati wa bunge la Mzee Msekwa. Anna Makinda ni janga la kitaifa as in janga la kitaifa. Spika gani anakaa anaongoza mipasho badala ya hoja za kitaifa?
 
Nadhani kilamtanzania hili swala analisubiri kwa hamu sana, ila ngoja tuvute subira kwanza hadi kesho tuone litakuwaje
 
yeah walisema mwisho kabisa mwa kikao ndo watalijadili, shaka yangu ni wameweka mwisho ili mpasuko wake usiyumbishe bunge na serikali ama wasilijadili kwa kina for mama makinda ataua hoja kwa kusema "muda ni mchache"
 
Huyu Bi Kidude akiona tu inakula kwake huwa anauchuna. Hivi ile ya Lema na Mtoto wa Mkulima kugeuka msanii na kudanganya wabongo ilishasomwa kweli? Nakumbuka uwongo wa kwanza Pinda alisema watanzania watatu wamekufa kumbe ni waTz wawili na mkenya mmoja, tehe tehe, Anne Semamba Makinda ni janga la taifa.
 
tusubiri ijumaa ila inaweza kuwekwa mwishoni baadae utasikia muda umekwisha with no conclusion... kaaz kwelkweli na huyu makinda
 
Aahh ile mbona wanaichakachua live maana wabunge waliopewa rungu wote vilaza!!!sasa wamejazwa mapesa watasema urongo mkilazimshwa sana mtapewa urongo mtulie!!JK na serikali yake sijui watajaficha wapi baada 2015 nawaonea huruma!!
 
kichwa cha habari cha mwanahalisi la leo kilikuwa 'Jairo Akaangwa'.
Kwa ufupi wanasema ..Jairo amepatikana na hatia ya kujipa mamlaka ya kutenda kinyume na maelekezo ya serikali; kukusanya fedha na kupanga matumizi yake , bila kibali cha hazina....!
 
Mi nadhani kuna umuhimu wa kukodisha snippers tuanze wavua magamba kwa nguvu...tukimaliza mafisadi yote tunahamia kwa wanaopenda wake za watu...
 
....Zikiwa zimebakia siku mbili bunge kuharishwa hakuna dalili wala taarifa za lini taarifa ya kuchunguza sakata la Jairo aliyekuwa katibu wa wizara ya nishati na madini itawekwa mezani kwa ajili ya majadiliano na maamuzi...Hii inaanza kutilia shaka dhamira ya bunge hili linaloongozwa na Bi Anne Makinda ambalo linaonekana kuanza kulemewa na hoja ya mswada wa mabadiliko ya katiba..Je,kuna taarifa za kusomwa hoja hii?

Nilisikia ni ijumaa ambayo ni siku ya mwisho ila cjui wameweka hiyo siku ili iweje?
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom