Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Huu ni upuuzi mtupu kamati imetoa ripoti ya kimagambamagamba.
 
Naomba mnisamehe nimeshindwa kuimaliza ripoti ya Nchimbi, inawasafisha polisi kwa kumwaga damu isiyo na hatia!!! Inawatwika CDM lawama zote? Upuuzi mtupu. Kwanza hata secretary aliyechapa ripoti hajui kazi, unawezaje 'ku-centre report muhimu kama hii!!!
 
Duh!! Nimechanganyikiwa kabisa na ripoti ya Ihema. Hata apetaiti ya ngono imeyeyuka kabisa. Acha nilie kwanza.
 
Mkuu BAK hii report iliwekwa Jana na mkuu n00b nikaapa kutoisoma kwasababu report ya Kamati nilikuwa najua watakacho andika ni kutetea serikali
 
Reactions: BAK
siku nyingine ukimsikiliza Tundu Lissu, Mkuu hautaumiza kichwa chako tena. nafikiri utakubaliana na chadema kuwa kutoa maoni kwenye kamati ya arusi ilikuwa ni kupoteza muda bure.
 
CDM waliikataa hii kamati ya Nchimbi, kamati hakukuwa na uwezekano wa kupata maoni kutoka kwa viongozi wa chama, CDM.
 
Ripoti ya Nchimbi ni janga la taifa na walioindaa ni wasaliti wa haki, usawa, amisha ya Mtanzania


A man who stands for nothing will fall for anything.

Malcolm X



Be peaceful, be courteous, obey the law, respect everyone; but if someone puts his hand on you, send him to the cemetery.
Malcolm X
For to be free is not merely to cast off one's chains, but to live in a way that respects and enhances the freedom of others.
Nelson Mandela
 
Waache walindane,wananchi wanaona.Iko siku watafikishwa mbele ya sheria kujibu ukatili wanaofanyia wananchi.Haki haiibiwi,ila inacheleweshwa.Hii inaonyesha matumizi mabaya ya madaraka na kodi za wavuja jasho wa Tanzani.Naamini iko siku itafika MUNGU atatutoa kwenye huu utawala wa hila.
 
Hongerani wajumbe kwanza pokeeni pongezi nyingi kwa kufanya kwa uadilifu na umakini wa hali juu; yakhe twaelewa haikuwa kazi rahisi kwa wajumbe kutekeleza majukumu yenu; ripoti safi imekamilika na ina vigezo vyote muhimu; yakhe wote twajua vyanzo vya vurumai zile; ripoti muafaka asiyokubaliana nayo atupe yake tusome.
 
ngoja nikapige kibarua nisije nikachafua siku yangu kwa kusoma upuuzi wa hawa wapuuzi.
 
Sasa naungana na wale waliopinga uteuzi wa ile kamati ya MHE NCHIMBI, mbali na picha tulizoziona wakimsurubu na kumtoa roho, ETI hawahusiki.................!!!
 
Mimi hata sijapoteza muda wa kusoma ripoti ya Nchimbi. Nimesoma mpaka katikati na kuona siasa mtupu

Na ile ya MCT nayo tangu mwanzo inaonesha ni zile zile habari tulokuwa tunasoma magazetini

MIMI NASUBIRI RIPOTI YA TUME INAYOONGOZWA NA MANUMBA IKIMSHIRIKISHA TUMAINI MAKENE. BILA SHAKA HAPO TUTARAJIE USHAHIDI WA KISAYANSI(FORENSIC)

Bomu la machozi haliwezi kusambaratisha mwili wa binadamu kwa kiwango kile. Mfano taarifa ya awali ya polisi inasema KITU "KIZITO" mimi naona kizito ina implicit meaning ya bomu la kivita

POLISI WALIKUWA NA LENGO LA KUUA HAKUNA UBISHI ushahidi ni jinsi walivyopiga lile bomu kwa ukaribu. Sasa sioni kitachowazuia iwapo ile ile bunduki inayotumika kufyatulia mabomu ya machozi inaweza kufyatulia bomu la kivita(tazama mabandiko na link hapo chini)

Kuua kwa bomu la machozi kunaweza kusameheka. Kwa askari wa kuzuia ghasia hiyo ni ajali kazini, ila bomu la kivita linapotumika katika mazingira yale ni mauaji yaliyokusudiwa. Sasa kutokana na upotoshaji wa tukio hili tutategemea uwajibikaji kuanzia ikulu maana hata rais ametoa taarifa zinazolenga kuuficha ukweli

 
Ndugu wana jamii forum kama mlivyojionea wenyewe kwenye vyombo vya habari jana taarifa mbili zikitoa ripoti tofauti juu ya suala moja hii haingii kabisa akilini. Sasa je ripoti ipi ni ya ukweli?
 
Kwa ujumla ripoti hii imekidhi hadidu za rejea za kamati, kumbukeni nchi inakasumba ya kuundwa kamati/tume mara kwa mara hasa kwenye masuala yanayohusu serikali na serikali hiyo hiyo ambayo huwa inaunda tume ama unaweza kuita siku hizi kamati baada ya wananchi kueleweshwa na Tundu Lissu, kwa kifupi hadidu za rejea huwa zinalenga kundoa hasira za wananchi kwa serikali jinsi suala fulani lilivyoshughulikiwa, hivyo basi sikutegemea kama Jaji Ihema atakuwa na jipya.:shock::shock::hatari:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…