Mpango wa Marekani kuiondoa China kwenye sekta ya madini barani Afrika ni hatari kwa maendeleo ya Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG211431316181.jpg


Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani, hasa kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za madini adimu zinazotumika kwenye sekta za utengenezaji wa magari yanayotumia umeme na vifaa mbalimbali vya kuvuna nishati ya jua. Afrika, bara lenye utajiri mkubwa wa madini hayo limerudi tena kwenye ufuatiliaji mkali wa nchi za magharibi. Bahati mbaya ni kuwa ufuatiliaji huo, si kama tu unalenga kupata mgao katika madini hayo kwa ajili ya kuendeleza sekta hizo, bali unalenga kuizuia China kuwa na ushirikiano wa kina na nchi za Afrika kwenye sekta ya madini.

Mwezi Juni mwaka huu, taasisi ya amani ya Marekani (United States Peace Institute) iliandaa mdahalo kuhusu mchango wa China kwenye ukuaji wa sekta ya madini barani Afrika, na matokeo yake kwenye masuala ya amani na usalama barani Afrika. Pamoja na kuwa mdahalo huo ulijificha kwenye jina la amani na usalama, undani wake ulikuwa ni sekta ya madini barani Afrika, na hasa kuhusu jinsi Marekani na nchi za magharibi zinavyoweza kushindana na China kwenye sekta ya madini barani Afrika.

Katika kipindi kati ya mwaka 2016 hadi mwaka 2022, ushiriki kwenye sekta ya madini barani Afrika kwa China, Umoja wa Ulaya uliongezeka kwa kasi, China imechukua nafasi ya kwanza, Umoja wa Ulaya umechukua nafasi ya pili, lakini Marekani imekuwa ya mwisho. Ni vizuri ikikumbukwa kuwa ni katika kipindi hicho hasa (2017 – 2021), Marekani chini ya Rais Donald Trump, iliendesha sera ya kuliweka pembeni bara la Afrika, kipindi ambacho China na Umoja wa Ulaya walikuwa na harakati za kuhimiza ushirikiano na nchi za Afrika kwenye sekta ya madini.

Kutoka na kuwa ushirikiano huo umeonekana kuzifanya China na Umoja wa Ulaya kuitangulia Marekani kwenye ushindani kwenye soko la kimataifa kwenye sekta ya magari yanayotumia umeme, ambayo malighafi yake muhimu ni madini yanayotoka Afrika, Marekani imekuwa inatafuta kisingizio cha kuizuia China, na kwa kiasi fulani kuzikwamisha nchi za Ulaya, kuwa na ushirikiano wa kina kwenye sekta ya madini, kwa kisingizio cha utatanishi kwenye masuala ya amani.

Uzuri ni kwamba takwimu zilizotolewa kwenye mdahalo huo zimeonesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2019, China iliwekeza dola bilioni 10 za kimarekani kwenye sekta ya madini katika eneo la Afrika kusini mwa sahara. Na fedha hizo ni pamoja na uwekezaji wa moja kwa moja, malipo ya kodi na hata kwenye uwekezaji kwenye miundombinu mbalimbali inayolenga kusaidia maisha ya watu. Kwa ufupi fedha zilizowekezwa na China kwenye nchi za Afrika zinaonekana, na zimekuwa na manufaa kwa nchi za Afrika.

Uwekezaji kwenye sekta ya madini si jambo geni kwa nchi za Afrika. Nchi za magharibi zimekuwepo kwenye sekta hiyo kwa muda mrefu sana, lakini matokeo ya uwekezaji huo kwa nchi za Afrika yamekuwa ni mbaya na ya kusikitisha. Mfano mzuri ni ule ambao umekuwa ukionekana kwenye nchi za Afrika Magharibi, ambako watu wa huko wamekuwa wakilalamika kutonufaika na maliasili zao za madini kutokana na uwekezaji wa nchi za Ulaya.

Ni wazi kuwa kukaribishwa kwa uwekezaji wa China kwenye sekta hiyo barani Afrika kunatokana na kanuni ya kunufaisha (win-win situation) ambayo ndio msingi wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na nchi nyingine. Hii ni tofauti na kanuni ya baadhi ya nchi za magharibi ambazo uwekezaji wake unaishia kuchimba madini na kuacha mashimo tu, bila kuwa na uwekezaji wowote ule wa maana.

Nchi za Afrika zimekuwa zikikaribisha uwekezaji wowote wenye manufaa kwa watu wake, ndio maana China imekuwa mbele ya nchi za Ulaya na Marekani kwenye uwekezaji huo. Marekani ambayo tangu Rais Biden aingie madarakani inaonekana kuwa na mtazamo chanya kwa Afrika, pia ina fursa ya kuwekeza barani humo. Kama uwekezaji wake utakuwa na manufaa kwa bara la Afrika bila shaka utakaribishwa, lakini lengo la kuifukuza China na kuchimba madini na kuacha mashimo barani Afrika, basi uwezekano wa kukaribishwa ni mdogo sana
 
The crazyness is wazungu wamekaa miaka 200+ barani Africa wameshondwaje kudhibiti madini wakati mchina hana miaka zaidi ya 20 barani. Wazungu mda mwingine ni wehu na chizi wao mkuu ni mwafrika anae ruhusu yote hayo kufanyika.
 
Back
Top Bottom