Ripoti ya "ajabu" ya NAPE huko Houston...!

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Ni ajabu na inashangaza..,

Katika ziara ya Nape inayoendelea hivi sasa nchini marekani kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo katika zama za sasa na upepo wa kisiasa ulivyo hasa ndani ya CCM ni sawa kuyaita matukio hayo kuwa ni ajabu na yasiyotegemewa hasa kwa mtu kama Nape kulingana na umri wake na hata nafasi yake. Miongoni mwa matukio hayo nitayataja baadhi, ambayo Nape ameonyesha uwezo mkubwa wa kisiasa na uelewa wa siasa za kimataifa na mahusiano ya kidplomasia, pale alipofanikiwa kwa mara moja kumaliza mgogoro ambao ulidumu kwa muda mrefu baina ya watanzania waliopo jimbo la texas jijini houston, mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni. Uwezo huu wa Nape kumaliza mgogoro mkubwa na tata kwa watanzania hao kwa muda mchache umeonekana ni wa ajabu kwani wengi walishindwa hapo kabla,alinukuliwa mmoja wa watanzania waishio jijini humo anayejulikana kwa jina la bwana Kittoga.

Nape pia alisisitiza kwa watanzania wa houston hasa wanaCCM kuwa lazima chama kisogezwe kwa wanachama kiutendaji na kimaamuzi na kusisitiza kuwa hilo ni agizo la Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Hivyo kuwataka wafungue matawi zaidi ili kuwafikia wengi zaidi kwa ukaribu na urahisi zaidi wa kufuatilia na kushughulikia shughuli za chama.

Lakini jambo lingine ambalo pia liliwashangaza wengi ni upeo binafsi wa Nape pale ilipofika wasaa wa maswali ya papo kwa hapo.,ambapo Nape alitumia muda mwingi wa mkutano wake katika hili ambapo watanzania hao wa houston walipata kuuliza juu ya hali halisi ya uchumi na maisha ya watanzania, ndipo Nape alipowaeleza kwa undani juu ya changamoto zinazoikabili serikali ya awamu ya nne na chama kama taasisi inayoisimamia serikali na pia kuelezea mafanikio yaliyopatikana chini ya CCM, kwa namna ya kipekee kabisa ya ufafanuzi na tafsiri sahihi ya matukio yanayoendelea Tanzania.

Na ilipofika wakati wa kuelezea juu ya falsafa ya chama inayotawala vichwa vya wengi nae Nape aliitolea maelezo, kuwa ni dhana iliyopotoswa sana kitafsiri hasa na wapinzani lakini aliwahakikishia kuwa hiyo ni falsafa ya mabadiliko makubwa katika chama yenye kulenga kubadili taswira mbaya ya chama na kukipa chama nguvu mpya kiutendaji na maamuzi na pia umaarufu zaidi na kukubalika hasa kwa vijana.

Alisisitiza kuwa "falsafa ya kujivua gamba na vita vya ufisadi ndani ya Tanzania ni vitu vinavyoenda sambamba,kwani zote vita dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi"

Aidha alimalizia kwa kuwataka Wana CCM kutumia matawi yao ya Chama kuwaunganisha Watanzania badala a kugeuka vijiwe vya majungu na kubaguana kwa vigezo vyovyote vile, huku akiwataka kuweka Utanzania wao kwanza kuliko itikadi na tofauti zao malimbali.

Nape anaendelea na ziara yake nchini Marekani yenye lengo la kukagua uhai wa chama, ambapo atatembelea Columbus-Ohio, New York na atamalizia Washington Dc, kabla ya kurejea nchini Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.
 
Suti bei gani hapo? ningependa aninunulie za huko! chama kutumia milions kwajili ya kwenda kusuluhisha wanachama huko Marekani? Mbona msisuluhishe haya makundi ndani ya CCM hapa kitaani? Najua makundi yapo na nyie mlikiri, sasa kwanini hizo resources msingezirumia kumaliza migogoro yenu kwanza? Haya tour njema
 
Inasikitisha!
Kama Watanzania hao waliridhika na majibu ya Nape, huku wakijua waziwazi hali halisi ya Mtanzania wa kawaida, BASI nashawishika kuzua shaka juu ya uzalendo wao, na huenda walifika Tanzania zamani mno!
 
Inasikitisha!
Kama Watanzania hao waliridhika na majibu ya Nape, huku wakijua waziwazi hali halisi ya Mtanzania wa kawaida, BASI nashawishika kuzua shaka juu ya uzalendo wao, na huenda walifika Tanzania zamani mno!
Kwanini wategemee majibu ya NAPE wakati wao wenyewe wanaweza wakatembelea nchini, au kufanya tafiti ndogo tu za hali ya uchumi na kipato kwa Mtanzania?
Huenda kweli wengi walioko huko ni watoto wa zile familia bora...ambapo matatizo wanafanya kuyasikia kama simulizi katika kitabu cha NGANO ZA KALE.
 
Nyie wabeba box wapika chips na wakaaanga mandazi rudini mjumuike na mama/baba lishe huku bongo kuijenga nchi.
Pombaf! Mnaenda nchi za watu then mnaenda kugombana huko. Akili matope na mwigizaji wenu huyo wa kaole...mwambieni aache kujipaka carolite itamuua!
 
Nape ni NURU na TAA ya matumaini yaliopotea CCM kwa siku nyingi.Anawanyima usingizi wapinzani wake na anazidi kuwatimulia vumbi, ushahidi ni Igunga.viva nape viva ccm viva kikwete.
 
Napenda jinsi ambavyo Nape ameamua kujipulizia tarumbeta yake mwenyewe huko Ughaibuni kwa hili na lile kila uchao huko. Raha jipe mwenyewe mkuu endapo wana JF tunaona tu utupu kwa utendaji wako na kauli tata kwenye mikutano mbalimbali.

Hebu tengenezesha hata kapicha kwenye photoshop ili ikawaonyeshe 'wanaokuamini' jinsi unavyoshangiliwa kwa kuwa mmbunifu sana kutatua migogoro kuliko hata rais Kikwete kama ilivyodaiwa hapo juu.
 
Umeshaanzisha id nne tarehe 16 june, id hizo zimeanzisha thread kuhusu houston leo mapema, zimechangia..umeona haitoshi.
Umetumia id nyingine tena, umejiandikia report yako na kuileta humu....
Unaonyesha jinsi ulivyo mkangafu!
 
Baanda ya kutoka ughaibuni Nape yalazima tukuvue gamba maana siku 90 ulizoziahidi zilikwisha badala yake unakimbilia ughaibuni.
 
Ni ajabu na inashangaza..,

Katika ziara ya Nape inayoendelea hivi sasa nchini marekani kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo katika zama za sasa na upepo wa kisiasa ulivyo hasa ndani ya CCM ni sawa kuyaita matukio hayo kuwa ni ajabu na yasiyotegemewa hasa kwa mtu kama Nape kulingana na umri wake na hata nafasi yake. Miongoni mwa matukio hayo nitayataja baadhi, ambayo Nape ameonyesha uwezo mkubwa wa kisiasa na uelewa wa siasa za kimataifa na mahusiano ya kidplomasia, pale alipofanikiwa kwa mara moja kumaliza mgogoro ambao ulidumu kwa muda mrefu baina ya watanzania waliopo jimbo la texas jijini houston, mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni. Uwezo huu wa Nape kumaliza mgogoro mkubwa na tata kwa watanzania hao kwa muda mchache umeonekana ni wa ajabu kwani wengi walishindwa hapo kabla,alinukuliwa mmoja wa watanzania waishio jijini humo anayejulikana kwa jina la bwana Kittoga.
KWENYE RED NI UDHAIFU MWINGINE WA NAPE! APPOINTMENT YAKE ALIYOPEWA NA MWENYEKITI WAKE WA CHAMA NI CUCOMPLEMENT , NA SIYO KUUONYESHA UMMA UDHAIFU WA BOSI WAKE!!! we do not work in organisations this way! - DEBE TUPU!!!!
 
Kwa maelezo ya Tandaleone ni kwamba Rais Kikwete alishindwa kutatua mgogoro wa Houston lakini Nape kafanikiwa! Kama hii habari ya kweli basi matatizo ya ccm ni makubwa kuliko tujuavyo.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
To be honest mi sioni kile kinachofanya hii iwe issue ya kujadili. Sijaona chochote Nape alichofanya kwenye taarifa hiyo. Time wastess!!
 
Hivi watu nane si familia hiyo?
Picha aliyopiga nape hapo sijui houston ilikuwa na watu nane.

swali?

Unampongeza katibu mwenezi wa chama chenye wanachama 5000000 kwa ajili ya kusuluhisha ugomvi wa watu nane?
mgogoro ndani ya chama chake ili uishe unahitaji wenezi wangapi?

Tuingie kwenye mahesabu kama katibu mwenezi mwenye uwezo kama ulivyomsifia ameweza kusuluhisha watu nane pamoja na yeye ili kusuluhisha wanachama milioni tano=5000000/8=625000.

Mnahitaji makatibu wenezi wenye upeo mkubwa kama nape laki sita na ishirini na tano elfu ili migogoro ndani ya CCM iishe.
 
Mbona siamini kuwa, kuishi nje ya tanzania unakuwa slow wa kufikiri. Mbona sisi huku tunaona kuwa nepi ni vuvuzela!!!???? Ccm yenyewe inamwita ni kansa, sasa nyie huko mnamwona ni dhahabu. Yaani nyie kweli ni kansa nyingine. Huo ni mfupa ambao hata fisi hawezi kuula.
 
Back
Top Bottom