Ripoti ya "ajabu" ya NAPE huko Houston...!

Ripoti ya "ajabu" ya NAPE huko Houston...!

Nyie wabeba box wapika chips na wakaaanga mandazi rudini mjumuike na mama/baba lishe huku bongo kuijenga nchi.
Pombaf! Mnaenda nchi za watu then mnaenda kugombana huko. Akili matope na mwigizaji wenu huyo wa kaole...mwambieni aache kujipaka carolite itamuua!

Mkuu wasamehe kwa hayo wanafanya. Utamaduni wa kutembeza bakuli umewaingia sana.
 
damn right!
Umesema vyema... Nape ni nuru na taa ya matumaini yaliyopotea CCM, sio Tanzania.... ni CCM!!!

at least ume-qualify statement yako....

As far as I am concerned, Nape is significant to CCM, and not Tanzania

Am I right?
 
Kuna vitu vingine vya k.is.enge sana...eti nape anaendelea na ziara yake inchini marekani kukagua uhai wa chama.......

uhai wa ccm marekani??!!
 
Mbona siamini kuwa, kuishi nje ya tanzania unakuwa slow wa kufikiri. Mbona sisi huku tunaona kuwa nepi ni vuvuzela!!!???? Ccm yenyewe inamwita ni kansa, sasa nyie huko mnamwona ni dhahabu. Yaani nyie kweli ni kansa nyingine. Huo ni mfupa ambao hata fisi hawezi kuula.

Mkuu kwa taarifa yako hakuna ukweli wowote katika taarifa hiyo. Mtanzania mwenye kujua mambo hawezi kuamini lolote katika taarifa hii.
 
Kuna vitu vingine vya k.is.enge sana...eti nape anaendelea na ziara yake inchini marekani kukagua uhai wa chama.......

uhai wa ccm marekani??!!

Mkuu punguza hasira njaa ni kitu kibaya sana. Huondoa common sense na utu wa kawaida.
 
Ni ajabu na inashangaza..,

Katika ziara ya Nape inayoendelea hivi sasa nchini marekani kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo katika zama za sasa na upepo wa kisiasa ulivyo hasa ndani ya CCM ni sawa kuyaita matukio hayo kuwa ni ajabu na yasiyotegemewa hasa kwa mtu kama Nape kulingana na umri wake na hata nafasi yake. Miongoni mwa matukio hayo nitayataja baadhi, ambayo Nape ameonyesha uwezo mkubwa wa kisiasa na uelewa wa siasa za kimataifa na mahusiano ya kidplomasia, pale alipofanikiwa kwa mara moja kumaliza mgogoro ambao ulidumu kwa muda mrefu baina ya watanzania waliopo jimbo la texas jijini houston, mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni. Uwezo huu wa Nape kumaliza mgogoro mkubwa na tata kwa watanzania hao kwa muda mchache umeonekana ni wa ajabu kwani wengi walishindwa hapo kabla,alinukuliwa mmoja wa watanzania waishio jijini humo anayejulikana kwa jina la bwana Kittoga.

Nape pia alisisitiza kwa watanzania wa houston hasa wanaCCM kuwa lazima chama kisogezwe kwa wanachama kiutendaji na kimaamuzi na kusisitiza kuwa hilo ni agizo la Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Hivyo kuwataka wafungue matawi zaidi ili kuwafikia wengi zaidi kwa ukaribu na urahisi zaidi wa kufuatilia na kushughulikia shughuli za chama.

Lakini jambo lingine ambalo pia liliwashangaza wengi ni upeo binafsi wa Nape pale ilipofika wasaa wa maswali ya papo kwa hapo.,ambapo Nape alitumia muda mwingi wa mkutano wake katika hili ambapo watanzania hao wa houston walipata kuuliza juu ya hali halisi ya uchumi na maisha ya watanzania, ndipo Nape alipowaeleza kwa undani juu ya changamoto zinazoikabili serikali ya awamu ya nne na chama kama taasisi inayoisimamia serikali na pia kuelezea mafanikio yaliyopatikana chini ya CCM, kwa namna ya kipekee kabisa ya ufafanuzi na tafsiri sahihi ya matukio yanayoendelea Tanzania.

Na ilipofika wakati wa kuelezea juu ya falsafa ya chama inayotawala vichwa vya wengi nae Nape aliitolea maelezo, kuwa ni dhana iliyopotoswa sana kitafsiri hasa na wapinzani lakini aliwahakikishia kuwa hiyo ni falsafa ya mabadiliko makubwa katika chama yenye kulenga kubadili taswira mbaya ya chama na kukipa chama nguvu mpya kiutendaji na maamuzi na pia umaarufu zaidi na kukubalika hasa kwa vijana.

Alisisitiza kuwa "falsafa ya kujivua gamba na vita vya ufisadi ndani ya Tanzania ni vitu vinavyoenda sambamba,kwani zote vita dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi"

Aidha alimalizia kwa kuwataka Wana CCM kutumia matawi yao ya Chama kuwaunganisha Watanzania badala a kugeuka vijiwe vya majungu na kubaguana kwa vigezo vyovyote vile, huku akiwataka kuweka Utanzania wao kwanza kuliko itikadi na tofauti zao malimbali.

Nape anaendelea na ziara yake nchini Marekani yenye lengo la kukagua uhai wa chama, ambapo atatembelea Columbus-Ohio, New York na atamalizia Washington Dc, kabla ya kurejea nchini Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.
Kama wamemtegemea nape basi mwendawazimu yeyote aweza kuwa wa msaada kwao pindi wanapoingia kwenye migogoro.
 
embu basi wekeni hata picha moja yenye wanachama hata kumi tu wakiwa na huyo Nape hili tujue the significance of this useless post. Jamani amna siasa nje ya Tanzania kinachoendelea ni uvujaji wa hela za walipa kodi tu.
 
Ni ajabu na inashangaza..,

Katika ziara ya Nape inayoendelea hivi sasa nchini marekani kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo katika zama za sasa na upepo wa kisiasa ulivyo hasa ndani ya CCM ni sawa kuyaita matukio hayo kuwa ni ajabu na yasiyotegemewa hasa kwa mtu kama Nape kulingana na umri wake na hata nafasi yake. Miongoni mwa matukio hayo nitayataja baadhi, ambayo Nape ameonyesha uwezo mkubwa wa kisiasa na uelewa wa siasa za kimataifa na mahusiano ya kidplomasia, pale alipofanikiwa kwa mara moja kumaliza mgogoro ambao ulidumu kwa muda mrefu baina ya watanzania waliopo jimbo la texas jijini houston, mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni. Uwezo huu wa Nape kumaliza mgogoro mkubwa na tata kwa watanzania hao kwa muda mchache umeonekana ni wa ajabu kwani wengi walishindwa hapo kabla,alinukuliwa mmoja wa watanzania waishio jijini humo anayejulikana kwa jina la bwana Kittoga.

Nape pia alisisitiza kwa watanzania wa houston hasa wanaCCM kuwa lazima chama kisogezwe kwa wanachama kiutendaji na kimaamuzi na kusisitiza kuwa hilo ni agizo la Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Hivyo kuwataka wafungue matawi zaidi ili kuwafikia wengi zaidi kwa ukaribu na urahisi zaidi wa kufuatilia na kushughulikia shughuli za chama.

Lakini jambo lingine ambalo pia liliwashangaza wengi ni upeo binafsi wa Nape pale ilipofika wasaa wa maswali ya papo kwa hapo.,ambapo Nape alitumia muda mwingi wa mkutano wake katika hili ambapo watanzania hao wa houston walipata kuuliza juu ya hali halisi ya uchumi na maisha ya watanzania, ndipo Nape alipowaeleza kwa undani juu ya changamoto zinazoikabili serikali ya awamu ya nne na chama kama taasisi inayoisimamia serikali na pia kuelezea mafanikio yaliyopatikana chini ya CCM, kwa namna ya kipekee kabisa ya ufafanuzi na tafsiri sahihi ya matukio yanayoendelea Tanzania.

Na ilipofika wakati wa kuelezea juu ya falsafa ya chama inayotawala vichwa vya wengi nae Nape aliitolea maelezo, kuwa ni dhana iliyopotoswa sana kitafsiri hasa na wapinzani lakini aliwahakikishia kuwa hiyo ni falsafa ya mabadiliko makubwa katika chama yenye kulenga kubadili taswira mbaya ya chama na kukipa chama nguvu mpya kiutendaji na maamuzi na pia umaarufu zaidi na kukubalika hasa kwa vijana.

Alisisitiza kuwa "falsafa ya kujivua gamba na vita vya ufisadi ndani ya Tanzania ni vitu vinavyoenda sambamba,kwani zote vita dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi"

Aidha alimalizia kwa kuwataka Wana CCM kutumia matawi yao ya Chama kuwaunganisha Watanzania badala a kugeuka vijiwe vya majungu na kubaguana kwa vigezo vyovyote vile, huku akiwataka kuweka Utanzania wao kwanza kuliko itikadi na tofauti zao malimbali.

Nape anaendelea na ziara yake nchini Marekani yenye lengo la kukagua uhai wa chama, ambapo atatembelea Columbus-Ohio, New York na atamalizia Washington Dc, kabla ya kurejea nchini Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.
Zingatia red! sijui mgogoro ungemalizika vipi kwa rais kufanya ziara peke yake au ndo unataka kusema rais alishindwa kuutatua, na kama ndo hivo ni nini uwezo wa Nape vs Rais
 
hivi nani anaweza kunionyesha ofisi za matawi ya DEMOCRATS na REPUBLICANS hapa Tanzania?

mkuu mbona yapo! kigamboni, nenda mpanda kuna tawi, ubungo symbion, kama sikosei nyamongo geita au resolute kwa ,alias, kigwangala. i stand to be corrected!
 
Hivi hao wakimbizi huwa wanapiga kura wakati wa uchaguzi? Ima maana Nape yuko kwenye ziara ya Mkoa wa kichama Marekani. Enyi wakimbia shida, mngekuwa mnayajua yanayotokea huku hata msingethubutu kumsikiliza huyo vuvuzela, kashindwa kusuluhisha mgogoro wa UVCCM Arusha, amekimbilia huko kula bata! Na wakitimiza mission yao ya kuwamaliza Anti-DOWANS nchi haitakalika!
 
Ina maan Nape akiwa nje ya nchi anakuwa na akili zaidi au tuseme basi amefunguka macho
 
...Yaani hii ni moja ya thread ya upupu ya mwaka...!! Eti JK alishindwa kumaliza mgogoro...... !! Uwezo wa kujibu hapo kwa hapo wa Nape yaani sifa hizi ni sawa na mtu kumsifia Manji kwa kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani mwenye dhamana pia ya kusimamia na kuondoa wizi !!
 
sijui kama amewaambia huku hakuna umeme wa uhakika kama huko,sukari na kila kitu bei juu dola moja 1,800/ hawajui anvyozunguka kuuwa ccm ili akija na ccj yake awe juu........
 
Once again, Hebu wawatolee uchafu wao wa magamba huko Marekani.
 
Kama nape ndo suluhisho kwani nawaombea mpoteze mawazo ya kurudi Bongo maana nyie mnaonekana mzigo kwa wapenda maendeleo na mabadiliko ya kisiasa,mtu kama kashindwa kutatua hapa leo mnasema ana uwezo mkubwa,laaa!
Nimeghaili siendelei kujadili hoja kuhusu uwezo wa Nape
 
Nape ni NURU na TAA ya matumaini yaliopotea CCM kwa siku nyingi.Anawanyima usingizi wapinzani wake na anazidi kuwatimulia vumbi, ushahidi ni Igunga.viva nape viva ccm viva kikwete.
Ninani aliyapoteza matumaini ya sisiemu? Nape alikuwa wapi wakati matumaini hayo yanapotea?Halafu kwanini unasema uongo, mbona Nepi hakuruhusiwa na mheshimiwa sana Rostam Azizi kukanyaga Igunga na alipo kaidi Mukama alimkemea kama mtoto mdogo. Kwa taarifa yako Nepi hana nuru yoyote sana sana yeye ni gundu, na ameyashika makorodani ya simba muda si mrefu atarudi kwao Singida na kilio cha mtu mzima.
 
Mbona habari yako ni ya kiujumla kama kawaida ya habari zisizo na kichwa? Unasema alikwenda kutatua matatizo ya wana CCM Houston; Mbona hakuna picha kudhihirisha upatanishi? na Ijumaa Houston alikutana na viongozi wa upinzani wa CCM -- Jumamosi alikutana na jumuia ya Watanzania wapi alipata muda huo wa kuutatua mgogoro? Sasa kama umetatuliwa Viongozi ni kina nani sasa?

Upo USA jaribu kutupa in and out and the outcome --- hakuna cha kuficha...

IMG_3380.jpg

IMG_3382.jpg
Hawa ndio waliokuwa na mgogoro huko ughaibuni? Mbona sura zao zinaonesha niwatu wenye msongo?
 
ccm wajanja sana wameamua kusuluhisha mgogoro wa nje coz wanajua 2015 nchi haitakuwa mikononi mwao hivo wanataka watu wa kuwapokea huko ughaibuni watakapoikimbia kwa kuogopa hasira za wananchi,endelea kusuluhisha nape na kujiandalia makazi.
 
Hawa ndio waliokuwa na mgogoro huko ughaibuni? Mbona sura zao zinaonesha niwatu wenye msongo?

hawa ndio wana ccm wenyewe wa houston waliobakia wengine wote walikuwa wanashangaa porojo za Nape . kwa ufupi mji wa houston unawakazi watanzania wasiopungua 1000 waliodhuria mkutano huo walikuwa watu 20 na wengi wao hawakuwa wanachama wa CCM. KWAHIYO MTU ANAYEKWAMBIA HOUSTON KUNA CCM ANACHEKESHA KWANI KUNA WAVIZIAJI WACHACHE WANAOTAFUTA PESA ZA RAIHISI.
 
Hakuna jipya! Upuuuzi mtupu! who is NAPE by the way?! kwangu ni upuuzi!
 
Back
Top Bottom