Ripoti ya "ajabu" ya NAPE huko Houston...!

Ripoti ya "ajabu" ya NAPE huko Houston...!

Badala watekeleze ahadi walizotoa ktk kampeni tangu 2005,akili yao yote ipo ktk uchaguzi wa 2015!!.Ile ya maisha bora
kwa kila Mbongo waulizeni pindi wakija tena huko.Huu ugonjwa si wa Nape peke yake ni dondandugu sugu ktk
 
Ni ajabu na inashangaza..,

Katika ziara ya Nape inayoendelea hivi sasa nchini marekani kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo katika zama za sasa na upepo wa kisiasa ulivyo hasa ndani ya CCM ni sawa kuyaita matukio hayo kuwa ni ajabu na yasiyotegemewa hasa kwa mtu kama Nape kulingana na umri wake na hata nafasi yake. Miongoni mwa matukio hayo nitayataja baadhi, ambayo Nape ameonyesha uwezo mkubwa wa kisiasa na uelewa wa siasa za kimataifa na mahusiano ya kidplomasia, pale alipofanikiwa kwa mara moja kumaliza mgogoro ambao ulidumu kwa muda mrefu baina ya watanzania waliopo jimbo la texas jijini houston, mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni. Uwezo huu wa Nape kumaliza mgogoro mkubwa na tata kwa watanzania hao kwa muda mchache umeonekana ni wa ajabu kwani wengi walishindwa hapo kabla,alinukuliwa mmoja wa watanzania waishio jijini humo anayejulikana kwa jina la bwana Kittoga.

Nape pia alisisitiza kwa watanzania wa houston hasa wanaCCM kuwa lazima chama kisogezwe kwa wanachama kiutendaji na kimaamuzi na kusisitiza kuwa hilo ni agizo la Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM. Hivyo kuwataka wafungue matawi zaidi ili kuwafikia wengi zaidi kwa ukaribu na urahisi zaidi wa kufuatilia na kushughulikia shughuli za chama.

Lakini jambo lingine ambalo pia liliwashangaza wengi ni upeo binafsi wa Nape pale ilipofika wasaa wa maswali ya papo kwa hapo.,ambapo Nape alitumia muda mwingi wa mkutano wake katika hili ambapo watanzania hao wa houston walipata kuuliza juu ya hali halisi ya uchumi na maisha ya watanzania, ndipo Nape alipowaeleza kwa undani juu ya changamoto zinazoikabili serikali ya awamu ya nne na chama kama taasisi inayoisimamia serikali na pia kuelezea mafanikio yaliyopatikana chini ya CCM, kwa namna ya kipekee kabisa ya ufafanuzi na tafsiri sahihi ya matukio yanayoendelea Tanzania.

Na ilipofika wakati wa kuelezea juu ya falsafa ya chama inayotawala vichwa vya wengi nae Nape aliitolea maelezo, kuwa ni dhana iliyopotoswa sana kitafsiri hasa na wapinzani lakini aliwahakikishia kuwa hiyo ni falsafa ya mabadiliko makubwa katika chama yenye kulenga kubadili taswira mbaya ya chama na kukipa chama nguvu mpya kiutendaji na maamuzi na pia umaarufu zaidi na kukubalika hasa kwa vijana.

Alisisitiza kuwa "falsafa ya kujivua gamba na vita vya ufisadi ndani ya Tanzania ni vitu vinavyoenda sambamba,kwani zote vita dhidi ya matumizi mabaya ya rasilimali za nchi"

Aidha alimalizia kwa kuwataka Wana CCM kutumia matawi yao ya Chama kuwaunganisha Watanzania badala a kugeuka vijiwe vya majungu na kubaguana kwa vigezo vyovyote vile, huku akiwataka kuweka Utanzania wao kwanza kuliko itikadi na tofauti zao malimbali.

Nape anaendelea na ziara yake nchini Marekani yenye lengo la kukagua uhai wa chama, ambapo atatembelea Columbus-Ohio, New York na atamalizia Washington Dc, kabla ya kurejea nchini Tanzania wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.

Hapo penye RED mmeniacha hoi WaTZ mlioko huko US. Iweje muamini kitu msichokijua. Hii ni sawa na kuuliza kuku ana miguu mingapi wakati wewe unayeuliza huna idea kabisa kuku yukoje na hapa jibu lolote utakalopewa utaliona sahihi kabisa. Hiki ndicho mnachomsifia nacho Nape .i.e. IGNORRANCE Yyenu kwa mambo yalivyo sasa TZ. SHAME ON YOU" kwa sababu hamkuweza kuwa na independent verification ya aliyosema Nape na hapo sichelei kusema nyie mna akili butu na isiyokuwa analytical na hamna msaada wowote kwa nchi yenu zaidi ya ushabiki. Kwa bahati mbaya taarifa alizowapa Nape ni za kuendeleza utawala wa CCM kwa kuficha ukweli ambao sisi tulioko huku tunauona ila ninyi mnapigwa changa la macho kwa hadaa ya kuimarisha chama na kudumisha umoja. Ndani ya CCM kwenyewe hapa TZ hakuna umoja inakuwaje mnapigwa tobo bila kushtuka au ni yale yale ya uchu wa madaraka yamewapumbaza. NASHUKURU TULIOKO TZ TUNA AKILI, UPEO NA ANALYTICAL MIND KULIKO NINYI NA TZ ni ya walioko TZ ninyi endeleeni kuwa GUINESS PIG za CCM ila sisi tumekataa na tutaendelea kukataa.!!!
 
mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni
kwahiyo Nape anaakilim kuliko Mzee wa Msoga a.k.a Mkwereee, ama kweli hamna chama , wote humo ccm ni kaputi tu
 
mgogoro ambao ulishindwa kumalizika hata pale ambapo Rais alifanya ziara nchini humo hivi karibuni
kwahiyo Nape anaakili kuliko Mzee wa Msoga a.k.a Mkwereee, ama kweli hamna chama , wote humo ccm ni kaputi tu
 
........Uwezo wa Nape jamani tunaujua, hv majuzi tu kwenye kipindi kinachorushwa na Star tv cha Tz tunayoitaka, alitimuliwa vumbi na Jussa na Marando kweli kweli, sasa huko Marekani kama mnamwona wa ajabu napata mashaka na uwezo wenu wa kufikiri, pengine kulingana na kazi mnazotumikishwa huko, heri mbaki huko huko hamna msaada wowote wa kifikra hata mkirudi nyumbani
 
Habarini Watanzania wenzangu mlipo popote duniani.
Habari juu ya Nape kuhusu kilichotokea Houston Texas kama zilivyoandikwa hapa kwenye jukwaa letu kuu na kwenye blog mbali mbali hasa Michuzi zimepotoshwa kwa kiasi kikubwa sana.

Tunawahakikishia watanzania kuwa tutawaletea yale yaliyojiri houston Texas.

Wakazi wa Houston wana uchungu mkubwa sana na maisha duni ya ndugu zao wanaoishi Tanzania, wakijua wazi uduni huu kwa asilimia kubwa ni ubovu wa uongozi wa CCM kwa zaidi ya miaka 30. Watanzania walionyesha kutokuridhishwa kabisa na vile serikali ya CCM inavyotenda na jinsi inavyotawala. Walieleza wazi bila kumumunya maneno jinsi nchi inavyoliwa na CCM wakibakia bila kutoa maamuzi hasa ya kuwajibisha wazembe na wahujumu. Watanzania walieza matatizo ya umeme, shule, huduma za jamii na vita dhidi ya ufisadi jinsi CCM ilivyoshindwa kuvikabili.

Watanzania tunaandaa ripoti na jinsi mambo yalivyokwenda ndani ya jiji la Houston.
 
Mbona siamini kuwa, kuishi nje ya tanzania unakuwa slow wa kufikiri. Mbona sisi huku tunaona kuwa nepi ni vuvuzela!!!???? Ccm yenyewe inamwita ni kansa, sasa nyie huko mnamwona ni dhahabu. Yaani nyie kweli ni kansa nyingine. Huo ni mfupa ambao hata fisi hawezi kuula.
Correctly put. Hata hao wanaomsikiliza ni Kansa juu ya kansa.
 
Nape ni NURU na TAA ya matumaini yaliopotea CCM kwa siku nyingi.Anawanyima usingizi wapinzani wake na anazidi kuwatimulia vumbi, ushahidi ni Igunga.viva nape viva ccm viva kikwete.

kule igunga NAPE alishiriki kwa namna gani? na pia tathimini ya waangalizi wa uchanguzi huo wame toa ripoti gani?
 
Mbona habari yako ni ya kiujumla kama kawaida ya habari zisizo na kichwa? Unasema alikwenda kutatua matatizo ya wana CCM Houston; Mbona hakuna picha kudhihirisha upatanishi? na Ijumaa Houston alikutana na viongozi wa upinzani wa CCM -- Jumamosi alikutana na jumuia ya Watanzania wapi alipata muda huo wa kuutatua mgogoro? Sasa kama umetatuliwa Viongozi ni kina nani sasa?

Upo USA jaribu kutupa in and out and the outcome --- hakuna cha kuficha...

IMG_3380.jpg


IMG_3382.jpg

Loh...hayo mashati mapya ya kijani nadhani wamepewa na Nape mmependeza!
 
Mashavu yako. Umeona hii ndio taarifa ya kutuletea ma'analysts? Maisha ya anasa ya watu na sifa za kijinga endeleen nazo nyie wenyewe (magamba)!
 
Nape ameenda kufanya shopping chini ya mwamvuli wa kusuluhisha mgogolo wa CCM USA.Hivi hao wanachama wangapi?Inasikitisha ni bora angelienda kimya kimya chini ya kivuli kingine.Hapa nyumbani CCM mambo hovyohovyo ndani ya CCM kila kukicha,kama usuluhisho ungelianzia hapa.CHARITY BEGINS AT HOME.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
........Uwezo wa Nape jamani tunaujua, hv majuzi tu kwenye kipindi kinachorushwa na Star tv cha Tz tunayoitaka, alitimuliwa vumbi na Jussa na Marando kweli kweli, sasa huko Marekani kama mnamwona wa ajabu napata mashaka na uwezo wenu wa kufikiri, pengine kulingana na kazi mnazotumikishwa huko, heri mbaki huko huko hamna msaada wowote wa kifikra hata mkirudi nyumbani
Wewe kweli bonge bonge aka bwenyenye..,watu wa dizaini yako huwaga na uwezo mdogo sana wa kutafsiri mambo..,hivyo sishangai unapokuja kuyaongea mambo uliyosimuliwa (nina uhakika haukuangalia mdahalo huo) bila kuwa na usahihi wake...!
 
Habarini Watanzania wenzangu mlipo popote duniani.
Habari juu ya Nape kuhusu kilichotokea Houston Texas kama zilivyoandikwa hapa kwenye jukwaa letu kuu na kwenye blog mbali mbali hasa Michuzi zimepotoshwa kwa kiasi kikubwa sana.

Tunawahakikishia watanzania kuwa tutawaletea yale yaliyojiri houston Texas.

Wakazi wa Houston wana uchungu mkubwa sana na maisha duni ya ndugu zao wanaoishi Tanzania, wakijua wazi uduni huu kwa asilimia kubwa ni ubovu wa uongozi wa CCM kwa zaidi ya miaka 30. Watanzania walionyesha kutokuridhishwa kabisa na vile serikali ya CCM inavyotenda na jinsi inavyotawala. Walieleza wazi bila kumumunya maneno jinsi nchi inavyoliwa na CCM wakibakia bila kutoa maamuzi hasa ya kuwajibisha wazembe na wahujumu. Watanzania walieza matatizo ya umeme, shule, huduma za jamii na vita dhidi ya ufisadi jinsi CCM ilivyoshindwa kuvikabili.

Watanzania tunaandaa ripoti na jinsi mambo yalivyokwenda ndani ya jiji la Houston.
Nyie watu wa houston hamsomeki..,wengine wanasema NAPE alifanya kikao na watu saba tu wote wanaCCM.,wengine wanadai kuwa walikuwepo watu wengi na ni wapinzani ambao walienda na mabango yao na NAPE akawapokea mabango hayo..,wengine walidai walisafiri kutoka newyork mpaka houston kufuata mkutano wa NAPE., na bado wengine waliandika ripoti ya kusahihisha upotoshaji na katika ripoti hiyo wakadai NAPE hakufanya mkutano na wanahouston..,nawe unasema unaandaa ripoti yako..,lakini naitabiri kuwa ni pumba nyingine katika zilizotangulia.,tayari umeanza kujichanganya katika post yako..,makinika hapo kwenye blue na red....!
 
Kama ni muhimu kuweka Utanzania kwanza, mambo ya kuanzisha Matawi ya Vyama vya siasa nje yanasaidia nini ??? Kuna matawi mangapi ya CDM, CUF, TLP, NCCR MAGEUZI, PPT-Maendeleo n.k.

alama ni jembe na nyundo; chama cha wakulima na wafanyakazi, hapana shaka wakulima na wafanyakazi wa kitanzania wapo pia huko ng'ambo
 
Back
Top Bottom