Ripoti mali za CCM: Mwakyembe, Bulembo, Shaka (UVCCM), Sixtus Mapunda, Makatibu 11 wa Mikoa hawachomoki

hata nyumba za serikali uuzwaji wake unaufisadi na kujinufaisha zaidi kibinafsi,maana walizinunua kwa bei cheee
 
Mwenyekiti wao alishasema hawafukui makaburi au wewe hukumsikia?
 
Ndugu, Wazazi wangu wote ni CCM, NA kuna wengi ni wanachama wa ccm , NA sio wezi wala waporaji. Japokuwa mie sio mshabiki wa chama chochote, ninafuata kile ninachokiona kina faida kwa nchi yangu.

Ndugu usiwatukane wenzio , kumbe wanaweza kuwa wazuri kukushinda wewe NA Uwapendao.
Hao ndugu zako labda hawajapata nafasi za kupiga madili.
Kwa ujumla kila mwanaccm ni FISADI muda tu ndo unawatofautisha. Mmoja alikuwa FISADI jana, mwingine ni FISADI leo na mwingine ni FISADI Kesho.
 
Chadema na ninyi basi hakikini mali zenu basi,sio mnagombana tu na keyboard kwa yasiyo wahusu
 
Wezi wanakamatana wenyewe kwa wenyewe.
Jana Rais Magufuli alielekeza sekretariate na viongozi mbalimbali kuchukua hatua kali sana kwa wabadhirifu wa mali za chama huku wengine wakisubiri vikao vya chama. baadhi ya majina yaliyojitokeza katika ripoti hiyo ni kama ifuatavyooo

1. Bulembo: Anashutumiwa kwa kuuza mali za wazazi ikiwemo shule ya Tegeta sekondary kwa bei ya kutupwa. vile vile anatuhumiwa kutumia zaidi ya shillingi millioni 876 kutoka kwenye akaunti ya wazazi bila spending summary kujulikana,

2. Mwakyembe: Anahusishwa na makampuni yaliyofunguliwa chini ya CCM. kutokana na record zilizoko BRELA, Mwakyembe ameonekana mara nyingi akiwa katika makapumpuni hayo. Makampuni hayo yalikuwa yanaiingizia Chama mammilioni ya fedha ila fedha hizo hazikuweza kurekodiwa popote pale kwa miaka mingi.

3. Sixtus Mapunda: Katika shamba la Igumbiro, Iringa Mapunda alijipatia zaidi ya millioni 260 kwa kuuza mashamba hayo huku akifoji muhtasari ya baraza ya wadhamini ya kwamba wamekubali mashamba hayo yauzwe. kwanza, hakuna baraza lililoketi na kupitisha maazimio hayo, pili zaidi ya fedha hizo hazikuwahi kuingia ndani ya jumuiya.

4. Shaka A Shaka: Huyu kwa sasa ni Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, kwa kipindi kifupi alichokaa, zaidi ya millioni 650 hazijulikani zilipo ikiwemo fedha za mrejesho za mikopo, HSC, na hata tender mbalimbali zilizofanyika chini yake mahesabu yake yamekuwa hayajulikani. pia, katika ununuzi wa magari, mikataba, uchaguzi ulioisha n.k

vile vile zaidi ya makatibu wa mikoa 11, nao wameonekana na kudhibitika kuwa walifanya ubadhirifu. Makatibu wakuu 4 ambao wawili kati yao kwa sasa ni wakuu wa wilaya. wabunge 5 na watumishi wengine ndani ya chama.

Vikao vitakaa muda wowote na Magufuli anaenda kutikisa nchi kwa mara nyingine tena.
 
Hii ni njema sana na heshima ya JPM itarudi na huu ndio wakati mzuri wa kucheza siasa , pia afanyie kazi ushauri anaopewa kuhusu bashite ,huyu ndiye aliyeanza kuharibu image yake

Akianza na bashite , pia kuna timu membe ,na kukisafisha chama kama ripoti inavyosema , nawakikishieni , CCM na nchi ya Tanzania , watanzania watafurahia sana

Maana sasa Mambo yameenda kwenye reli
Rubbish and pathetic! Eti nchi inaenda wapi? Hili anguko la uchumi itawachukua miaka 100 kurudi mlikokuwa mwaka 2015!
 
Ni Kwasababu hata Hao CCM nao walizipata kwa njia isiyo halali. Cha mlevi huliwa na mgema..... Mijizi ya CCM
 
Jana Rais Magufuli alielekeza sekretariate na viongozi mbalimbali kuchukua hatua kali sana kwa wabadhirifu wa mali za chama huku wengine wakisubiri vikao vya chama. baadhi ya majina yaliyojitokeza katika ripoti hiyo ni kama ifuatavyooo

1. Bulembo: Anashutumiwa kwa kuuza mali za wazazi ikiwemo shule ya Tegeta sekondary kwa bei ya kutupwa. vile vile anatuhumiwa kutumia zaidi ya shillingi millioni 876 kutoka kwenye akaunti ya wazazi bila spending summary kujulikana,

2. Mwakyembe: Anahusishwa na makampuni yaliyofunguliwa chini ya CCM. kutokana na record zilizoko BRELA, Mwakyembe ameonekana mara nyingi akiwa katika makapumpuni hayo. Makampuni hayo yalikuwa yanaiingizia Chama mammilioni ya fedha ila fedha hizo hazikuweza kurekodiwa popote pale kwa miaka mingi.

3. Sixtus Mapunda: Katika shamba la Igumbiro, Iringa Mapunda alijipatia zaidi ya millioni 260 kwa kuuza mashamba hayo huku akifoji muhtasari ya baraza ya wadhamini ya kwamba wamekubali mashamba hayo yauzwe. kwanza, hakuna baraza lililoketi na kupitisha maazimio hayo, pili zaidi ya fedha hizo hazikuwahi kuingia ndani ya jumuiya.

4. Shaka A Shaka: Huyu kwa sasa ni Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, kwa kipindi kifupi alichokaa, zaidi ya millioni 650 hazijulikani zilipo ikiwemo fedha za mrejesho za mikopo, HSC, na hata tender mbalimbali zilizofanyika chini yake mahesabu yake yamekuwa hayajulikani. pia, katika ununuzi wa magari, mikataba, uchaguzi ulioisha n.k

vile vile zaidi ya makatibu wa mikoa 11, nao wameonekana na kudhibitika kuwa walifanya ubadhirifu. Makatibu wakuu 4 ambao wawili kati yao kwa sasa ni wakuu wa wilaya. wabunge 5 na watumishi wengine ndani ya chama.

Vikao vitakaa muda wowote na Magufuli anaenda kutikisa nchi kwa mara nyingine tena.
Hongera JPM kwa mara nyingine tena.Nilijua kwamba baadhi ya watu na hasa makatibu wa Mikoa na Wilaya wana kesi za kujibu.Ngoja tusubiri movie.Go,go Magu,go.Watatuelewe tu,CCM sio shamba la bibi.
 
Ni Kwasababu hata Hao CCM nao walizipata kwa njia isiyo halali. Cha mlevi huliwa na mgema..... Mijizi ya CCM

Hivi kwenye huu uhakiki hakuna Mali ambazo chama chetu kimejikuta kinazimiliki wakati sio halali yake??

Hii report ingekuwa na maana sana kwetu wapenda haki kama kuna Mali zinaitwa za CCM ila sio zao.

Au hata wajifanye zimewashinda kuziendesha wanazirudisha serikalini ili ziendelezwe.

Bado huwa naamin viwanja vya michezo wanavimiliki isivyo halali, pia sioni mantiki ya wao kuvimiliki given vinatumika kwa wote.
Busara itumike virudi serikalini.

Kama ambavyo serikali inatafuta haki zake kwenye airtel na makampuni mengine, vivyo hivyo hivi viwanja virudi kwa mwenyewe serikali.

Viwanja vya wananchi.
 
kila mwanaccm "either directly or indirectly is a thief"
Sio kweli.Mimi ni mwana CCM, lakini sio mwizi na kwa muda mrefu nimekerwa sana na tabia za wana CCM walio wengi za kukumbatia mafisadi kwa nia ya kupata maslahi binafsi.Jambo hili limekiathiri sana chama.

Nikiri kwamba upo pia wizi wa mali za chama moja kwa moja kama ambavyo ripoti ya Bashiru imeonyesha.Hili si jipya,tulilipigia kelele sana lakini hakuna aliyejali.Tunamuomba Mwenyekiti atumie mamlaka aliyonayo kukisafisha chama.Chama ni kichafu na kinanuka.Tumechoka kuwa na chama mfu.Kwa muda mrefu sisi wengine tumeonekana kama hatufai kwa sababu ya kukemea uovu chamani.Mungu si Athumani,we now can see some light in the tunnel.Asante Mwenyekiti.Hata hivyo kazi bado ni kubwa.Katika hili ningeomba chaguzi ndani ya chama nazo zitupiwe macho,hizi ndizo zinazoingiza watu wasiofaa,wanaolinda na wanaotetea maovu chamani.
 
Hapo kwa Mwakyembe K uanzisha makampuni niliwahi kusikia kuwa ndio mwanzilishi wa PMCL kampuni inayomiliki Uhuru FM, hii Uhuru FM kuna ufisadi pale wa kufa MTU ,na moja ya chanzo changu nasikia walikua wafungue TV ,toka 2010 na vifaa hivi wamepewa TV Fulani maarufu kwa vijana kupitia muenezi yule alitimuliwa ktk uwaziri ...

Km kweli Magu yuko makini ktk hili ataenda na wengi hapo Ccm ,hasa ktk makapuni yao ..
 
Back
Top Bottom