Ripoti Maboresho kwenye Wizara ya Elimu 2015-2020

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Ripoti ya Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Tano katika Sekta mbalimbali inaonesha kuwa kumekuwa na ongezeko la asilimia 32 ya idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya msingi mwaka 2020 ukilinganisha na hali ilivyokuwa miaka mitano iliyopita, huku idadi ya shule za msingi ikiongezeka kutoka shule 16,899 mwaka 2015 hadi mwaka 18,152, ikiwa ni sawa na ongezeko la shule za msingi kwa asilimia 7.

Ripoti hiyo imebainisha pia kuwa idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari (kidato cha I hadi IV) imeongezeka kwa asilimia 41 tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015, huku idadi ya shule za sekondari ikiongezeka kutoka shule 4,708 mwaka 2015 hadi shule 5,143 mwaka 2020, sawa na ongezeko la shule za sekondari kwa asilimia 9.

Zaidi, idadi ya wanafunzi wanaojiunga na mafunzo ya ufundi stadi (VET) imeongezeka kwa asilimia 63 kutoka hali ilivyokuwa mwaka 2015 huku idadi ya wanfunzi wanaodahiliwa katika vyuo vya Ufundi ikiongezeka kufikia asilimia 57 tofauti na hali ilivyokuwa mwaka 2015.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, zaidi ya jumla ya shilingi trilioni 1 zilitolewa kwa ajili ya elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari, wakati zaidi ya shilingi trilioni 2.2 zikitolewa kwa ajili ya mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu. Idadi ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya Elimu ya Juu imetajwa kuongezeka kutoka wanufaika 125,126 mwaka 2015 hadi kufikia wanufaika 132,119 mwaka 2020 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 6 ya wanufaika wa mikopo ya Elimu ya Juu.
 
Safi sana kwa rais John Pombe Magufuli
Tutegemee maendeleo makubwa zaidi kwenye elimu miaka mi5 ijayo

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom