RIPOTI MAALUM: Mtandao wa ufisadi, siri hadharani

RIPOTI MAALUM: Mtandao wa ufisadi, siri hadharani

Huyo kanjibhai ni hatari,anahusika pia katika ishu ya radar na kuiuzia serikali magari na helikopta mbovu za jeshi
 
Tuna shukuru kwa ripoti hii.. Kama kawaida yetu tutalalamika na mwisho tutasahau,na mafisadi yanaendelea kutuibia tu..

Najuta kuwa Mtanzania
 
Ovyooooooo

Ndugu uliyoyasema yana ukweli kabisa , baada ya malalamiko ya ndugu Nape , CCM iliamua kufanya uchunguzi chini ya kamati ya maadili iliyokuwa inaongozwa na Andrew Chenge ! Just imagine ,CHENGE mkuu wa kamati ya maadili ! Hatimaye Nape akapewa Ukuu wa wilaya kwao kusini na baadaye kidogo akawa katibu mwenezi .
 
nadhani kama ni kujitaftia laana ya vizazi vyetu vijavyo ni kuikumbatia ccm
inachukiza sana kwa mambo haya yanayofanyika
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Aisee hio subash iko miliki M.M.STEEL mikocheni hiyo ni mizi bana hiyo ni chori.....
 
watz wengi hatuna shida na mtu kutajirika, ila atajirike kwa uhalali, baada ya uchaguzi mkuu kuisha nlipata kutembelea ndani ya kiwanda cha kiboko ambacho kuna kiwanda cha sayona na kiboko pipes niliona gari aina ya canter ikibanduliwa picha za kampeni za urais ndani ya compound hyo , nikaunganisha matukio nikaona hapa kuna kitu, kwnini mfanyabiashara mkubwa atumie mali yake kufanya kampeni tena kwa siri wakati ana haki ya kufanya kwa uwazi.

Na hili swala si la mdhaa jamani hawa watu wanakwiba wanakimbia maana wanakuwa na uraia wa nchi 2 mfano wa somaiya wa radar.
 
Mmmmmmmmmhhhhhh napita tu ngoja nimalizie ka novel kangu ka "the lost symbol" nipate akili ya kuja kujadili huu uzi
 
Ni wakati wetu sasa kuonyesha kwa vitendo kama walivyofanya MAFAROA WALALA HOI WOTE WALIJUMUIKA TAHRIR SQUARE KUPINGA RAIS WAO
 
Kwa tunaopenda mabadiliko na maendeleo yenye kuleta tija kwa Watanzania wote, tuna jukumu la kumuelimisha kila ambaye yupo karibu nasi juu ya maovu haya yanayofumbiwa macho na CCM.

Chama hiki kimeingia ubia na mafisadi ili kutuangamiza, hivyo ni haki yetu sote kukikataa na kutowachagua tena kuongoza taifa hili. Twende mijini, vijijini na kila kitongoji kumwambia kila Mtanzania atakayesikia kuhusu mambo mabaya tunayofanyiwa. Hii kazi tusiachie tu vyama vya upinzani viifanye, nasi tushiriki kwa pamoja kutokomeza jinamizi hili.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Huu usemi wa kama una ushaidi ulete au tupatie ili tuwezekufanyiakazi suala husika, imekuwa fimbo yakuwachapia wale waleta hoja muhimu. Juzi tulisikia mwanasheria mkuu na waziri mkuu wakitaka mleta hoja awapelekee ushahidi wa waficha fedha nje. Hii inaonyesha viongozi wetu wote wanatetea uozo uliko ndani ya taasisi zetu nyeti. Pia inaonyesha kuwa kuna vibaraka wao tunaokwenda nao sambamba, wakiwatetea wahujumu uchumi wa nchi yetu. Watanzania walala hoi inabidi kujipanga, kwani MSAFARA WA MAMBA NA KENGE WAMO.

Ni muhimu sana kuonyesha ushahidi (wa mazingira au halisi). kutuhumu mtu bila ushahidi ni UMBEA
 
Bila kuchapana bakora hatuambulii kitu, hawa jamaa wamejilimbikizia mali, na serikali iliyoko madarakani inawalinda kwa kuweka taasisi zenye mkanganyiko wa utendaji kama takukuru na kutuhadaa kwa kusema serikali inalifanyia kazi!
 
Haya mambo yanazunguka zunguka tu katika maeneo haya. Kwa sasa naomba kuweka comment yangu hii ya last week!

Wakuu

Takriban zaidi ya miaka mitano sasa tangu ulipofanyika mkutano wa hadhara wa kihistoria ambayo umebakia katika kumbukumbu ya vitabu na rejea zingine, kama mojawapo ya hallmarks za vita dhidi ya ufisadi. Ni mkutano uliofanyika Viwanja vya Mwembeyanga, Dar es a Salaam, ambapo mbele ya vyombo vya dola vyooooooote nchini, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willbrod Slaa pamoja na Kamanda Tundu Lissu, mbele ya viongozi wakuu waandamizi wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe, walitaja majina 11 ya watuhumiwa wa ufisadi mkubwa ndani ya nchi hii, akiwemo Rais na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa na Rais na Mwenyekiti wa sasa wa CCM, Jakaya Kikwete.

Mbali ya kutaja majina hayo, CHADEMA ilitoa hadharani ushahidi wa wazi na kina wa ufisadi huo mkubwa ambao watu hao 11 walikuwa wanatuhumiwa kuhusika kushiriki. Wakaenda mbali na kuutangazia umma wa Watanzania na dunia nzima kuwa, bado wanao ushahidi mwingine na wataendelea kuutoa kadri ya muda, unaowafungamanisha watu hao na tuhuma za ufisadi mkubwa wa uporaji wa rasilimali za Taifa katika kashfa mbalimbali kubwa kubwa.

Kwa kujikumbushia na kwa faida ya mjadala, majina yaliyotajwa katika ushahidi huo wa tuhuma za ufisadi mkubwa ni pamoja na

TUJIKUMBUSHE ORODHA YA 2007
1. Dr. Daudi T.S. Balali
2. Andrew J. Chenge
3. Basil Pesambili Mramba
4. Gray S. Mgonja
5. Patrick P.R Rutabanzibwa
6. Nazir Karamagi
7. Nimrod Mkono
8. Rostam Aziz
9. Edward Lowassa
10. Benjamin W. Mkapa
11. Jakaya Mrisho Kikwete

Hakuna hata mmoja kati ya hao aliwahi kukanusha ushahidi uliotolewa, mbali ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kukanusha kutohusika na ufisadi, kisha baadhi yao, mmoja mmoja kwa nyakati tofauti, wakatishia kwenda mahakamani kushtaki, kitu ambacho hakuna hata mmoja aliwahi kufanya tangu 2007 hadi leo.

Kwa nini mjadala huu ni muhimu sana

List of Shame, yaani hiyo orodha ya aibu ya watuhumiwa wa ufisadi, wakati mwingi huitwa orodha ya mafisadi, ilifungua pazia muhimu sana ambalo hadi leo limekataa katakana kujifunga au kufungwa. Mkutano huo ulifungua pazia la vita dhidi ya ufisadi kwenye Mahakama Kuu ya Umma. Ilikuwa ni baada ya akina Samuel SItta na wenzake kubana kwa hila na makeke, wakitoa maneno ya kejeli dhidi ya Dkt. Slaa, wakizuia asiwasilishe ushahidi wa ufisadi huo Bungeni na kutaja majina, ili Bunge lifanye kazi yake ya kusimamia, kushauri na kuiagiza serikali kwa niaba ya wananchi.

Ufisadi mkubwa mkubwa kama wa Tangold, Meremeta, Richmond, Dowans, Kiwira, Minara ya BOT, EPA, Rada, ndege ya rais na kila aina, ukatajwa kwa ushahidi na kuzungumzwa hadharani. Ni baada ya hapo, nchi nzima ikaitikia wimbo wa vita hiyo na kurudia rudia kibwagizo chake cha ufisadi. Bila uoga. Hadi leo mambo hayajawahi kuwa sawa tena.

Bahati mbaya sana pamoja na ukweli na uhalisia huo kuwekwa bayana, hadi leo hakuna uwajibikaji wowote ambao umefanyika. Na inawezekana ni kwa sababu, Watanzania hawajawahi kudai kwa nguvu kubwa uwajibikaji na haki kutendeka katika hili. Kwa uhakika, kama hakutakuwa na uwajibikaji na haki kuonekana ikitendeka katika jamii, ni vigumu sana watu kuweza kuhubiri amani na utulivu wakaeleweka, unless they are big jokers.

Kutokana na kukosekana kwa uwajibikaji na haki kutendeka, no wonder kuwa tumeamua kuwa Taifa la kuzalisha kashfa ya ufisadi moja baada ya nyingine. Ndiyo maana Ndugu Zitto amekuja na jina lake la Fisadistan. The Land of corrupt.

No wonder bado tunaogelea katika lindi la ufisadi, ambapo sasa tumeongeza orodha ya mafisadi, kwa kashfa ya mabilioni ya rushwa katika mafuta na gesi, yaliyofichwa huko Uswisi. Hakuna uwajibikaji. Naandika haya Nikijua kuwa Dkt. Slaa amewahi kutoa updates za orodha ile ya mafisadi kwa kuongeza majina na ushahidi mwingine hasa juu ya kashfa ya uuzwaji wa nyuma za umma na Kampuni ya Kagoda. Hakuna uwajibikaji wala uwajibishwaji.

No wonder juzi, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipomuuliza Waziri Mkuu Pinda bungeni nini hatma ya mabilioni yaliyofichwa na nchi ya nchi katika visiwa mbalimbali Kama vile Mauritius, New Jersey, Luxemburg, Uswisi, Grenanda na maeneo mengine mengi ambayo yana favour mafisadi kufanya hivyo, hakuwa na jibu sahihi kuwaambia Watanzania. Yaani serikali haijui nini cha kufanya, if you read between lines...


 
Sijui hata niandike nini...dah!!Inaniuma kweli....hivi watanzania ni nani amewaroga?yupo hai kweli?
 
subash ndiye aliyemjengea jk majumba migombani-moroco na msoga!ndiye mwenye kujenga msata-bmoyo,mwenge-tegeta etc
 
Kila mara ninaposikia mambo haya huwa ninatafakari kwanini tuendelee kuilipia kodi zetu TAKUKURU. Hawa jamaa ni hopeless kweli. Kama mtu mmjoa au kikundi kidogo cha watu wanaweza kujua undani wa hujuma hii, iweje taasisi kubwa kama TAKUKURU na TISS wakae kimya kiasi hiki.

Mbaya zaidi ni pale mkuu wa nchi amapokuwa na kauli za kisanii as if anaongea na watoto wadogo. Watanzania tunatakiwa kufanya maamuzi magumu dhidi ya JK na kundi la mashogazake such as EL, Nepi N, Ben
 
el na kambi yake hawatufai, hata kidogo! Hawa ni wezi tu! Nashangaa sana watu wanaowashadadia!

huwa sielewi wanamshabikia sanaa mpaka wanashangaza. Sijui huwa wanatumia nini kufikiri wenzetu hawa? Ni makal.....ooo au sijui nini hasa hebu wanajanvi tusaidieni kuwatafakari wenzetu wenye ushabiki na el.
 
Back
Top Bottom