Wale waliokuwa wanaishi kwenye vibanda kule Benghazi ukiwaambia wameharibu nchi nzima kwao ina tofauti gani? Huo uharibifu unawapata waliokuwa wakiishi vizuri. Umepanic tu bure, upumbavu wa mkulima humuathiri mkulima lakini upumbavu wa mfalme ni janga la taifa zima.
Hoja yangu haiondoki kwa kuwa Libya imeharibika, bado ni ujinga wa Gadaffi ndio umeharibu Libya. Kupata nafasi ya kuongoza haimaanishi akili zako zinaongezeka, wewe utabakia kuwa mwanadamu tu na siku moja utakufa.
Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakaa madarakani akiasisi taasisi imara badala ya yeye kujiimarisha. Ujinga wa umungu mtu ni kwamba, when you are gone, you go with your dreams. Kama unafikiri Waafrika tunapenda kutupa lawama kwa viongozi wetu basi hujui maana ya DHAMANA na UWAJIBIKAJI. Ulitaka tukamlaumu nani? Tulaumu 'mabeberu'?