UHURU JR
JF-Expert Member
- Jul 24, 2014
- 18,252
- 9,662
Ni matatizo gani unayoyakusudia na ni nchi gani hizo ambazo hazina matatizo kwa sababu ya kubadili uongozi?Sijui unamaanisha nani ni mjinga lakini amini nakuambia, nchi zile ambazo zimeweka utaratibu wa kubadilishana madaraka hazina matatizo, matatizo yapo kwenye nchi ambazo viongozi hawataki kuondoka mpaka waondolewe.
Unayo hakika gani kuwa wale waliokuwa wanakaa vibandani ndio hao hao wako uhamishoni kama wakimbizi? Kama waliamini kumuondoa madarakani Gadaffi ndio ulikuwa ukombozi kwao, walikwambia kuwa hawakujua kuwa kutakuwa na gharama ya kulipa?
Halafu wewe unashangaza sana. Tuna rasilimali na nguvu kazi ya kutosha, unadhani tunakwama wapi kama sio kwenye uongozi?
Mfano wako wa CCM na CDM sijui vimefanyaje mimi sijauelewa
Na kwanini waafrika matatizo yetu yawe viongozi tu miaka nenda rudi kwani hao viongozi tunawapata wapi?
Ni maisha gani walikuwa nayo walibya yenye kuhitaji ukombozi wenye gharama za kuvumilia hichi wanachopitia? Ni humo kukaa kwenye vibanda ndio kuliko hitaji ukombozi wenye gharama ya vita?