Rip..

sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,277
Nikiwa kama mdau mkubwa wa JF Tech, Gadgets & Science Forum naomba kutoa pole nyingi kwa ndugu na jamaa wa waliopoteza maisha katika ajali ya meli huko Zanzibar. Najua hapa si mahali sahii saaaana kutoa post hii (na ndo maana nikatanguliza nikiwa kama mdau mkubwa wa jamvi hili sababu wengine kama mimi nikifungua tu JF hapa ndo pa kwanza na naweza hata nisifungue jamvi lingine mpaka natoka), ila lamsingi nnalotaka kusema ni hili, hivi nchi yetu hii ni kweli imeshindwa kabisa kuwa na hata mifumo midogo tu ya mawasiliano baina ya vyombo vikubwa vya usafiri (kama vile simu za upepo) au mawasiliano kati ya chombo na office yake? Technologia yetu tunayojivunia inakua iko wapi kama haitusaidii!!? Leo nimsesoma habari moja gazetini juu ya ajali hiyo, Nahodha alienusurika anahojiwa na vyombo vya habari akasema (nanukuu na link ya habri hiyo gonga maneno yake) : "Tulijaribu kufanya kila jitihada ili kuokoa hali hiyo, lakini tulishindwa na tukaamua tuiache meli na kuanza kutoka, hapo tena kila mmoja alikwenda kwa upande wake,​Kwa kweli siwezi kusema kama ni uzembe au la umefanyika, lakini wakati inatokea hali hii tulipishana na meli ya MV Jitihada na kuwapa ishara ya kuzama, lakini hawakutusaidia.." sasa huyo ni baharia wa meli anasema hivyo...dah..mi sijui bwana..!! anaway, poleni sana ndugu zetu..na si ajabu ukakuta kuna wana JF wenzetu au ndugu zao wamepoteza maisha humo ndani...tupeane taarifa wakuu!!

Amen!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom