RIP Symbian. Now it is officially dead !

Chief-Mkwawa

Platinum Member
Joined
May 25, 2011
Posts
32,279
Reaction score
44,416
wakati leo nokia wakitangaza mapato yao na kuonyesha comeback ya nguvu pia wametangaza habari za kuhuzunisha sana kwamba nokia 808 ndio simu ya mwisho ya symbian na kuanzia leo symbian is dead



so kama una simu ya symbian itunze stock ikiisha ustegemee kupata nyengine
 
Mmmh tuone nayo windows phone itawafikisha wapi...maana competition imewatupa vibaya.
 
Hawa jamaa sijui kwa nini huwakuja android?!


Sent from my LT26i using Tapatalk 2
 
Hawa jamaa sijui kwa nini huwakuja android?!


Sent from my LT26i using Tapatalk 2

mkuu nokia amefanya maamuzi ya busara sana kwenda windows phone ila kwa akili ya haraka unaweza ukaona kama ni mistake.

Android kuna king mmoja tu samsung basi peke yake ndio anafaidi.

-htc kila siku faida zinashuka anatoa simu kali hamna anaenunua
-lg ana biashara nyingi ila part inayomuingizia hasara kubwa ni simu
-sony ameamua kuacha kutoa simu ndogo now anatoa flagship tu profit margin ndogo


nokia ameenda wp na sasa yeye ndo amekua king. Tofauti ya wp na android ni kwamba kwenye windows phone kila kitu anafanya microsoft wewe oem una deal na hardware tu. Wakati android inabidi uimprove na software.

Kutokana na nokia kutodeal na software amefanya improvement kubwa sanaaaaaa. Vitu hivi nokia kavofanya 2012
-camera ya 41mp
-lens inayostahamili mitikisiko
-wireless charging
-best night shot
-screen inayogusika hadi na gloves
-mashine ya 3d cover
-na vingine vingi


angalia na mapato 2012
-january hadi march- nokia hasara dola 1.7 billion
-april hadi june- hasara dola 1 billion
-july hadi september- hasara milion 700 dola
-october hadi december- faida milion 500

so mkuu tumpe nokia muda mengi yanakuja. Na ujio wa windows blue nokia atazidi kupaa
 
tatizo platform kama windows and ios ziko locked sana hupati freedom kama tunayoipata kwenye symbian or android.
Of course strategy za elop sijazipenda za kutaka kutuforce kwenye windows ilibid atupe freedom ya kuchoose platform kwa kuendelea kusupport meego and symbian.
 

ila thanks kwa rooting na custom rom ndio maana android ina freedom so ni just mda flani tu kabla watu hawajaanza kuichakachua na hio wp8 uone vitu vitakavyoanza kutiririka

maana hamna os ambayo ilikua imebanwa kama hii os ya tablet windows rt ila ishachakachuliwa na now inaingia soft za arm za desktop
 

Hata iphone ukivaa gloves waweza tumia touch.....
And about 3D technology, its not their invention, they just said that people will be able to print their own covers, what nokia did was creating files for the printer (software files).
 


Chief mkwawa unaonekana ni mpenzi sana wa nokia !! Si vibaya sana kupenda kitu lakini ni busara zaidi kama utatambua udhaifu wa unachopenda . Nokia walitabiriwa siku nyingi sana kuwa. Uamuzi wao wa kung'ang'ania closed system. Symbian na hiyo window unayosema , ungewapeleka kwenye Hasara . Kimsingi google walipokuja na open system ya android , watengenezaji wengi wa simu hasa wadogo wadogo ambao walikuwa wakipata tabu sana kushindana na giant nokia , wakaona ni golden chance ya wao kutengeneza faida , ikumbukwe kuwa. Android watengenezaji wanadili na hardware tu. Nokia kwa kujiamini kuwa alikuwa na wataalamu waliobobea kwenye hardware na software ,akadhani kuwa angeweza kushindana na kuishinda Googles Android . Ndo kosa lao Samsung unaosema ndo kinara wao ni kweli lakini nadhani wajua kuwa samsung anatengeneza simu za fleva nyingi i.e bada window symbian , pamoja na android .kwa hiyo unaposema ndo "kinara "zingatia hauzi simu za jukwaa moja ! . Unatabiri nokia atazidi kupaa sidhani kama ni sahihi .wanunuzi wa gadget siku hizi wanazingatia sana gharama na uimara na last customization, mambo ya identity siku hizi sio sana. Kikwazo kikubwa kwenye product za nokia ni gharama, hilo halina ubishi ,nokia Asha touch series very limited application ni wastani wa laki tatu bongo , huawei ascent , by far the best ni wastani wa laki mbili !! . Dunia ya leo watu hawataki monopoly tena ndo maana hata hizo window product zinaface ushindani mkubwa sana hasa kutoka kwa linux systems ,ambazo nyingi ni free open systems ,
Chief Sahihisha nilipokosea!!!!
Usiku mwema!!!
 
Hata iphone ukivaa gloves waweza tumia touch.....
And about 3D technology, its not their invention, they just said that people will be able to print their own covers, what nokia did was creating files for the printer (software files).

ok iphone hazipo nyingi kuna
-iphone ya 1
-iphone3
-iphone3gs
-iphone4
iphone4s
-iphone 5

ipi inatumia gloves? Lete na ushahidi maana ndo naskia kwanza kwako wewe

kuhusu 3d printing mkuu nokia wamerelease 3d printer yao walioimodify na inauzwa dola 2000 zaidi ya milion 3 za kibongo.

Ishu hapa si nani amegundua 3d printing bali ni nani ameileta kwanza kwenye simu maana hata wireless charge sio nokia aliogundua ile ye ndo wa kwanza kutengeneza accessories za kucharge wirelessly kama qi-pad, fatboy pillow na jbl power up
 

1. Nakubali mimi ni nokia fan hilo nakubali

2. Si kweli kua microsoft wanapata tabu kwa competition nyengine sababu hadi leo changanya os zote mac, linux, ubuntu, red linux market share yao haijafika 10% so still microsoft ni leader.

3.mkuu kuhusu samsung kutumia os nyingi ni sawa lakini je zinalipa? Bada os ya samsung wave haina market share hata 1% na wp nayo hana kitu zaidi ya 90% zinatoka android kwenye smartphone.

4.ishu ya uimara sasa mkuu unataka umfananishe na nani? Maana vitu vinavyofanana na uimara wa simu za nokia ni mawe, vyuma, bunduki sababu angalia lumia 920 ni flagship lakini imebondwa na nyundo, ikakanyagwa na gari, imechomwa visu na kila kitu ila still ipo nzima

5.mkuu mafanikio ya asha hayaji kwa kwa kitu kimoja tu zile ni simu basic ambazo hazikuangushi, wengi wanazifanya simu za biashara. Let say nina galaxy s3 yanini tena nimiliki galax pocket? Simu yangu ya 2 itakua asha maana inakaa na charge na inafanya mambo basic kama kuingia net, kutuma mail na kufungua documents

6.mkuu simu za nokia smartphone zinakuja mwezi wa 2 hapo barcelona kwenye mobile world congress (mwc) nokia wanatarajiwa kutoa simu 6 na mbili kati ya hizo ni lumia 920 successor nyembamba zaidi yenye aluminium na nyengine ni first pureview 41 mp camera kwenye windows phone 8.

Pia nokia sasa hivi anasambaza simu ya laki 4 bora zaidi duniani nokia lumia 620 yenye processor ya s4 snapdragon (better than galaxy s2) na ram ya 512 yenye uwezo wa memory hadi 72gb.

Vyote hivyo vinaonyesha comeback ya nokia so mkuu its not about monopoly its about quality utakayoipeleka kwenye soko. Nafkiri 2013 utakua mwaka mzuri sana kwa nokia
 

tofauti ya android sio kuwa na custom rom tu bali developer anaruhusiwa kutengeneza app yoyote na kuipost kwenye store lakini ios na wp zinawalimit madeveloper sana ndio maana ios haina browser kama firefox, opera mobile sababu developer huruhusiwi kutumia engine yake wanataka urely kwenye webkit, huo ni nimfano mojawapo nakumbuka hata google voice ilizuiwa mwanzoni.
 

hahaha mkuu usinkumbushe malware. Huo ujinga wa kupost apps bila kukaguliwa ndio umeifanya android iwe os ya kitoto.

Waziri mkuu wa uingereza disrael anasema kuna uwongo wa aina tatu
lies, damn lies na statistics. Twende kwenye statistics.

-Google wameeka security kwenye playstore kudetect malware ila university ya columbia wakaplant malware kwenye store asilimia 15 tu vikakamatwa.

-kwa siku zinaingia app 560 playstore zenye malware

-kati ya hizo zipo 28,398 ambazo fsecure imezidetect kama hatari zaidi enye uwezo hadi wa kuiba bank data (google hawajui)

so mkuu usisifie kusubmit app bila kukaguliwa wengine wana roho mbaya mkuu

then kuhusu hao kina mozzila mkuu wp8 ina apps unique kupambana na ios na android usikazane kua na apps kama zao eka zako unique mfano apps kama metrotube imeiweka kwenye shame official android apps ya youtube na ya ios youtube.

Same kwenye browser kuna kitu kinaitwa surfcube yenye 3d interface wengi wa iphone na android wanaitaman

 
Ni kweli gharama zinamshusha sana NOKIA.
 

uko sawa kinachoisaidia android isimame ni uhuru uliopo ukilinganisha na platform kama iOS.

i hate android imekopi vingi kutoka iOS halafu ina bugs nyingi & slow...
 

:-o ndugu, kama gloves as gloves iphone zote zinaweza kuwa touched kwa kutumia gloves, iphone uweke karatasi juu basi still unaweza touch. Au kuna special gloves unaongelea? Lakini kama ni glove tu ya kawaida basi bila ya wasi unabofya, and besides sijaona touch screen kama
Ya iphone hana mpinzani hapo!

Well sometime you really have to use your common sense, buying 2000USD plus materials to make the cover, for just personal use???!!! Whats the advantage? How much does an original case cost? Why go thru the hussle?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…