Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,825
- 730,232
Kwanza nitoe pole nyingi sana kwa ndugu jamaa na marafiki wa mzee Ngosha. Mzee amemaliza safari yake kwa amani kwa kutimiza ndoto na dhamira yake ya muda mrefu ya kumkabidhi mkuu wa nchi picha tatu za marais wastaafu alizochora kwa mkono wake.
Taarifa za kuwepo hai mtu aliyechora nembo ya taifa na hali aliyonayo ziliibuliwa kwa mara ya kwanza na kituo cha habari cha ITV. Haraka haraka serikali ilitoka ilikotoka na kuchukua jukumu la kumhudumia mzee huyu fukara aliyekuwa hana mke watoto wala ndugu, akiishi kwenye chumba kimoja Buguruni malapa kwa hisani ya mwenye nyumba na majirani.
Ni wakati huohuo habari hizi zikienea kwa kasi ilijitokeza familia iliyojitokeza kupinga habari za marehemu mzee Ngosha, na kudai kwamba baba yao ambaye pia ni marehemu kwa sasa ndio mchoraji halisi wa nembo ya Taifa.
Kituo kimoja cha habari kilifika nyumbani kwa familia hii na kufanya nayo kipindi akiwemo mke wa marehemu, watoto na hata wajukuu. Habari zao zilitoa mwanga fulani kuhusiana na nembo ya taifa.
RAI YANGU
Kwa ajili ya kuweka historia sawa, kutenda haki na kuepuka upotoshaji serikali ichukue jukumu la kiutafiti na kutoa taarifa kamili na sahihi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.