Tusker Bariiiidi
JF-Expert Member
- Jul 3, 2007
- 5,554
- 2,160
Nimepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Bw. Muganyizi Mutta ambaye mpaka umauti unamkuta alikuwa anafanya kazi Aggrey & Clifford kampuni inayojihusisha na kuandaa matangazo na Matamasha hapa nchini.
Ilikuwa Jumamosi tarehe 16/09/2017 umauti ulimkuta ghafla baada ya kupatwa na shinikizo la damu. Kabla ya hapo Marehemu Muta amefanya kazi kwenye kampuni mbalimbali kama vile Roots na Airtel kwenye nafasi hiyo hiyo ya kuwa meneja wa Matangazo na Matamasha.
Marehemu Muta atakumbukwa na wengi kwa kuwa mbunifu wa Matangazo mbalimbali yaliyowahi kukamata vyanzo vingi vya vyombo vya habari Tanzania. Marehemu Muta ataagwa kesho katika kanisa la Katoliki Hananasif Kinondoni kuanzia saa sita mchana na atazikwa kwenye makaburi ya Kinondoni kesho alasiri.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa.