Simulizi: Kikokotoo

Mogambi

JF-Expert Member
May 25, 2012
209
351
KIKOKOTOO
David Ngocho Samson

UTANGULIZI

Hakuna aliyejua sababu ya madhila yaliyomkumba mstaafu, tena ambaye enzi za ujana na maisha yake ya Kazi, alikuwa mtu aliyekuwa na nafasi nzuri, na maisha yaliyotosha sifa za kuitwa maisha bora. Lakini fununu mitaani zilienea kuwa, mstaafu huyo, afisa wa serikali, ilisemekana kwamba aliingia mkataba na kampuni moja ya ukopeshaji fedha miaka michache kabla ya kustaafu kwake.

***

SEHEMU YA KWANZA

Alipozinduka, mzee Muganyizi alijikuta hospitalini, maji ya drip yakitiririka taratibu na kuingia mwilini mwake kupitia sindano iliyochomwa mkononi mwake. Alijitutumua na kujaribu kunyanyua kichwa chake lakini alihisi uzito usiomithilika sambamba na maumivu makali kiasi cha kuhisi kichwa kinauacha mwili. Nesi aliyekuwa anamhudumia alipomuona mgonjwa wake akihangaika, alimshauri alale na asifanye jambo lolote ambalo lingemzidishia maumivu.

Hakuwa mkaidi, alimsikiliza nesi na kutuliza kichwa chake kwenye godoro huku maumivu yale makali yakimpa wazimu. Maana hakujua kama alipatwa na kizunguzungu au yalikuwa maruweruwe. Kwake, yote yalikuwa sawa tu. Alijituliza taratibu, huku kuwa kwake macho wazi, kukimpa nafasi ya kufunguka fahamu zake.

Taratibu fahamu zake ziilianza kumrejea moja baada ya nyingine. Na kwa kweli, hazikumpa nafuu yoyote aliyotarajia. Maisha yake siku za karibuni yalikuwa hayasomeki kabisa. Alishindwa kujua ni wapi alipokosea kiasi cha kuyapa mwelekeo hovyo kabisa maisha yake, tena wakati ambao alidhani angepata fursa ya kufurahia maisha baada ya kulitumikia taifa kwa uaminifu kabisa.

Kijana wake wa mwisho, kitinda mimba, Mutahaba, au mwite tu Muta, alikuwa ndani ya gereza kwa tuhuma za ujambazi na mauaji. Kijana mdogo tu wa miaka thelathini kasoro mmoja. Alikuwa kijana wake wa pekee kwa sasa, baada ya kaka zake kusemekana kwamba walikwishatangulia mbele za haki kwa kifo katili cha kunyongwa hadi kufa. Sasa, huyu aliyebaki kama tegemeo pekee na yeye alikuwa anasota gerezani, na kwa ugumu wa maisha na ukata aliokuwa nao, hata dhamana ilikuwa imeshindikana kwa ajili ya kumweka huru.

Muganyizi hakuwa na mke kwa takribani miongo miwili sasa. Ingawa alimpenda sana mkewe, ajali iliyomuacha na kilema cha mguu, haikumbakiza mke wake kipenzi mama Rutashobya. Hata hivyo alijitahidi na aliamini kwamba alikuwa baba na mlezi makini kwa wanawe wanne na hasa yule kitinda mimba, Muta.

Hakutaka kabisa wanae wapitie masahibu aliyopitia yeye enzi za utoto wake. Alipokumbuka umande na umbali aliotumia kila siku kwenda na kurudi shule bila viatu hata kufikia hatua ya kupasuka miguu, Muganyizi alijibidiisha kwenye kazi wanae wasiyapitie hayo.

Mungu alimjaalia, kwani yeye alisoma enzi za uongozi wa mwalimu J.K Nyerere, elimu bila malipo kwa ufadhili wa serikali, ambapo alitia bidii na hatimaye kubarikiwa kazi katika wizara ya elimu na kupata cheo cha afisa elimu wilayani Sumbawanga kama ajira yake ya kwanza. Bidii yake ya kazi na kujihusisha na miradi binafsi mbalimbali hasa kilimo katika bonde la ziwa Rukwa ikamwezesha kusomesha wanae shule za kisasa. Shule za malazi nchi jirani ya Kenya. Vijana hao walipofuzu elimu zao za awali, msingi na sekondari, wakapata nafasi ya kusoma elimu ya juu katika vyuo vikuu mbalimbali.

Familia yake ilikuwa ni mfano wa kuigwa. Kijana wake wa kwanza Rutashobya, alifanikiwa kupata shahada yake ya biashara chuo kikuu Cha Dar es salaam na baadaye akaendelea na shahada ya uzamivu chuo Kikuu Cha Oxford nchini Uingereza. Alipotokea hapo Oxford na kurejea nyumbani, serikali haikukawia kumpa kazi, hasa kwa kuzingatia kuwa Enzi hizo wasomi wa kiwango chake walikuwa wachache mno. Serikali ikamwajiri kuitumikia katika taasisi nyeti kabisa kwa uchumi wa nchi, Benki kuu ya Tanzania (BOT).

Kijana wa pili, Byarugaba yeye pia alifuzu mafunzo ya uhasibu pale IFM na baadaye akaendea shahada yake ya uzamivu katika chuo Kikuu cha Witwatersrand nchini Africa ya kusini, na baada ya hapo alirejea nyumbani na kuajiriwa na shirika la umeme TANESCO makao makuu kama mhasibu.

Binti yake wa pekee Kokushubira, yeye aliamua kuwa mwalimu, hivyo mara baada ya kuhitimu shahada yake ya kwanza pale chuo Kikuu Cha Dar es salaam, hakusita kwenda kufundisha huko manispaa ya Morogoro.

Mutahaba alikuwa kijana wake wa mwisho. Kipenzi cha familia. Huyu alizaliwa na kujikuta katika familia iliyosheheni ukwasi na furaha. Kila alichohitaji alikipata bila shida wala kuwaza. Alijikuta akiishi maisha ya kifalme, asiijue shida wala rangi yake.

Miaka ikasonga, maisha yalizidi kuchanua na kunawiri. Familia ya Muganyizi ilibarikiwa. Lakini nani kaiona kesho?

***

Ilikuja taarifa, haikuwa nzuri. Rutashobya kijana wake mkubwa, alituhumiwa kwa ubadhirifu na upotevu wa kiasi kikubwa cha fedha za umma katika benki kuu ya taifa (BOT). Hali ikawa tete. Kesi ikatinga mahakamani, ushahidi ukakusanywa, ikathibitishwa na mahakama kwamba ni kweli kulitokea ubadhirifu mkubwa wa fedha.

Ilikuwa kweli kwamba ubadhirifu ulifanyika, lakini haikuwa kweli kwamba Rutashobya alihusika.

Hata hivyo, Ruta ndiye aliyekuwa na dhamana ya ofisi, waliofanya ubadhirifu walikusudia kumwangushia jumba bovu, hivyo ndivyo iliyokuwa. Ruta akaona kuliko jela bora awe mkimbizi ughaibuni. Bila kuacha unyayo Ruta akafutika nchini. Mahakama ikaamuru mali zake kufilisiwa. Kwa mara ya kwanza familia ya Muganyizi ikapata doa.

Kwa kiasi fulani hali hiyo iliitikisa sana familia ya Muganyizi, kila kona ya nchi na hata nje ya mipaka ya nchi, habari hizo zilivuma kama upepo wa kisulisuli, juu ya familia hiyo kuitia serikali hasara kubwa ya kifedha. Mitaani nako, raia hawakuacha kutwa kucha kuinyoshea vidole familia hiyo na kuwabatiza majina hovyo na dhalili kama wezi, mafisadi na hata kuwaombea balaa.

Kutokana na hali hiyo, Byarugaba kijana wake wa pili, aliacha kazi na kuamua kufanya biashara binafsi. Fununu zikaeleza kuwa, hakuacha kazi bali naye kama kaka yake alifukuzwa kazi kwa sababu ambazo hazikuwa na mashiko, wengi wakihusisha tukio hilo na ile kashfa iliyomkumba kaka yake, Rutashobya, ubadhirifu wa fedha za umma.

Baada ya kufanya maamuzi ya kuacha kazi na kuamua kufanya biashara, Mungu hakumtupa mkono Byarugaba, biashara yake ya electronics ilishika kasi, hata akawa ni msambazaji mkubwa wa vifaa vya electronics jijini Dar es salam. Alikuwa na duka kubwa kabisa katika moja ya mitaa maarufu ya Kariakoo. Hakuishia kusambaza Dar es salaam pekee. Byarugaba alikuwa na mawakala kila mkoa nchini kwa kipindi cha muda mfupi sana.

Katika harakati zake za kibiashara, safari moja, Byarugaba alisafiri kufuata mzigo huko ng'ambo, nchini China. Haikujulikana nini hasa kilitokea, lakini Byarugaba hakurejea tena nchini. Hali iliyoipa familia yake wasiwasi mkubwa. Wakati, familia ya Muganyizi inaanza kukubaliana na sintofahamu ya kijana wao kupotelea ng'ambo, taarifa zilizothibitishwa na ubalozi nchini China, baadaye zilidai Byarugaba na kaka yake Rutashobya walikamatwa kwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya na kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa. Habari hizo zilimfika mzee Muganyizi kama mshituko, zilimfadhaisha mno mzee huyo kiasi cha kumfanya apoteze kabisa ufanisi katika kazi huku afya yake ikiporomoka kila kulipokucha! Kama isingekuwa Muta, Muganyizi ingekuwa habari za jana. Asingemudu kuukabili msiba huo mkubwa wa vijana wake wawili. Si kwa sababu Muta alimsaidia kuukabili msiba ule bali Muta sasa alibaki tumaini pekee la mzee huyu.

Kutokana na sonona, Muganyizi aliamua kutumia muda wake mwingi kumuomba Mungu na kufanya kila liwezekanalo ili kumsimamisha Muta.

Muta, tofauti na wanawe ambao sasa ilisemekana ni marehemu, hakuwa na kazi wala hakujua namna ya kujisimamia. Maisha yake yote hata kufikia miaka ishirini na kenda, maisha kwake ilikuwa ni matumizi tu, hakujali namna na wapi zilitoka, pesa zilitumika tu huku zikiingia. Alizoeshwa hivyo.

Vifo vya Ruta na Byarugaba vilikuwa pigo kubwa sana kwake Muganyizi lakini hofu yake kubwa sasa ilikuwa juu ya mwanae ambaye sasa alijutia malezi aliyompa na kujilaumu.

Alifanikiwa kumtafutia kazi, lakini Muta hakutaka kabisa habari za kazi. Hakuzoea kufanya kazi, alichojua ni kufanyiwa kazi. Vipi aanze kumuita mtu mwingine bosi ilhali yeye alikuwa kazoea kuitwa bosi? Ilikuwa changamoto ambayo hakuwa tayari kuikubali. Nyota iliyong’ara sasa ilianza kufifia na kupotea. Muta alipoteza dira.

Muganyizi, hofu juu ya mwanae ikamtafuna na kumdhoofisha. Kila alichojaribu kufanya ili kuyapa dira maisha ya mwanae kilimuonesha ni kwa namna gani alikuwa amechelewa.

Jioni moja, aliamua hana namna nyingine zaidi ya kumhoji Muta anataka nini. Bila kusita, akajibiwa 'pesa', pesa nyingi za kutosha kuanzisha biashara kubwa au kampuni. Muganyizi akajipata njia panda. Pesa hakuwa nayo. Tangu walipopata msiba ule mkubwa, ni kama dunia iliwatenga na kuwapuuza, hata maswahiba wake wa karibu, nao walipotea. Jambo hilo la mtaji kwa Muta likauchoma moyo wake na kumtia sonona zaidi, lakini hakutaka kulipuuza. Alijikuta akilizingatia mno na kuliwazia sana.

Usiku wa siku hiyo hakupata usingizi mapema. Muganyizi alihisi mawazo yake yanamzomea kwa kila mbinu aliyotafakari kutumia kukabili hali ya mwanae. Nyumba yake kubwa sasa ilionekana kujawa na majitu ya kutisha, kila kona ya nyumba ile ilikuwa ni kana kwamba inamzomea. Kichwa chake kilimpwaya kabisa.

Usiku wa saa tisa, Muganyizi alijikuta akijicheka kwa dharau. Umri nao ulikuwa unamtupa mkono, ilikuwa imebaki miaka mitatu kustaafu! Alinyanyuka kitandani akawasha taa kisha akajitazama kwenye kioo kikubwa cha chumbani! Hakuliona lile tabasamu lililozoeleka. Ngozi yake sasa ilikuwa na makunyanzi kibao na hata kipara chake kilichong’ara zamani sasa kilifubaa na kutengeneza taswira ya bonge moja la kovu.

Wazo hilo la uzee likaamsha wazo jipya. Sasa alirejea kitandani na kupata usingizi. Alipoamka asubuhi alijinyoosha na kujitazama tena kwenye kioo. Alijaribu kutabasamu, kwa mbali akaona nuru. Aliingia bafuni na kuoga huku akiimba wimbo wa Bob Marley, 'no woman no cry!' Alitoka na kuingia kwenye gari lake na kuelekea kazini.

****

Ilikuwa ajabu kidogo. Siku za hivi karibuni hakuonekana kabisa kutabasamu, lakini leo, ah! leo alijawa na matumaini yaliyompa fursa ya kutoa tabasamu mwanana lililowashangaza watumishi wenzake ofisini kwake. Aliingia ofisini akiwa mwingi wa furaha. Alikuwa keshafanya maamuzi yake tangu jana usiku. Hapa alikuwa amekuja kwa kusudi moja tu la utekelezaji. Aliketi kitini, akapaisha macho yake dirishani, akatazama nje kwa muda, akawa anayaona magari yakipita barabarani kutokea kwenye ofisi hiyo ambayo ipo kwenye gorofa ya pili katika jengo hilo la serikali pasipo kuyatilia maanani. Alitazama kwa namna ambayo ilionesha huenda ingelikuwa mara ya mwisho kuitumia meza hiyo kwa kazi zake za kila siku. Uamuzi wake ulikuwa kustaafu kazi. Alipojiridhisha na alichokuwa anakitazama, mzee Muganyizi alirejesha akili yake ofisini hapo. Akavuta keyboard ya komputa yake ya ofisini, akatuliza mawazo na kuruhusu vidole kudurusu kifaa hicho. Aliandika barua, barua ya kuomba kustaafu mapema. Ulikuwa uamuzi mgumu kufanya, lakini aliamini ulikuwa uamuzi sahihi. Lengo lake likiwa kwamba wakishachakata taarifa zake, atapokea pensheni yake na hiyo iwe mtaji kwa mwanae Muta kutimiza ndoto yake ya kumiliki biashara aliyokusudia.

Alianza mchakato huo rasmi Ili kustaafu mapema.

Baada ya kumalizika taratibu zitakiwazo, sasa ilibaki hatua moja ya mwisho. Kupata pesa zake benki, pesa ambazo zingemfaa kijana wake Mutahaba. Huko ndiko alikodondoka na kuzimia na kujikuta akiwa hospitalini, akiwa ana drip mkononi, iliyoruhusu maji kuingia mwilini mwake.

Itaendelea kesho...
 
KIKOKOTOO
DAVID NGOCHO SAMSON

SEHEMU YA PILI

Baada ya kutoka hospitalini na kurejea nyumbani, Muganyizi aliendelea kujiuliza nini hasa kilichomtokea. Kesho yake asubuhi aliamka mapema akikusudia kuwahi kwenda katika tawi la kampuni moja ya ukopeshaji fedha, alikopata kukopa fedha miaka michache iliyopita. Lengo la kwenda kule ilikuwa ni kujiridhisha kwamba kuna kosa lilikuwa limefanyika benki ambalo lilipelekea fedha zake za malipo ya kustaafu kupelekwa kwenye kampuni ile kimakosa kama ilivyoonekana kwenye taarifa za akaunti yake ya benki. Bank statement..

Kumbukumbu zake zilikuwa sahihi kabisa. Ilikuwa ni takribani miaka miwili sasa tangu alipokopa fedha kwenye ile kampuni kwa ajili ya kushughulikia kesi ya mwanawe Muta, kipindi hicho Muta alihusishwa na wizi kwa njia ya mtandao, ambapo ilisemekana aliibia kampuni moja ya kusambaza filamu za kibongo kitita cha shilling million tano.

Muganyizi alikopa katika kampuni ile fedha taslimu tsh million kumi kwa makubaliano kwamba miaka michache mbeleni angelipa fedha hiyo kwa riba baada ya kupokea pensheni yake atakapostaafu. Kampuni ilijitanabaisha kuwa na riba ndogo Sana ya asilimia kumi tu.

Ajabu ni kwamba, baada ya kuandika barua ya kuomba kustaafu na kukubaliwa, ilionekana kwamba kiasi cha zaidi ya Tsh million mia moja ambazo alikuwa apokee kama pensheni kilihamishwa kutoka kwenye akaunti yake na kutumwa kwenye akaunti ile ya mikopo kulipa deni alilokopa kutoka kampuni ile. Taarifa hiyo Ilikuwa nzito mno kwake kuipokea na ndio maana alijikuta hospital asijue vipi alifika hapo.

Mzee Muganyizi alipaki gari lake kwenye viunga vya kampuni hiyo, akashika njia na kuelekea mapokezini. Alikaribishwa na wahudumu wa kampuni ile, na yeye bila kupoteza muda, akajieleza nini kilikuwa kimetokea na kwamba alitaka wafanye mpango wa kumrejeshea fedha zake. Mhudumu aliomba kuona vithibitisho vya kuchukua mkopo kwenye kampuni yao. Binti yule mwenye asili ya kiarabu au kiajemi hivi, alichukua mkataba ule na kuutazama vizuri halafu akamuuliza mzee Muganyizi kama hakuwa amesahau makubaliano waliyowekeana na kampuni. Muganyizi alimweleza kuwa hajasahau kwa sababu alikopa Tsh million kumi na walikubaliana angelipa tsh million 11 ikiwa ni pamoja na riba waliyomweleza kuwa ni asilimia kumi tu. Binti yule alimrudishia ile nakala yake ya mkataba na kumwambia asome upya tena kwa sababu yeye hakuona tofauti ya kilichokatwa na kile ambacho walikubaliana kwenye mkataba ule. Muganyizi aliupokea mkataba na kuuchunguza tena.

Hakuamini!!

Alivuta miwani yake toka kwenye mfuko wa koti na kuivaa, aliinamia karatasi na kusoma tarakimu zilizoandikwa 100,000,000/=. Nguvu zilimwishia, mapigo yake ya moyo hayakueleweka sasa, aliweza kuyasikia yanavyodunda na kuhisi jasho likijaa viganjani mwake. Kama vile kipofu, mzee alipapasa kutafuta kiti, alipofanikiwa kukishika alikaa chini, taratibu lakini kwa yakini, sauti zote ziliaanza kufifia na kubaki kimya, akawa kama yupo kwenye chumba cha ajabu kisicho na uhai. Kwa muda, akili yake ilikuwa kama imepigwa ganzi. Alitulia kimya, kilichosikika ni mapigo yake ya moyo tu! Nayo yalimfanyia kusudi kwa kule kudunda kwake kulikosikika kwa sauti kubwa ungedhani ni mdundo wa dufu.

Alipofanikiwa kupata nguvu kidogo na kutuliza moyo, Muganyizi alinyanyuka taratibu huku akiyumba yumba, alisimama kidogo, miguu ikapata stamina tena akaendelea na safari yake kuondoka kutoka kwenye viwanja vya kampuni ile. Alilifikia gari lake na kuliwasha na safari ikaanza. Alipokanyaga break, alikuwa anatazamana na bar moja hivi nje kidogo ya mji. Hakuwa mlevi, alikunywa pombe kali mara chache sana kwa sababu alizodai ni za kitabibu akiwa nyumbani, tena kidogo Sana kwa kipimo maalum. Lakini leo hii, baada ya yale yaliyommaliza nguvu hapo awali, alihisi eneo lile lingeweza kumpa faraja na kumuondolea lindi la mawazo aliyokuwa anawaza bila kuelewa kitu kwa siku hiyo.

Aliingia kaunta, akaagiza pombe kali na kujitafutia kona ya ufichoni na kuanza kuzinywa. Kadri alivyozidi kuzibugia ndivyo lile tukio la jana benki na la leo kwenye kampuni yalivyozidi kumpa maswali kuliko liwazo, alibaini pombe zilikuwa hazimsaidii, alinyanyuka huku akiyumbayumba, akamwita mhudumu na kulipa bili yake kisha akatoka hapo bar.

Ingawa alikuwa kalewa, bado alikuwa na uwezo wa kuliendesha gari lake. Aliendesha kwa mwendo wa kawaida kuelekea nyumbani kwake. Alipofika kwenye makutano ilipo barabara ya kuelekea kwenye mtaa yalipo makazi yake, aliishuhudia lorry kubwa aina ya scania ikimfuata upande aliko kwa spidi kali sana. Ni kama ulevi ulimtoka ghafla, kitendo kile kikayaokoa maisha yake ambayo yangepotea kwa ajali ya uso kwa uso na scania. Gari lake aina ya Noah liligongwa upande wa nyuma na kusukumizwa kwenye mtaro pembezoni mwa barabara. Alichomoka kwenye usukani na kufanikiwa kutoka ndani ya gari bila kuumia zaidi ya kupata mshituko kwenye mguu wake ambao ulipata kupata kilema cha kudumu kwenye ile ajali iliyompokonya mke wake kipenzi.

Walioshuhudia ile ajali walikiri ulikuwa ni muujiza kwa mzee Muganyizi kutoka akiwa mzima, na kudai dereva wa scania alidhamiria kummaliza yule mzee.

Alipopata fahamu zake vema, Muganyizi alishindwa kuamini kuwa ile ilikuwa ni ajali ya kawaida. Kwa macho yake alimshuhudia dereva wa scania akimfuata kwa lengo la kumgonga. Mambo yaliyokuwa yanamtokea sasa yalimpa hofu kuu, alijaribu kujituliza kwa kujisemea 'ni mshituko tu, nitakuwa sawa!' Lakini hakupata picha, huenda ajali hutokea namna hii!! Alijiuliza lakini wala hakupata jibu.

Traffic walipowasili walifanya ukaguzi na kuandika faini kwa mzee Muganyizi, kwa madai kuwa alikuwa anaendesha akiwa amelewa na ndio sababu ya ajali. Baada ya kumalizana na matrafic , Muganyizi alifanya utaratibu wa kulitoa gari mtaroni likapelekwa gereji kwa matengenezo! Aliliacha huko na kuamua kuchukua taxi kuelekea nyumbani, alihitaji kupumzika. Aliposhuka kwenye taxi ilimbidi kuvuka barabara kuelekea mtaa wa pili yalipokuwa makazi yake. Alitazama huku na kule barabara ilikuwa nyeupe isipokuwa pikipiki kubwa aina ya Honda iliyokuwa imepaki pembeni mwa barabara hatua chache tu na kijana shababi akiwa juu yake. Muganyizi alichukua hatua, ikafuatiwa na ntingine akiingia barabarani, alipofika kati, alitahamaki kuliona lile Honda likiwa limewasha taa likija spidi huku dereva wake akionekana amedhamiria kumugonga, ile kutahamaki, alijikuta mtaroni, mguu wake mbovu ulikuwa unavuja damu gotini, akashukuru Mungu kwa mara ya pili aliokoka ajali iliyolenga kumdhulumu maisha yake. Pikipiki lile sasa likiwa limetokomea kizani kwa muda mfupi tu!

Sasa hofu yake ilizidi maradufu, hofu hiyo ikamtuma kuchukua tahadhari, alikumbuka, alipata kuandika namba za simu za kijana mmoja wakili kwenye kongamano la katiba pale Nkurumah Hall – University of Dar es salaam, jina lake Kajumulo.

Alimpigia simu, akajitambulisha na kumjulisha mazingira aliyokuwa nayo na hofu iliyompata kutokana na ajali hizo mbili na kuhitaji msaada wa kisheria hasa kutokana na utapeli ule aliokuwa amefanyiwa na kampuni ile ya mikopo. Alimaliza mazungumzo huku akimpa mawasiliano na anuani ya makazi yake. Sasa alikuwa na hakika kuwa huenda matukio haya yalihusiana na utapeli wa pesa zake za pensheni.

Haikumchukua muda kufika kwake ingawa maumivu ya mguu sasa yalikuwa makali mno. Aliingia getini kwake akiwa hana hamu kwa madhila aliyokumbana nayo siku hii. Siku ilimchachukia vibaya! Akadhamiria akiingia ndani hatoki tena hadi kesho, lakini loh! Ile kuvuka kizingiti cha geti mzee akajikuta ana kwa ana na mdomo wa bastola, akahamaki! Kijana mnene, mwenye madevu na masharubu, aliyevalia miwani mikubwa iliyofunika macho yake hadi kwenye uso huku kichwani akiwa na mzula mwekundu alikuwa nyuma ya bastola ile! Moyo ulimlipuka pah! Alipojaribu kumkazia macho, Muganyizi alidondoka chini baada ya kupokea kibao kizito kutoka kwa jambazi yule, alipojaribu kuinua kichwa chake, Alikutana na macho makavu ya jambazi, yamewiva na kukolea wekundu kama vile damu zimevilia machoni mwa kijana huyo.

‘Mkataba, nataka mkataba wa mkopo, haraka’ Jambazi aliongea, sauti nzito yenye mikwaruzo, na harufu nzito ya sigara, ugoro au bangi ikamvamia kiasi cha kumfanya Muganyizi akohoe.

Jambazi yule alidhamiria kukipata alichofuata na si vinginevyo. Sauti yake, mwonekano wake vyote vilidhihirisha hilo!

Kwa hofu na woga, Muganyizi alijibu;

‘Kwenye mkoba kijana wangu, upo humu kwenye mkoba, tafadhali nihurumie kijana, shida zangu zitaniua muda si mrefu, usichafue mikono yako kwa damu yangu nakuomba’ alikuwa anatetemeka.

Jambazi lile lilichomoa makaratasi kwenye mkoba, jina la kampuni ile lilisomeka vema kabisa kwenye makaratasi yale, jambazi kwa furaha likamtazama Muganyizi kwa tabasamu halafu likamuonesha ishara ya kuchinja shingo halafu likachomoa bastola kutoka kwenye koti lake refu la kikorea. Kutahamaki, Muganyizi alidondoka chini mithili ya gogo huku damu zikifoka kifuani mwake!

Itaendelea...
 
KIKOKOTOO 03
DAVID NGOCHO SAMSON

Muganyizi alifumba macho yake na kujaribu kusali sala yake ya mwisho. Tayari alihisi malaika mtoa uhai amemtembelea. Damu iliyokuwa inafoka kifuani kwake sasa ilimwelemea kwa uzito. Akili zake zikamshawishi kufumbua macho ili ashuhudie dakika zake za mwisho, walau aende na picha ya tukio la kufa kwake. La haula! Shabaash! Sasa alibaini chanzo cha uzito ule! Yule jamaa alikuwa kamlalia kifuani mithili ya gogo, kimya kimya akigugumia kwa maumivu na damu zikichuruzika pembezoni mwa midomo yake. Hapo ndio alipobaini kuwa damu zile hazikuwa zake bali za jambazi yule aliyekuwa kadhamiria kumuua!

Hakuelewa kilichotokea, kumbukumbu zake zilionesha kwamba, kabla ya kuanguka, alimshuhudia jambazi lile likinyoosha mkono uliokuwa na bastola uelekeo wa kifua chake!

Mzee Muganyizi, anafanya jitihada za kunyanyuka lakini mguu wake mbovu haukumruhusu. Katika jitihada hizo, Muganyizi alijikuta akiupokea mkono wa kijana mmoja ambaye alionekana kumsaidia. Hatimaye alimudu kusimama, alipomtazama vizuri kijana huyo, Muganyizi aliishiwa nguvu kabisa! Miguu yake ilikosa ushirikiano na mwili, ikawa kama imeelemewa kwa uzito wake mwenyewe. Kama ni balaa, hili lilikuwa ni babalao! Ni kama aliruka majivu na kukanyaga moto. Alimtambua vema kijana huyo, angewezaje kumsahau? Alikuwa kaongezeka uzito, hata ngozi ya uso wake ilikuwa imenawiri vema na kuweka mnururisho angavu. Bila shaka maisha yalikuwa yamemnyookea kijana huyu! Alijivuta taratibu, akitamani angerudi enzi zake alipokuwa angali kijana mdogo, enzi zile alizomudu kukimbia kila asubuhi kwenda shuleni, peku bila viatu kwa umbali wa maili nane hivi! Lakini sasa hakuwa na ujanja, miguu yake mwenyewe ilikuwa imemchoka, na hata alipoiamrisha, haikumtii tena! Aliilaani kimoyomoyo ilipomuacha aadhirike kwa kukosa stamina ya kumzuia asiende mrama. Alianguka chini mithili ya gunia la mchele!

Kijana yule alimsogelea na kumshika bega, Muganyizi mkojo ukamtoka wala asijue, huku ukelele wake wa kuomba msaada, ukiishia kusikika ubongoni mwake, usisikike hata na sikio lake mwenyewe.

‘Pole mzee wangu,’ Yule kijana alitamka. Muganyizi akaona maajabu, hiyo pole alikuwa anapewa yeye au kuna mtu alikuwa anapita!? Alijiuliza pasi na WA kumpatia jawabu. Alibaki anamtazama kijana yule asijue nini cha kujibu.

‘Sina nia mbaya na wewe mzee wangu, najua unahofia kwa vile ni mimi niliyekusainisha mkataba ambao sasa umekusababishia yote haya’ kijana aliendelea kujieleza. Kidogo mzee huyo ajibu kwa hamaniko, "Ndiyo, Ni wewe, Ni wewe uliyeniingiza mkenge, Bata mzinga mkubwa wewe", lakini hakuwa hata na ujasiri huo. Alisalia kimya kama zoba, macho kayakodoa kama mjusi aliyebanwa mlangoni.

Muganyizi alibaki kaduwaa asiye na uhakika na hisia zake kwa wakati ule!

‘Mengi yametokea na kwa kweli kilichofanyika dhidi yako nilikuja kugundua baadae na nilipojaribu kuhoji walinigeuka……’ hakumaliza sentensi yake, machozi yalianza kumtiririka kijana huyo, huku akiongea kwa kwikwi akatamka;

‘…. Siamini kama baba yangu amekufa kwa kukosa fedha ya upasuaji wa tezi dume, yote hayo kwa sababu kampuni ilinifilisi kwa madai eti niliwaibia’. Kijana alijifuta machozi na kumalizia;

‘…..mimi pia ni mhanga wa ile kampuni mzee wangu, baba yangu amekufa kwa sababu yao’

Muganyizi sasa alivuta makini yake na kujikuta akimuonea huruma kijana yule. Huruma ile ikamfanya amkumbuke kijana wake Muta, mwanae kipenzi ambae sasa alikuwa jela, jela kwa sababu hakuwa na pesa ya kumwekea dhamana! Machozi yakamtoka mzee wa watu!

‘Hawa watu ni lazima warejeshe fedha zako mzee, nipo tayari kusaidiana na wewe kuhakikisha haki inatendeka na matapeli hawa wanawajibishwa, lakini sasa hapa kuna kazi ya kufanya mzee wangu’ kijana alimaliza kuzungumza huku akijitambulisha kwa jina moja la Aidani.

‘Tunahitaji kuwataarifu polisi kuhusu huu mwili’ Muganyizi sasa alimudu kutamka.

‘Ndio mzee, hebu ngoja nikachukue vocha hapo gengeni, simu yangu haina salio la kutosha’ Aidan aliongea huku akiashiria kutoka. Muganyizi akakumbuka alikuwa na kifurushi chake cha wiki ambacho alikuwa bado kukimaliza.

‘Unaweza kutumia yangu kijana’ alitamka huku akimkabidhi Aidan simu yake.

Aidani alichukua simu ya mzee Muganyizi na kuanza kupiga huku akimkabidhi bastola yake mzee Muganyizi ambaye aliipokea kwa hofu, akishindwa kusema hapana kwa gagaziko lililompata. Yule kijana akatoka nje ya geti huku akizungumza kwa msisitizo na huyo aliyempigia simu.

Haikuchukua muda mrefu, kitu kama dakika tano hivi, Muganyizi alisikia ving’ora vya gari za polisi nje ya geti lake. Aligeuka amuone Aidan lakini kijana huyo hakuonekana. Hiyo haikumpa wasiwasi, huenda alikuwa nje kuwapokea polisi! Alihitimisha hivyo. Akajikongoja taratibu kuelekea getini ili kuungana na Aidani kuwapokea polisi, oh daah!! hakuamini macho yake. Polisi wote sita walikuwa wamenyoosha silaha zao dhidi yake alipotokeza getini tu. Hali hiyo kidogo ikamchanganya! Vipi tena polisi wamuone adui? Moyoni alijifariji kwamba ile ilikuwa ni kuchukua tahadhari. Faraja hiyo ikayeyuka pale alipomsikia afisa mmoja akiwasiliana na mkuu wake, juu ya kumpata muuaji alipojaribu kutoroka, na kudai mwonekano wake ulikuwa sawa kabisa na maelezo ya raia mwema aliyetoa taarifa polisi, tena kuongezea kuwa muuaji alikuwa na bastola mkononi. Kusikia kauli hiyo, kukamnyong'onyeza Mzee Muganyizi.

Muganyizi akageuka huku na kule ili kumuona Aidan ambaye angesaidia kunyoosha maelezo, Aidan hakuonekana! Mara akasikia sauti ya kikamanda kutokea kwenye kipaza sauti kwenye moja ya gari la polisi ikimtaka aweke silaha chini na kujisalimisha kwa hiari kwa Jeshi la polisi.

***

Muganyizi alipiga magoti akairusha bastola mbali kuwaelekea polisi na kunyanyua mikono yake juu ishara ya kutii amri bila shurti. Askari mmoja, bila shaka mkubwa miongoni mwao kwa mwili, sio cheo, kwa tahadhari sana akamsogelea na kumkagua kama alikuwa na silaha nyingine zaidi au la! Zoezi hilo lilipomalizika, Muganyizi aliwekwa pingu na kwa uangalizi wa hali ya juu akatupwa kwenye land Rover la polisi ambapo alijibamiza kwenye chuma cha ukingo wa bodi la gari hilo. Wakati anajaribu kujiweka sawa alishuhudia mwili wa marehemu jambazi aliyeuwawa na Aidan ukidondoka juu yake mithili ya gunia la mahindi. Gari liliondolewa kwa kasi kuelekea kituo cha polisi. Bila kujitambua, taratibu Muganyizi alijikuta akizama kwenye usingizi mzito. Muda si mrefu, akatopea usingizini asijue a wala ba ya kilichoendelea baada ya hapo.

Alipokuja kushituka, Muganyizi alijikuta hospitalini, akihudumiwa na nesi, pembeni yake, binti yake Koku akiwa mwenye majonzi tele akiwa anamtazama kwa huruma. Kwa mbali aliweza kumuona askari mwenye silaha akiwaangalia kwa udadisi na tahadhari. Hakujua yote hayo yametokeaje ghafla ghafla kwa sababu hakuwa na habari kwamba tayari siku mbili zilikwishapita tangu tukio la kukamatwa kwake na wale Askari wa Jeshi la polisi.

‘Baba’ Koku alitamka machozi yakicheza cheza machoni huku akijitahidi yasidondoke chini.

‘Pole baba yangu’ chozi like halikuhimili kusalia jichoni, likamdondoka Koku. Muganyizi akajaribu azungumze lakini akashindwa. Ulimi wake ulikuwa mzito, hakuweza kutamka chochote. Chozi likamtoka. Koku akamkumbatia na kumpa faraja. Kumbato lake likampa tumaini. Kwa mara nyingine tena akajaribu atamke neno, lakini maumivu aliyoyapata hayakuwa na mfano. Sasa aligundua, kwamba taya yake ya kulia haikuwa sawa. Nesi akamweleza kutulia na kutojaribu kuzungumza kwa muda ule kwa sababu taya yake ndo ilikuwa imehudumiwa muda si mrefu.

Katika harakati zile za mshikemshike na polisi, alipojibamiza ubavuni mwa gari, taya yake ilisogea kidogo na kufuatia tukio lile alizima na hio ndo ikawa sababu iliyompelekea kuwepo pale hospitali.

Alipomudu kujongea pale kitandani, Muganyizi alitoa ishara ya kuhitaji kalamu na karatasi. Kwa msaada wa nesi kalamu na karatasi vililetwa na yeye akamudu kuandika maneno yaliyosomeka;

‘Wakili Kajumulo, 071411**08’

Alishusha kalamu na kutuliza kichwa kwenye kitanda, akauruhusu usingizi umvae.

***

‘Wafungwa waua na kuwapokonya silaha polisi magereza, ni gereza la Ukonga’ liliandika gazeti la kisima cha habari.

‘Wanatafutwa kwa mauaji ya polisi magereza’ likahanikiza gazeti la 'matukio' likiwa 'limedamshi' na sura za wafungwa kadhaa na miili ya marehemu askari magereza!

Hivyo vilikuwa ni vichwa vya baadhi ya magazeti vikiwa na picha za baadhi ya watuhumiwa hao. Kwenye mitandao ya kijamii hiyo ndo ilikuwa habari ya siku. Mijadala yote ikilenga tukio kubwa na la kutisha lililokuwa limefanywa na wafungwa dhidi ya polisi magereza.

Koku akiwa pale hospitalini, akifuatilia maendeleo ya baba yake ambaye sasa alikuwa ni mtuhumiwa wa mauaji, ghafla aliliachia gazeti likadondoka chini huku yeye mwenyewe akilifuata chini mzimamzima. Alijikuta anadondoka chini na kuzimia.

Habari aliyokuwa amesoma kwenye mtandao kupitia simu janja yake ilikuwa nzito kupokelewa na moyo wake mwepesi. Miongoni mwa watuhumiwa wale wa mauaji ya polisi alikuwemo Muta kwa mujibu wa habari ile iliyopambwa kwa sura ya mdogo wake Muta kwenye ukurasa wa kwanza tu wa gazeti la mtandaoni. Habari hiyo ikamfadhaisha na kumshitua moyo. Ikampelekea kuzimia. Manesi wakamwahisha wodi ya Wanawake na kumpa huduma ya kwanza.

Kiki alipozinduka, alikuwa ametundikwa drip ya maji na kulazwa kwenye kitanda wodi ya wanawake pale hospitalini.

Tukio hilo la kutisha la mauaji ya polisi lilipelekea kuongezwa ulinzi zaidi kwa Muganyizi, huku magazeti ya udaku yakiunganisha habari ya vifo vya Byarugaba na Rutashobya, tukio la Muta kuua na kutoroka gerezani na hili la kukamatwa kwa mzee Muganyizi kwa tuhuma za mauaji ya mtu ambaye jina lake halikujulikana haraka na hivyo kuipaka vibaya matope familia ya Mzee Muganyizi.

Habari hizi zikaenea kwa haraka mithili ya mlipuko wa covid 19 na kusambaa kwa kasi na kujizolea umaarufu ulimwenguni kote.

Itaendelea...
 
KIKOKOTOO 04
DAVID NGOCHO SAMSON

Miezi saba ilikuwa imekatika sasa tangu Muta alipohukumiwa kifungo jela kwa kosa la ujambazi na mauaji, kikiwa ni kifungo chake cha mara ya pili baada ya kifungo cha awali ambapo alituhumiwa kutapeli pesa kwenye kampuni moja ya usambazaji wa filamu za kibongo pesa nyingi. Kwa sehemu sasa alikuwa ameyazoea maisha ya jela. Safari hii, Muta alimudu kutazama upande wa pili wa maisha kwa mtazamo tofauti na ule wa awali. Mtazamo uliomuonesha kuwa zaidi ya pesa na matumizi yake, maisha yalikuwa na maana pana zaidi ambayo huenda hakuna binadamu aliyemudu kutoa tafsiri yake toshelevu.

Akiwa kwenye kona yake aliyozoea kulala mle gerezani, eneo chafu kabisa kwa mtu wa haiba yake kuishi, alikuwa kazama kwenye dimbwi la tafakuri nzito, akitafakari hali yake ile ambayo hakuelewa nini hatima yake. Zaidi, alimlaumu sana baba yake kwa kushindwa kumtoa katika hali ile ya mateso, wakati alijua fika kuwa mzee wake alikuwa anachukua mafao yake mwaka huo. Alijitazama na kuona alivyokuwa amedhoofika. Siku za mwanzoni, alishindwa kula kabisa chakula cha jela, ugali uliopikwa kwa pumba za mahindi na hata wakati mwingine pumba za ngano, maharage maarufu zaidi gerezani hapo kwa jina la 'ndondo' yaliyosheheni wadudu wadogo weupe na weusi, mbaya zaidi ndondo zenyewe zikihesabika, ukiacha bahari ya maji moto yaliyochemshwa na kutiwa chumvi eti ndio mchuzi. Haikuwa rahisi kuzoea. Kwa bahati mbaya sana pia, hakuna aliyeonesha kujali. Alipobaini hakuna anayejali na kwamba hata kama angelikufa kusingekuwa na tofauti, aliazimia kuikubali hali ile. Alianza kwa kujilazimisha kula na hatimaye ratiba ya chakula cha jela ikamkaa vema kichwani. Maisha yakasonga. Afya yake ikarejea. Akaanza na mazoezi ya mwili, mwili ukakubali. Akapata heshima na kujipatia ukubwa gerezani. Mwenyewe akijiita 'mtemi Muta'. Heshima aliyoipata baada ya kumchakaza kwa ngumi mbabe aliyekuwa anaheshimika gerezani hapo maarufu kama Pandu.

Leo hii akiwa kwenye kona yake pendwa, alikuwa peke yake, utemi wake ukiwa umevuliwa rasmi, wapambe wake wote akiwa amewapoteza baada ya kutokea mbabe zaidi yake pale gerezani.

Gerezani alikuwa kaingia jabali la mtu, hakujulikana jina, ingawa wafungwa wenzie sasa walimbatiza jina 'Nondo'. Nondo alikuwa amehukumiwa jela kwa kosa la kupora kwa kutumia silaha. Tukio ambalo lilihusisha mauaji ya kutisha ya tajiri mmoja maarufu sana kwa jina la Mr. Masebo (Pedezyee Sebo), mfanyabiashara wa vinyago jijini Dar es salaam na mmiliki wa club za usiku mbalimbali jijini humo. Mr. Masebo kwa upande wa pili alikuwa ni mtu hatari sana ikisemekana kwamba alikuwa miongoni mwa waagizaji nguli wa madawa ya kulevya nchini, akiwatumia zaidi wasanii wa bongo muvi, wanamitindo, na wanamuziki kama punda wa kufanikisha biashara zake hizo, wakibebeshwa madawa hayo toka nchi moja kwenda nchi kusudiwa. Pia, ilijulikana kuwa alikuwa na hisa nyingi kwenye makampuni mbalimbali ya kifedha nchini. Taasisi za ukopeshaji fedha kwa riba.

Kwa taarifa za uhakika kutoka kwa waliohudhuria hukumu ya Nondo pale mahakamani, zilidai kwamba, Nondo aligundulika kuhusika na mauaji ya Mr. Masebo kutokana na taswira yake kunaswa kwenye camera za CCTV zilizokua zimetandazwa kuzunguka mjengo wake wa kisasa uliokuwa nje kidogo ya jiji la Dar es salaam maeneo ya Mkuranga mkoani Pwani. Jengo hilo matata la Mr. Masebo lilikuwa na walinzi wenye mafunzo maalum lakini Nondo alifanikiwa kupenya na kuinyofoa roho ya Masebo na kutokomea zake huku akiwaacha walinzi wale katika ulemavu wa kudumu. Tukio hilo likamfanya Nondo kuwa miongoni mwa majambazi hatari waliokuwa wanatafutwa na mkono wa sheria.

Kukamatwa kwake ilisemekana kulikuwa kwa kizembe sana kwa mtu wa kaliba yake. Alikamatwa katika club mojawapo ya Mr. Masebo akiwa anakula raha na watoto wawili wa kike kutoka arabuni. Mmoja kushoto kwake na mwingine kulia kwake. Wanawake warembo na wenye kujua kutumia miili na maumbo yao kama kitega uchumi.

Wakati polisi walipomfikia, Nondo hakuonesha jitihada zozote za kujitetea au kukimbia. Alitii amri bila shurti. Ima alishindwa ujanja kutokana na eneo alilokuwa au hakujua kilichokuwa kinamkabili. Lakini hata kama alihusika, basi huyu hakuwa yule Nondo hatari kama alivyotambulika kote jijini. Huyu huenda kaponzwa na ufanano wake na Nondo. Polisi wale wakahisi hivyo, maana jamaa huyu alikuwa kondoo. Alichojua labda ni Wanawake tu. Polisi hawa walielekea kuamini hivyo.

Nondo aliswekwa rumande kungojea kupelekwa kwa shauri lake mahakamani. Kwa vile kesi yake Ilikuwa yenye kuvuta makini za raia na wafuatiliaji wa mambo, shauri lake lilienda mahakamani mapema, huku upelelezi ukishika hatamu kwa mwendo kasi.

Kesi yake haikuchukua muda, ilimalizika haraka kwani Nondo alikiri makosa aliyokuwa amesomewa. Alipoulizwa kama alimuua Mr. Masebo, Nondo alijibu kwa kujiamini kabisa mbele ya hakimu kwamba ni kweli alihusika na kumuua Mr. Masebo na kwamba angepata habari kuwa hakufa basi wasingemkamata kwa sababu angehakikisha Masebo anakufa kwanza kabla ya yeye kuonekana mbele za mtukufu hakimu. Alidai kwamba kwa vile serikali ilijua maovu ya Mr. Masebo lakini ikaamua kufumbia macho, basi watu wa aina yake walihitaji kuzaliwa zaidi ili kudhibiti kuangamia kwa wengi kulikotokana na matajiri wachache sampuli ya Mr. Masebo kujitajirisha huku wakitumia binadamu wenzao mithili ya mipira ya kuvaa uumeni wakati wa tendo la ngono na kutupiliwa mbali baada ya tendo hilo.

Kwa kuzingatia ushahidi wa kamera na tamko lake mwenyewe, hakimu alimuhukumu Nondo kwenda jela kwa miaka 30 kama onyo kali kwa wengine wenye tabia kama yake.

Nondo akakutana na Muta kwenye gereza la Ukonga na huzuni ya Muta ikawadia. Nondo alivyoingia gerezani ikawa ni mwisho wa utemi na ubabe wa Muta gerezani.

Alipoingia jela, Nondo akakutana na sifa na hofu iliyotawala mle gerezani kutoka kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Muta. Basi yeye Nondo akacheka kwelikweli. Cheko la dharau. Hakutaka kuamini kuwa kuna mtu mwenye sifa zile mle gerezani. Naam, labda kwa sababu aliingia gerezani kwa kupenda na kwa lengo maalum. Au labda yeye alikuwa na sifa zaidi ya hizo alizoaminishwa kuwa ni za kipekee. Kabla ya kuoneshwa malazi yake yatakapokuwa, wapambe wa Muta walimfuata na kumpleka mputa mputa kwa bosi wao! Alipofikishwa mbele ya mtemi, aliamriwa kupiga magoti na kutoa heshima kwa mtemi wao. Ndio , Muta sasa alikuwa ni amiri jeshi kwenye jeshi aliloanzisha gerezani. Alikuwa ni mtawala mwenye heshima kubwa. Heshima iliyotokana na kumpindua mtabe aliyekuwepo kabla hajaingia gerezani. Mfungwa aliyejulikana kwa jina Pandu. Heshima hii, Muta aliipata baada ya kuingia kwenye pambano na Pandu na kufanikiwa kumchakaza vibaya kwa kipigo. Pandu akapigwa marufuku kushiriki kwa namna yoyote ile kwenye harakati ambazo zingeonesha anataka kupata kiti chake. Muta akatangaza serikali ya kiimla yeye mwenyewe akiwa ndio dikteta kwenye serikali hiyo.

Katika kujihakikishia kuwa anadumisha utawala wake gerezani, Muta akatengeneza propaganda nyingi na kuzieneza gerezani. Raia wake wakaziamini, sifa zake zikawa kemkem. Wengi wakiamini ni kweli Muta alikuwa na uwezo wa juu zaidi wa kichawi. Kwamba alikuwa na nguvu ambazo hakuna mchawi angeweza kufikia. Akawajaza watu wake hofu , akaanzisha mfumo wa kodi kwa kila kichwa gerezani. Kodi hiyo ilikusanywa kila mfungwa alipotembelewa. Chochote alicholetewa, asilimia 40 ilimegwa kupelekwa kwa mtemi. Wafungwa wapya walijazwa simulizi za kutisha za Mtemi Muta, simulizi ambazo wala hazikuwahi kutokea. Muta kwa sehemu kubwa akaishi jela kama mtawala na maisha yake yakiwa sawa na raia wa kawaida nje ya gereza isipokuwa Uhuru wa kuzurura..

Nondo alipofikishwa mbele ya mtemi na kulazimishwa kupiga magoti, alikataa kutii amri. Kitendo hicho kikamkasirisha sana mtemi. Muta akafanya jitihada ya kuamka ili kumuadabisha mfungwa huyu mgeni. Hata hivyo askari wake mtiifu akamuomba yeye ndo amuoneshe mshenzi yule ambaye hakutaka kufuata sheria za serikali ya Muta, nini maana ya kutii amri. Ngeumkeni akarusha ngumi moja yenye uzito wa kilo tano hivi na point kadhaa. Ngumi hii ililenga kuutawanya kabisa uso wa Nondo, lakini kwa ustadi wa hali ya juu, Nondo akaepa, na kumshindilia Ngeumkeni konde moja lililompata barabara panapo mbavu zake, Ngeumkeni akadondoka chini mithili ya gunia la viazi na kulamba vumbi miguuni pa Nondo. Kuona vile askari wengine wa Muta wakajazwa upepo wa hasira, wakamvamia Nondo kwa pamoja. Tayari raia wa gereza la ukonga wakawa wamekusanyika kushuhudia pambano hilo kali dhidi ya serikali ya Muta na muasi mmoja aliyejiita Nondo. Kwa mpambano uliokuwa unaendelea, ni dhahiri muasi huyu alikuwa amejipatia wafuasi wa kutosha. Zilisikika kelele nyingi za kumshangilia kutokana na uwezo aliouonesha. Hofu ikamvaa Muta, hasira zikamjaa hadi pomoni, alikuwa anadhalilishwa, na hakujua angekuwa nani bila utemi wake mle gerezani. Asingeshindwa kizembe, angewezaje kuikabili aibu, na si wote walimuogopa kwa zile sifa zake za kichawi? Na ule ustadi wa kumng’oa Pandu?

Wapambe wa Muta walivyoshuhudia ile hasira yake, wakajua Nondo atapoteza maisha yake. Wakajaribu kumsihi Nondo aombe msamaha kama anapenda uhai wake. Wakamhakikishia kwamba hakuna mtu angeweza kufanya kitendo kile alichofanya na abaki salama katika utawala wa Muta. Wengi waliamini kilichokuwa kinafuata ni mazishi kwa Nondo. Nondo kusikia hivyo ndo kwanza akacheka sana tena kwa dharau iliyomchanganya zaidi Muta.

Muta akaendelea kumkazia macho Nondo moyoni akitamani ushawishi wa propaganda zake uliokuwa unafanywa na wafuasi wake watiifu dhidi ya Nondo utazaa matunda. Ah! wapi? Nondo ndo kwanza alizidi kuonesha unondo wake. Muta akafanikiwa kutamka kwa sauti tetemeshi,

‘Wewe ni nani unayediriki kujeruhi askari wangu, unadiriki kusimama mbele zangu kwa kiburi na majivuno! Haa! Hunijui kwa kweli! Usipojirudi nakurudi, iwe mfano kwa wengine wanaodhani wanaweza kuleta ujinga kama huu kwenye utawala wangu, mimi ndio Muta, …..’ hakufanikiwa kumaliza maelezo yake kwa hadhira, Kwa dharau kubwa, Nondo alimgeuzia Muta kisogo na kuwakabili wale raia wa gereza ambao walilipuka kwa kelele za kushangilia. Nondo aliwatazama washangiliaji wale kwa jicho la kujionesha yeye ni bingwa halafu akawanyamazisha kwa ishara ya kuweka kidole cha pili baada ya gumba lake mdomoni na kutoa sauti ya ‘sh-sh-sh’. Gereza na wafungwa wale kwa umoja wao wakatekwa na ukimya wa ghafula, nadhani kwa shauku ya kusikia muasi alitaka kusema nini.

“Ati naulizwa mimi ni nani? Nitawaambia, mimi naitwa Buda aka Nondo, muuaji ambaye ametukuka, muuaji wa mafisadi na watu wenye kuonea wanyonge. Naam, naitwa Nondo. Kama wewe ni fisadi, basi time (muda) yako imefika upate hukumu unayostahili. Wewe ni adui wa Nondo na lazima utashughulikiwa vilivyo!” Nondo akamaliza, lakini ile ageuke kumtazama Muta, Muta akamvaa Nondo mzimamzima na kumwangusha chini, akawa amekaa juu yake, lakini katika hali ambayo watu hawakutarajia, walimshuhudia Muta akipaa juu na kisha kutua hatua chache kidogo mbele ya Nondo kwa kishindo kikuu! Nondo akamfuata Muta na kisha akamnyanyua juu mithili ya katoto kadogo. Muta akawa amedhilika kupita kawaida.

‘Bila shaka huyu naye ni fisadi, kwa sasa nitampa onyo, na nitafanya uchunguzi wangu taratibu, nitakapobaini ufisadi wake, nitamhukumu sawasawa na sheria zangu dhidi ya mafisadi’ gereza likarindima kwa kelele za shangwe, wafungwa wale wakifurahia mapinduzi yaliyokuwa yamefanyika dhidi ya dikteta wao Muta.

Itaendelea..
 
KIKOKOTOO 06
DAVID NGOCHO SAMSON

Gabby ni Askari magereza ambaye amefanya kazi na jeshi hilo kwa miaka 15 sasa. Maisha yake sio mabaya na wala sio mazuri sana. Yana unafuu wa wastani, maana haombi mtu kula kwa familia yake. Hata hivyo, ni mtu mwenye masikitiko juu ya nduguye Tuzo ambaye huu sasa ni mwaka wa tatu haijulikani alipo. Tuzo, mbaye ni kaka yake wa toka nitoke, alikuwa ni mwanasiasa ambaye alijipambanua kwa sera za upinzani dhidi ya zile za serikali tawala. Alikwishajitengenezea jina kubwa kwa kuwa upande huo. Lakini kama ilivyo kawaida kwa kundi la mzee Kidevu mrithi wa pedezyee Sebo, walitumia umaarufu wake ili kutengeneza rapsha na muhali miongoni mwa raia, na kufanya serikali iwe sehemu ya lawama. Kwa sababu kwa kadri ambavyo kundi la mzee kidevu walivyoichonganisha serikali na raia, serikali ilipolivalia njuga suala husika, ndivyo wao walivyotanua upenyo wa kufanya mambo yao yaliyowaingizia fedha za kutosha. Biashara zao haramu. Hao, ndio waliomteka Tuzo na kutengeneza gumzo na sintofahamu ya kisiasa nchini kufuatia kupotea kwake. Aidani, alihusika na utekaji huo.

Gabby alipopokea ugeni wa Nondo siku kadhaa nyuma, alifurahia zaidi ujumbe aliokwenda nao Nondo. Hatimaye angeondokana na sononeko. Maana alihisi kuwa sehemu ya taasisi ambayo ilihusika na mateso ya raia wasio na hatia akiwemo nduguye Tuzo. Mpango wa Nondo ukampa tumaini la kuyaanza upya maisha yake. Familia yake ingemkosa kwa muda lakini hatimaye ingeishi maisha yaliyo bora. Bintiye mkubwa sasa alikuwa mwaka wa mwisho chuo kikuu. Kijana wake wa pili tayari alikuwa kaajiriwa serikalini kama afisa wanyama pori na alikuwa akifanya kazi huko Manyara. Mkewe mpenzi, alikuwa kamzika mwaka mmoja uliopita. Kama mpango wa Nondo ungefanyika kikamilifu, hakukuwa na shaka kwamba angekuwa sehemu ya mabadiliko.

Nondo alimsimulia Gabby habari kadhaa za kile kilichokuwa kinaendelea nchini nyuma ya mapazia. Akaongezea chumvi mambo kadhaa na kuyatia ladha. Gabby akayapokea yote kama ukweli hasa kwa vile tayari alikwisha jiandaa kisaikolojia dhidi ya serikali. Ni kama alikuwa mkao wa tayari akisubiri tu apewe sababu ili iwe kigezo cha kufanya maamuzi ambayo ni dhahiri alikuwa akiyatafakari kwa muda mrefu sasa.

Nondo alimweleza mpango wa kuingia gerezani, gereza alikofungwa Muta, na akamweleza kuwa baada ya muda fulani, angepaswa kuondoka mle gerezani akiwa na Muta na baadhi ya wafungwa na pia akamweleza lazima kungetokea madhara kiasi kwa askari hasa kama wangelazimika kupambana. Gabby angekuwa ufunguo wa kuondoka mle gerezani.

Alitakiwa siku ya tukio, ahusike kuwafunga pingu, lakini pia angelazimika kuwa na hizo funguo na kukaa na kundi la Nondo ambalo lingehitaji kutoroka. Yeye Nondo alikuwa kaandaa gari uraiani ambalo lingewabeba eneo fulani kwa mtindo wa kusababisha ajali ya karandinga la polisi. Gabby aliridhia. Hivyo tukio hilo lingefanyika, na Gabby angewafungua pingu Nondo na wenzie, wangeshuka kwenye karandinga na kufutika eneo la tukio kwa gari ambalo huku uraiani lilikuwa limeandaliwa kwa kazi hiyo.

***

Ukweli ni kwamba hatimaye usiku wa siku hiyo, Nondo na Muta walifanikiwa kutoroka gerezani, huku nyuma wakipoteza maisha ya askari kadhaa wengine wakiwa kwenye hali mbaya.

Habari ya tukio lao ikagubika nchi nzima na kuitiisha chini ya hofu kuu!

Usiku wa tukio lao la kutoka jela ulikuwa usiku wa aina yake kwa Muta. Mipango waliyopanga wakiwa gerezani ilikuwa kama ndoto ambayo Nondo aliamua kumpa Muta ili kumpa matumaini. Hakujua kama ingelikuwa halisia lakini aliamua kuiamini kama namna ya kujipatia tumaini. Hata hivyo yeye binafsi hakuwahi kuwaza kama kuna siku angefanya tendo la kishujaa kama hili ambalo walikuwa wanalizungumzia wakiwa ndani. Hakuona sababu ya kulipinga hasa kwa vile aliona ni wazo ambalo lilimpa tumaini na mtazamo wa tofauti na ule aliokuwa amejengewa tangu mtoto, mazoea ya kuandaliwa na kutekelezewa kila kitu bila yeye kutia bidii au nguvu zake binafsi.

Alfajiri ya siku hiyo, Muta alishuhudia miale ya macheo ikipenyeza kingo za mlango uliyofunga selo yake. Muda si mrefu atakuwa anakabili kifo kama si uhuru wake tena! Akili yake ikagoma kukubali adhabu ya kifo, moyo wake hata hivyo ukawa na kila dalili ya hofu. Angefanyaje? Simulizi juu ya mzazi wake na madhila aliyokuwa amekabili siku za karibuni, kuwepo kwake ndani kungepelekea kupoteza mzazi wake huyo kizembe kabisa. Kufa nini?! Asiyekufa nani? Kila mtu hufa mara moja, kinachoangaliwa ni aina ya kifo alichokufa mtu na nini alichoacha kama mwendelezo wa maisha yake hata baada ya kufa. Heri kufa kunakoashiria uzazi wa historia njema kwa kizazi kijacho. Heri kufa ukipigania haki kuliko kufa ukilamba miguu ya mtesi wako.

Alijitazama mikono na miguu yake, akajichukia. Alikuwa ameisha kabisa. Afya yake haikuwa ile aliyokuwa nayo siku zote. Hapo wazo na mikakati ya Nondo ikamkolea na sasa akaona uhalisia wake ukitekelezeka. Hakuwa na jinsi, kama ni kufa, basi alihiari kufa akijaribu kujiokoa na si kwa njaa na udhoofu huu aliokuwa nao.

Saa moja na nusu hivi, walipandishwa kwenye karandinga la magereza tayari kwa kuhamishiwa kwenye gereza lenye ulinzi madhubuti (Maximum Security) kutokana na aina ya makosa yao, mauaji. Hii ingeweza kuwa safari yao ya mwisho. Alijiwazia Muta, lakini pia walidhamiria iwe safari ya uhuru.

Safari yao iliendelea, Muta, Nondo na wafungwa wenzao wote wakiwa kimya, huenda wakitafakari nini hufuata baada ya kifo, huko mbinguni au motoni. Siku nyingi Muta hakuhudhuria ibada. Sasa alimhitaji Mungu. Akatamani angeyasikia maombi yake. Aliomba kitu kimoja tu, baada ya hii operesheni yao, abaki hai.

Eneo la tukio lilikuwa jirani sasa, Nondo alimpa Gabby ishara ya konyezo. Mara gari kubwa semitrela likiwa limeiva kwa spidi lilitokeza njia panda na kulivaa karandinga la magereza na hii ikatokeza ajali mbaya sana kuwahi kutokea. Watu wakiwa wanashangaa nini kinaendelea, walishuka vijana wawili wenye bastola na kuwashambulia askari magereza waliokuwa wanaugulia majeraha. Wakati huo huo, Gabby akaingiza karata yake mchezoni. Dakika mbili mbele, Nondo, Muta na baadhi wa watu wao waaminifu, walikuwa huru dhidi ya pingu. Gari aina ya landrover, ikiwa na abiria kadhaa ikatimuka na kuacha vumbi nyuma. Muta, Gabby na Nondo na wale vijana wakiwa abiria wa gari hilo. Gari hilo lilifanikiwa kutokomea pasipo kuacha alama. Nyuma ikabaki simulizi za watu walioshuhudia tukio hilo. Gabby akiwa na jeraha kubwa la risasi nyuma ya kisogo, asijue maana hakuwa hai tena. Hadi wanafika eneo la kubadili gari, Ndiyo Nondo na wenzake waligundua hawakuwa na Gabby ila mwili wake. Wakaamua kuuacha mwili huo kwenye landrover lile, walijua lazima gari hiyo ingepatikana na ikiwa na mwili wa Askari magereza, Gabby angepatiwa maziko ya Heshima ya shujaa. Ndio, kwa sababu hakuna aliyejua uhusika wake. Hata hivyo, kifo chake pia kiliwatia simanzi kubwa Nondo na wenzake. Walimwomboleza.

***

Kikao nyeti sana kilikuwa kinaendelea katika jengo mojawapo la marehemu Masebo. Miezi na siku kadhaa sasa zilikuwa zimekatika tangu alwattan Masebo kudhulumiwa uhai wake na mtu aliyejiita Nondo. Pale ambapo kundi hili la mzee Masebo lilipodhani Nondo amedhibitiwa, wakapashwa habari za kutoka gerezani na kufanya mauaji makubwa ya askari waliokuwa wakimweka chini ya uangalizi wa mkono wa sheria.

Tayari ilikuwa imeshajulikana mrithi wa kiti cha Masebo, na ndiye hasa aliyeitisha kikao hiki nyeti ili kujiwekea tahadhari na kutafuta namna ya kumpoteza kabisa Nondo. Walikuwa na majukumu makubwa ya kuhakikisha himaya yao inadumu na kufanya shughuli zake kama kawaida.

Mzee mwenye asili ya kituruki, mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa viwanda kadhaa vya kuzalisha nondo na saruji. Mdau mkubwa wa chama kimojawapo maarufu cha siasa nchini. Mtu aliyejitengenezea heshima kubwa ndani na nje ya Afrika ya mashariki na kati. Mzee Rahul Baldev alimaarufu mzee Kidevu. Huyu ndio alikuwa sasa anashikilia kiti kilichoachwa na marehemu mzee Masebo.

Miradi ya genge lao halifu, ikiwa ni pamoja na makampuni ya ukopeshaji fedha ambayo kwa kutumia wanasheria wabobezi wachumia tumbo, walifanikiwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa idara za usimamizi wa fedha za serikali, kutengeneza mitandao ya kiwizi iliyolenga hasa kujilimbilikizia mali kwa kiwango cha juu, ikiwemo kuwaibia fedha wastaafu mafao yao. Tayari walikwisha tengeneza maadui wengi, na hata kudiriki kuua wale walioonesha namna fulani ya ung’ang’anizi wa kudai haki zao baada ya kutapeliwa. Watumishi wa serikali kwenye idara za mifuko ya hifadhi ya jamii, walitumiwa kutoa orodha ya watumishi ambao walikuwa kwenye mipango ya pensheni, na wale waliokuwa na miaka mitatu kabla ya kustaafu. Genge la Masebo na Kidevu lilipopata orodha hiyo, kazi yao Ilikuwa moja tu. Kuwarubuni wazee hao na kuondoka na mafao yao.

Kikao cha leo kililenga kubaini na kuweka mikakati ya kushughulika na watu ambao sasa walianza kuonesha changamoto kwenye kundi lao na hata kufikia kiwango cha kumuua mmoja wao. Kiongozi wa kundi lao. Pedezyee Sebo. Majina mahsusi yakiwa ni Nondo na Muta ambao sasa ilisemekana wapo nje ya gereza na hawakujua mipango na lengo lao.

Mipango ilipangwa ikapangika, Aidani na wenzake wawili walipewa jukumu la kuwatafuta na kuwapoteza kabisa Nondo na Muta kwa gharama zozote zile. Fedha na kila kitu walichohitaji kwa jukumu hilo kiliwekwa sawa na sasa Aidani na wenzie waliingia mtaani kuwatafuta wabaya wao.

***

Majira ya saa kumi usiku, katika hospitali ya taifa Muhimbili. Kelele za ving’ora vya ambulance zikiashiria mgonjwa aliye mahututi, zilisikika na mageti yakafunguliwa haraka. Gari ile ikazama ndani. Mtu aliyeonekana kuwa taabani alipokelewa na manesi na kuwahisha kwenye wodi ya uangalizi maalumu (ICU). Madaktari wawili wakazama wodini kucheki hali ya mgonjwa na pia kutoa huduma za kitabibu zaidi. Nondo aliyekuwa kavalia kidaktari zaidi, alijipenyeza kwa wagonjwa na moja kwa moja akaelekea kwenye kitanda alichokuwa amelazwa mzee Muganyizi. Kwa taarifa zilizokuwa zimetolewa rasmi, mzee Muganyizi alihitaji kupata matibabu zaidi nchini india na kibali cha rufaa hiyo kilikuwa dhahiri. Mzee huyo alipaswa kuwahishwa na ndege ya alfajiri saa kumi na moja. Ndege binafsi ilikuwa imeandaliwa kwa zoezi hilo.

Ndege binafsi iliyoandaliwa kwa zoezi la kumsafirisha mgonjwa ilinyanyuka taratibu katika viwanja vya hospitali ya Muhimbili ikiwa na abiria wanne. Mzee Muganyizi, Nondo, Muta na Koku. Koku alikuwa haamini kinachoendelea. Ni kama alikuwa ndotoni. Lakini ulikuwa ni ukweli. Maelezo zaidi huenda angepewa mbele ya safari. Kimya kilitawala ndege ile ilivyokuwa inakata mawingu na kuliaga anga la Tanzania na kuingia anga la kimataifa.

Kwa upande wa pili, Aidan na wenzake kwa kutumia mbinu zao za kijasusi walifanikiwa kuingia hospitalini na kukutana na habari za rufaa ya Mzee Muganyizi kwenda nchini India. Hilo halikuwaingia akilini. Mtu aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi kwa tuhuma za mauaji anapewa rufaa ya kwenda India. Waligundua tayari walikuwa wamechelewa. Mpango wao ulikuwa umegonga panapo ukuta wa zege. Sasa kuliko wakati mwingine walikuwa wameachwa njia panda. Muta na Nondo wakiwa nje, mzee Muganyizi akiwa hai, hiyo ilikuwa dalili mbaya sana kwa kundi lao. Ikiwa na maana kuwa vita Ilikuwa imetangazwa rasmi. Walimhofia zaidi Nondo kwa jinsi alivyoweza kuondoka na uhai wa pedezye Sebo akivuka vikwazo vya ulinzi lukuki.

Mawasiliano yalifanyika. Bila shaka hii ilikuwa ni vita kubwa iliyokabili genge la mzee Kidevu na wenzie. Wenzao waliokuwa serikalini walikuwa waingie kwenye vita kwa kutumia nafasi zao serikalini. Ikasukwa mipango mingine. Muganyizi na familia yao sasa walitangazwa ni kundi hatari la kigaidi na walitafutwa kokote kule wakiwa hai au wafu.

Kama ilivyo kawaida, vyombo vya habari vikaja na hadithi kubwa. Simulizi ya Muganyizi na familia yake kutoroka nchini, ikiwa ni siku moja baada ya Muta na wafungwa kadhaa kufanya mauaji ya maafisa gereza na kutokomea uraiani. Simulizi ikanogeshwa na tamko la waziri wa mambo ya ndani aliyetangaza familia hiyo kuwa ni kundi la kigaidi, Waziri huyo, alikuwa anatumika kutoa taarifa hiyo si kwa maslahi ya nchi bali ya kundi la mzee Kidevu na wajanja wao waliokuwa wamepenyezwa katika nafasi muhimu kwenye Jeshi la Polisi na Usalama wa taifa.

Itaendelea....

Kwa maoni 0629077792
 
KIKOKOTOO 07
DAVID NGOCHO SAMSON

Kimya kilitawala ndege tangu waondoke pale Muhimbili, bila shaka kwa mshangao au hamaki ya mipango iliyokuwa imesukwa na Nondo. Muta alishindwa kunyamaza tena. Mipango iliyokuwa imepangwa na Nondo ilikuwa mipango ya hali ya juu sana na bila shaka iliyokuwa imesheheni ufadhili wa kimataifa. Kwa hakika Nondo hakuwa mtu wa kawaida. Muta alijikuta na maswali mengi yaliyohitaji majibu ili kumpa wepesi.

‘Nadhani ni muda mwafaka utueleze A hadi Z ni nini hasa kinaendelea!’ Muta aliuliza akiwa amemkazia Nondo jicho la kutaka majibu haraka.

‘Sawa, kwanza niwape pole kwa madhila yaliyoikumba familia yenu. Najua maswali ni mengi sana juu yangu. Lakini niwaombe tu muwe na subira, mara tutakapotua tunapoenda mtayapata majibu ya maswali yenu yote mnayojiuliza. Lakini kwa kifupi tu, mimi ni mpiganaji mzalendo kwa taifa langu. Ambaye nimeyatoa maisha yangu kupigania haki na kweli kwa ajili ya ustawi wa taifa langu. Mimi pamoja na wenzangu, tupo kwa ajili ya kurekebisha na kuifanya Tanzania iwe nchi inayofaa kuishi kwa amani kwa kila mtanzania. Na tupo kinyume na taasisi ya serikali au ya kiraia yenye mrengo wa kukandamiza haki za wengine. Sisi ni wajamaa halisi tunaoishi bado Ili kushughulika na watu wanaodhani wanaweza kumiliki watu wengine.’ Nondo alijieleza kwa kifupi. Unaweza kutuita watu wasiojulikana! Alimalizia.

Safari iliyokuwa haijulikani mwisho wake ni wapi, sasa ilifika tamati. Ndege ilitua nje kidogo ya jiji la Johanesburg, ndani ya fensi moja kubwa na thabiti, lililosheheni ulinzi madhubuti. Ndani ya fensi hiyo mlikuwa na uwanja wa ndege ambako ndege ndogo za kukodi zilimudu kutua bila mushkeli. Eneo hili lilikuwa kubwa sana, kuonesha lilimilikiwa aidha na kampuni kubwa ambayo Ilikuwa na uwezo wa kumiliki ndege binafsi au kutumia huduma za ndege binafsi. Muganyizi alipokelewa na madaktari wataalam na kupelekwa ndani ya jengo moja mle ndani, katika chumba ambacho kilikuwa na kila kitu kinachohitajika kwenye theater ya kisasa kabisa ya hospitali ya kisasa. Daktari yule bila shaka raia wa Kijapani alikuwa amhudumie mzee Muganyizi kwa kiwango cha kimataifa.

Ndani ya fensi kubwa iliyozunguka eneo hilo, kulikuwa na majengo makubwa makubwa mfano wa magodauni ya kuhifadhi mitambo ya ujenzi. Ilikuwa kambi ya ujenzi bila shaka. Lakini hii ikiwa na upekee wa tofauti na kambi ambazo alipata kuziona kule Tanzania. Humu kulikuwa na ofisi za kisasa kabisa kuonesha kuwa kulikuwa na harakati za kudumu ukiachilia mbali kazi za muda za ujenzi.

Koku alikabidhiwa chumba cha kulala kilichokidhi mahitaji yake yote, na Muta vivyo hivyo. Huduma zilitolewa kama ilivyostahiki familia ya kifalme hivi! Maswali yakawa ni mengi zaidi. Katika mjengo ule mlikuwa na chumba maalum kilichokuwa kimejaza vifaa taarifa vya kiinteligensia vya hali ya juu. Mawasiliano ya taasisi nyeti, na baadhi ya watu mahsusi waliokusudiwa, yalinaswa na kuhifadhiwa katika moja ya komputa kwenye kile chumba. Na si kwa Tanzania tu bali walinasa mawasiliano mbalimbali ya watu kusudiwa kokote kule duniani. Ilikuwa ni server(mtambo wa kuhifadhia data) moja makini sana. Watu wasiojulikana bila shaka walikuwa wamejipanga. Kitu ambacho Muta na nduguze hawakujua na kubaki kujiulizani nani aliyewezesha kundi hili kufanikisha mipango yao kimkakati namna vile?

‘Ndugu yangu Muta, sasa ni wakati mwafaka wa wewe kutoka kwenye ndoto za wavulana. Ni wakati mwafaka uingie kwenye ujana na utu uzima. Unaweza kuona ni kwa namna gani maisha yako ya kitoto yamepelekea hali aliyonayo baba yako. Ni wakati wa kuwajibikia makosa yako. Tutakuwepo hapa kwa siku tano hivi, halafu mimi na wewe, tutarejea kwa siri Tanzania. Huko tutakuwa na kazi moja tu. Kusambaratisha kundi la Mzee Kidevu. Ni kundi hovyo sana ambalo linajipanga kuongoza nchi yetu kinyonyaji na kiutumwa sana. Bila shaka umesikia mambo ambayo yamekuwa yanafanyika huko. Watu wanaonewa, uhuru wa watu umehujumiwa, wazalendo wanatekwa na watu wasiojulikana, ambao si sisi. Wakati inajulikana kabisa ni watu wa Kidevu na washirika wao walioko madarakani.. Kwa kijana anayejitambua, hali hii haikubaliki. Watu tulikuwa na kazi zetu nzuri tukizifanya kwa uadilifu kwa manufaa ya taifa, lakini tukatengenezewa zengwe tukafilisiwa na hata wengine kudhulumiwa uhai wetu. Hali hii haikubaliki. Haikubaliki hata kidogo, wafanyabiashara haramu, wakishirikiana na wanasiasa uchwara watunyamazishe kwa kauli za kinafiki kuonesha kuwa sisi ni wasaliti wao ndo wazalendo. Uzalendo ni kudhulumu haki za watu? Haki za wazee ambao wamelitumikia taifa kwa unyenyekevu na uzalendo mkubwa, leo wanaishia kupata maumivu na hata kufa kwa kutapeliwa mafao yao na watu wachache wanaodhani wao ndio wenye kustahili maisha kuliko hao wazee?

'Dhulma ilikofikia, inatuhitaji sisi vijana kufanya mabadiliko ya kimkakati kuzuia nchi yetu kutumika kama genge la wanyang’anyi. Haiwezekani kundi dogo la wafanyabiashara wahalifu wenye utajiri wa hila, utajiri unaotokana na dhulma, wawe na nguvu hadi ya kuamrisha serikali. Haiwezekani ndani ya nchi huru baadhi ya wananchi wageuke mabwanyenye kuwanyonya wenzao pasi na haki kutendeka. Kama serikali haifanyi kitu, sisi tunaojua kinachoendelea tukiamua kunyamaza, tutakuwa ni sehemu ya huo udhalimu. We must do something, be ready to face even death, ili wengi wapone. Tunahitaji kuwa kama Yesu, kufa kwa ajili ya wengi ikibidi.'

Maelezo ya Nondo yalimwingia vema. Ni kweli alikuwa na ndoto na mawazo ya kitoto. Haya aliyoyashuhudia kwa siku kadhaa yalimpa kujua nini maana ya kuwa mwanaume kama itumiwavyo kijamii ukiachana na ile ya kimaumbile. Kumbukumbu ya jinsi walivyotoka jela sasa ilijirejea kichwani mwake kama muvi ya kimarekani. Alipoambiwa anatakiwa kuingia kwenye mazoezi ya kiinteligensia na kivita, Muta akaridhia na kutia bidii. Baada ya kuiva kikamanda, Muta alikuwa habari nyingine. Alikuwa tayari kuingia uwanjani akikusudia kutubia dhambi zake kwa vitendo.

***

Simu aliyopokea usiku wa manane, ilikuwa bado inamsumbua kichwa chake kujaribu kutafsiri kila neno aliloulizwa. Ni kweli alikuwa anajulikana vema na kazi yake hasa ndo iliyomtambulisha vizuri katika jamii. Utetezi wa wanyonge. Naam. Yeye mwenyewe alikikubali cheo hicho kutokana na watu wengi kumuona hivyo na hata kumtambulisha kwa cheo hicho. Mtetezi wa wanyonge. Ukiachana na sifa hiyo ambayo ilitokana na kazi yake, lakini maandiko yake yenye wafuasi wengi kwenye mitandao ya facebook, instagram na hata tweeter, ilimfanya awe ni mtu mwenye kutazamwa na kufuatiliwa kwa karibu na ‘watu’ wa serikali, wanaharakati wenzake na watu wa upinzani. Tayari alikuwa ni jina kubwa lenye heshima kubwa nchini. Wakili wa kujitegemea, Paschal Kajumulo.

Mara nyingi alialikwa kwenye matamasha na makongamano ya kisomi katika vyuo mbalimbali nchini, kwenye mikutano ya taasisi mbalimbali za kiraia na maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Alikuwa ni mtu mwenye tajiriba ya pekee.

Usingizi uliokuwa umempitia ulimshawishi kukata simu ile kwa mara ya kwanza kisha akaendelea kulala. Mara baada ya kukatika simu ikaita tena mara ya pili, akaikata tena, mara hii akijiaminisha kuwa sasa mpigaji ataelewa kuwa alikuwa hahitaji usumbufu aina hiyo. Alivyoitua tu juu ya drawer la kitanda chake, ikaita tena. Safari hii wakili Kajumulo akaamua kuipokea japo kwa kughafilika kiasi.

‘Naomba upige asubuhi tafadhali” Kajumulo aliongea kabla ya kumsikiliza aliyekuwa anampigia. Shida ya kuwa maarufu ndiyo hio. Unakuwa mtumishi kama si mtumwa wa wale wanaokupa huo umaarufu.

‘Hapana wakili, hili ni la muhimu zaidi. Lazima iwe sasa?’ ilikuwa sauti laini ya kike, sauti nzuri kusikiliza. Wakili nae binadamu, alikuwa na udhaifu mkubwa hasa lilipokuja suala la warembo.

‘Oh, nani mwenzangu? Wakili alihoji, usingizi na shuka akivitupilia kule!

‘Maisha yako yapo kwenye hatari ndugu wakili na tupo kwenye mpango wa kuyaokoa!’

'Whuat?!’ wakili alihamaki.

Haikuwa mara ya kwanza kupokea vitisho vya aina hii. Kutokana na kazi yake, mara kadhaa alikuwa anakumbana na vitisho vya namna hii. Juzi tu alikuwa kapokea simu, iliyomtahadharisha dhidi ya kujihusisha na kesi ya mzee Muganyizi. Alipotafakari, akahisi huu ni mtego wa wale watoa vitisho wa juzi. Akilini mwake akajaribu kuona namna gani ya kujinasua. Moyoni mwake, tofauti na miaka mingine, akahisi hofu. Mapigo yake ya moyo yalikuwa yanaenda kasi.

‘Ndiyo Wakili, hii si vitisho vya wahanga wa kesi zako, la hasha. Upo kwenye hatari kubwa sana na sisi tungependa tuulinde uhai wako, kwani tunaamini uhai wako ni sehemu ya mapambano dhidi ya dhulma nchi hii.' Sauti ya mdada upande wa pili wa simu ilimalizikia kwa swali.

‘Tunapenda kujua upo upande gani wakili, wa dhulma au wa haki?’ swali hilo likawa ni suala tata sana kwa wakili Kajumulo. Hakujua anaongea na watu wa upande upi. Lakini kwa kutumia akili za kuzaliwa, alijua karata aliyokuwa nayo mkononi kwa wakati huo ni kuelekea upande wa hao watu walau ili apate muda wa kufanya chochote.

‘Nimekuelewa, napenda kujua mpango wenu!’ Kajumulo alijibu.

‘Uko upande gani ndugu Wakili?’ mwanadada yule aliuliza kwa msisitizo.

‘Msimamo wangu haujawahi kuyumbishwa, sijabadilika, huyu ni kajumlo mtetezi wa wanyonge. Hilo linafahamika. Kama wewe hujui sasa umejua. Sasa nieleze wewe ni upande upi? Wewe ni mwenzangu au uko upande gani hasa? Najua nina marafiki serikalini na uraiani, si kila mtu wa serikali au uraiani ana mtazamo sawa na wangu na si kila mtu kwenye pande hizo mbili yu kinyume changu. Wapo waovu kwa wema serikalini na uraiani. Upande wangu haujawahi kuwa serikalini au kundi fulani la watu, wala si upinzani. Upande wangu daima umekuwa ni haki!” Kajumulo sasa alikuwa anatapatapa, japo kuwa aliongea kwa sauti ambayo upande wa pili uliitafsiri kama kujiamini, ukweli ni kuwa Kajumulo alikuwa anatokwa na jasho jembamba la hofu asiyoijua.

‘Sawa wakili, sisi ni watu wasiojulikana tulioamua kuwa walinzi na watetezi wa wanyonge na taifa kwa umajumui wake. Kazi zetu hasa ni kuilinda nchi dhidi ya madhalimu wanaoihujumu nchi na kundi lao wanalobatiza jina eti 'watu wasiojulikana' ikiwa wanajijua vema kuwa ni baadhi ya watu ndani ya serikali kwa ufadhili wa kundi fulani la wafanyabiashara, ndio watekelezaji wa maovu husika.’

'Mpango uliopo hivi sasa ni kutekwa kwako na watu wasiojulikana, sasa, watu wasiojulikana wanaofahamika na wengi ni wale wanaoteka na kuwaua kikatili wanaharakati, wanasiasa wanaokinzana na serikali na hata watu maarufu walio tofauti na serikali, ikiwa ni njia dhalimu inayotumiwa na wafanyabiashara hao, kuifarakanisha serikali na raia. Miongoni mwao wapo baadhi ya polisi ambao wapo kwenye orodha ya malipo kutoka kwa wafanyabiashara hao. Polisi hao wamekuwa wakitumika kuwatangaza watu hao kuwa watu wasiojulikana, huku uchunguzi ukishindwa kubaini chochote kwa sababu wanakuwa wanajichunguza wenyewe. Na watu wasiojulikana wengine ndio sisi ambao nimeshakueleza kazi zetu. Una chaguzi mbili, kutekwa na watu wasiojulikana sisi au kutekwa na watu wasiojulikana wao. Kwa ufupi tu, kesi yako ya hivi majuzi iliyompa ushindi mheshimiwa Makulilo Mbunge wa upinzani ambaye amekuwa akiikosoa sana serikali ndiyo sababu ya kutekwa kwako.” Mwanadada yule sasa alikuwa anazungumza naye si kwa simu tena bali ana kwa ana. Haikuyumkinika kwa Kajumulo mwanadada huyo alimudu vipi kuingia ndani mwake na kuwepo muda wote sebuleni kwake na sasa akiwa kaingia kabisa chumbani kwake bila hata ya kuhisi chochote kitu kilichoashiria uvamizi.

Simu yake ya mkononi ilimdondoka kwa butwaa, na kwa haraka sana akanyanyua mikono yake juu. Dada yule mwenye kuvalia Burka iliyoufunika mwili wake vema yasionekane hata macho! Sasa alitoa sauti ya kiume hasaa. Sauti ya kikamanda.

‘Tunao muda mfupi sana Wakili, ni vema tuutumie vyema. Vitu, zikiwamo document zako muhimu ni vema tukazipakia tuondoke zetu” Kijana huyo wa kiume sasa alifunua burka yake ili Kajumulo apate kumuona huku akiwa yuko bize kukusanya vitu na electronics muhimu za Kajumulo. La haula, hakuwa mwingine, bali Nondo. Kijana ambaye miezi kadhaa nyuma alimkatalia huduma yake ya kumwakilisha katika kesi ya mauaji ya dhalimu Masebo na kukiri kuua kortini. Naam kijana ambaye alikuwa anasakwa na vyombo vya usalama kwa kutoroka mkono wa sheria na kutekeleza mauaji mengine ya askari magereza akishirikiana na kijana mwingine aitwaye Muta. Muta ambaye alikumbuka vema siku chache hapo awali, baba yake alimpigia simu na kumueleza habari za kutishiwa uhai wake huku uraiani na hata kabla ya kuingilia kesi yenyewe akakutana na habari gazetini, Mzee Muganyizi alikuwa katoweka hospitalini kwa kile kilichodaiwa rufaa ya kutibiwa huko nchini India.

Baada ya mazungumzo, Kajumulo akaomba muda wa kuyatafakari haya! Kesho ya usiku huo, Nondo alimweleza, angetekwa na watu wasiojulikana. Amekuwa akipiga kelele juu ya watu wasiojulikana na sasa wameamua kumteka yeye mwenyewe! Akamweleza ujio wake usiku huu, ni kwa sababu ya taarifa hizo za kutekwa kwake. Kwamba aliona kumuokoa, heri amfuate kabla hajafuatwa.

Alipotafakari sana, akaona ni heri kutekwa na watu wasiojulikana (upande wa Nondo) waliokuwa kinyume cha watu wasiojulikana!(upande wa mzee Kidevu)

Itaendelea....
 
KIKOKOTOO 08
DAVID NGOCHO SAMSON

Taarifa za watu kutekwa kwa siku za karibuni zilikuwa si habari mpya tena. Watu kadhaa walisemekana kupotea na baadae kuokotwa kwenye fukwe za pwani ya Dar es salaam wakiwa maiti ambao ama waliuwawa kwa kipigo au kwa kuzamishwa kikatili kwenye bahari ya hindi huku mikono yao ikiwa imefungwa nyuma na miguu pia ikiwa imefungwa kwa kamba. Watu hawa, walipookotwa, wengi hawakuripotiwa. Vyombo vya habari sasa viliripoti habari zenye mwelekeo wa kuifurahisha serikali tu, haikuyumkinika kwa nini iwe hivyo. Lakini, vyombo vya habari, vingi vikimilikiwa na wafanyabiashara ambao walikuwa sehemu ya genge hilo la mzee Kidevu, wasingeweza kujichonganisha kwa serikali, na walipoamua kuripoti, basi ilikuwa katika ama kuonesha uhusika wa serikali dhidi ya upinzani kwa lengo la kuchochea moto wa mifarakano au kujipendekeza kwa serikali ili kujiepusha na uchunguzi ambao ungebaini uhusika wao kwenye migogoro walioihandisi wenyewe. Maovu mengi yalifumbiwa macho na baadhi ya polisi, hasa waliokuwa kwenye orodha ya malipo kutoka kwenye genge la wafanyabiashara hao, ingawa walikuwa na jibu la matukio hayo, hawakusema.

Serikali haikuwajua wahusika. Hakuna uchunguzi uliobaini chanzo, sasa ilikuwa wazi kila tukio la hovyo na kihalifu, lilitekelezwa na 'watu wasiojulikana'. Hata pale waziri mwenye dhamana alipotakiwa kutoa maelezo, jibu lilikuwa ni hilo na sana sana alihisia kuwa huenda miili ile iliyookotwa ikiwa imeharibika ilikuwa ya maharamia wa Somalia waliotoswa huko baharini katika harakati zao za uharamia. Au maharamia wa kisomali bila shaka walitekeleza mauaji ya watu wasio na hatia na kuitosa miili yao baharini na mawimbi yakawaleta kwenye fukwe za Tanzania. Lakini licha ya taarifa hiyo kutoka kwa Waziri wa mambo ya ndani, ndugu Ayoub Mlacha, miili hiyo haikufanyiwa uchunguzi kwa sababu eti ilikuwa imeharibika vibaya. Bila shaka ilikuwa sababu tosha. Waziri na genge la wahalifu, walikuwa kundi moja na Kidevu. Watu hawa kwa makusudi walifanya hayo, huku wakifahamu wazi wanaichonganisha serikali na raia wake.

Licha ya mazoea hayo ya maovu na uhalifu usiokuwa na chanzo wala maelezo, taarifa ya kutekwa na kupotea katika mazingira yasiyoeleweka ya Wakili maarufu Paschal Kajumulo ilivuma pasipo kuvumishwa. Watu wa mzee Kidevu serikalini, kwenye taarifa hii walionekana kutilia maanani. Vitisho vingi vikamiminwa na wasemaji wa vyombo vya usalama. Zawadi zikatangazwa kwa yule ambaye angewezesha kupatikana kwa Wakili huyo na yule ambaye angetoa taarifa ya kuonekana kwake. Mitandaoni kukaenezwa propaganda, eti Kajumulo atakuwa anatafuta umaarufu hivyo anajaribu kujiteka na baadae akipatikana awe ametengeneza jina.

Propaganda hizo zikashadadiwa haswaa na wale vijana wa chama tawala ambao huenda kwa kutofahamu nini kinaendelea, walijikuta wakiwa kipaza sauti cha genge la mzee Kidevu. Wakasahau kuwa Kajumulo alikuwa wakili wa kujitegemea. Maarufu tayari, asiyehitaji kiki kujulikana.

Hali hiyo ikaushitua upinzani. Huyu Kajumulo, leo kawa rafiki wa polisi, kiasi cha kuwatia uchungu wamtafute kumuokoa kwa fedha za wavuja jasho! Lakini, wapinzani hao waliokuwa kifungoni, kifungo cha hofu, na labda kwa woga wa kupotezwa, wengi walikuwa kimya wasiweze kutoa maoni yao! Waliothubutu hapo awali walionja joto ya jiwe. Wakina Tuzo nduguye Gabby. Kwa sasa upinzani ulikuwa jina tu! Wapinzani machachari wote ama walikuwa korokoroni kwa kesi za kubumba, mateka kwenye kambi ya genge la mzee Kidevu au ahera wakibarizi kwenye fukwe za huko.

Bila upinzani madhubuti, genge la mzee Kidevu, halikuwa na shaka juu ya operesheni zao. Kwa sehemu kubwa walijiaminia sana fedha zao ambazo ziliwanyamazisha wapinzani na watu wa chama tawala, wakapitisha agenda za kundi hilo kwa kura nyingi za ndio. Kwa uwezo wao, ilifikia mahali, mzee Kidevu akapewa jina la utani, King Maker. Akiwa pia Ni mfadhili mkubwa wa chama Kikuu cha upinzani. Na kama tujuavyo sote, mbwa hata angekuwa mkali namna gani, haung'ati mkono unaomlisha.

***

Matukio yasiyo na majibu juu ya watu kutekwa na kupotea ambayo yaliichonganisha serikali na wananchi, hasa pale yalipohusishwa na siasa, yalimtia wasiwasi rais wa nchi Mheshimiwa Kassimu Kuliboja maarufu zaidi Kama KK. Akaitisha kikao cha Baraza la mawaziri. Alihitaji ufumbuzi wa kitendawili kile. Waziri wa mambo ya Ndani, Mheshimiwa Ayoub Mlacha alipaswa kuwajibika kulitolea suala hilo ufafanuzi.

Katika kujitetea, waziri huyo ambaye alitumikia kundi la mzee Kidevu, akajaribu kuwatwika wapinzani lawama. Ilikuwa ni njia rahisi zaidi waliyotumia watu hao. Mara zote, walijua kucheza na pande hizi mbili. Serikali dhidi ya upinzani, upinzani dhidi ya serikali.

'Mheshimiwa rais, hili suala limefanyiwa uchunguzi na jeshi la polisi. Vyama vya upinzani vinajaribu kufanya makusudi, kujiteka na kutangazia dunia kuwa serikali ndio inawateka…'

'Wanajiteka na kujiua kabisa kwa sababu hiyo? Kweli? Nadhani hata sasa waziri Ayoub umeshindwa kazi yako. Nilitegemea uje na majibu yenye maana na si hizi ngonjera zako za kila siku. Haiwezekani matukio haya yaendelee kutokea mara kwa mara na unacholeta kama utetezi hakina suluhu.' Rais Kassimu Kuliboja alizungumza kwa kwa ukali. Sifa mojawapo ya KK ni kwamba hakuvumilia uzembe wa makusudi na alikuwa mchunguzi wa mambo kabla ya kuamua.

Waziri Ayoub alikaa kimya baada ya kujitetea kwa mara nyingine akiomba muda zaidi kulimaliza jambo hilo. Kikao hicho kikaendelea, mikakati ikiweka jinsi ya kudhibiti mlipuko huo wa mauaji uliopewa jina 'watu wasiojulikana'. Wakakubaliana kuunda kikosi kazi ambacho kingelivalia njuga suala hilo na kulitokomeza kabisa. Waziri wa mambo ya ndani akapewa jukumu la kuunda kikosi kazi hicho kwa kushirikiana na IGP. Waziri Ayoub Mlacha akajikuta anatabasamu japo kwa kificho. Hofu kuwa angeondolewa kwenye nafasi yake ikiondoka kabisa.

Siku moja baada ya kikao cha Baraza la mawaziri, katibu mkuu kiongozi ikulu akaitisha mkutano na waandishi wa habari ikulu. Kulikuwa na teuzi mpya na mabadiliko kadhaa yaliyofanywa na Mheshimiwa rais KK. Jina la waziri wa Mambo ya ndani likatajwa. Aliyekuwa naibu wa wizara hiyo Mheshimiwa James Merkiad akatajwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo huku naibu wake akitajwa Mheshimiwa Galata Mhisa. Kijana mdogo ambaye alikuwa kaingia bungeni kwa mara ya kwanza. Ambacho wengi hawakujua ni kwamba Mheshimiwa Galata Mhisa alikuwa afisa mwandamizi wa idara nyeti ya usalama wa taifa na kuteuliwa kwake pia kulikuwa kwa kimkakati.

Siku kadhaa hapo nyuma, Galata Mhisa alikuwa kakutana ikulu na Rais Kassimu Kuliboja na moja ya mambo waliyozungumza ilikuwa taarifa ndefu aliyokuwa amemwandikia Mheshimiwa Rais kuhusiana na mambo ya wasiojulikana'. Ripoti ile ambayo ilikuwa imechambua vilivyo suala lile, iligusia uhusiano wa karibu uliokuwepo kati ya waziri Ayoub Mlacha na kiongozi wa genge la wafanyabiashara haramu, Rahul Baldevu ama muite mzee Kidevu. Ni taarifa hiyo iloyopelekea Rais kuitisha kikao cha mawaziri ili kuthaminisha taarifa zile dhidi ya Mlacha na hatimaye kufanya uteuzi mpya.

Baada ya uteuzi ule, Rais aliongea na Galata Mhisa kwa kina, na kumpa majukumu kadhaa nje ya ule mpango wa baraza la mawaziri. Jukumu la kufuatilia uendeshwaji wa genge la mzee Kidevu, hatimaye aje na mpango wa kulisambaratisha kabisa genge hilo.

***

Habari za kutumbuliwa kwa waziri Ayoub Mlacha, zilimfikia kama mshituko. Alikuwa amejiaminisha tayari kuwa nafasi yake angedumu nayo, na kwamba ingekuwa muda mwafaka wa kumzuga Mheshimiwa Rais kwa kukamata wapinzani kadhaa na kuwabambika makosa kadhaa, kama ambavyo waliamua kwenye kikao chao cha siri baada ya kikao cha Baraza la mawaziri.

Kwenye kikao hicho cha siri, waziri Ayoub Mlacha aliweka mipango yote ya Baraza la mawaziri mbele ya wajumbe wa kikao hicho cha genge chini ya mwenyekiti Rahul Baldev. Alipokwisha toa taarifa hiyo, wakasuka mpango mkakati uliokusudia kumwonesha Rais kuwa rai yao ya awali juu ya wapinzani kujiteka na kuteka watu ilikuwa ni rai ya kweli. Walikusudia kurejesha imani ya Rais Kassimu kwa waziri Ayoub Mlacha na safari hii wakikusudia kumfanya Rais ajisikie hatia kwa kumdhania hakuwa akifanya kazi yake vizuri. Hawakujua hawajui.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, aliwapa mpango mahsusi. Walikuwa watengeneze kambi ya uasi huko kwenye pori lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es salaam, eneo la mabwepande. Kungewekwa silaha za aina mbalimbali hapo kambini. Wangewachukua vijana wao na kuwavika fulana za chama kikuu cha upinzani. Hilo lingeambatana na kutekwa kwa viongozi kadhaa wa upinzani na kuwapeleka eneo la tukio. Ambacho kingefuatia, ingekuwa taarifa kamili ya upelelezi kupikwa ambayo ingeonesha kuwa kuna kambi huko porini. Katika kuonesha uhalisi wa mbinu yao hiyo, kijana machachari wa upinzani ambaye alikuwa ni mwandishi wa habari, aliyepata kutekwa miaka miwili hapo awali na kundi la Masebo na Kidevu, Tuzo, nduguye marehemu Gabby angepatikana akiwa hai katika kambi hiyo. Lakini pia, walikusudia awepo wakili maarufu Paschal Kajumulo. Ni wakili ambaye alionekana kuwa msumbufu kwao na hiyo ililenga kumdhoofisha na kummaliza kabisa nguvu katika kazi hiyo.

Wakati wanapanga mikakati hiyo, hawakujua kuwa tayari unga umezidi maji. KK alikwisha fanya mabadiliko na hata alipokuwa anatoa majukumu mapya kwa wizara ya Mambo ya ndani, alikuwa anayatoa kwa viongozi wapya.

Ayoub Mlacha akiwa kwenye safu ya viongozi wenzake kwenye ule mkutano na waandishi wa habari ikulu, akasikia Rais Kassimu akitamka jina la James Merkiad kama waziri wa wizara yake. James Merkiad ambaye alikuwa naibu wake. Macho yakamtoka wakati akijaribu kujishikiza vizuri kwenye kiti chake. Tumbo lilikata kwa mshituko mkubwa. Akajishikiza hapo kwa matumaini kuwa huenda alikuwa anabadilishiwa wizara.

Waandishi wa habari nao kwa kupenda kunusa nusa habari za kichonganishi, wakaelekeza kamera zao kwake. Alitia huruma. Hadi Rais Kassimu anamaliza kutangaza mabadiliko ya Baraza lake, jina la Ayoub Mlacha halikutajwa mahali. Hiyo ikiwa na maana kwamba, hakuwa waziri tena. Mbaya zaidi, Mheshimiwa Rais Kassimu aliendelea kuelezea uozo uliokuwa umeikumba wizara hiyo, mambo ya watu kutekwa na 'wasiojulikana' na kisha serikali kupata kashfa, akiwataka viongozi wateule wa wizara hiyo akiwamo katibu mpya wa wizara Ndugu Manuela Manguye, mwanamama ambaye KK aliweka rekodi yake ya utendaji mzuri kwenye kadamnasi hii, walivalie njuga na kuwatia hatiani wahalifu hao waliobatizwa jina na polisi 'watu wasiojulikana'.

Ilipomalizika hotuba ya Mheshimiwa Rais Kassimu Kuliboja, Ayoub Mlacha akionekana mwenye furaha ya kubandika, alijitutumua kuwapa mkono wa pongezi wateule wapya. Halafu akatafuta upenyo, akatoweka ikulu akikimbia maswali ya waandishi wa habari. Alikuwa kaaibishwa mno, na kwa sababu hiyo, alikusudia kulipa kisasi kikubwa kwa Rais Kassimu Kuliboja. Lakini alikuwa na uwezo huo?

Taarifa hiyo ya kuondolewa kwenye uwaziri, ilimfikia Rahul Baldev, mwenyekiti wa genge la wafanyabiashara wahalifu, wakawa wameweka kikao. Katika kikao hicho ambacho Ayoub Mlacha hakualikwa, wafanyabiashara wale waliamua kuachana na habari za Ayoub. Hawakuwa tayari kuunganishwa naye katika kile ambacho kilitangazwa na Mheshimiwa Rais kama uchunguzi dhidi ya waziri huyo wa zamani. Lakini, hata hivyo ilikuwa wamechelewa. Tayari uhusiano wao na waziri huyo wa zamani ulikwishajulikana. Kilichotokea ikiwa ni matokeo ya uhusiano wao.

Ayoub Mlacha akajikuta njia panda. Akipoteza nafasi ya uwaziri, lakini pia wafanyabiashara wale wakimuondoa kwenye orodha yao ya malipo na kumtenga kabisa. Hawa hawakukomea hapo, biashara zake alizoanzisha kwa majina bandia walizichukua wakidai wanafidia hasara ya kukatisha mkataba ghafla. Yaani ikiwa na maana kuwa, makubaliano ya yeye kuwa sehemu ya kundi lile ilishikiliwa na nafasi yake ya uwaziri. Bila uwaziri hawakumhitaji. Ayoub Mlacha akafilisiwa mali zake kidhalimu na genge la mzee Kidevu huku pia akionywa kukaa kimya na kutishiwa maisha endapo taarifa zao zingevujishwa kwa watu wa serikali. Akajikuta kifungoni. Kifungo cha uhuru wake, akiwa amedhalilika vya kutosha.

Akiwa ameondoka kwenye nyumba ya waziri, Ayoub Mlacha akarejea nyumbani kwake yeye na familia yake. Huko pia akakutana na mambo ya ajabu. Alikuwa kawekewa ulinzi wa watu kutoka kundi la mzee Kidevu. Si hivyo tu, pia camera za CCTV zilitandazwa hadi chumbani na bafuni kwake. Aibu gani hiyo? Akatafakari sana. Maisha ya familia yake yawe kitabu wazi kwa watu wasiojulikana?' Akioga wamuone, akiwa kwenye faragha na mkewe wamuone. Udhalilishaji gani huo!.

Ayoub Mlacha akaamua kujiepusha na hali hiyo. Akamweleza mkewe kuwa anatoka. Akachukua gari lake na kuingia barabarani. Akaendesha gari hilo kwa mwendo wa hatari. Akikusudia kujimaliza kwa ajali. Naam, Kesho yake, taarifa ya kifo cha aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani Mheshimiwa Ayoub Mlacha, ikaripotiwa na vyombo vya habari kote nchini. Kifo hicho kilitokana na mwendo kasi ambao baadaye ulimshinda nguvu. Akaondoka na Raia mmoja aliyekumbwa na ajali ya kugongwa kwa gari lake. Hata hivyo, habari za mpita njia huyo, wala hazikuripotiwa, aliripotiwa waziri pekee. Hayo ndio mambo ya waandishi na waandikiwa. Hawana haja na taarifa za watu wasio na umaarufu. Habari, sharti iwe ya mtu maarufu, ikimhusu mtu wa kawaida, basi iwe ya majanga yanayoondoka na maelfu ya watu.

Habari ya kupotea kwa Mlacha ilikuwa njema kwa mzee Kidevu na genge lake. Hicho ndicho kitu walichokitaka watu wa mzee Kidevu. Hawakuwa salama kama mtu mwenye siri zao, alikuwa huru nje ya genge lao. Ingewagharimu pakubwa. Walikuwa na uzoefu na hilo. Na hasa hasa akiwa ni mwanasiasa, wao waliwaita wanasiasa kuwa ni 'malaya'. Hawakuwaamini malaya. Malaya hawakawii kubadili mabwana na kumweka uchi bwana wa zamani ili kumkoga bwana mpya.

Familia ya Mlacha ikiwa kwenye maombolezo ya kuondokewa na mpendwa wao, ikafikwa na ugeni. Wageni hao walikuwa wamevalia mavazi maalumu ya kazi, maovaroli marefu yenye chata mgongoni, One to ten company limited. Watu hao wakawaeleza walipigiwa simu na marehemu siku moja kabla ya kifo chake akiwataka waje kuondoa mfumo wa ulinzi wa CCTV cameras pamoja na wale walinzi wapya waliowakuta hapo nyumbani. Wakafanya hivyo. Wakaondoa ulinzi wao pamoja na makamera nyumbani kwa marehemu. Waziri huyo wa zamani akazikwa na habari zake zikasahaulika. Msiba huo ukiwa umehudhuriwa na watu halaiki kubwa. Bila shaka Ayoub Mlacha alikuwa mtu wa watu.

Itaendelea....
 
Watu mnasoma kimyakimya Sana jamani. Semeni neno wandugu!
 
KIKOKOTOO 09
DAVID NGOCHO SAMSON

Mzee Muganyizi afya yake iliimarika sasa. Madaktari walifanya kazi kubwa kumsaidia na sasa kulikuwa na matumaini ya kupona vema kabisa. Hapa alikuwa na bintiye Koku wakifanya mazoezi ya kutembea kwenye mitaa ya jiji la Johannesburg. Mzee Muganyizi akaona huo ni wasaa muafaka kuweza kumshukuru bintiye kwa kuweza kumtafutia tiba nje ya nchi. Ilionekana kwamba mzee Muganyizi hakuwa na kumbukumbu ya nini hasa kilitokea hadi kufikia hapo walipo. Wataalamu huita hali hiyo, partial amnesia. Kusahau mambo kadha wa kadha hasa baada ya ajali. Lakini sasa kidogo kidogo fahamu zake zilikuwa zinamrejea.

'Asante sana mwanangu Koku kwa kunisaidia matibabu. Umevaa viatu vya kaka zako na umefanya jambo kubwa sana. Nasikitika nimekuingiza kwenye madeni ambayo huenda utayatumikia kwa muda mrefu sana. Kwa hilo mwanangu, msamehe bure baba yako.' alizungumza mzee Muganyizi, akainua macho amtazame binti yake. Alikuwa analia, machozi yakimtiririka shavuni Koku.

'Oh, mwanangu nimekukosea sana najua. Ni gharama kubwa, Siwezi jua umezipataje hizo fedha lakini kama kuna namna ilikulazimu ku….'

'Hapana baba, nalia kwa furaha napokuona ukiwa umerejea katika afya njema. Asante kwa kurudi. Unajua umekaa kwenye 'coma' kwa muda gani? Miezi mitatu. Ninayo furaha sana kukuona ukizungumza nami tukijibizana. Miezi mitatu awali nilikuwa nazungumza nawe hunijibu. Asante sana Mungu kwa kutenda muujiza huu' Koku aliongea akamalizia kwa kuonesha ishara ya msalaba.

'Kuhusu gharama na matibabu yako, kusema kweli mimi sijui chochote. Nachojua ni kwamba, Muta na kijana mmoja aitwaye Nondo ndio wamefanya mipango ya matibabu yako.'

'Muta alishatoka jela?'

'Hakutoka, alitoroka.'

'Hivi ni kusema anasakwa na polisi?'

'Si yeye pekee. Sote tunasakwa na polisi. Alipofanikiwa kutoroka jela, alikuja hospitalini ulikokuwa umelazwa nikikuuguza, kwa bahati mbaya sana nilikuwa nimesoma mtandaoni juu ya mauaji ya Askari magereza na niliposoma kuwa Muta anahusishwa na mauaji hayo, picha yake ikiwa ukurasa wa mbele wa habari ile, nilizimia. Lakini kwa vile nilikuwa hospitalini madaktari walinihudumia haraka na kuniondoa kwenye hatari. Siku moja baadaye, ulinzi ukiwa umeongezwa kufuatia habari ile, nilishangaa Muta na huyo kijana Nondo wakiingia wodini na kunichukua. Nilifuatana nao tukaingia kwenye ambulance na wewe ukiwamo ndani ya ambulance ile, gari likaondolewa hadi nje ya hospitali ambako kulikuwa na ndege binafsi ikitungojea. Tulipanda humo na kuletwa huku. Hicho ndio kitu kilichotokea.' Koku alimweleza baba yake.

'Oh maskini wanangu nimewaangusha sana. Sasa hamwezi kuishi hata kwa amani nchini mwenu na mmelazimika kuwa wakimbizi.'

'Usiseme hivyo baba, hujatuangusha kwa lolote. Umewajibika kwa kadri ulivyoweza. Ni bahati mbaya sana kuwa haya yametokea, lakini si kwamba umeyasababisha wewe. Kitu ambacho tunapaswa kufanya ni kumshukuru Mungu kwa uhai na kwa afya njema.'

'Naam, Sasa Muta yuko wapi na huyo Nondo? Maana natamani kweli niwaambie Asante kwa kuniwezesha kupona.'

'Kwa sasa wamerejea Tanzania. Wameapa kuwashughulikia wale matapeli waliopora mafao yako na kukusababishia hali ile.'

'Oh maskini mwanangu. Kisasi hakijawahi kuleta ridhiko zaidi ya majuto zaidi. Kama watu wamejiweka karibu na polisi, atawawajibisha namna gani? Mungu awasaidie.'

'Amina baba, Mungu atakuwa upande wao.' Koku alimweleza baba yake, na sasa walikuwa jirani kabisa na kambi ile waliyoishi ndani yake. Kwa mara ya kwanza waligundua maandishi yaliyokuwa nje ya fensi ya kambi ile jirani na geti kubwa la kuingia ndani. RuBya Group of companies.

Walipokuwa wanaingia getini walishangaa kuona mabadiliko makubwa yamefanyika ndani ya Muda mfupi waliotoka kwenda mazoezini. Kulikuwa na kila dalili kuwa kungefanyika tafrija humo ndani kwani ilisemekana wakurugenzi wa makampuni walikuwa na kikao cha nusu mwaka katika eneo hilo.

Walichogundua baadaye ni kwamba hapo palikuwa ni makao makuu ya RuBya Group of companies kwa upande wa Afrika. Makao makuu ya RuBya kimataifa yakiwa nchini China huko Shanghai. Makampuni ya RuBya yalijihusisha zaidi na ujenzi wa majengo hasa maghorofa marefu, barabara na miundombinu mingine kama mabwawa ya uzalishaji umeme na kadhalika. Ni makampuni ambayo yalikuwa na sifa za utendaji kazi bora kiasi cha kuaminiwa na serikali nyingi mwenye miradi mikubwa ya kitaifa.

Koku na baba yake hawakuwa na uhusika wowote na hayo, hivyo walijongea taratibu na kwenda kwenye nyumba waliyokabidhiwa mle ndani.

'Hili kampuni ndio limefadhili matibabu yangu sivyo?' Muganyizi akamuuliza bintiye.

'Sina hakika, lakini bila shaka wamefadhili makazi na chakula. Si unaona kila siku tunahudumiwa na wafanyakazi wa kampuni?'

'Unaonaje tukatumia muda huu kuwaambia hao wakurugenzi Asante?'

'Ni jambo jema, lakini tutakuwa hatujawatendea haki Muta na Nondo. Wao ndio waliojua namna ya kupata ufadhili huu. Wao ndio wanaostahili kutuongoza kwenye kutoa shukrani zetu. Tuvute subira kwanza warejee, halafu tutayafanya haya.'

'Umeongea hoja kubwa mwanangu. Hebu tuvute subira kwanza.'

'Asante kwa kunielewa baba.' Koki alimweleza babaye.

***

Galata Mhisa alikuwa kwenye ofisi yake mpya ya naibu waziri. Leo alikuwa anakabidhiwa majukumu yake ya ofisi hiyo. Alikuwa mwingi wa bashasha, na tabasamu lilionekana kutamalaki midomoni mwake kila wakati. Alikuwa ameaminiwa na Mheshimiwa Rais kushika wadhifa huu mkubwa akiwa bado kijana tena ikiwa ni mara tu baada ya kuingia bungeni kwa mara ya kwanza. Alijihisi mwenye bahati kubwa sana. Alikusudia kuitendea haki nafasi hiyo ili asimwangushe Mheshimiwa Rais kiutendaji.

Minong'ono ilikuwa imeshaanza kuenea nchini juu ya uzoefu wake. Wengi wakidhani Mheshimiwa Rais Kassimu alifanya uamuzi hovyo wa kumteua kijana huyo mdogo ambaye hana uzoefu wowote kama mbunge seuze unaibu waziri. Lakini walipohoji juu ya uzoefu wake naibu waziri, walionekana kushadadia sana uteuzi wa James Merkiad kwa nafasi ya waziri wa mambo ya ndani akirithi kiti cha Ayoub Mlacha. Kwa mtu mwenye jicho la tatu, angeweza kuona namna media walivyokuwa wakijenga uhasama kati ya viongozi hao wawili hata kabla ya kuanza Kazi zao.

Walikosea mno!

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa nao hawakusalia nyuma. Walikuwa mstari wa mbele kuhakikisha tabiri zao hatimaye zinakuwa sahihi kwa kuandika tabiri zao za namna ofisi hiyo ingelimshinda kijana huyo. Galata Mhisa.

'Galata Mhisa ni nani?' liliandika gazeti la siasa zetu, ukurasa wa mbele wa gazeti hilo ukipambwa na sura yenye tabasamu ya Mheshimiwa naibu waziri huyo. Kwenye kurasa za ndani mchambuzi aliyejiita Jerry Prenge, hakuandika cha maana zaidi ya kufukua historia binafsi ya maisha ya kijana huyo akiwa mdogo. Historia ya kulelewa kituo cha watoto yatima akiwa hamjui mzazi wake ni nani? Katika kujaribu kuonesha dosari ya uteuzi wake, mwandishi akatoa mifano kadhaa ambayo ilionesha ni namna gani watu waliotokea mazingira kama aliyokulia Galata Mhisa wanavyokuwa mbali na mambo ya kijamii, wenye kujitenga, wenye uchungu mwingi, ubinafsi uliopitiliza, kutokujali na kujikinai. Akamaliza kwa swali, 'je huyu atakuwa na upekee gani? Hatatuangusha kwa sababu hizo tajwa? Yetu macho!'.

Lakini mwandishi huyu bila shaka alisahau kabisa kuwa madhaifu hayo walipachikwa watoto hao, sio kweli kuwa walijitenga bali walitengwa, hawakuwa mbali na jamii, jamii Ilikuwa mbali nao, eti wabinafsi? La hasha, walijua kujitegemea baada ya jamii kukataa wasiitegemee, hawakujali na kujikinai? Ah, uongo tu. Wao walithamini zawadi ya uhai waliopewa, walikuwa tayari kuulinda kwa gharama yoyote ikiwamo kuuhatarisha uhai huo. Hata hivyo, kwa naibu waziri Galata Mhisa, hayo yote wala hayakuendana na haiba yake. Kituo alicholelewa baada ya kutengwa na wazazi na jamii nyingine, kilimpa tumaini jipya, kilimfundisha kuwa, walimwengu wana mengi. Hakupaswa kuzingatia mabaya bali mema. Naye, aliwekeza kwenye mema. Alikuwa mwema.

'Aliokotwa kwenye kikapu nje ya kanisa la kilokole, mtu ambaye alikataliwa na mama yake mzazi, Si ajabu kuwa hata waumini wale na mchungaji wao mtakatifu waliona itakuwa dhambi kumfadhili, wakaamua kuitupia serikali ya kijiji mzigo wake. Serikali hiyo nayo haikumtaka, wakamkabidhi kwenye kituo cha watoto yatima. Huyu ambaye tangu kuzaliwa alikataliwa na jamii kumpa nafasi hiyo ni sawa na kumpa uwanja wa kulipiza kisasi.' gazeti lilizidi kumchambua naibu waziri Galata Mhisa

'Wanasaikolojia wameshatueleza, ni mara chache sana ukakuta watoto wa sampuli yake kuwa watu wazima wenye kuleta tija.

'Alipokuwa shule ya msingi, Galata alikuwa nunda, asiyeongea kwa maneno bali vitendo. Vitendo vyake navyo vilikuwa ni ukatili mtupu. Kumbukumbu zinasema, aliwahi kumgomea mwalimu wake adhabu na alikuwa tayari kufukuzwa shule. Hakuwa na heshima. Huyo ndio leo kakabidhiwa dhamana ya kuongoza wizara nyeti. Wizara ambayo jeshi la polisi lipo chini yake. Wacha tuone cheche zake…' mwandishi aliendelea kutiririka kwa makala iliyolenga kuuaminisha umma kwamba mtu huyo Galata Mhisa kwa historia ya utoto wake, lilikuwa kosa kubwa kumkabidhi nafasi ya uwaziri.

Mwandishi huyo aliyeandika kwa kina taarifa hizo, aliegamia upande mmoja tu wa mabaya ya Mheshimiwa Galata, tena mabaya yenyewe hayakuwa mabaya. Mwandishi hakujishugulisha kutaka kujua kwa nini aligomea adhabu na kwa nini alikuwa mkimya na kulazimika kufanya vitendo kama alivyoelezea mwandishi huyo.

Hakueleza ukweli kwamba, Galata Mhisa hakupenda kuona haki haitendeki tangu yu mtoto. Kwamba hata kugomea adhabu, Ilikuwa kwa sababu mwalimu hakutenda haki na alikusudia kumwadhibu kwa uonezi. Mtu ambaye hakujua kujipendekeza, mtu ambaye alisimama upande wa haki, mtu ambaye hakujua maneno mengi yasiyo na maana, vipi misimamo hiyo madhubuti iwe dhana ya kumuita hafai? Galata Mhisa alishangazwa na akili duni ya mwandishi. Kwa sifa hizo, alidhani alifaa zaidi kuwa kiongozi na si kinyume chake.

Walikuwa wanakosea sana.

Kudhani hayo yote yangekuwa kikwazo. Hawakujiuliza ni namna gani alivyomudu kufikia kiwango hicho. Hawakujiuliza kama alikuwa na uwezo gani wala hawakuweza kutabiri angeleta mabadiliko gani. Asiyejua maana haambiwi maana! Galata Mhisa alikuwa kwenye nafasi aliyostahili. Mpuuzi alikuwa yule ambaye aliona sawa kumhukumu mtu kwa kutumia historia ya zamani. Kwa maana ni mpuuzi pekee anayeweza kudhani watu hawakui, hawabadiliki na wanabaki kuwa walivyokuwa watoto hata wanapoonekana kuwa si watoto tena.

Aliketi kwenye kiti na kuanza kupitia taarifa moja baada ya nyingine. Baadaye akaona heri kupata taarifa kamili na maelezo toshelevu kutoka kwa wahusika. Akaitisha kikao na IGP, kamishina wa uhamiaji na DPP. Wakazungumza mengi na kuweka mikakati sawa. Baadaye jioni, Galata Mhisa akakutana na kijana mwenzie, mtu ambaye walishirikiana vema kwenye ile kazi ya usalama wa taifa. Kiberenge wa Lwikondo.

Kiberenge wa Lwikondo, alikuwa kijana shababi, mstaarabu kwa haiba yake. Sukari ya warembo. Alikuwa mtanashati hasaa. Uzuri wa haiba yake, ni kuwa Lwikondo alikuwa kinyonga awezaye kujibadili kufuatana na mazingira aliyomo. Hata ilikuwa kwamba kwenye kazi yao hii, alikuwa kiraka kilichofaa kuziba pengo aina yoyote. Alipoamua kuwa mwalimu, Lwikondo alikuwa mwalimu kwa kila hali na wanafunzi wake walifaulu vema mitihani yao. Alipoamua kuwa mwanasheria, hata mwenye hatia aliukwaa ushindi asiamini. Alipojifanya mfanyabiashara, Lwikondo alikuwa kibopa kweli kweli.

Lwikondo akamdokezea Naibu waziri mabadiliko ndani ya genge la mzee Kidevu dhidi ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani na jinsi ilivyopelekea kifo chake. Kiberenge wa Lwikondo aliyajua hayo maana kama ilivyokuwa kwa wafanyabiashara, na yeye alikuwa mfanyabiashara ambaye alichomekwa kwenye kundi lile kama mtu wa mfumo. Katika mkutano huu, Galata Mhisa pia alitambua njama ya kuwindwa na genge hilo awe mtu wao kama ilivyokuwa kwa Ayoub Mlacha. Galata Mhisa akatabasamu. Walipaswa kufanya jambo. Wakaweka mikakati yao sawa.

'Haha, nakukaribisha sana kundini komredi, uwe kitendea kazi chetu kama ilivyokuwa kwa marehemu!' Lwikondo alimweleza Mhisa.

'Hahaha, halafu mkiona siwafai mnipoteze kama mlivyomfanyia Mlacha? Mimi mshahara wangu unanitosha kamaradi.'

'Haha, hataki utajiri huyu. Ila sasa, ni vema kuweka idara zote chini ya wizara yako kwenye mstari nyoofu. Maana kitachofanyika wala si miujiza. Ni pesa tu.'

'Unataka kunambia niongeze mishahara ndio wasichukue rushwa? Haha, miaka nenda rudi binadamu hajawahi kuridhika na pesa iwe nyingi au chache. Ila.. Naam, nimepata wazo jinsi ya kulishughulikia hilo'

'Wazo gani?'

'Unanifahamu zaidi ya hivyo. Napenda zaidi kuzungumza kwa vitendo. Mapema sana utaona hilo wazo. Nambie, Nancy mzima?'

'Hajambo, keshajifungua!'

'Na hukutaka nijue kwa nini?'

'Nilitaka ujue, sema umekuja kikazi zaidi. Dume limeingia mjini. Jina lake aitwa Nelson Madiba.'

'Hahaha dah, Madiba karejea kivingine.'

'Noma'

'N'ifikishie hongera zangu kwa Nancy, mwambie nimem-misi sana. Na bwana mdogo Madiba, nitatafuta muda nije kumsabahi!'

'Hakuna shida Mheshimiwa Naibu Waziri, wizara ya Mambo ya ndani. Salute kwako mzee baba.' Lwikondo alizungumza kwa tabasamu na kumaliza kwa kutoa salute. Mheshimiwa Galata Mhisa akabaki anatabasamu tu kwa furaha. Wakaagana.

Kikao cha pili, Mheshimiwa Galata Mhisa aliketi na kamishina wa TRA pamoja na kamishina wa Taasisi ya kupambana na rushwa. Akawapa maelekezo mahsusi.

Mheshimiwa John Magesa, aliingia ofisini kwa Naibu waziri mapema kama walivyokubaliana na Naibu Waziri kwenye simu. John Magesa ndio alikuwa kamishina wa TRA.

'Karibu sana kiongozi, habari za asubuhi?' Galata Mhisa alimkaribisha kwa bashasha huku wakishikana mkono.

'Asante Sana mkuu. Nikasema niwahi sana iwezekanavyo maana walishasema wahenga, mwitikio wa kwanza hudumu zaidi, nami sikutaka nikujengee mwitikio hasi hata kidogo.'

'Hahahah, bwana John una maneno wewe. Karibu sana ndugu yangu. Nimefurahishwa na jinsi ambavyo umenipa heshima hiyo.'

'Naam, ndivyo ipaswavyo kuwa. Nitumie nafasi hii kabisa kukupongeza sana Mheshimiwa Galata kwa kuaminiwa na Rais kwa nafasi hii adhimu. Hongera sana ndugu yangu.' Magesa aliongea huku akiukabidhi mkono wake wa pongezi kwa kijana huyo.

'Nashukuru sana. Ni matumaini yangu kuwa kwa ushirikiano kati yangu na idara yako kaka John, tutamuonesha Rais na umma kwa ujumla kwamba hayajafanyika makosa kwa teuzi zetu.'

'Hakika. Nakuhakikishia ushirikiano wa kutosha Mheshimiwa'

'Asante Sana. Kaka John nimekuita kwa sababu nataka unisaidie katika kukitegua kitendawili cha wasiojulikana'.

Wasiojulikana na TRA, hii ni very interesting. Magesa aliwaza.

'Naam Mheshimiwa, nakusikiliza.'

'Uchunguzi wangu umenionesha kundi hilo la wasiojulikana actually ni watu wanaojulikana kabisa. Ni kundi dogo la watu ambao wana nguvu kubwa kiuchumi. Wafanyabiashara mashuhuri na wenye majina. Nataka upitie taarifa zao ili tuweze kujua kama kuna namna wanakwepa kodi na kama ndiyo, hiyo ndio njia pekee ya kuweza kulisambaratisha kabisa genge hilo. Ninayo majina hapa. Tafadhali sana usije kushawishika na fedha zao, maana wao kuhonga sio suala gumu. Na tayari ninawawinda kwenye upande huo. Kama utashawishiwa kwa rushwa, basi uwe mzalendo katika kuhakikisha tunawakuta hao wapuuzi na hatia ya kujaribu kutoa rushwa.' Naibu Waziri Galata Mhisa alizungumza huku akitoa bahasha kwenye drawer la meza na kumkabidhi kamishina Magesa.

'Nikuhakikishie tu ndugu waziri, habari hii imefika sehemu salama nami nitatekeleza kama ulivyoelekeza. Hongera sana. Kwa namna hii, hili kundi litasambaratika mapema kabisa. Naamini kuna kitu alikiona Mheshimiwa Rais kukukabidhi ofisi hii.'

'Usinambie na wewe ulikuwa umeshawishiwa na makala za mahasimu wangu?'

'Haha, kiduchu tu' Magesa alizungumza na wote wakacheka na halafu wakaagana.

Alipokuwa anatoka mle ofisini, kamishina Magesa akakutana na kamishina wa Taasisi ya kupambana na rushwa, Mheshimiwa Sebastian Komba. Wakasabahiana halafu kila mmoja akashika hamsini zake. Magesa akatikisa kichwa kwa kukubali kwamba Mheshimiwa Galata Mhisa alikuwa amejipanga. Na mikakati yake bila shaka ilikuwa makini.

Mambo yalikuwa yanajipanga kama alivyoyakusudia Mheshimiwa Galata. Wiki mbili baadaye, taarifa ya TRA ikaonesha ukwepaji kodi na uingizwaji wa bidhaa nchini kwa njia za magendo kulikofanywa na kampuni ya One to ten, kampuni iliyomilikiwa na Rahul Baldev, ukipenda muite mzee Kidevu. Ikiwa kesi hiyo ni ya moto, Kidevu akaitwa mahakamani kwa tuhuma za ukwepaji kodi. Akajua mambo ni rahisi kama ilivyokuwa awali. Akachukua mamilioni na kumhonga mwanasheria wa serikali na nyingine kwa hakimu. Haikuishia hapo, akahonga mamilioni kwa afisa aliyekuwa anaendesha kesi. Hakujua ni mtego. Hamadi, afisa wa Taasisi ya kupambana na rushwa akawachukua video ya ushahidi katika matukio yote matatu. Hakimu, mwanasheria na afisa mashitaka wakauingia mkenge. Ushahidi wa video wakipokea rushwa. Galata Mhisa alikusudia kutoa fundisho kwa Taasisi hizo ambazo ziko chini ya wizara yake kuwa mambo yamebadilika.

Haikuwa imeishia kwa Rahul Baldev pekee, kila mfanyabiashara kwenye orodha ya Naibu Waziri, alikuwa aidha anasota rumande kwa makosa ya uhujumu uchumi au alikuwa tayari kapandishwa kizimbani kujibu tuhuma husika. Wakati hayo yakishika hatamu, tayari IGP alikuwa ameweka makachero wake kufuatilia watu wa kazi wa genge la mzee Kidevu.

Itaendelea....
 
KIKOKOTOO 10
DAVID NGOCHO SAMSON

Habari za uteuzi mpya wa waziri wa mambo ya ndani, Nondo na Muta walizipata wakiwa kwenye harakati kujipanga kufilisi makampuni ya mzee Kidevu na washirika wao. Hiyo ndio njia waliyokuwa wameona ni sahihi kwa lengo la kulipiza kisasi kwa kifo cha baba yake Nondo na dhulma ya pesa za baba yake Muta. Habari hizo zikawafanya wasitishe mpango wao kwanza kwa nia ya kuona nini ulikuwa mwelekeo wa uongozi mpya wa wizara dhidi ya wasiojulikana hasa baada ya kuisikiliza ile hotuba ya Mheshimiwa Rais KK.

Katika kujipanga upya, wakaamua kurejea nchini Africa ya Kusini kutoa nafasi walau ya miezi miwili kuona nini serikali ilikusudia.

Wakiwa Africa ya Kusini, wakapata habari za kukamatwa kwa kundi la mzee Kidevu, kundi ambalo walikuwa wanaliwinda. Nondo akashituka.

Hey, Ina maana Kumbe wale watu walikuwa genge na walishirikiana na baadhi ya watu serikalini? Akazidi kuwaza. Katika Mawazo yake hapo awali, Nondo alidhani hawa walikuwa ni watu ambao walitumiwa na serikali katika kunyanyasa raia na hata wapinzani.

Alikuwa amekosea sana.

Sasa kulimpambazukia kuwa alikuwa akiwaza tofauti kabisa na ukweli wa mambo. Uteuzi mpya na kutumbuliwa kwa marehemu Mlacha, kulionesha nini hasa kilikuwa kikifanyika serikalini.

Nondo akaamua kuwekeza nguvu zake kwingine. Aliamua kuwaachia jeshi la polisi kazi ya kupambana na wahalifu. Lakini hata hivyo, akikusudia kuwapima kama kweli walikuwa wapo kwenye vita hiyo kindakindaki.

Akaandika waraka mrefu sana wa barua, akauambatanisha kwenye barua pepe yake kwa naibu Waziri Galata Mhisa. Kwenye waraka huo, alionesha namna gani wastaafu kadhaa wamekufa katika kuonewa na genge la marehemu Pedezyee Sebo na mrithi wake Rahul Baldev. Akamweleza wapi walikohifadhi pesa hizo, na jinsi ulinzi ulivyoimarishwa hapo. Akawataja viongozi wa kimafia wa kundi hilo, Aidan na watu wake. Lakini pia akaorodhesha orodha ndefu ya baadhi ya maaskari wenye vyeo vikubwa kwenye jeshi hilo ambao walishirikiana kwa karibu na genge la mzee Kidevu. Akautuma waraka huo na kujipatia muda wa miezi miwili ili kuona matokeo ya kazi yake. Uzuri ni kuwa Nondo alimfahamu Naibu Waziri Kama mtu wa mfumo. Angehakikisha anafanya uchunguzi kwanza na baada ya hapo bila shaka angechukua hatua stahiki.

Naibu waziri Galata Mhisa hakumwangusha. Ndani ya mwezi mmoja tu alianzisha operesheni Loan sharks, mabwanyenye hao waliokuwa kwenye orodha ndefu aliyoandika Nondo, wakatiwa nguvuni. Walikuwa na mali mengi bila vyanzo vya kueleweka walikozipata. Wakapewa shutuma ya uhujumu uchumi. Habari hizo zikamfikia Buda Nondo. Nondo akajua sasa ni muda mwafaka wa kufanya mchezo wa Robinhood. Akarejea tena nchini. Safari hii akiwa na Muta ambaye alikwisha kwiva kikamanda.

***

Habari za operesheni loan sharks zilipokelewa vema na wananchi. Wengi wakajitokeza barabarani kwa maandamano ya kumpongeza naibu waziri Galata Mhisa. Kila Kona ya nchi makongamano yalisikika. Nini? Kumshukuru Mungu kwa ajili ya serikali makini ya Rais Kassimu Kuliboja. Hata hivyo ilijulikana kuwa ni wizara ya Mambo ya ndani hasa iliyokuwa ikizungumziwa.

***

Udhaifu wa binadamu upo katika ubinafsi na kupenda kuonekana bora zaidi ya wengine. Haikuwa katika mipango yake naibu waziri Galata Mhisa kutengeneza jina na sifa nyingi. Hata hivyo uwajibikaji wake na kismati chake kiling'aa na kumtangaza kote nchini kwa kazi zake makini. Kwa vyovyote vile, kampeini za kusifia kazi za Naibu waziri Galata Mhisa, zilishika kasi na ghafla likawa ni jina lenye kusikika zaidi nchini na ndani ya serikali. Yeyote aliyeanzisha kampeini hizo, aidha alijua anafanya nini au alikuwa na nia safi kabisa. Hata hivyo, nia yake hiyo ilizidi kumtengenezea naibu waziri Galata Mhisa wapinzani na maadui lukuki.

Katika ofisi yake, alianza kuona mabadiliko ya kimahusiano kati yake na mkuu wake kicheo. Waziri James Merkiad alikuwa na kijiba cha roho dhidi yake. Waziri huyo, hakupendezewa na sifa kibao zilizomwangukia na hata jinsi ambavyo alisikilizwa zaidi juu ya Mambo ya wizara hiyo na Mheshimiwa Rais kuliko alivyosikilizwa yeye. Akajenga chuki. Akataka kumwangushia jumba kwa kadri ya sifa alizokuwa nazo. James Merkiad, chuki binafsi ikamkutanisha na mwandishi wa habari, ambaye alitumika vibaya na genge la wafanyabiashara hatari, genge la Rahul Baldev aka mzee Kidevu. Yaliyokuwa yawe mahojiano ya ana kwa ana na waziri wa mambo ya ndani na mwandishi huyo, yakageuka njama dhidi ya naibu waziri Galata Mhisa.

'Mheshimiwa waziri, wizara ya Mambo ya ndani imeonesha mabadiliko makubwa kiutendaji ndani ya miezi miwili tu tangu utangazwe kuwa waziri. Kabla ya hapo ulikuwa naibu wa wizara hii. Je ni kusema mtangulizi wako alikuwa anazuia nyota yako kung'aa kiutendaji ama namna gani?' mwandishi huyo maarufu wa kituo maarufu cha redio nchini na magazeti kadhaa ya habari za kiuchunguzi, Jerry Prenge, alihoji.

Waziri James Merkiad alitambua hilo halikuwa swali bali dhihaka. Dhihaka kwamba tangu unaibu waziri wake hata sasa alikuwa cheo tu na jina lake halikutambulika wala kutamba kiutendaji. Dhihaka kwa sababu, sifa hizo ilikuwa wazi kuwa ni za naibu wake Galata Mhisa. Hawa hawa waandishi ndio walikuwa wakimpaisha Naibu wake wakisahau jina lake kwenye sifa hizo. Akaona unafiki mkubwa nyuma ya swali la mwandishi huyo!

'Marehemu Mlacha na Mimi tulifanya kazi bega kwa bega, hivyo utendaji wake na utendaji wangu vilihesabiwa kama kazi ya timu moja. Ninachofanya ni kuendeleza tuliyofanya kwa pamoja.' James Merkiad alijibu kwa hamaki. Ni dhahiri alichukizwa sana na kusudio la mwandishi Jerry Prenge ambaye alionesha kumdharau. Kwa sehemu, Jerry Prenge alijua anaelekea kuzuri hasa baada ya kumuona Waziri James anaonesha hisia ambazo alikusudia kuchokoza.

'Tunafahamu kuwa marehemu Mlacha alitumbuliwa kabla ya kifo chake, sababu haikuwahi kuwekwa bayana. Kwa maelezo yako hayo, wataka kuuaminisha umma kuwa kutumbuliwa kwake hakukuwa kwa haki'?' Jerry Prenge akatupia tena shambulio lililokusudia kumlainisha Waziri James ili iwe rahisi kupandikiza mbegu ya chuki dhidi ya Naibu Waziri Galata Mhisa. Kitu ambacho ndicho kilikuwa lengo lake hasa.

'Ndugu mwandishi sijasema kitu kama hicho, tafadhali usiniwekee maneno mdomoni. Maamuzi ya Rais yalikuwa na sababu…..' Waziri James Merkiad sasa alikuwa anatapatapa. Huu ulikuwa mchezo wa hisia. Kucheza na hisia zake kijeuri ili kumdhalilisha. Asingeruhusu hilo litokee.

'Sababu gani?' Jerry Prenge hakumpa nafasi Mheshimiwa James kuweka kauli ya kutaka kumdhibiti, alikwishamsoma na kubaini kuwa waziri huyo sasa alikuwa anajiandaa kufunga majadiliano zaidi. Akamkatiza kwa hilo swali. Kama alivyomtarajia, Waziri James Merkiad akatoa kauli ya kudhibiti mwelekeo wa mahojiano yao.

'Naomba ujikite maswali yako kwenye hoja iliyokuleta, sidhani kama umekuja kujua mambo yaliyokwisha kupita…'

'Wewe ndio umeyaibua ndugu waziri. Enewei, unaweza kuzungumzia vipi kasi ya Mheshimiwa naibu waziri Galata Mhisa kiutendaji? Mtaani jina lake linavuma zaidi na wengi hawajui kama ni naibu waziri, wanadhani yeye ni waziri kamili, na hata kunao ambao hawakujui wewe kabisa.' Sasa Jerry Prenge alikusudia kuyaendesha mazungumzo haya. Kama Mheshimiwa Waziri James atasimama kuondoka, maana yake angeonesha chuki dhahiri. Kama akijibu kwa jaziba pia ataonesha anakereketwa na wivu dhidi ya mafanikio ya Naibu wake, na kama akionesha kusifia atathibitisha kuwa yeye si chochote kitu kwenye utendaji wizarani hapo. Jerry Prenge alikuwa kamweka kikaangoni dhahiri.

'Lengo la swali lako ni nini ndugu mwandishi? Hii ni wizara moja, anachofanya naibu waziri kina baraka zangu.' James Merkiad roho ikamchonyota kwa maumivu. Huyu mwandishi alikusudia kuichochea chuki yake dhidi ya Galata Mhisa, na ilionekana kana kwamba mwandishi huyo aliweza kuusoma uso wake na kugundua kwamba kila alipotamka jina la naibu wake, sura yake ilijikunja kwa chuki.

'Ndugu waziri, huko mashariki ya kati, enzi za zamani sana alikuwepo kijana mchungaji wa kondoo katika familia ya mzee mmoja maskini...' Jerry Prenge sasa aliamua kumchota mzima mzima na kumweka kwenye kiganja cha mkono wake. Akatoa simulizi iliyokusudia kumfanya Waziri James Merkiad aone jinsi ambavyo usingizi wake wa pono ulikuwa unamtoa njiani.

'.......familia hiyo haikuwa na chochote cha kuitambulisha kiutawala maana haikuwa ukoo wa kifalme. Kijana huyo alikuwa na talanta ya kucheza vema vyombo vya muziki hata roho ya msikilizaji ikasuuzika kwa ustadi wake. Ustadi huo ukamfanya mfalme kumfanya kijana huyo awe mpiga vinanda wake kama sehemu ya burudani na liwazo kwake. Kijana huyo hakukosea, alitumia nafasi hiyo vema na ndipo mfalme alipata kujisikia vyema rohoni mwake. Hata ikawa usingizi wa mfalme ulikuja tu, aliposikiliza sauti na kinanda cha muziki wa kijana yule. Kijana huyo akajipatia umaarufu kote nchini, hata ikawa mfalme alipofanya ziara, hakushangiliwa yeye bali alishangiliwa yule kijana. Ikawa kwamba kijana anajulikana na kuongelewa hata kuliko mfalme.

'Wanasema sauti ya watu wengi ni sauti ya Mungu. Kukubalika kwa kijana yule kulimfanya awe na sifa zaidi ya mfalme. Hata viongozi wa dini ambao kwa taratibu za nchi ile walihusika kumtangaza mfalme, nao wakawa ni wafuasi wa kijana yule. Wakasikika wakisemezana kuwa, kijana yule astahili kuwa mfalme. Hilo lilikuwa kosa sawa na uhaini. Kwa tamaduni za taifa lile, habari za mtawala mpya kuzungumzwa akiwapo mtawala madarakani ilikuwa kusudio la uhaini.

Ukafanyika mpango wa kumtawaza kijana awe mfalme ilhali mfalme bado alikuwa hai, tena mwenye siha njema kabisa. Mfalme alipoletewa habari hizo na watu wake wa karibu. Alimkasirikia sana kijana yule aliyejua vema kumburudisha. Akaazimu kumtimua nchini mwake.' Jerry akaweka kituo na kumwangalia usoni Waziri James Merkiad kuona maneno yake yamekuwa na mwitikio gani kwa waziri huyo. Waziri alikuwa kavutiwa na simulizi yake na hata akataka kujua kama kijana hatimaye alifukuziwa mbali au kuuwawa.

'Enhee, bila shaka mfalme alimshughulikia ipasavyo kijana huyo mwenye kukosa shukrani hata kutaka ajulikane zaidi yake!?' Waziri James Merkiad akauliza.

'Hapana, mfalme alipofanya maamuzi hayo, alikuwa keshachelewa. Wananchi walimpenda sana huyo kijana, habari hizo zikawahuzunisha sana. Kwa umoja wao, wananchi wote Wakaandamana kumtaka kijana arudi na sio tu kurejea nchini, bali walimtaka yeye ndio akalie kiti cha mfalme. Hawakumtaka tena mfalme wao wa zamani.' Jerry Prenge akaongea kwa masikitiko.

'Alaa!' waziri akatamka akiwa ameghafirika kweli kweli, Kisha akatoa kauli;

'Itakuwa walichezea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa majeshi ya mfalme. Shenzi kabisa. Wanadhani ni rahisi kuchezea dola?' Waziri James Merkiad alizungumza kwa namna iliyoonekana kumpatia faraja binafsi. Kisa hicho alikifananisha na uhusiano uliokuwepo kati ya Rais KK na Naibu Waziri Galata Mhisa. Hivyo, kwa vile yeye aliitazama nafasi ya Rais KK kwa matamanio kwenye uchaguzi ujao, wakati ambao KK angeng'atuka madarakani kwa mujibu wa katiba, aliona huyo Galata Mhisa ndio huyo kijana aliyeonekana kupendwa kuliko hata mfalme. Kwenye simulizi hiyo, James Merkiad alitamani kijana huyo afe. Kwa maana kufa kijana huyo, kwenye hisia zake ingekuwa sawa na kufa kwa Naibu wake Galata Mhisa ambako kungempa yeye nafasi ya kuwa mrithi wa kiti cha Rais.

'Kwa bahati mbaya sana' Jerry Prenge aliendeleza simulizi.

'.. kijana huyo alikubalika hadi jeshini, lakini pia, kwa mujibu wa katiba ya nchi ile, jeshi lilikuwa mali ya wananchi, hivyo, mfalme alipoonekana kuwa upande tofauti na wananchi wake, tayari ilitafsiriwa kuwa ni adui wa taifa.' Jerry Prenge akamwangalia Waziri James Merkiad ambaye alionesha hisia ya kuvunjika moyo.

'Wananchi wakamtimua mfalme na kijana akakabidhiwa kiti cha ufalme.' Jerry akatamka na kumaliza simulizi yake. Merkiad alikuwa kwenye tafakari nzito.

'Nadhani umenielewa kwa mfano huo ndugu waziri. Shida iliyomkumba mfalme ni kuchelewa kupata taarifa na hivyo kuchelewa kufanya maamuzi' Jerry Prenge akamwaga sumu zake halafu huyo akajiondokea zake.

Waziri James Merkiad akakaa na kutafakari sana. Wivu ukamtafuna mno, hata akawa ni mtu mwenye huzuni mwingi. Akaamua lazima atamfanyia kitu kijana huyo Galata Mhisa kabla hajachukua nafasi yake.

Saa mbili za usiku, James Merkiad akanyanyua simu yake, akaandika tarakimu kadhaa kutoka kwenye kadi aliyoachiwa na mwandishi Jerry Prenge, halafu akaipachika simu hiyo sikioni.

'Mheshimiwa waziri!' sauti kutoka upande wa pili ikasikika.

'Nataka tukutane kwa mazungumzo zaidi mimi na wewe'!' Waziri James Merkiad akaunguruma kwenye sikio la Jerry Prenge.

'Hamna shida Mheshimiwa waziri. Nakuja wapi?'

'Njoo nyumbani.'

'Sawa Mheshimiwa waziri.'

Dakika arobaini na ushei hivi, Gari la mwandishi Jerry Prenge lilifunguliwa geti kwenye makazi ya waziri wa mambo ya ndani, Mheshimiwa James Merkiad. Baada ya kuipaki gari kwenye eneo aliloelekezwa na mlinzi, alikaribishwa na msaidizi hadi kwenye chumba cha stadi ndani ya nyumba ile ya serikali. Humo alimkuta waziri James Merkiad akiwa ameketi mwenye huzuni na usowe umesawijika kwa sonona.

'Naam Mheshimiwa waziri, nimeitika mwito Ndugu yangu.' Jerry Prenge akatamka kwa namna ya kuchokoza mada. Tangu awali alijua Waziri James Merkiad keshaingia mtungoni. Hapa alikuwa amekuja kumaliza kazi. Kumtoa mtungoni na kumhifadhi kwenye chombo mahsusi ampeleke nyumbani kama kitoweo.

'Nataka uniambie lengo hasa la wewe kuniuliza maswali yale. Unataka nini Jerry?' hakuhitaji mzaha. Waziri alikuwa siriazi kweli kweli. Tafakari yake ya muda mrefu, ilikuwa imempatia dokezo. Alishakuwa mpenzi wa makala za mwandishi huyo kwa siku nyingi, hasa kwa sababu zilikuwa zikimbeba na kumjengea taswira chanya kwa wananchi. Bila shaka hata haya maswali yake, japokuwa yalionesha mwelekeo wa kumghafirisha, Basi kulikuwa na sababu. Je, alikengeuka na kumuona kenge? Au alitaka Sasa alipwe fadhila kwa zile sifa alizokuwa akimmwagia kwenye makala zake? Alijikuta Hana jawabu, akaamua heri aupate ukweli kutoka kwenye chanzo halisi. Kutoka kwa mhusika mwenyewe.

'Very well Mheshimiwa. Naona umeona bora wende kwenye hoja moja kwa moja. Iko hivi, hadi muda huu tunapozungumza, ni wazi kwako na kila mtu kuwa bwana mdogo ameushika moyo wa Mheshimiwa Rais, hilo lipo wazi kama uchi wa mbuzi jike. Mwelekeo wa kisiasa unaonesha bwana mdogo anazidi kukubalika sana miongoni mwa makundi mbalimbali ya jamii. Si kwa vijana wala wazee. Mbaya zaidi, hadi ndani ya chama ana mvuto wa aina yake.

'Baada ya uteuzi wako kama waziri wa mambo ya ndani, minong'ono ilienea kote nchini kuwa wewe ungeweza kushika nafasi ya KK anapong'atuka madarakani. Minong'ono hiyo ilichangiwa kwa sehemu kubwa na makala ambazo nimekuwa pia naandika kwenye magazeti, mijadala ambayo haikuishia tu kwenye gazeti langu bali iliibua mijadala kwenye radio na kwenye mijadala ya runingani pia.

'Niliibua mijadala ile nikilenga kukupa uwanja wa kucheza na saikolojia ya raia ili kujitengenezea mazingira ya kuchukua nchi, lakini hukuchangamkia fursa. Badala yake, imefikia mahali bwana mdogo amebadili kabisa mwelekeo. Watu waliosoma makala zangu za kumchafua na kumbeza bwana mdogo na kukutukuza wewe, sasa wana mashaka. Wanahitaji kitu cha kuwarudishia Imani. Imani kwamba, bwana mdogo ni mtu wa mihemuko na hawezi kuendesha nchi itakiwavyo bali wewe.' Jerry Prenge akatia kituo hapo akijifanya kutafakari kwa kina, lakini alikuwa yuamchora tu waziri James Merkiad. Akamuona waziri huyo akihangaika kwa tafakuri nzito kabla hajamrejelea na swali la msingi.

'Hivyo wanishauri mimi nifanyeje?' Jerry akachekelea moyoni. Windo lake limenasa. Kama utani vile.

'Ninalo wazo Mheshimiwa waziri.' Jerry Prenge akajifanya sasa ananong'ona. Akamuona waziri James akinyanyua masikio mithili ya sungura kwa kuvuta makini yake. Naam, waziri akajiweka vizuri kwenye kiti chake huku akijivuta mbele kumsogelea Jerry Prenge ambaye waliketi wakitazamana mkabala.

'Nitahitaji uhakika kuwa hata baada ya kukueleza wazo langu, hutonigeuka. Lengo langu ni jema, lengo langu ni kukutakia wewe nafasi ya urais. Sioni anayefaa kuchukua nafasi ya KK isipokuwa wewe. Huyu bwana mdogo ana kila dalili ya kuiwania nafasi hiyo. Kumbuka imesalia miaka mitatu tu KK ang'atuke kwa mujibu wa katiba.'

'Unataka uhakikisho gani Jerry?'

'Nataka neno lako tu, kwamba hutanigeuka na kuanza kuninyooshea kidole.'

'Kama lengo lako ni jema vidole vinatokea wapi?'

'Lengo ni jema, ila njia ya kulifikia lengo ni ngumu. Inahitajika maamuzi ya kibabe.'

'Maamuzi ya kibabe. Ok, Kama unadhani kuwa sitakubaliana na mpango wako, ondoka, nenda zako. Kama unadhani unao mpango wa maana, tafakari kama unaweza kunishirikisha. Ninayo mambo mengi ya kufanyia kazi, sihitaji mojawapo liwe kuwaza eti Jerry Prenge ana mpango gani.' Waziri James Merkiad aliongea huku akisimama.

'Ah, keti tafadhali waziri. Bila shaka umeniita ukitaka kuujua mpango wangu. Keti nikueleze!' Jerry akasihi.

Waziri James Merkiad akaketi akiwa tayari kusikiliza mpango wa Jerry.

Itaendelea......
 
KIKOKOTOO 06
DAVID NGOCHO SAMSON

Gabby ni Askari magereza ambaye amefanya kazi na jeshi hilo kwa miaka 15 sasa. Maisha yake sio mabaya na wala sio mazuri sana. Yana unafuu wa wastani, maana haombi mtu kula kwa familia yake. Hata hivyo, ni mtu mwenye masikitiko juu ya nduguye Tuzo ambaye huu sasa ni mwaka wa tatu haijulikani alipo. Tuzo, mbaye ni kaka yake wa toka nitoke, alikuwa ni mwanasiasa ambaye alijipambanua kwa sera za upinzani dhidi ya zile za serikali tawala. Alikwishajitengenezea jina kubwa kwa kuwa upande huo. Lakini kama ilivyo kawaida kwa kundi la mzee Kidevu mrithi wa pedezyee Sebo, walitumia umaarufu wake ili kutengeneza rapsha na muhali miongoni mwa raia, na kufanya serikali iwe sehemu ya lawama. Kwa sababu kwa kadri ambavyo kundi la mzee kidevu walivyoichonganisha serikali na raia, serikali ilipolivalia njuga suala husika, ndivyo wao walivyotanua upenyo wa kufanya mambo yao yaliyowaingizia fedha za kutosha. Biashara zao haramu. Hao, ndio waliomteka Tuzo na kutengeneza gumzo na sintofahamu ya kisiasa nchini kufuatia kupotea kwake. Aidani, alihusika na utekaji huo.

Gabby alipopokea ugeni wa Nondo siku kadhaa nyuma, alifurahia zaidi ujumbe aliokwenda nao Nondo. Hatimaye angeondokana na sononeko. Maana alihisi kuwa sehemu ya taasisi ambayo ilihusika na mateso ya raia wasio na hatia akiwemo nduguye Tuzo. Mpango wa Nondo ukampa tumaini la kuyaanza upya maisha yake. Familia yake ingemkosa kwa muda lakini hatimaye ingeishi maisha yaliyo bora. Bintiye mkubwa sasa alikuwa mwaka wa mwisho chuo kikuu. Kijana wake wa pili tayari alikuwa kaajiriwa serikalini kama afisa wanyama pori na alikuwa akifanya kazi huko Manyara. Mkewe mpenzi, alikuwa kamzika mwaka mmoja uliopita. Kama mpango wa Nondo ungefanyika kikamilifu, hakukuwa na shaka kwamba angekuwa sehemu ya mabadiliko.

Nondo alimsimulia Gabby habari kadhaa za kile kilichokuwa kinaendelea nchini nyuma ya mapazia. Akaongezea chumvi mambo kadhaa na kuyatia ladha. Gabby akayapokea yote kama ukweli hasa kwa vile tayari alikwisha jiandaa kisaikolojia dhidi ya serikali. Ni kama alikuwa mkao wa tayari akisubiri tu apewe sababu ili iwe kigezo cha kufanya maamuzi ambayo ni dhahiri alikuwa akiyatafakari kwa muda mrefu sasa.

Nondo alimweleza mpango wa kuingia gerezani, gereza alikofungwa Muta, na akamweleza kuwa baada ya muda fulani, angepaswa kuondoka mle gerezani akiwa na Muta na baadhi ya wafungwa na pia akamweleza lazima kungetokea madhara kiasi kwa askari hasa kama wangelazimika kupambana. Gabby angekuwa ufunguo wa kuondoka mle gerezani.

Alitakiwa siku ya tukio, ahusike kuwafunga pingu, lakini pia angelazimika kuwa na hizo funguo na kukaa na kundi la Nondo ambalo lingehitaji kutoroka. Yeye Nondo alikuwa kaandaa gari uraiani ambalo lingewabeba eneo fulani kwa mtindo wa kusababisha ajali ya karandinga la polisi. Gabby aliridhia. Hivyo tukio hilo lingefanyika, na Gabby angewafungua pingu Nondo na wenzie, wangeshuka kwenye karandinga na kufutika eneo la tukio kwa gari ambalo huku uraiani lilikuwa limeandaliwa kwa kazi hiyo.

***

Ukweli ni kwamba hatimaye usiku wa siku hiyo, Nondo na Muta walifanikiwa kutoroka gerezani, huku nyuma wakipoteza maisha ya askari kadhaa wengine wakiwa kwenye hali mbaya.

Habari ya tukio lao ikagubika nchi nzima na kuitiisha chini ya hofu kuu!

Usiku wa tukio lao la kutoka jela ulikuwa usiku wa aina yake kwa Muta. Mipango waliyopanga wakiwa gerezani ilikuwa kama ndoto ambayo Nondo aliamua kumpa Muta ili kumpa matumaini. Hakujua kama ingelikuwa halisia lakini aliamua kuiamini kama namna ya kujipatia tumaini. Hata hivyo yeye binafsi hakuwahi kuwaza kama kuna siku angefanya tendo la kishujaa kama hili ambalo walikuwa wanalizungumzia wakiwa ndani. Hakuona sababu ya kulipinga hasa kwa vile aliona ni wazo ambalo lilimpa tumaini na mtazamo wa tofauti na ule aliokuwa amejengewa tangu mtoto, mazoea ya kuandaliwa na kutekelezewa kila kitu bila yeye kutia bidii au nguvu zake binafsi.

Alfajiri ya siku hiyo, Muta alishuhudia miale ya macheo ikipenyeza kingo za mlango uliyofunga selo yake. Muda si mrefu atakuwa anakabili kifo kama si uhuru wake tena! Akili yake ikagoma kukubali adhabu ya kifo, moyo wake hata hivyo ukawa na kila dalili ya hofu. Angefanyaje? Simulizi juu ya mzazi wake na madhila aliyokuwa amekabili siku za karibuni, kuwepo kwake ndani kungepelekea kupoteza mzazi wake huyo kizembe kabisa. Kufa nini?! Asiyekufa nani? Kila mtu hufa mara moja, kinachoangaliwa ni aina ya kifo alichokufa mtu na nini alichoacha kama mwendelezo wa maisha yake hata baada ya kufa. Heri kufa kunakoashiria uzazi wa historia njema kwa kizazi kijacho. Heri kufa ukipigania haki kuliko kufa ukilamba miguu ya mtesi wako.

Alijitazama mikono na miguu yake, akajichukia. Alikuwa ameisha kabisa. Afya yake haikuwa ile aliyokuwa nayo siku zote. Hapo wazo na mikakati ya Nondo ikamkolea na sasa akaona uhalisia wake ukitekelezeka. Hakuwa na jinsi, kama ni kufa, basi alihiari kufa akijaribu kujiokoa na si kwa njaa na udhoofu huu aliokuwa nao.

Saa moja na nusu hivi, walipandishwa kwenye karandinga la magereza tayari kwa kuhamishiwa kwenye gereza lenye ulinzi madhubuti (Maximum Security) kutokana na aina ya makosa yao, mauaji. Hii ingeweza kuwa safari yao ya mwisho. Alijiwazia Muta, lakini pia walidhamiria iwe safari ya uhuru.

Safari yao iliendelea, Muta, Nondo na wafungwa wenzao wote wakiwa kimya, huenda wakitafakari nini hufuata baada ya kifo, huko mbinguni au motoni. Siku nyingi Muta hakuhudhuria ibada. Sasa alimhitaji Mungu. Akatamani angeyasikia maombi yake. Aliomba kitu kimoja tu, baada ya hii operesheni yao, abaki hai.

Eneo la tukio lilikuwa jirani sasa, Nondo alimpa Gabby ishara ya konyezo. Mara gari kubwa semitrela likiwa limeiva kwa spidi lilitokeza njia panda na kulivaa karandinga la magereza na hii ikatokeza ajali mbaya sana kuwahi kutokea. Watu wakiwa wanashangaa nini kinaendelea, walishuka vijana wawili wenye bastola na kuwashambulia askari magereza waliokuwa wanaugulia majeraha. Wakati huo huo, Gabby akaingiza karata yake mchezoni. Dakika mbili mbele, Nondo, Muta na baadhi wa watu wao waaminifu, walikuwa huru dhidi ya pingu. Gari aina ya landrover, ikiwa na abiria kadhaa ikatimuka na kuacha vumbi nyuma. Muta, Gabby na Nondo na wale vijana wakiwa abiria wa gari hilo. Gari hilo lilifanikiwa kutokomea pasipo kuacha alama. Nyuma ikabaki simulizi za watu walioshuhudia tukio hilo. Gabby akiwa na jeraha kubwa la risasi nyuma ya kisogo, asijue maana hakuwa hai tena. Hadi wanafika eneo la kubadili gari, Ndiyo Nondo na wenzake waligundua hawakuwa na Gabby ila mwili wake. Wakaamua kuuacha mwili huo kwenye landrover lile, walijua lazima gari hiyo ingepatikana na ikiwa na mwili wa Askari magereza, Gabby angepatiwa maziko ya Heshima ya shujaa. Ndio, kwa sababu hakuna aliyejua uhusika wake. Hata hivyo, kifo chake pia kiliwatia simanzi kubwa Nondo na wenzake. Walimwomboleza.

***

Kikao nyeti sana kilikuwa kinaendelea katika jengo mojawapo la marehemu Masebo. Miezi na siku kadhaa sasa zilikuwa zimekatika tangu alwattan Masebo kudhulumiwa uhai wake na mtu aliyejiita Nondo. Pale ambapo kundi hili la mzee Masebo lilipodhani Nondo amedhibitiwa, wakapashwa habari za kutoka gerezani na kufanya mauaji makubwa ya askari waliokuwa wakimweka chini ya uangalizi wa mkono wa sheria.

Tayari ilikuwa imeshajulikana mrithi wa kiti cha Masebo, na ndiye hasa aliyeitisha kikao hiki nyeti ili kujiwekea tahadhari na kutafuta namna ya kumpoteza kabisa Nondo. Walikuwa na majukumu makubwa ya kuhakikisha himaya yao inadumu na kufanya shughuli zake kama kawaida.

Mzee mwenye asili ya kituruki, mfanyabiashara maarufu na mmiliki wa viwanda kadhaa vya kuzalisha nondo na saruji. Mdau mkubwa wa chama kimojawapo maarufu cha siasa nchini. Mtu aliyejitengenezea heshima kubwa ndani na nje ya Afrika ya mashariki na kati. Mzee Rahul Baldev alimaarufu mzee Kidevu. Huyu ndio alikuwa sasa anashikilia kiti kilichoachwa na marehemu mzee Masebo.

Miradi ya genge lao halifu, ikiwa ni pamoja na makampuni ya ukopeshaji fedha ambayo kwa kutumia wanasheria wabobezi wachumia tumbo, walifanikiwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa idara za usimamizi wa fedha za serikali, kutengeneza mitandao ya kiwizi iliyolenga hasa kujilimbilikizia mali kwa kiwango cha juu, ikiwemo kuwaibia fedha wastaafu mafao yao. Tayari walikwisha tengeneza maadui wengi, na hata kudiriki kuua wale walioonesha namna fulani ya ung’ang’anizi wa kudai haki zao baada ya kutapeliwa. Watumishi wa serikali kwenye idara za mifuko ya hifadhi ya jamii, walitumiwa kutoa orodha ya watumishi ambao walikuwa kwenye mipango ya pensheni, na wale waliokuwa na miaka mitatu kabla ya kustaafu. Genge la Masebo na Kidevu lilipopata orodha hiyo, kazi yao Ilikuwa moja tu. Kuwarubuni wazee hao na kuondoka na mafao yao.

Kikao cha leo kililenga kubaini na kuweka mikakati ya kushughulika na watu ambao sasa walianza kuonesha changamoto kwenye kundi lao na hata kufikia kiwango cha kumuua mmoja wao. Kiongozi wa kundi lao. Pedezyee Sebo. Majina mahsusi yakiwa ni Nondo na Muta ambao sasa ilisemekana wapo nje ya gereza na hawakujua mipango na lengo lao.

Mipango ilipangwa ikapangika, Aidani na wenzake wawili walipewa jukumu la kuwatafuta na kuwapoteza kabisa Nondo na Muta kwa gharama zozote zile. Fedha na kila kitu walichohitaji kwa jukumu hilo kiliwekwa sawa na sasa Aidani na wenzie waliingia mtaani kuwatafuta wabaya wao.

***

Majira ya saa kumi usiku, katika hospitali ya taifa Muhimbili. Kelele za ving’ora vya ambulance zikiashiria mgonjwa aliye mahututi, zilisikika na mageti yakafunguliwa haraka. Gari ile ikazama ndani. Mtu aliyeonekana kuwa taabani alipokelewa na manesi na kuwahisha kwenye wodi ya uangalizi maalumu (ICU). Madaktari wawili wakazama wodini kucheki hali ya mgonjwa na pia kutoa huduma za kitabibu zaidi. Nondo aliyekuwa kavalia kidaktari zaidi, alijipenyeza kwa wagonjwa na moja kwa moja akaelekea kwenye kitanda alichokuwa amelazwa mzee Muganyizi. Kwa taarifa zilizokuwa zimetolewa rasmi, mzee Muganyizi alihitaji kupata matibabu zaidi nchini india na kibali cha rufaa hiyo kilikuwa dhahiri. Mzee huyo alipaswa kuwahishwa na ndege ya alfajiri saa kumi na moja. Ndege binafsi ilikuwa imeandaliwa kwa zoezi hilo.

Ndege binafsi iliyoandaliwa kwa zoezi la kumsafirisha mgonjwa ilinyanyuka taratibu katika viwanja vya hospitali ya Muhimbili ikiwa na abiria wanne. Mzee Muganyizi, Nondo, Muta na Koku. Koku alikuwa haamini kinachoendelea. Ni kama alikuwa ndotoni. Lakini ulikuwa ni ukweli. Maelezo zaidi huenda angepewa mbele ya safari. Kimya kilitawala ndege ile ilivyokuwa inakata mawingu na kuliaga anga la Tanzania na kuingia anga la kimataifa.

Kwa upande wa pili, Aidan na wenzake kwa kutumia mbinu zao za kijasusi walifanikiwa kuingia hospitalini na kukutana na habari za rufaa ya Mzee Muganyizi kwenda nchini India. Hilo halikuwaingia akilini. Mtu aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi kwa tuhuma za mauaji anapewa rufaa ya kwenda India. Waligundua tayari walikuwa wamechelewa. Mpango wao ulikuwa umegonga panapo ukuta wa zege. Sasa kuliko wakati mwingine walikuwa wameachwa njia panda. Muta na Nondo wakiwa nje, mzee Muganyizi akiwa hai, hiyo ilikuwa dalili mbaya sana kwa kundi lao. Ikiwa na maana kuwa vita Ilikuwa imetangazwa rasmi. Walimhofia zaidi Nondo kwa jinsi alivyoweza kuondoka na uhai wa pedezye Sebo akivuka vikwazo vya ulinzi lukuki.

Mawasiliano yalifanyika. Bila shaka hii ilikuwa ni vita kubwa iliyokabili genge la mzee Kidevu na wenzie. Wenzao waliokuwa serikalini walikuwa waingie kwenye vita kwa kutumia nafasi zao serikalini. Ikasukwa mipango mingine. Muganyizi na familia yao sasa walitangazwa ni kundi hatari la kigaidi na walitafutwa kokote kule wakiwa hai au wafu.

Kama ilivyo kawaida, vyombo vya habari vikaja na hadithi kubwa. Simulizi ya Muganyizi na familia yake kutoroka nchini, ikiwa ni siku moja baada ya Muta na wafungwa kadhaa kufanya mauaji ya maafisa gereza na kutokomea uraiani. Simulizi ikanogeshwa na tamko la waziri wa mambo ya ndani aliyetangaza familia hiyo kuwa ni kundi la kigaidi, Waziri huyo, alikuwa anatumika kutoa taarifa hiyo si kwa maslahi ya nchi bali ya kundi la mzee Kidevu na wajanja wao waliokuwa wamepenyezwa katika nafasi muhimu kwenye Jeshi la Polisi na Usalama wa taifa.

Itaendelea....

Kwa maoni 0629077792
Mkuu namba 5 umeruka badala yake namba 6umeandika mara mbili
 
Mkuu namba 5 umeruka badala yake namba 6umeandika mara mbili
KIKOKOTOO 5

Utemi wa Muta sasa ulikuwa mashakani. Mbabe wake alikuwa amejitokeza na kumfedhehesha kwa kumdhalilisha yeye na serikali yake. Kama ilivyo kawaida ya binadamu, Muta alijikuta hana rafiki tena. Hata askari wake waaminifu nao sasa walionekana kushobokea mtemi mpya aliyekuwa amefanya mapinduzi ya hatari.

Muta alibana kwenye kona yake na kujiona bonge la zoba, bwege mtozeni! Zumbukuku ulimwengu uko huku, mgeni wa dunia. Kwa masaa mawili sasa alikuwa ameketi eneo hilo hilo akiwaza na kuwazua. Alipozingatia sana, aling’amua kwamba maisha yake yalijawa upepo na utupu mtupu.

Hakuwa na kitu, hakuwa na kitu cha maana alichoweza kusema ni chake. Utawala wake gerezani pia alibaini ilikuwa ni upepo tu, hakukuwa na chake. Alikuwa anaishi maisha yasiyokuwa na dira. Akiwa ni maskini wa mwisho ambaye hata hivyo, hakumudu kujikwamua kwenye hali hiyo. Alikuwa bonge la tegemezi. Utegemezi aliojengewa na familia yake. Alijidharau! Akajitoa thamani na sasa aliamua kujitoa ufahamu.

Alijinyanyua kizembe na kumfuata Nondo. Ujasiri ambao hakujua ulikotokea ukampeleka kwa adui yake kwa lengo la kumkabili ili kujua hatima yake;

‘Haya sasa, umekuwa mtemi wewe, nini hatima yangu kwenye utawala wako?’ Muta aliongea huku akijiuliza kama Nondo alistahili kujibu hilo swali lake! Moyo wake ulitamani kabisa kuuliza swali aina hiyo, swali la nafasi yake kwenye maisha, lakini angemuuliza nani.

Bila shaka alitamani kuuliza swali hilo kwa mamlaka yenye uwezo zaidi yake, ni vile tu hakuwa na uhakika kama mamlaka hiyo haswa ilikuwa ni hii au ni ipi? Labda lingekuwa swali la kumuuliza Mungu, aliyemuweka kwenye dunia hii na yeye akijikuta hajitambui hata katika umri huo mkubwa wa miaka thelathini na ushee sasa. Lakini wapi alipokuwa huyo Mungu!? Kama angemsikia na kumpa jibu mwafaka kwa swali lake hilo! Ndio, jibu la hilo swali na mengine mengi aliyokuwa nayo. Maswali kama nini hasa kilikuwa kinaendelea kwenye familia yake, kuhusu kaka zake, baba yake na yeye mwenyewe! Akakumbuka aliabudu mali za baba yake na nduguze akamsahau Mungu. Na sasa, alihisi kumhitaji Mungu zaidi. Lakini, je alistahili kweli hata kumsogelea Mungu angali alimtenga na kuwategemea wanadamu ambao sasa hawakuonesha nia ya kumsaidia zaidi ya kumkejeli na kumfanyia dharau? Alijikuta akitafakari mambo hayo kwa uzito uliostahili.

Nondo alimtazama usoni Mutahaba, akamuonea huruma. Akamwangalia jinsi alivyokua hana tumaini, hata hivyo, alimudu kumtolea tabasamu na halafu akamshika begani, kisha akamsogelea jirani na kumnong’oneza kitu sikioni.

‘Nisikilize vizuri na unielewe Muta, humu gerezani nimekuja kwa misheni mahsusi. Nimekufuata wewe, nataka kukutoa humu, hivyo basi, zingatia sana maelekezo ntakayokuwa nakupa. Kwa sasa, tunahitaji kuendelea kuwa maadui na tuwaaminishe askari na wafungwa wote kwamba sisi ni maadui wakubwa, baada ya muda usiokuwa mrefu nitakueleza kwa nini nakutoa humu gerezani' Nondo alimaliza kuongea.

Bila kutarajia, wakati Nondo anaondoa midomo yake sikioni kwa Muta, akapokea kibao kizito sana shavuni mwake halafu kwa dharau vile Muta akamsogelea na kumnong’oneza kitu.

'Sihitaji kutoka humu mjinga wewe! Sina haja ya kutoka humu kwenda kushuhudia uozo uliojaa huko uraiani. Bado hujanishawishi blood fool wewe!’

Ilionekana kama sasa Nondo alikuwa anataka kutoa pigo kali dhidi ya adui yake Muta. Alimvuta kwa nguvu Muta ikawa kama wanajaribu kupigana mieleka. Na kwa sauti iliyosikika kidogo Nondo akatamka;

‘Mjinga mmoja wewe, baba yako umemwacha uraiani ananyanyaswa na wajinga, unajifanya mtemi huku na huwezi hata kumsaidia mzee wako. Pumbavu kabisa wewe! Kama hupo interested haina shida, lakini tambua nimechukua risk kubwa kujaribu kukutoa humu kwa ajili ya mzee wako. Blood fool mwenyewe!’

‘Mzee wangu ana nini kwani? Nambie, mzee wangu na shida gani huko uraiani?’ Muta sasa alikuwa na hasira kweli na si utani na alitamka hayo akiwa amemkaba shingoni kijeuri.

‘Mjinga mkubwa, hivi unadhani baba yako ameshindwa kukutoa humu? Mara ya kwanza si alikutoa? Baba yako yuko kwenye hali mbaya kiuchumi kwa sababu amekokotolewa kiinua mgongo chake chote na washenzi huko nje na sasa wanataka kummaliza ili kuondosha kabisa ushahidi, unadeka deka tu humu ndani. Kuwa mwanaume sasa. Jaribu kuwajibika wewe mtemi Zuzu!’ Nondo alitamka.

‘Wewe ni nani unajifanya kujua sana masuala ya familia yangu, unataka nikuamini na huna sababu ya maana kunishawishi, au umetumwa uje kunimaliza humu ndani huku unaleta mambo ya kutunga?’ Muta akahoji tena.

“Shauri yako, ni juu yako kuniamini au kutokuniamini. Cha msingi, wewe si mtoto tena na unapaswa kuwajibika kwa familia yako!’ Nondo alitamka na kumsukumia ukutani Muta. Muta alidondoka na kujikwaruza kidole chake cha mwisho, na damu kidogo zikaonekana kugandia kwenye mkwaruzo ule. Kwa hasira akamfuata tena Nondo na kumtandika ngwara moja mujarabu sana, Nondo akadondoka chini. Muta akamfuata.

‘Una mpango gani?’ akamhoji tena.

‘Nitakueleza, hatua kwa hatua’

***

Uhasama uliojitokeza kati ya Muta na Nondo ulikuwa dhahiri pale gerezani kiasi kwamba wafungwa walilazimika kujigawa kiufuasi. Wapo walioamua kuendelea kuwa upande wa Muta na wapo walioamua kuasi na kujipendekeza kwa Nondo ili kuunda serikali mpya. Hata askari magereza nao kutokana na mvuto wa kisiasa uliojitokeza kwa namna ya kipekee mle gerezani nao walijikuta wakijigawa kiushabiki kwenye makundi hayo hasimu. Hakuna aliyejua siri iliyokuwepo kati ya Muta na Nondo. Wengi waliamini kulikuwa na uadui halisi dhidi ya watu hao wawili.

Maisha yalisonga ndani ya gereza. Mipango ya Muta na Nondo nayo ilizidi kusukwa na kukamilika kwa siri kubwa. Walitunga simulizi za kuzushiana na mashabiki zao wakazikomalia na hata wengine kuumizana alimradi tu kutetea upande waliouamini kwenye mgogoro ule. Muta alifanikiwa kuanzisha upya mtandao wake wa awali uliomwezesha kupata mahitaji na huduma mbalimballi nje ya gereza aidha kwa kutumia askari magereza au watu ambao walikuja kuwatazama pale gerezani.

Jioni moja, yapata saa kumi na moja, Muta alipata mgeni. Mgeni alikuwa ni Masele rafiki yake ambaye kama ilivyokuwa kwa Muta alikuwa ni kipenzi cha familia na ambaye waliishi maisha ya kutumia tu fedha bila kujihangaisha kuzitafuta. Alikuwa ni rafiki yake tangu utoto wakati wanasoma kule nchini Kenya wakiwa ni watoto kutoka familia bora tu waliomudu kusoma katika shule ile. Kwa muda sasa, Masele alikuwa ndiye mgeni pekee ambaye alikuwa anakuja kumuona na kumletea baadhi ya mahitaji mbalimbali kwa kadri alivyohitaji. Hata hivyo kwa siku hii, Masele alikuja na taarifa ya kusikitisha kuhusu mzee Muganyizi. Taarifa hii ndio ilimfanya Muta aamini kwamba alichokuwa ameelezwa na Nondo kilikuwa na ukweli. Taarifa hii ililandana vema na taarifa aliyogusia Nondo walipokuwa wanapambana gerezani hapo awali. Baba yake, mzee Muganyizi alikuwa hospitali hoi kwa kipigo cha polisi eti kwa tuhuma za mauaji ya mtu ambaye jina lake halikufahamika haraka ambaye hata mtoto mdogo angegundua kwamba ni jambazi au kibaka tu asiye na lolote la kustahili kuuawa na mzee huyo mstaarabu. Yule kijana mnuka ugoro na bangi aliyeuwawa na Aidan. Ilisemekana ati mzee wake (Muganyizi) alikuwa pia anatuhumiwa kumiliki silaha (bastola) kinyume cha sheria na kwamba silaha hiyo ilithibitika kuhusika kwenye mauaji mengine kadha wa kadha yaliyokuwa yamechunguzwa hapo awali na polisi.

Muta akapandwa na wazimu kama si hasira. Ni kweli alikuwa anadhani baba yake hataki kumtoa ndani kwa kusudi la kumuadhibu, au ili ajifunze kuwa kama kaka zake ambao hadi wanapotea kwenye maisha yao walikuwa wanajituma kutafuta mali na wakafanikiwa kuyapata kupitia shughuli na biashara mbalimbali ukiachia mbali kazi zao. Alipopata taarifa hii ya kutapeliwa pesa nyingi kiasi kile, Muta akajikuta anakumbuka maisha ambayo mzee wake alikuwa anampatia. Ni mtu ambaye alimlea katika makuzi ya kupata kila kitu alichohitaji. Si kila baba alimudu kufanyia vijana wake hayo. Bila shaka baba yake alikuwa anaonesha jinsi gani alikuwa anamjali. Akajiona mwenye hatia kumdhania tofauti ikiwa yeye ndiye ilikuwa chanzo cha mkopo huo uliompelekea mzee wake kuwa kwenye hatari hii ya kutaka kuuawa na wale watu wabaya.

Nondo alikuwa amemsimulia uhatari wa hao watu, jinsi walivyomfilisi mzee wake na kumfanya mzee wake ajinyonge kwa aibu ya maisha ambayo hakutarajia ayaishi uzeeni kwake. Kitendo ambacho kiliumba kisasi ndani yake dhidi ya watu wale na hivyo kumfanya Nondo atopee kwenye ulevi wa kupindukia hadi hapo alipookolewa kwenye tope hilo na mtu ambaye alijulikana kwa jina la McLaren Gallus. Mtu huyo alimpeleka kwenye kituo maalumu cha kusaidia watu walioathirika na ulevi, akasaidiwa kuondokana na ulevi uliokithiri, hata kufikia hatua ya kuachana kabisa na pombe. Baada ya hapo, McLaren Gallus alifadhili mafunzo ya kikomando kwa Nondo nchini Japan, akawa ni zaidi ya Jasusi.

Akapata ujuzi uliomwezesha kufanya utafiti wake binafsi na kugundua kuwa mmiliki wa ile kampuni ya ukopeshaji iliyojitangaza kwa mbwembwe na kupewa jina kwa lugha ya kiingereza alikuwa ni Mr. Masebo. Kampuni iliyohusika na kifo cha baba yake. Kifo cha fedheha na aibu. Alipobaini na maovu mengine ya Masebo na jinsi ambavyo kila mwaka alipoteza nguvu kazi ya taifa, vijana, kwa madawa ya kulevya na magonjwa ya zinaa kutokana na biashara zake chafu za madanguro ndani ya kumbi zake za usiku. Nondo aliazimia kumteketeza kabisa na kumtowesha katika dunia. Lakini hakujua kama Mr. Masebo hakuwa peke yake, bali ulikuwa ni mtandao uliohusisha hadi vigogo katika serikali iliyokuwa madarakani.

Baada ya mazungumzo na Masele, Muta akiwa amefadhaishwa mno na taarifa hiyo ya mzee wake Muganyizi, alimfuata Nondo. Kichwani kwake akitafakari kauli za Nondo hapo awali juu ya kuwajibika. Ikamuuma zaidi alipokumbuka kwamba alikuwa amebaki mtoto wa kiume pekee kwa mzazi wake huyo, akang’amua jinsi gani Muganyizi alimpenda. Ambavyo alikuwa radhi kuvuja jasho ili yeye Muta atumie. Na sasa alikuwa kwenye dhahama kubwa kwa sababu yake yeye.

‘Wanataka kumuua mzee wangu, haitoshi pesa walizomtapeli bado wanataka kumpoteza’ Muta aliongea kwa namna ambayo tunaweza kuiita 'kilio cha samaki'.

‘Labda ungenifaa zaidi nje ya gereza hili ukimtetea mzee wangu. Kama tunahitaji kutoka, huu ndio muda mwafaka. Vinginevyo watammaliza mzee wangu. Hii itakuwa kazi ya huyo ibilisi Aidan. Tukizidi kukawia humu ndani tutamkosa mzee wangu' Muta alilalama kama mtoto mdogo, huku mafua ya ghafula yakimkamata. Mafua ya hasira na uchungu! Kwa hali aliyokuwa nayo, hata Nondo aliona hatari ambayo ingetokea kama wangezidi kubaki mle gerezani. Huenda Muta angepoteza uhai kwa kufanya maamuzi yasiyo na busara kwa hisia za chuki na hasira zilizokuwa zimemvamia kwa wakati huo.

‘Ok, ebu tuliza mtima kwanza. Habari ya Aidan naifahamu vema, nilikueleza jinsi mtu huyo amebaki kuwa hatari kwa nafasi ya Mr. Masebo. Kama kweli yupo kwenye mkasa huu, basi itakuwa ni hatari kweli, kwa sababu huyo mjinga atataka kufuta ushahidi wowote ule unaoweza kumhusisha na utapeli wanaofanya. Itabidi mpango wetu tuutekeleze tonight (usiku huu). Nitafanya mawasiliano na kikosi Kazi huko nje ili tuchomoke tukamshughulikie huyo mshenzi kabla hajamdhuru mzee wako.’ Nondo alimpa mpango mkakati wa jinsi ambavyo tukio lingekuwa.
 
KIKOKOTOO 11
DAVID NGOCHO

Nondo na Muta waliporejea nchini, walikuwa na mpango mahsusi. Waliupa jina mpango huo, 'operesheni rejesha tumaini'. Mpango huo ulihusisha kukusanya habari za wale wazee waliodhulumiwa fedha zao, walio hai na waliokufa. Walihitaji kanzidata ya watu hao ili kuweza kuipeleka orodha hiyo kwa waziri kwa ajili ya kuitaka serikali kuwafidia. Hilo likiwa lengo la operesheni hiyo mahsusi. Operesheni iliyoenda sambamba na ile ya serikali ya 'operation loan sharks'

Waliingia jijini Dar es salaam na kujiwekea kambi Kigamboni. Kutokea hapo, walianzisha harakati za kutafuta vijana ambao wangekuwa tayari kuifanya kazi hiyo. Waliweka tangazo la kutafuta vijana ambao walikuwa tayari kufanya kazi yenye pato la wastani, kazi ambayo ingedumu kwa muda wa mwezi mmoja tu. Haikuwa ngumu kupata ofisi ya muda kwa ajili ya kufanyia usaili wao. Pesa huongea. Ufadhili mnono wa makampuni ya ujenzi, Rubya group of companies, yaliwezesha zoezi hilo kufanyika kwa ufanisi.

Katika hali iliyoonesha ombwe kubwa la ajira, tangazo lao lilivutia ushiriki wa vijana waliomaliza vyuo vikuu zaidi ya elfu mbili ndani ya siku mbili. Hayo yakiwa ni maombi yaliyotumwa kwa barua pepe. Ikiwa wao walihitaji vijana 50 pekee ambao wangesambazwa mikoani kwa ajili ya kukusanya habari za wastaafu nchini. Harakati hizi zikisajiliwa kama taasisi ya utafiti, ambayo ilikusudia kukusanya habari za wazee waliostaafu na hali za maisha yao baada ya kulitumikia taifa kwa uaminifu.

Zoezi la usaili lilifanyika, wakajipatia vijana makini mia moja ikiwa ni ongezeko la watu hamsini zaidi. Waliona Kidogo kile kigawanywe kwa wengi. Posho ya 30,000/= kwa siku kwa mtu waliyopanga awali sasa waliigawa ikawa 15,000/= ili vijana wengi wapate unafuu wa hali zao za kusota bila kazi mitaani na vyeti na CV zao ndani ya bahasha za kaki.. Kigezo kikubwa cha kuwapata hao kilikuwa uyatima uliotokana na wazee wao kufariki kutokana na majanga ya mikopo iliyopelekea kudhulumiwa pensheni zao. Walimtafuta mtu makini wa kuendesha zoezi hilo, wao wakiwa nyuma ya mapazia kukwepa kujulikana maana bado walikuwa wanatafutwa kwa kutoroka jela.

Wiki mbili baadaye, vijana hao wakiwa wamesambazwa mikoani kote nchini, walikuwa wanatuma taarifa za wazee waliostaafu katika kipindi cha muongo mmoja ambao Rahul Baldev na wenzake walikuwa wameingia kwenye biashara hiyo. Pamoja na kutumia utaratibu wa kitafiti wa kutumia maswali andaliwa (questionnaire), pia walikusanya majina na kiasi cha pensheni zao na namna zilivyotumika. Zoezi hilo likawezesha kupata taarifa muhimu walizohitaji.

Kwa mara nyingine, ripoti ya utafiti huo ikaandikwa vema kabisa na kusambazwa kwenye taasisi, idara na hata wizara mbalimbali za serikali. Lakini zaidi ya hilo, barua nyingine ndefu iliambatanishwa kwenye barua pepe, imfikie waziri Galata Mhisa. Kwenye barua hiyo, Nondo alipendekeza serikali kuona umuhimu wa kuwafidia wadhulumiwa kutokana na fedha zile zilizotaifishwa kutoka kwa wale wahujumu uchumi. Fedha ambazo zilihifadhiwa kwenye kasiki majumbani mwa hao mabwanyenye.

'…..Mheshimiwa waziri, maisha wanayoishi wazee hao ambao wamelitumikia taifa hili kwa uadilifu, ni maisha yasiyo na mwelekeo. Wamejikatia tamaa. Wamekuwa walevi wa kupindukia, ni kama vile wako tayari kumkabili zirael muda wowote. Si hivyo tu, nayaandika haya kwa uchungu mwingi kwa sababu marehemu baba yangu, alikumbwa na umauti kwa sababu ya kutapeliwa. Habari za utapeli wa fedha zake ambazo kwa miaka yote alizisotea, akizipangia mipango, halafu ghafla tu zikaangukia mikononi mwa hao mabwanyenye, zilikuwa habari nzito ambazo moyo wake wenye matumaini tele, haukuweza kuhimili. Alipatwa na kiharusi na baada ya miezi michache, sonona na msongo wa Mawazo na hali ya kuchanganyikiwa kusikotabirika, vilimletea giza la mauti. Giza hilo likamtwaa mzee wangu akiwa hana tumaini tena. Akiwa amekufa moyo kabla ya mwili. Washenzi hao, walimuuua mzee wangu akili, moyo na roho kabla ya kumuua mwili.

Nimekupa mfano wa mzee wangu mwenyewe. Waliokufa kwa aina hiyo ya mateso miongoni mwa wazalendo wa taifa hili, ni wengi mno. Ni kama vile taifa hili lina dhambi ya kuwaua watu wake lenyewe. Hii bila shaka ni kasumba mbaya sana. Wewe ni kijana ambaye umekua ukijua nini maana ya maisha haya ya udhalili. Afadhali yako, uliyaona mateso ungali mtoto na kadri ambavyo umeendelea kukua, umezidi kujiimarisha na kujiondoa kwenye mateso huku ukijijengea imani na matumaini ya kuizika historia mbaya. Maisha yako ni mfano bora wa maisha yenye mwelekeo chanya. Nami nakupongeza kwa kuweza kuyatengenezea mwelekeo bora maisha yako na ya taifa hili. Ndio maana nakuaminia kuwa hata hili utalimudu.

Vijana wengi hawana wafikiriacho zaidi ya kujimaliza baada ya wazazi wao waliokuwa wamewategemea kuondoka mikono mitupu. Tumebakiwa tunapata walevi na watumiaji wa madawa ya kulevya, na mmomonyoko mkubwa sana wa maadili. Sonona na msongo wa mawazo sasa imekuwa chanzo kikubwa cha magonjwa ya akili miongoni mwa wananchi wenzetu.

Kama vijana, ambao tumebahatika kubaki timamu hata baada dhoruba hizi kali, tunalo jukumu la kubadili mwelekeo wa taifa. Kwa Sasa, naona jukumu hili linakuangukia wewe. Hii ni vita inayotakiwa kupiganwa kwa akili kubwa. Ni vita ambayo itakutengenezea maadui wenye nguvu ya fedha, lakini utakuwa shujaa miongoni mwa raia wa taifa letu tukufu.

Kama ningekuwa kwenye nafasi ya kufanya maamuzi, ningeweza kushiriki kikamilifu kuondoa sumu inayokabili taifa. Lakini kwa nafasi yangu, nimekuwa nashughulika na mtu mmoja mmoja, hasa wale vichwa wa genge hilo la wafanyabiashara. Kama hujanitambua mimi ni nani, sasa umepata fununu.

Nashukuru kwa vile umefanyia kazi Ile orodha ya mwanzo…..'

Hayo yalikuwa baadhi ya maneno katika waraka huo mrefu aliouandika Nondo kwa naibu waziri Galata Mhisa.

Baada ya kusoma waraka huo, Naibu waziri Galata Mhisa aliwasiliana na Kiberenge wa Lwikondo. Akamshirikisha habari hiyo kwa kumpa waraka huo ambao alikuwa ameu-print. Ilifaa waongee na kuona njia ya kulifanyia kazi hilo suala.

'Huyu Aidan, ambaye amekuwa kama mwendesha operesheni za genge la watu wasiojulikana, tunamshughulikia vipi?' Galata Mhisa alimhoji Lwikondo. Nondo alikuwa ameeleza masikitiko yake kwamba mtu huyo ambaye amekuwa akiendesha operesheni za genge la mzee Kidevu alikuwa huru, na sasa alikuwa anajipanga kukabili jeshi la magereza ili kuwaondoa kimya kimya watu wake. Hizo zilikuwa ni hisia zake kwa jinsi alivyotokea kumfahamu Aidani.

'Kama kusudio lake ni kudili na askari magereza na watu waliopo ndani ili kwamba hatimaye watoke, njia ya kupata taarifa za mipango yao, ni kumpeleka mhusika ambaye ataweza kuzikusanya vema taarifa zao. Mhusika ambaye anatambuliwa kwenye genge hilo. Ikumbukwe kwamba miongoni mwa watu wa hilo genge, kwa wajuavyo wao, ni pamoja na mimi mwenyewe. Hivyo Mheshimiwa Galata, nadhani itabidi sasa nikamatwe kama walivyokamatwa wao, niwekwe pamoja nao, ili niendelee kuipata mipango yao kama ilivyokuwa huku uraiani. Mheshimiwa waziri, nipo tayari kwa misheni hiyo.' Kiberenge wa Lwikondo alionekana kuelewa kusudi la kuitwa na Galata Mhisa. Na ni kweli kuwa hilo lilikuwa ombi alilotaka kumuomba Lwikondo alipoamua kumuita.

Kesho ya siku hiyo, vyombo vya habari vikaandika habari za kukamatwa kwa bwanyenye mwingine. Hilo jina la mabwanyenye sasa lilivuma sana kufuatia operesheni ya Naibu waziri, operesheni loan sharks. Kiberenge wa Lwikondo akawa ameingia ndani. Huko akakutana na watu wa genge la mzee Kidevu.

'Huyu kijana ni nani hata kutufanyia hivi? Who is he?' mzee Kidevu aliongea wakiwa wamekusanyana kikundi ndani ya gereza la 'Shimo la kisiwani'.

'He is a nobody. A loner. A once thrown away kid. Kwa sasa anadhani ametuweza. Lakini hili haliwezi kuwa. Lazima tuweze kuendesha harakati zetu tukiwa bado ndani. Tunahitaji mkono huko nje kuendesha operesheni za kutoka humu shimoni.' Lwikondo aliongea kwa chuki sana. Kwa hisia kiasi ambacho maneno yake yalionekana kupewa uzito. Kila mmoja wao alionekana kukubaliana na wazo lake.

'Tunaye kijana wetu kwenye media, tumtumie kumchafua huyo bwana mdogo, lakini hata kama kuna uwezekano atutafutie vijana wanaoweza kufanya kazi na sisi huko nje'. Alizungumza mmoja wa wajumbe wa kikao hicho.

'Msiwe na wasiwasi, muda si mrefu tutakuwa nje. Yule kijana wetu wa media, hadi kufikia muda huu ameshamwingiza waziri James Merkiad kwenye box letu. Muda wowote hicho kibwana mdogo mtasikia habari za kifo chake. Mpango uliopo ni kumuondoa kabisa Galata, na hakuna namna nzuri zaidi ya kumtumia bosi wake. Nilitaka pia niwashirikishe hili Ili kila mmoja wetu hapa ahusike kwenye changisho la malipo ya operesheni hiyo. Merkiad anataka billion moja na nusu. Lengo likiwa ni kuzitumia fedha hizo kuanza kuandaa mazingira ya kuitwaa ikulu. Na mimi nadhani hizo fedha tutakuwa tunawekeza tu, kwa maana akishaingia madarakani atakuwa kibaraka wetu na tutatumia fursa hiyo kurudisha fedha zetu.'

'Shida itakuwa kuzichukua fedha hizo, maana mie zangu za benki wamezigandisha. Kwenye kasiki lazima nihusike mimi mwenyewe.' Lwikondo akachombeza tena.

'Hiyo haina shida, Jerry Prenge ameshamsainisha Merkiad mkataba wa dili hili. Cha kufanya ni kumtumia Jerry kuzikusanya fedha hizo kwa watu wetu waaminifu nyumbani. Kama Aidan angekuwepo nchini, ingekuwa rahisi zaidi kumtumia, lakini yupo Afrika ya kusini kufuatilia yule mzee ambaye ametuingiza kwenye mkenge huu na kijana wake. Mzee Muganyizi, Muta na yule Nunda.'

'Ni Nondo bwana, wacha tusimsumbue kwanza Aidan, amalizane na hao washenzi. Hao vijana ni hatari sana. Hivi mimi naomba wafe kwanza ndio tutolewe humu shimoni, hapa ni salama zaidi kuliko kuwa nje vijana hao wakiwa hai.' alizungumza mzee Chuwa. Kila mmoja alionekana kukubaliana nao. Ajabu kuwa walijiona salama zaidi gerezani kuliko uraiani. Hivyo ndivyo Nondo na Muta walivyoogopewa na genge hili la wazee 'Mafia'.

Mipango hiyo ilimfikia Naibu Waziri Galata Mhisa jioni hiyo hiyo. Akashangazwa sana jinsi Waziri James Merkiad alivyokuwa amemjengea chuki. Kwa vile alikuwa na ukaribu sana na Mheshimiwa Rais, Galata Mhisa alipata chajio ikulu. Akamshirikisha taarifa hizo nzito jinsi ambavyo mwenzake alivyokuwa kikwazo kwenye harakati zao kwa maslahi yake binafsi ya kuutaka urais. Isingekuwa msaada wa teknolojia, huenda Mheshimiwa Rais angemdhania kijana huyo kuwa sasa ana tamaa ya kupata uwaziri kamili na anajaribu kumharibia mwenzake. Lakini, teknolojia ilimbeba Galata Mhisa.

Mheshimiwa Rais alijionea na kusikiliza mazungumzo ya wafungwa hao mabwanyenye wakiongea mipango yao ambayo ilimhusisha waziri Merkiad, kwamba alikuwa kwenye njama za kumwangamiza Naibu wake. Teknolojia ilifanya miujiza hiyo. Ile miwani ya macho aliyovaa Lwikondo siku zote, Ilikuwa pia ni camera inayorekodi matukio kwa kadri alivyopendelea. Na kwa vile alikuwa hapo kwa kazi maalum, hakupata kikwazo dhidi ya kazi hiyo. Mambo kama haya kikawaida yalifanyika kama siri sirini na watu hula viapo kuwa sehemu ya siri daima.

Hata hivyo, Rais Kassimu Kuliboja hakuwa mtu wa mihemko. Mambo yake mengi alifanikiwa kwa sababu alikuwa si mtu wa kuchotwa kihisia. Alipokea taarifa hii, lakini alikusudia kuifanyia uchunguzi wa kina. Kulikuwa na mwanya ambao angemudu kuutumia kuthibitisha habari zile. Ukusanywaji wa fedha na makabidhiano ya fedha kwa waziri Merkiad ulikuwa bado kufanyika.

'Ok, sasa kijana wangu, hili lisikupe shida. Kwa sasa kuwa mpole kama vile hujui hizi njama. Mimi nitalivalia njuga hili suala. Nitabaini mbivu na mbichi. Nikishaujua uhakika wa suala hili. Utaona matokeo yake. Usijaribu chochote kwa sasa. Wewe tulia, niachie mimi.' Rais alimsisitiza Naibu Waziri Galata.

Baada ya kuagana na Mheshimiwa Rais Kassimu, Galata Mhisa aliondoka kurejea nyumbani. Alipofika nyumbani, kwa mara ya kwanza alikaa mbele ya laptop yake, akaingia kwenye Barua pepe, akajibu Barua pepe ya karibuni aliyotumiwa na Nondo. Aliona Kuna haja ya kufanya hivyo kwa mtu ambaye alionekana kuwa na nia njema naye.

'Aidani yupo Afrika Kusini akikuwinda wewe. Habari hizi zimetoka kwenye chanzo cha kuaminika. Chukua tahadhari tafadhali.' Galata akabonyeza send, ujumbe huo ukamwendea Nondo.

ITAENDELEA....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom