RIP muasisi wa MOSAD Rafael 'Rafi' Eitan

RIP muasisi wa MOSAD Rafael 'Rafi' Eitan

MOSSAD wako vizuri lakini nadhani sehemu nyingine wanazidisha na kufanya propaganda ili kutishia watu hasa maadui zao (Psychological Warfare). Warusi na Wamarekani walikuwa wanatumia sana hii mbinu kipindi cha vita baridi. Mashirika ya kijasusi yakitoa taarifa usiziamini sana, nyingi huwa zimechakachuliwa au siyo za kweli.

Binafsi naamini CIA na MI6 zina mikono mirefu sana kuliko MOSSAD: Hata leo hii ukiwatoa CIA na MI6 sidhani kama Israeli inaweza kuwa salama hata kidogo. Edward Snowden anasema taarifa zote kutoka NSA vyombo vya ujasusi vya Israel hupewa bure bila kuchujwa.

Mfano mzuri kabisa, mikakati dhidi ya Iran nchi ya Israeli haiwezi kufanikisha yenyewe peke yake mpaka Marekani na Uingereza, kama angekuwa anaweza basi angekuwa keshamtwanga Iran mapema sana lakini huo uwezo hana.

Meir Dagan baada ya kustaafu alipohojiwa kuhusu Israel kuvamia Iran alisema "Iran is a big for Israel to fry alone" Akashauri kabisa Israel isijidanganye kuvamia Iran, madhara kwake yatakuwa makubwa sana.

CC: chige

Mkuu, wewe huwa nakubali hoja zako.penye ukweli unasema ukweli. Lakini kuna wengine humu ushabiki umewajaa na kukimbilia kukashifu imani za wengine.
 
Huyu jamaa alikuwa ni kitu kingine kabisa

R.I.P



Kina David Kimche watamkumbuka kwa mengi

Kuweka record sawa muanzilishi wa Mossad ni Ben-Gurion mwaka 1951 March 2 Ben aliwaita heads wa 5 intelligence agencies akawaambia anataka kuiweka Israel intelligence-gathering activities itakayofanya kazi nje ya Israel na itaitwa "Ha Mossad le Teum"

Na kiongozi wa kwanza wa Mossad alikuwa Reuven Shiloah aliyepoteza mamilioni ya dola kwenye operation ya kumtafuta mtoto mmoja hivi
Ndio Ben Gurion akaambiwa na gwiji Mwingine huyu jamaa hafai basi tena Reuven akaachia ngazi kama Chief wa Mossad na mikoba yake akaivaa Meir Amit

Meir Amit moja ya watu ambao Israel itawakumbuka daima kwa kufanikiwa kuiteka Mig-21
Wakati huo ikiwa ni moja ya ndege za kivita hatari Pilot wake akiwa Munir aliyekuwa Mu Iraq mwenye asili ya Uyahudi akakubali kuirusha Mig 21 kwenda Turkey kwenye base ya Marekani kisha wakaijaza mafuta na kuruka tena kwenda North Israel .

Kwa makubaliano ya ndugu zake wote kama arobaini hivi waondolewe Iraq na kupelekwa Israel na malipo ya Dola milioni moja

Sasa hivi naona Mig 21 zikikatiza anga la Tanzania natamani kulia machozi ila ndio hivyo tena uwezo wetu mdogo tunatumia ndege za miaka 50 nyuma

Jamaa zetu badala ya kuwa watu wasio julikana wangejitahidi hata kuiba Sukhoi hapo kwa Museveni
Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna huyu mnyama... Tafuteni historia yake na mission zake, nadhani kwenye hiyo mission na huyu alikuwa director... Isser Harel, (Isser Halperin), Israeli spymaster (born 1912, Vitebsk, Belorussia, Russian Empire was spymaster of the intelligence
and the security services
 
Naelewa lakini Wayahudi wamekuwa watata sana hata kabla ya vita ya pili ya dunia, maana kuna kikundi cha Wayahudi kama 40,000 kikiongozwa na Vladmir Lenin, Kamanev na Trotsky na wenzake walipundua Urusi yote na kuvuruga kabisa mzani wa dunia. Kuna kigenge kingine cha Wayahudi kilikuwepo kule Ujerumani na Austria kikiongozwa na Theodor Herlz ndiyo kilimpokonya Ujerumani ushindi wa vita ya kwanza ya dunia mwaka 1917. Kuna kigenge kingine cha Wayahudi ndicho kikiongozwa na Paul Warbug ndicho kilitengeneza The Federal Reserve ya Marekani ambayo ndiyo inaendesha Marekani ya leo.

Hapo bado hatujawataja wakina Nathan Rotschild na watoto zake waliotawala mifumo yote ya benki ya Ulaya hadi leo hii, wana kitu gani cha ziada maana kama utata hawajaanza leo. Hata kabla ya mateso na kufukuzwa Yerusalem historia inatuambia walikuwa wanafanya makubwa sana.



Do you believe in Eugenics? It works very well: The Jews have been practicing it for centuries.
Wakuu Wick na Red Giant do you believe in Eugenics Programme?
Mkuu leo ndiyo nimejua hiyo dhana/process inaitwa eugenics. Hii imekuwa ikifanyika tangu kale sana, leo hii wanyama kama mbwa na wote tulio wadomesticate na mazao tunayolima yametokana na kuendelea kuzalisha kilicho bora. Ila siamini kama hii kitu inafanyika kwa binadamu kama mpango kabisa. Kama ni kweli basi ni hatari, hawana tofauti na wanazi na ishu zao za kuzalisha race bora.
 
Moja ya unyang'au wa huyu jamaa ni kipindi kile wamewapandikizia Waajemi Stuxnet Virus. Sijui huwa wanawazaga nini hawa jamaa yani. Hivi mkuu mng'ato unaukumbuka huu umafia waliofanyiwa Iran kwenye vinu vyao vya nyuklia ?
Nilicheki documentary ya ishu. US waliunda hii kitu wakawapa waisrael. bila kukubaliana waisrael wakaitumia kuaattack wa Iran. Wa US walimind sana. IIla huko tuendako itakuwa ni cyberwarfare tu, sijui tumejipangaje?
 
Kuna kajamaa kalikuwa kana jazwa ujinga na gadafi ati kaiteke bongo halafu kapate msaada kutoka kwa bwana huyo wa libya aliyekuwa anataka kutumia nguvu zake za mafuta kuifanya afrika ya dini moja. Sasa bwana !!!! hako kajamaa hakatamsahau huyu marehemu alivyokuja kuwachukua watu wake kibabe pale kampala tena kwa kutoa taarifa. Ni kwa vile mzee wa MOSSAD atakuwa mbinguni huko anakula bata wengekutana na huyo Dadaa mweusi tii kama lami lakini gadafi alimdanganya kuwa ni mwarabu!! mkongoto ungeendelea
 
Ila linapokuja suala la utaifa nadhani Wayahudi ni watu makini sana. Jamii yao iko very Meritocratic, kuna sehemu niliwahi kusoma kwamba kule Israel huwezi kupanda cheo kwa kupitia mjomba wala shangazi. Ukizungua hata uwe kiongozi wao mkubwa lazima wakuue ili uwe mfano. Kuna yule Waziri Mkuu wao Yitzak Rabbin aliyetaka kufanya makubaliono na wapalestina wakati wayahudi hawataki jamaa walimtwanga risasi akafa.

NB: Israel usipokuwa na uwezo huwezi kuwa kiongozi wa ngazi za juu hata siku moja,hasa kwenye vyombo vya usalama.
hii kitu ni muhimu sana. wanasema kwenye vita ya siku sita maafisa wa kiarabu walikuwa wameweka sababu ya baba na mjomba, Israel waliwekwa kiuwezo. Sijui tutafika huko? maana ile list ya watoto wa wajomba BOT ilikuwa hatari>
 
Si kwa warabu tu au Muslims sema chuki kwa waabudu shetani nawachukia of course
 
Mkuu leo ndiyo nimejua hiyo dhana/process inaitwa eugenics. Hii imekuwa ikifanyika tangu kale sana, leo hii wanyama kama mbwa na wote tulio wadomesticate na mazao tunayolima yametokana na kuendelea kuzalisha kilicho bora. Ila siamini kama hii kitu inafanyika kwa binadamu kama mpango kabisa. Kama ni kweli basi ni hatari, hawana tofauti na wanazi na ishu zao za kuzalisha race bora.
Mkuu Eugenics inafanyika sana kwenye hii dunia. Fuatilia zaidi utajionea mwenyewe.
 
hii kitu ni muhimu sana. wanasema kwenye vita ya siku sita maafisa wa kiarabu walikuwa wameweka sababu ya baba na mjomba, Israel waliwekwa kiuwezo. Sijui tutafika huko? maana ile list ya watoto wa wajomba BOT ilikuwa hatari>
Wanahistoria wanasema Meritocracy ndiyo ilifanya Ujerumani iwe na nguvu kijeshi kuliko mataifa yote duniani kuanzia karne ya 19 mwishoni hadi 20 katikati. Wao ndiyo nchi ya kwanza duniani kuanzisha The Generals Staff kwenye jeshi lake ndipo dunia nzima tukaiga.

The Generals Staff ilikuwa inafanya kazi ya kusoma historia za majeshi ya dunia na kupanga mikakati ya kivita. Wao ndiyo walikuja na mbinu za kulinda mioundombinu nyeti wakati wa vita kama reli (Protection of Critical Infrastructure and Installations).

Sasa ili kujiunga na Generals Staff ni lazima usome miaka 3 kwenye chuo cha kijeshi na kufaulu mitihani kwa alama za juu sana. Walikuwa wanasoma hesabu, sayansi, lugha ngeni kama kirusi na jiografia. Nasikia wanajeshi wachache sana walikuwa wanafanikiwa kuhitimu miaka mitatu.

Mfalme wao aliweka sheria kabisa kwamba ni Marufuku wanasiasa au wanajeshi wa kawaida kuingilia kazi za The Generals Staff, huku akiamuru kwamba makamanda wote wanaongoza vita lazima wawe na mwambata kutoka The Generals Staff wakitoa ushauri wa kijeshi. Wariruhusiwa kukataa amri zisizo na mashiko kutoka kwa kamanda na kukata rufaa kwa mfalme.

Ulaya nzima wakati wanatumia mfumo wa kifalme na majina ya familia ili kupata vyeo kwenye nafasi nyeti, Ujerumani hakufanya hivyo. Ndiyo maana wanasema hata alipotwangana vita na Ufalme wa Austria na Ufaransa aliwashinda vibaya kwasababu majeshi yao yalikuwa yamejaa wajomba, baba mdogo na wapwa.

Uchina ya kale ndiyo walikuwa wanafanya hadi mitihani ya taifa ili kupata vyeo. Na iliwasaidia sana kupata watu kama Confucius na Sun Tzu Wu.

NB: Hao watoto wa wakubwa huko BOT, TISS, JWTZ, POLISI na PCCB mimi wala sina shida nao kabisa mkuu, kama waliingia huko kwa vigezo na sifa basi ni haki yao. Hata leo hii Raisi akiamua kuweka wasukuma huko BOT mimi sina shida kama watakuwa wameingia kwa vigezo na sifa.
 
Nilicheki documentary ya ishu. US waliunda hii kitu wakawapa waisrael. bila kukubaliana waisrael wakaitumia kuaattack wa Iran. Wa US walimind sana. IIla huko tuendako itakuwa ni cyberwarfare tu, sijui tumejipangaje?
Mkuu mimi sina utaalamu sana, lakini ninachojua ni kwamba Cyber Operations au Cyber Warfare huwa zinakuwa ni Support Operations ambazo hutumika kusaidia Military Operations on the ground zifanyike vizuri na kwa urahisi. Maana Cyber Warfare in sehemu kuu mbili, CNE (Computer Network Exploitation) and CNA (Computer Network Attacks).

Mbinu hizo mbili ambazo nimezitaja hapo juu hutumika kuvuruga utendaji kazi wa miundombinu ya adui kama Benki na mifumo mingine ya kipesa ya nchi au mifumo ya mawasiliano kwa kutumia DoS Attacks -Denial of Service Attacks. Wakati haya yanaendelea uvamizi halisi wa kijeshi unaweza kufanyika sasa kwasababu nchi inakuwa imezoroteshwa kwa kiwango kikubwa.

Mfano mzuri ni jinsi Urusi alivyovamia Crimea mwaka 2014, na Georgia mwaka 2008. Mifumo yote ya mtandao ya nchi hizi ilivurugwa huku majeshi ya Urusi yakifanya uvamizi kwa urahisi.

NB: Mpaka sasa mbali na mashambulio makubwa kama yale ya Estonia mwaka 2007 na Stuxnet kule Iran mwaka 2010 sijawahi ona Cyber Attacks katika kiwango kile ambacho filamu za Hollywood zinatuonesha.

Bado sana huenda huko mbeleni ikaja tokea, Ila Cyber Warfare inaenda kuwa sehemu muhimu sana katika vita vya dunia ijayo.
 
Honestly, sikuwa nakijua but kwa nilichokisoma na mie nitakuwa muumini mtiifu sana wa hiyo Eugenic programming.
Hahaha, Cuzin Eugenics ni ukatili wa hali ya juu sana: Ina maana wale wote ambao mnawachukulia kama wadhaifu ndani ya jamii itabidi muwatoe kabisa wasiendelee kuzaliana.
 
Ila linapokuja suala la utaifa nadhani Wayahudi ni watu makini sana. Jamii yao iko very Meritocratic, kuna sehemu niliwahi kusoma kwamba kule Israel huwezi kupanda cheo kwa kupitia mjomba wala shangazi. Ukizungua hata uwe kiongozi wao mkubwa lazima wakuue ili uwe mfano. Kuna yule Waziri Mkuu wao Yitzak Rabbin aliyetaka kufanya makubaliono na wapalestina wakati wayahudi hawataki jamaa walimtwanga risasi akafa.

NB: Israel usipokuwa na uwezo huwezi kuwa kiongozi wa ngazi za juu hata siku moja,hasa kwenye vyombo vya usalama.
Sure, mfano Bibi ni mtu mwenye IQ kubwa mnoo, lakini ni mtaalamu wa masuala ya buashara na uchumi mnoo, unaambiwa ameubadikisha Israel kiuchumi mnoo na kuirudisha katika ramani, Tangu vita ya lebanon na kujiuzulu ovyo kwa mawaziri na kuongezeka ushawishi wa Iran huyu jamaa alipokamata dola, mpaka leo yupo, ni more than 10 years sasa. Israel wanaangalia uwezo mnoo. Kweli unapozungumzia Ubepari au uajamaa ni unazungumzia nadharia za wayahudi
 
Stuxnet worm kilikua ni kirusi hatari mnoo kuwahi kutengenezwa, hata marrkani yenyewe iliyotengeneza ilikua haijajiandaa kukabiliana nacho; kwa ufupi ingeweza sababisha hata milipuko ya vinu vya nyuklia duniani; Iran ilipopigwa kama sio kwa msaada wa warusi kuja kushtukia ingekua habari ingine leo; maana ni kirusi advance sana: Yah its true vita kubwa sasa duniani ni vita ya kimtandao; nakumbuka mara baada ya Iran kugundua ni shambulizi iliita vijana wote wataalam wa mitandao kujiunga na jeshi la cyber la Iran kujitolea, walifanya dukuzi kadhaa na kushambulia kidogo marekani:
Mfano Venezuela imeshambuliwa mitambo yake ya umeme kwa kupigwa cyber attack. Vita ya sasa iko more digital zaidi , nakumbuka Israel iliwahi piga shambulizi moja Iran kama nusu saa hivi mifumo ya ulinzi yote ikagoma kufanya kazi nchi nzima: Ambayo ilikua ni meseji kuwa tunaeza kukufanya chochote.
 
Naam, jamii za watu wa mashariki ya kati wanajua sana kujipanga vizuri. Hata Waarabu wanajua sana kujipanga, hasahasa kwenye Financial Management: wananishangaza sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi, kipindi flani nikiwa marekani nilikuja kuona kuwa degree yenye heshima marekani ni MBA. hata ukiwakuta waarabu wanasoma huko ni MBA, kwa ufupi NI kuwa taifa ili lisonge mbele linahitaji wataalamu wa management nzuri na biashara; Taifa haliitaji madaktari au ma engeneer wengi au wanasiasa wengi; Nooo. Management ni kila kitu; asilimia kubwa ya wanasayansi wa Marekani sio wazawa; but top management ni wamarekani.
 
Mkuu kama manyanyaso hata weusi wamenyanyaswa sana huko Marekani lakini mbona hawabadiliki kabisa na kila siku wanazidi kuvurugikiwa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu weusi wa marekani wanatumika kwenye kifungo cha ubaguzi bila wao kujijua; ni watu wa kuliaaa tuu na full chuki. Gavy aliwapa somo weusi wenzake kuwa kulalamika haisadii, tusome tumiliki biashara kubwa kila mahali tutaheshimiana, (...) ni story ndefu kidogo, mwanzo waliwini, baadae hujma sikaingia; kama ni kuteswa na kukataliwa kwenye hii dunia watu wa mashariki ya kati wanaongoza( anti semitic) chuki kwa watu wa mashariki ya kati ni kubwa mnoo ulaya kuliko kwa watu weusi
 
Back
Top Bottom