RIP John Ngahyoma

na John Ngahyoma hatunae! EEh Mungu mlaze pema huko paradiso pamoja na marehemu wengine
 
Wanajamii nimetoka kusikiliza Clouds FM muda si mrefu imetangazwa kwamba Mwanahabari wetu Mkongwe John Ngayoma amefariki leo saa moja asubuhi nyumbani kwake Segerea. Imetangazwa kuwa Marehemu alikuwa akisumbuliwa na Saratani ya Ini kwa muda mrefu na alishawahi kupelekwa India kutibiwa mara kadhaa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema.

John Ngayoma - R.I.P Brother!
 
Poleni wafiwa na tasnia ya habari Tanzania..Tutakumisi bro!
 
RIP John Ngahyoma
Mungu aipe familia nguvu na ustahimilivu ktk kipindi hiki kigumu
 
R.I.P J. Ngahyoma, kiukweli jamaa alikuwa fit sana kwenye utangazaji. Sauti yake nilikuwa nikiifananisha na ya Marehemu David Wakati
 
unajaribu ku-insinuate nini?

Ukisema R.I.P John inatosha kabisa.

Naomba niende off topic kidg. Hv mtu akijawa na majipu alafu akawa anakohoa sana then anapungua kabisa yaweza kuwa kisukari? Manake swahiba wangu Ngahyoma nae mazingira haya alikuwa nayo!
 
Sisi sote ni waja wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea. Poleni wafiwa wote kwa ujumla.
 
Mtangazaji mahiri sana,namkumbuka sana wakati huo yupo ITV miaka ya 1994 au 1996.RIP Ngayoma!
 
RIP bwana John N.Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie,apumzike kwa amani.Amina
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom