Rimoti ya hii TV inanitesa

Rimoti ya hii TV inanitesa

Wakuu habari zenu?

Nilinunua tv ya mtumba aina ya sharp 32 inches , TV naipenda na sina mpango wa kuipiga chini hivi karibuni ila changamoto ya hii tv ilikuja bila rimoti na nimetafuta bila mafanikio lakini sipati remote yake.

Natumia kifaa chenye infrared port lakini sion kabisa ikikonect, Pia nimejaribu universal rimoti moja bila mafanikio , naombeni msaada kokote kule itakakoweza aptikana ata kama pengine mtu anayo na tv ilishaharibika aniuzie.

TV ni Smart TV na model yake ni Sharp lc 32Hi 5332kf model yake

IMG_2698.jpg
 
Ndio maana tunaotumia simu kuwasha TV simu lazima iwe na infared. Sasa wewe unataka utudanganye
Sorry mkuu! Unatumia Simu kuwasha TV? Inakua ndiyo remote? How's that possible aisee I've never heard/seen it before🤔
 
Sorry mkuu! Unatumia Simu kuwasha TV? Inakua ndiyo remote? How's that possible aisee I've never heard/seen it before[emoji848]
Yes it's possible, ila tu kama simu unayo tumia ina infrared... Mfano simu za Xiaomi nyingi zina infered.

Huwa zinakuja na built in remote app, au waweza pakua play store mfano nime attach remote za startimes dikoda.
Screenshot_2021-06-29-22-42-58-684_com.osfunapps.remoteforstartimes.jpg
 
kkoo remote unapata mitumba mingi kwenye machimbo.

pia kama unaweza kuingia menu angalia kama kuna option inaitwa HDMI CEC kama ipo na una kifaa chengine kama sabufa, home theatre, deki, tv box etc yenye hdmi CEC nayo unaweza tumia remote ya hiko kifaa chengine ku control tv.
 
TV na vifaa vingine vya muziki unaotumika majumbani, huwa vinatumia Infrared remote. Unapotumia simu kama remote inamaanisha simu hiyo ina Infrared capability, simu za zamani haswa za sinyEricson zilikuwa nyingi na infrared na ziliweza kuControl baadhi ya functionality za TV.

Feature kama Bluetooth na Wifi zinatumika zaidi kurusha media content au tu kufanya connectivity kati ya kifaa na kifaa.

Infrared imefanyika kuwa maalum kwaajili ya remote kwasababu kwanza haihitaji kufanyiwa pairing na mtumiaji, kila kitu kilichafanyika kiwandani, pia Infrared ni mawimbi ya masafa mafupi sana kulinganisha na bluetooth na wifi kitu ambacho pia ni usalama wa kifaa chako dhidi ya wanaokuzunguka.
 
Back
Top Bottom