Nimesikitishwa sana na hili jambo lililotokea leo.
Watu wameingilia Ukurasa wangu wa Instagram na kunizuia nisiingie kwenye account yangu. Lakini jambo baya zaidi wanalolifanya ni kuandika vitu au maneno ambayo hata sijawahi na sitamani kuyasema.
Nimeshangazwa sana na hili na sijui Nia ya kufanya hivyo ni nini? Malengo yenu hamtafanikiwa.
Mimi niko katika vikao vya halamashauri kupanga bajeti za Halmashauri yetu ya Chalinze.
Hayo maneno na matukio hata hayajawahi tokea.
Naomba utulivu katika kipindi hicho ambacho wataalamu wanafanya kazi ya kurudisha Ukurasa huu mikononi mwangu.