Ridhiwani Kikwete akana kufanya biashara na Polisi

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Lugumi, inayodaiwa kupewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi.

Ridhiwani ametajwa katika habari hizo kuwa ni mmiliki wa kampuni ya Lugumi pamoja na wamiliki wengine ambao ni Said Lugumi na aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema.

Akizungumza na gazeti hili, Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete alisema yeye hahusiki na kampuni yoyote ya Lugumi ingawa wana urafiki wa kawaida na mmiliki wa kampuni hiyo.

“Kwanza kabisa mimi si mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, hilo ni jambo la msingi kabisa watu waelewe na sijawahi kufanya biashara yoyote na Lugumi. Said Lugumi ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo tunafahamiana naye na ni rafiki yangu,” alisema Ridhiwani.

Ridhiwani alisisitiza kuwa hana uhusiano wa kibiashara na mtu huyo na kwamba hafahamu ni kwa nini amehusishwa na kampuni ya Lugumi.

“Hapa ni watu tu wanaamua kuingiza tu maneno yao, haya maghorofa ninayotajwa kumiliki Dar es Salaam hata sijawahi kutembelea ujenzi wake, wameamua kuniingiza, Lugumi nafahamiana naye binafsi tu lakini wananiingiza,” alisema Ridhiwani.

Alisema jambo hilo bado liko ndani ya Kamati ya Bunge na baadae ameliona kwenye magazeti ya juzi kuwa Jeshi la Polisi litatoa taarifa yao, hivyo asingependa kulizungumzia kwa undani. Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi.

Kamati hiyo ilipokutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema jeshi hilo

mwaka 2011 liliingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima ambavyo viko 108.

Alisema mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote ili hali vituo vilivyofungwa mashine hizo ni 14 tu, kati ya vituo vyote 108.

Ridhiwani alisema angependa jamii ifahamu kuwa hana uhusiano na kampuni hiyo kwa kuwa hafahamu kabisa hata malipo yaliyofanywa kati ya Serikali na kampuni ya Lugumi anasikia tu kama ambavyo watu wengine wamesikia.


Chanzo: Habarileo

 
Badala ya Ridhiwani kulalamikia vyombo vya habari na watu wanaoeneza habari kuhusu nyendo zake za kimaisha, lazima kwanza ujiulize/kujihoji yeye mwenyewe maswali kuhusu maisha yake.

Huwezi kuwa mtoto wa Rais halafu unakuwa na marafiki wa karibu ambao tabia zao au biashara zao ni questionable.

Watoto wa Marais/Mawaziri Wakuu na wafalme/Malkia wa nchi za Magharibi huwa wanachaguliwa mpaka marafiki wao na taasisi za usalama wao wa taifa. Hata sehemu wanazotaka kwenda kama vile nightclub lazima kwanza zipate security clearance.

Huyu Ridhiwani karibia kila mfanyabiashara mkubwa ukimuuliza anakwambia ni rafiki yake au wanafahamiana. WHY?

Kwa serikali zetu za Afrika ambazo hazina taasisi madhubuti, kuna uwezekano hawa wafanyabiashara wanatumia ukaribu wao na mtoto wa Rais katika kufanikisha biashara zao ambazo ni questionable.

Siyo kosa kwa wananchi kudhani kila ghorofa lefu nchini anamiliki yeye, hii inatokana na yeye kuzungukwa na wafanyabiashara ambao wengine ni matapeli.

Waingereza husema, birds of a feather flock together kwa maana kuwa, mara nyingi huwezi ukazungukwa na wafanyabiashara ambao ni questionable halafu wewe uwe unquestionable.

Hivi katika maisha ya kawaida, inawezekana kweli uwe na marafiki ambao ni wezi/matapeli halafu wewe usijihusishe kwa njia moja au nyingine?

Hata vitabu vya Mwenyezi Mungu vinatuambia, whoever walks with the wise becomes wise, but the companion of fools will suffer harm.
 
Ameshindwa kumkana Lugumi.

Huo urafiki utakuwa umetokana na ushirikiano wa kibishara

Huwezi kuambiwa mnaiba wote halafu unasema eti mwizi huwa ni rafiki yangu ila mimi siibi nae. Bora angekaa kimya kama alishindwa namna ya kujibu shutuma dhidi yake.
 
Akitumbuliwa tu naahidi 2020 nawapigia kura CCM, kweli nimesema toka moyoni, na nitashawishi zaidi ya watu 10,000 nyuma yangu kuipigia CCM kura.
Kwenye hii issue ndio mtajua unafiki wa Magu.

Wabunge ambao hivi sasa mnapelekwa mahakamani nanyi komaeni muhakikishe serikali nayo inawajibika katika hili.

Kila mtu abebe mzigo wake.
 
Huyu mtoto kila kibaya ni yeye tu, kuuza unga China yeye. Kuleta wawejezaji wa kuchoma mahindi toka China ni yeye. Hii ilitokana na ile kashifa ya kupeleka unga China baada ya kukamatwa serikali na watanzania wakabebeshwa zigo la wafungwa wa kichina kuja kuchoma mahindi na kuuza urembo mtaani huku wakitusanifu. Why mtoto huyu tu atie hasara taifa? Please akamatwe na kufungwa maisha.
 
Kwenye hii issue ndio mtajua unafiki wa Magu.

Wabunge ambao hivi sasa mnapelekwa mahakamani nanyi komaeni muhakikishe serikali nayo inawajibika katika hili.

Kila mtu abebe mzigo wake.
Unafiki wa Rais Magufuli kwa lipi?

Usitumie hisia kuharalisha hoja ambayo ina ugoko!

Hata ambao mpaka sasa wametumbuliwa mliwahi kusema Rais Magufuli hawezi kuwatumbua!

Kila siku mnabadilisha magori ya kisiasa!
 
Huyu mtoto kila kibaya ni yeye tu, kuuza unga China yeye. Kuleta wawejezaji wa kuchoma mahindi toka China ni yeye. Hii ilitokana na ile kashifa ya kupeleka unga China baada ya kukamatwa serikali na watanzania wakabebeshwa zigo la wafungwa wa kichina kuja kuchoma mahindi na kuuza urembo mtaani huku wakitusanifu. Why mtoto huyu tu atie hasara taifa? Please akamatwe na kufungwa maisha.
Yaani unaamini kama alikamatwa China kwa kosa la kuuza unga?

Yaani mtoto wa Rais wa nchi ambayo opportunity zote za kiuchumi ziko kwenye mdomo wake na kiganja chake unadhani anaweza kufanya mchezo wa kijinga kama kuuza au kusafirisha unga?

Think bigger!
 
Back
Top Bottom