Kuna mahali nimesoma RZ1 aliitisha kikao huko Iringa kwenye shule ya msingi hakuna kijana aliyetoka sanasana kulikuwa na watu kama 10 hivi,
Waache wahangaike! AIBU YAO AIBU YETU?
Hii hapa....ujue hapo ni unafiki tu; jamaa wana shida na vijana walimgomea! Ptu!
Ridhiwan anusurika kipigo
• Atimua mbio mkutanoni
na Francis Godwin, Iringa
MTOTO wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete, jana ameonja joto ya jiwe katika harakati za kumnadi baba yake, baada ya kutimuliwa wakati akijiandaa kukutana na wana CCM katika moja ya majengo ambayo kisheria hayaruhusiwi kufanyia mikutano ya kisiasa.
Ridhiwan ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) taifa, akiwa ameambatana na mshindi wa kura za maoni wa Jimbo la Iringa Mjini aliyeenguliwa, Frederick Mwakalebela na mmoja wa wagombea waliobwagwa, Jescar Msambatavangu, walifika katika Shule ya Msingi Ipogolo, wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kuwapatanisha Mwakalebela na mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Monica Mbega.
Kabla ya msafara wa Ridhiwan kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake kilicholenga kuvunja makundi ndani ya chama hicho, aliyekuwa mmoja wa wana CCM 12 walioingia katika kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo na kushindwa, Msambatavangu, alipita mitaani kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza Ridhiwan, lakini waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.
Hata hivyo, baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo, kwa ajili ya kukutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili, bado msafara wa Ridhiwan na wapambe wake walifika huku kukiwa na vijana wasiozidi 10.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mvutano mkubwa ndani ya ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Amani Mkeremi, kati ya viongozi wa UVCCM mkoa wakiongozwa na Katibu wa Mkoa, Rhoda George na wale wa vyama vya upinzani walioongozwa na Katibu Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata (CHADEMA) wakivutana juu ya CCM kuzuia wanafunzi kuendelea na masomo kwa ajili ya kampeni za uchaguzi.
Tukio hilo ambalo lilitokea majira ya saa 7 mchana lilisababisha mkuu wa shule kupata wakati mgumu kulitolea ufafanuzi, huku walimu wake wakijifungia ofisini kukwepa vurugu iwapo ingejitokeza kati ya wafuasi hao.
Akielezea tukio hilo, kiongozi wa vijana hao wa upinzani, Kimata, alisema walilazimika kuweka mtego katika shule hiyo baada ya kuona hekaheka za makada wa CCM.
"Kweli sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inakataza taasisi za umma kuingia katika kampeni ...sasa tulipatwa na wakati mgumu kuona CCM inatumia shule ya msingi kufanya kampeni ndiyo sababu ya kuweka ulinzi ili kuhakikisha sheria haivunjwi ...tunashukuru tumefanikiwa baada ya viongozi wa CCM kumkimbiza mgeni wa Rais Kikwete," alisema.
Hata hivyo, alisema kabla ya msafara wa Ridhiwan kufukuzwa shuleni hapo, kulikuwa kumetokea mvutano ndani ya ofisi ya mkuu wa shule, huku akitaka watu wa CCM wabaki ndani na wale wa upinzani watoke nje.
Hata hivyo alisema wao wameelekeza tuhuma zao kwa mkuu wa shule hiyo, ambaye amekuwa akionyesha ukada wake wazi wazi dhidi ya CCM hata kuruhusu shule hiyo kugeuzwa jukwaa la siasa kwa CCM.
Kwa upande wake, mkuu huyo wa shule alikiri akisema alipewa taarifa za CCM kuomba eneo la kufanya kikao na si kufanya kampeni na kukusanya vijana kama ilivyokuwa.
Hata hivyo alisema hana barua yoyote ya CCM kuomba darasa katika shule yake kwa ajili ya kufanya kampeni hizo.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa Rhoda, ambaye alikuwa mwenyeji wa Ridhiwan, alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi hakuweza kupokea, zaidi ya kukata.
Hata hivyo mmoja wa makada waliopo katika msafara huo alisema kikao hicho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kampeni za wagombea wa CCM kupitia vijana hao na kumaliza tofauti ya Mwakalebela na Mbega. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarest Mangalla, alipoulizwa na gazeti hili alisema hana taarifa zozote, kwa kuwa suala hilo halikuripotiwa ofisini kwake.