Ridhiwani Kikwete Avunja Makundi Iringa Na Kumpatanisha David Mwakelebela na Monica

Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2007
Messages
6,750
Points
2,000
Msanii

Msanii

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2007
6,750 2,000
Asilimia kubwa ya watoto waliozaliwa wakati wazazi wao wapo kwenye madaraka wana mtindio. simtoi RIZ1 ktk kundi hilo. pia amini kwamba nina mashaka hata na NAPE pia maana kumbe kule kuibua kashfa za UVCCM ni kwa sababu alitaka reputation ya kukwaa madaraka ndo maana amejiingiza ktk nafasi mbalimbali za juu kugombea. Na sasa ametulia kwa sababu amepewa uDC ambapo atajipanga na kuingia serikalini. Hivyo suala la akina RIZ1 kuwa wapatanishi ni sawa na kumwomba shetani apatanishe ndoa yenye ugomvi. Ina maana RIZ1 ana hekima sana za upatanishi na kuvunja makundi kuliko wazee na wasomi wenye hekima walioko ndani ya ccm? kwa nini aende yeye. ni kikao gani kilikaa na kupanga timu ya kampeni na kumweka huyo baradhuli ktk team? au timu ya kampeni hupangwa na mgombea?
Kweli kichwa ngumu huwa ni kigumu hata ukiunge kwa nazi na choroko

Sana sana mwakalebela na hao wengine et all watakuwa wamefarijika kutambuliwa na ukoo au familia ya mfalme kuwa atakumbukwa kwenye mgao wa kumbikumbi. Pia ahadi anazotoa RIZ1 kwa hao walioumizwa ni hoax maana baada ya uchaguzi ndipo mtakapofahamu kwa nini walitaka watulie sasa. CCM watatumia kila gharama kushinda ili wakishapata madaraka tena wanaongeza tope kwenye barabara ya kupandisha kilima cha maendeleo.
 
1

1954

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
6,328
Points
2,000
1

1954

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
6,328 2,000
... makundi huvunjwa na watu wenyewe mioyoni mwao wakiridhika sababu zilizosababisha kuwepo kwa makundi...Nakuhakikishia kuwa makundi bado yapo.

Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100.
 
NG'OTIMBEBEDZU

NG'OTIMBEBEDZU

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2010
Messages
842
Points
195
NG'OTIMBEBEDZU

NG'OTIMBEBEDZU

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2010
842 195
Like father like son
Mangula alimwambia jk avunje kundi la mtandao. Hajalivunja! Kinachotakiwa ni kwa huyu "Chief Mwailemale" aanze kuwaunganisha Super Six (SS) na EL maana ndio makundi yalikopata kasi yake.
Yeye mwenyewe pia ni muunda makundi mfano pale Yanga analo kundi, UVCCM imegawika kwa faida yake. Sasa anapita nchi nzima kuvunja makundi au kupima nguvu ya juju ambalo waliliweka na wanahisi limeanza kuishiwa nguvu.
 
Eeka Mangi

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Messages
3,181
Points
1,195
Eeka Mangi

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined Jul 27, 2008
3,181 1,195
Kuna mahali nimesoma RZ1 aliitisha kikao huko Iringa kwenye shule ya msingi hakuna kijana aliyetoka sanasana kulikuwa na watu kama 10 hivi,
Waache wahangaike! AIBU YAO AIBU YETU?
 
Tonge

Tonge

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Messages
696
Points
0
Tonge

Tonge

JF-Expert Member
Joined May 7, 2010
696 0
Pumbavuuuuuuuuu, huyu riz 1 ni kama nani, mijitu mizimaaa Mwaka na Monica imebebwa mikono na huyu kinda wa siasa na maisha, ati anawapatanisha, hivi hii nchi sasa inaongozwa kifalme au? Hamna maana kabisaaaaa, MWAKA HUU CCM CHALI TU.
 
Mr. Zero

Mr. Zero

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2007
Messages
11,329
Points
2,000
Mr. Zero

Mr. Zero

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2007
11,329 2,000
Pumbavuuuuuuuuu, huyu riz 1 ni kama nani, mijitu mizimaaa Mwaka na Monica imebebwa mikono na huyu kinda wa siasa na maisha, ati anawapatanisha, hivi hii nchi sasa inaongozwa kifalme au? Hamna maana kabisaaaaa, MWAKA HUU CCM CHALI TU.
Seriously, nimeshindwa kuelewa na wala siamini inakuwaje huyu kijana anakuwa na nguvu kiasi hiki mpaka watu wazima na akili zao anawapelekesha puta na mtoto mdogo ambaye hata miaka 5 iliyopita tulikuwa hata hatujamsikia.

May be ndiyo sababu ya wazee wa CCM kukaa kimya na kuiachia kazi familia!!!
 
Henge

Henge

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
6,909
Points
1,250
Henge

Henge

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
6,909 1,250
yaani kwa hali hii tulitaka mkapa na mwinyi wafanye nini hapo. ni bora wanapotulia na heshima yao inaongezeka saana tuu. NAWAHESHIMU WAZEE WANGU MWACHENI AANGAIKE MWENYEWE HUYO JK.
 
Kiby

Kiby

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2009
Messages
5,877
Points
2,000
Kiby

Kiby

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2009
5,877 2,000
Baba yake akiwa kama mwenyekiti wa nec iliyompora Mwakalabela ushindi wake alishindwa vipi kutotengeneza makundi kwa kuwaachia wananchi chaguo lao walilolichagua? Hiyo kazi ya ziada mpaka kulazimika kumwahidi mtu U-DC ili amrizishe Monica, kwani kuna mkataba gani na huyu Mbega unaolazimisha gharama kubwa namna hiyo? Hapa wadau kuna walakini kwa mkuu wetu wa nchi
 
Bill

Bill

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
5,366
Points
2,000
Bill

Bill

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
5,366 2,000
Pamoja na usanii wote wa Babake ameshindwa kuvunja makundi itakuwa huyu dogo, asubiri tu hiyo octoba 31 Babake aondoke Ikulu
 
K

Kilembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2009
Messages
1,183
Points
1,250
K

Kilembwe

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2009
1,183 1,250
Alainza baba, kafuatia mtoto inafuata zamu ya Salma sasa, tutaona tena Salam kamshika mkono Mwaka na Monica ne akipiga upatu kuwa kamaliza makundi! Mwaka huu mbona vituko, aaah lakini sawa JK si alisema Urais ni suala la FAMILIA! mimi nasubiri nione na MIRAJI Kikwete nae akiungana na wana familia wenzie!
 
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2009
Messages
2,223
Points
1,225
Jethro

Jethro

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2009
2,223 1,225
Kwa nini makundi ??

Makundi kuwepo ndani ya CCM si ajabu na yatakuwepo tuuu daima kama ni uongozi uliopo na unatumia madaraka vibaya na huku wana CCM wanona kabisa hilo jambo halifaaai. Viongozi wengi walioko madarakani ni watu wasio kuwa makini na utendaji wako pale kwa maslahi fulani fulani na si kukiongoza chama na wanachama wake hii kasumba ya kila mtu anaingia kwa siasa sijui ni imetoka wapi ni kuwa viongozi wameshindwa dhibiti rushwa na kuimarisha uchumi kwa wananchi na ndio maaana watu wanaona siasa ndiko kuna mianya ya kimaendeleo. hii ni mbaya kabisa.

Hivyo basi Riz 1 awemakini kwani asije akawa anajiaandalia maadui wake sasa na huko mbeleni watu watakuwa wameisha mjua udhaifu wake mapema na wengine hawatashindwa sema anatumia cheo cha baba yake kujitafutia uongozi kwa nguvu.
 
N

Nyumbu-

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
979
Points
250
N

Nyumbu-

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
979 250
Kuna mahali nimesoma RZ1 aliitisha kikao huko Iringa kwenye shule ya msingi hakuna kijana aliyetoka sanasana kulikuwa na watu kama 10 hivi,
Waache wahangaike! AIBU YAO AIBU YETU?
Hii hapa....ujue hapo ni unafiki tu; jamaa wana shida na vijana walimgomea! Ptu!


Ridhiwan anusurika kipigo
• Atimua mbio mkutanoni

na Francis Godwin, IringaMTOTO wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete, jana ameonja joto ya jiwe katika harakati za kumnadi baba yake, baada ya kutimuliwa wakati akijiandaa kukutana na wana CCM katika moja ya majengo ambayo kisheria hayaruhusiwi kufanyia mikutano ya kisiasa.
Ridhiwan ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM) taifa, akiwa ameambatana na mshindi wa kura za maoni wa Jimbo la Iringa Mjini aliyeenguliwa, Frederick Mwakalebela na mmoja wa wagombea waliobwagwa, Jescar Msambatavangu, walifika katika Shule ya Msingi Ipogolo, wakitaka kukutana na vijana wa eneo hilo ili mjumbe huyo aweze kuwapatanisha Mwakalebela na mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Monica Mbega.
Kabla ya msafara wa Ridhiwan kufika shuleni hapo kwa ajili ya kikao chake kilicholenga kuvunja makundi ndani ya chama hicho, aliyekuwa mmoja wa wana CCM 12 walioingia katika kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo na kushindwa, Msambatavangu, alipita mitaani kuwaomba vijana kwenda kumsikiliza Ridhiwan, lakini waligoma kwa madai kuwa hawadanganyiki na ujio wake.
Hata hivyo, baada ya vijana hao wa vijiweni kugoma kwenda katika shule hiyo, kwa ajili ya kukutana na mjumbe huyo kwenye chumba cha darasa la pili, bado msafara wa Ridhiwan na wapambe wake walifika huku kukiwa na vijana wasiozidi 10.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia mvutano mkubwa ndani ya ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Amani Mkeremi, kati ya viongozi wa UVCCM mkoa wakiongozwa na Katibu wa Mkoa, Rhoda George na wale wa vyama vya upinzani walioongozwa na Katibu Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata (CHADEMA) wakivutana juu ya CCM kuzuia wanafunzi kuendelea na masomo kwa ajili ya kampeni za uchaguzi.
Tukio hilo ambalo lilitokea majira ya saa 7 mchana lilisababisha mkuu wa shule kupata wakati mgumu kulitolea ufafanuzi, huku walimu wake wakijifungia ofisini kukwepa vurugu iwapo ingejitokeza kati ya wafuasi hao.
Akielezea tukio hilo, kiongozi wa vijana hao wa upinzani, Kimata, alisema walilazimika kuweka mtego katika shule hiyo baada ya kuona hekaheka za makada wa CCM.
"Kweli sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inakataza taasisi za umma kuingia katika kampeni ...sasa tulipatwa na wakati mgumu kuona CCM inatumia shule ya msingi kufanya kampeni ndiyo sababu ya kuweka ulinzi ili kuhakikisha sheria haivunjwi ...tunashukuru tumefanikiwa baada ya viongozi wa CCM kumkimbiza mgeni wa Rais Kikwete," alisema.
Hata hivyo, alisema kabla ya msafara wa Ridhiwan kufukuzwa shuleni hapo, kulikuwa kumetokea mvutano ndani ya ofisi ya mkuu wa shule, huku akitaka watu wa CCM wabaki ndani na wale wa upinzani watoke nje.
Hata hivyo alisema wao wameelekeza tuhuma zao kwa mkuu wa shule hiyo, ambaye amekuwa akionyesha ukada wake wazi wazi dhidi ya CCM hata kuruhusu shule hiyo kugeuzwa jukwaa la siasa kwa CCM.
Kwa upande wake, mkuu huyo wa shule alikiri akisema alipewa taarifa za CCM kuomba eneo la kufanya kikao na si kufanya kampeni na kukusanya vijana kama ilivyokuwa.
Hata hivyo alisema hana barua yoyote ya CCM kuomba darasa katika shule yake kwa ajili ya kufanya kampeni hizo.
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Iringa Rhoda, ambaye alikuwa mwenyeji wa Ridhiwan, alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi hakuweza kupokea, zaidi ya kukata.
Hata hivyo mmoja wa makada waliopo katika msafara huo alisema kikao hicho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kampeni za wagombea wa CCM kupitia vijana hao na kumaliza tofauti ya Mwakalebela na Mbega. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarest Mangalla, alipoulizwa na gazeti hili alisema hana taarifa zozote, kwa kuwa suala hilo halikuripotiwa ofisini kwake.
 
Nyange

Nyange

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Messages
3,226
Points
2,000
Nyange

Nyange

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2010
3,226 2,000
Hivi wakuu, huyu kijana mbona anazidi ku-lost/ Kwani babake akikosa uraisi atakula nini? kwani kazi yake ninini? mbona anashughurika na issue za babake? sisi kikwetumtoto akimaliza dalasa la saba, huwa anapewa kisehemu na wazazi wake, anajenga kijinyumba kando ya nyumba ya wazazi, halafu anafanya shughuri zake kivyake. Huyu kijana kama vile anasoma shule ya msingi!!. Yawezekana nati moja au mbili kichwani zimelegea!
 
K

kingwipa1

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2008
Messages
336
Points
195
K

kingwipa1

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2008
336 195
Hii imekaaje wana JF, Kweli Mwakalebela ana furaha au basi tu kakubali yaishe.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)Taifa, Ridhiwani Kikwete ,amewakutanisha Monica Mbega na Davidi Mwakalebela baada ya kuwapatanisha na kuvunja makundi katika kikao cha Baraza la Vijana mjini Iringa jana.
Monica ni mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini na Mwakalebela alienguliwa kuwania nafasi hiyo
Kubwa zima linajidhalilisha kwa kitoto eti limepatanishwa. Ukisikia ujuha ndo huooo!!! Na U-DC huupati ng'o, mwaka huu ni BOB Sila!! Angalia kipindi cha Uswazi cha eatv.
 
mzozaji

mzozaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2010
Messages
255
Points
0
mzozaji

mzozaji

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2010
255 0
He haya maajabu ya Musa.. Ina maana baba alishindwa kazi ndogo kama hiyo ndio akaiweza mwana? Kweli kuna tatizo..
 
N

Nsesi

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2008
Messages
374
Points
195
N

Nsesi

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2008
374 195
Mgogoro uliopo Jimbo la Iringa Mjini ni wananchi na uongozi wa CCM ambao ulikataa chaguo lao. Leo hii kuwakutanisha Mwakalebela na Monica eti ndio kuvunja makundi ni kujidanganya na ushahidi kwamba CCM imeishiwa, iko ICU ikisubiri kufanyiwa operation hapo Okt 31.

Mwakalebela kajidhalilisha, watu wazima kukalishwa na katoto huku kakiwafokea nao wakakubali inadhihirisha kwamba tuhuma zinazomkabili ni za kweli.
 
N

Nsesi

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2008
Messages
374
Points
195
N

Nsesi

JF-Expert Member
Joined Nov 20, 2008
374 195
Like father like son
Mkuu F2S,

Hii imekaa vizuri sana. Tofauti yao ni kwamba baba mrefu mtoto mfupi lakini mengine huhitaji kuelezwa, sura, akili, uelewa, vijitabia nk huulizi!!!!!
 

Forum statistics

Threads 1,343,116
Members 514,943
Posts 32,774,403
Top