Tatizo siyo Msigwa wana Iringa ndiyo waliwakataa CCM!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,307
33,925
Yaani hivi sasa CCM hapa Iringa wako bize kupambana na Peter Msigwa Mbunge wa Iringa mjini. Yaani harakati zao ukiziangalia wakati mwingine ni kama vile wamepata wazimu.

Jimbo la Iringa mjini limeshawahi siku za nyuma kuongozwa na Mfalamagoha Kibasa toka NCCR- Mageuzi wakati huo kwa miaka mitano 1995-2000 na baada ya hapo CCM kupitia kwa Monica Mbega ikaongoza kwa miaka kumi 2000 - 2010 alipochukua Msigwa.

CCM wanajifaragua kwamba kuchaguliwa kwa Msigwa kunatokana na makosa yao wenyewe lakini wanajisahaulisha kwamba Iringa walishawahi kuwakataa mwaka 1995. Iringa kuikataa CCM hakutokani na Msigwa hata kama yeye ni sehemu ya kichocheo cha kukataliwa kwa CCM kwani CCM kukataliwa Iringa ni Historia ya tangu mwaka 1995.

Msigwa mwaka 2015 alimpita mpinzani wake David Mwakalebela kwa zaidi ya kura elfu kumi kwa kupata kura 43, 154 dhidi ya kura 32,406 za Mwakalebela. Ukiangalia tofauti ya kura hizo zaidi ya elfu kumi utagundua kwamba ni wana Iringa ndiyo waliikataa CCM na si Msigwa peke yake.

CCM wanatafuta sababu zisizo na mashiko kumdhuru Msigwa kibinafsi na wala si kupambana naye kisiasa. Udhaifu wa CCM Iringa ni mkubwa kiasi kwamba haiwezekani bila ya dola kushinda uchaguzi wa Ubunge mwaka 2020.
 
Hofu ya nini mkuu mbona bado mapema?
Au tumuambie msigwa atue mzigo?
 
Hii inaitwa ukiweka maji naweka pilipili...

Sasa ndio utaelewa pilipili inatoka kwa maji?
 
Nyie ndio mmepanick. Kama mapema mbona wenzako wanazunguka hapa mjini kama wamewehuka?
Were mleta huu Uzi unatatizo la kutokutembea ujifunze Nadhani hapo iringa government hospital haina wodi ya vichaa njoo huku mirembe uone jinsi wagonjwa wa kichaa anavyopata matumaini ya kutoka wodini kila ukimtembelea na madaktari watakuambia nenda nae tu kichekesho mgonjwa huyo atang'ang'ania atoke na uniform za hospitali hapo ndo utajua ndugu yako hajapona kisawasawa
 
MABAKULI sasa hapo ndiyo umeandika nini?
CCM ni vichaa ambao iringa hawatarudi mpaka waache ukichaa wao Jana kuna mccm ameanza kumtaja mfugale atachukuwa iimbo kisa ni MTU wa iringa na jpm anamsifia mfugale Nao wanajifanya wana akili kama jpm niambie akiwa mbunge Huyo mfugale Ccm Ukichaa wao huo utakuwa umepona kweli na hasira na Ccm kujifanya machizi fresh samahani Allen kilewella verified user hasira zinanifanya usinielewe basi ccm iringa msiwape uongozi hata wsa mtaa tu
 
Umeondoa picha yako kama kawa unapokuwa mguu mmoja nje mwingine kuvizia ndani kupandishwa lori la Magufuli.. eeeeh

RC Hapi ataipaisha CCM sanaaa Iringa
Upinzani ni kuanza kujipakia wawezavyo.. ila wasiibe tu kama walivyozoea.. 😁

Kideo cha jana kilikuwa live hadi usiku..
 
Duh!! Mi nimejaribu kusoma mpaka kwa "rivasi" lakini wapi!! Sijaelewa kitu!
Ccm iringa wanadhani watarudi madarakani kwa kutuletea wagombea wenye urafiki na jpm kwa lipi alichokifanyia hapa Hao friends of jpm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom