OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 428
Wadau,hii ni sehem
ya mahojiano kati ya riz na gazeti la mwananchi!!hapa sasa ndio mtaona kwamba ile adhabu ilimlenga lowassa moja kwa moja,Lowassa kabaki kimya ila bado wanahaha kivuli chake.Mods naomba usiunganishe huu uzi na niwaombe msiuondoe watanzania wajionee mtoto wa rais alivyo lewa madaraka
Hata hivyo, Ridhiwani alidokeza kuwa wapo baadhi ya wanasiasa watakaokwama kufikia lengo hilo kutokana na kukabiliwa na kesi ndani ya chama, ambazo hakuzitaja wala kutaja wahusika.
Kuna watakaopungua kutokana na kesi zinazowakabili katika chama ambazo zinawafanya wapungukiwe sifa. Kwa maana hiyo kuna watu kama wanne hivi (wa Bara) unawatoa na ukiwatoa unabakiwa na watatu, sasa unaweza kujiuliza hao watakaobaki watatu, je, wanatosha?
Alipotakiwa kueleza iwapo angepewa nafasi ya kuteua mgombea mmoja wa CCM atakayepambana na vyama vingine katika uchaguzi mkuu mwakani, Ridhiwani alijibu kwa ufupi kuwa akisema, Hilo siwezi kujibu.
Amsaidia Membe
Ridhiwani pia alizungumzia uchaguzi wa ndani ya CCM akikiri kuwa alimsaidia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Membe kushinda ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Ni kweli katika uchaguzi wa NEC nilimsaidia Bernard Membe. Nilimsaidia si kwa sababu ya kuwa katika kundi lolote, ila nilimwona kuwa ana sifa ya kuingia kwenye NEC, hili jambo lazima watu waelewe, alisema Ridhiwani.