Ridhiwani Kikwete ataja 11 wanaotosha kugombea urais 2015

aseme mrithi wa jimbo la chalinze sio kusemea watanzania. asubiri chama chake kiteuwe huyo anayeweza kurithi safari za baba yake na upromota maana ndo kaz aliyoifanya kwa ufanisi baba yake
 
Mi ccm inawaza urais tuu!hizi demokrasia za kutawala miaka 10 ni hasara kwa nchi za kimasikini

bado wanawaza kuendelea kuongoza wakati mwisho wao umeshakaribia ukawa ni sumu ya kuuwa ccm na vibaraka wake wote
 
huyu dogo ameongea kaiwa kama nani????
I aksed my self the same question!

Atakuwa anajipanga kuhakikisha kuwa atakayeingia madarakani hana mpango wa kuwafuatilia na mali zao walizochuma!

Uchaguzi huu una Interests siyo tu kwa watakaoingia madarakani, bali pia wale wanaoondoka madarakani wana Interest kubwa kabisa, pengine kuliko wanaotaka kwenda ikulu!!

Na pia zama hizi kweli zimebadilika...Maana miaka ya nyuma, kauli kama hizi, tulizisubiri kutoka kwa vigogo ama wazee wa ccm ie mwalimu Nyerere!

Sasa hivi pesa ina power zaidi ndani ya ccm, hata wazee kama kina Mwinyi, Warioba, Butiku et al, hawana sauti kihivyo!
 
yani hiki kimwizi nacho kimekuwa kijitu cha kutubashiria rais? we are too low.. gazeti la mwananchi limekosa wa kuwahoji au ndo kujipendekeza
 
ANAWATAJA AKIWA KAMA NANI NDANI YA CHAMA,JE CHAMA KIMEMRUHUSU KUFANYA HIVYO,AU NI MAONGEZI WAYAFANYAYO NA BABA YAKE,KWELI CCM IMEKOSA UTAWALA WA KIPROTOCALY,NADHANI HI HAIKUWA KAZI YAKE KUZUNGUMZA LOLOTE KUHUSUANA NA HILO "the family has capture the govenment to its pocket why so?
 
...maajabu haya kumbe CCM ina wenyewe ni kauli ya ukweli kabisa!Ridhiwani hawezi kunisaidia mimi,baba yangu wala ndugu yangu sb hana issue nasi,alimsaidia membe ili ampe uwaziri akiwa rais huo ndio ukweli na membe ndio chaguo la mzee pia,hakika vyeo hivi vya kupeana na kupokezana kama ile riadha ya vijiti hakika safari hii hatuta kubali,hii ni nchi yetu sote,kama hivyo afadhali yai livunjike.

Yai likivunjika Masud Kipanya atatupa adhabu ya kubebaba watanzania wote kwa mara moja
 
Jamani mbona Hajamtaja mtu Ambae anatarajiwa kuwa ndio kiongizi msafi asie na makundi,ambae watu wengi wanatajia kuwa ndio atakuwa mrithi wa kikwete ambae ni Mh waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Peter Pinda.

Alishasema Hagombei yeye
 
ANAWATAJA AKIWA KAMA NANI NDANI YA CHAMA,JE CHAMA KIMEMRUHUSU KUFANYA HIVYO,AU NI MAONGEZI WAYAFANYAYO NA BABA YAKE,KWELI CCM IMEKOSA UTAWALA WA KIPROTOCALY,NADHANI HI HAIKUWA KAZI YAKE KUZUNGUMZA LOLOTE KUHUSUANA NA HILO "the family has capture the govenment to its pocket why so?

kwrli kabisa wasije wakawa wanakaa baba mama mtoto wanatupangia .....dogo huyo sjui vipi
 
Huyu ridhiwani kichwani ni mweupe pee kama baba yake.
Hapo hamna kitu. ....hawawezi kupeana urais kishkaji..tutachagua rais tunayemtaka na sio hao huyu kilaza alio wataja...hii nchi sio yao.
 
====
Mimi nikiwa Mtanzania nasikitishwa sana na kauli za kujirudia rudia za Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe akitumbukiza Tanzania katika LAANA. Mara hii Membe ananukuliwa na Vyombo vya Habari akilaani ISRAELI kwa mauaji yanayoendelea huko Gaza.
Mimi binafsi nimefuatilia vyanzo vingi vya Habari kuhusu yanayoendela Gaza, na haya ndiyo mambo 6 niliyojifunza:

  1. Hamas inayoongoza Gaza ndio walianzisha misuguano hii kwa kuwateka vijana watatu wa Israeli na kasha kuwaua. Kitendo hiki kilipongezwa sana na Hamas huko Gaza, kuashiria palikuwa na mahusiano ya moja kwa moja kati ya watekaji na chama hiki cha Hamass.
  2. Hamas walikuwa wakirusha roketi kuelekea miji ya Israeli bila kujali yatawaua raia au la, kitendo ambacho ni cha uchokozi.
  3. Israeli inatumia teknolojia kubwa sana kuyaharibu maroketi hayaya Hamas kwa kutumia IRON DOME SYSTEM kabla hayajaleta madhara yoyote. Ndiyo maana hadi sasa, hakuna muisraeli hata mmoja ameuliwa na roketi hizi zaidi ya 1,000 zilizorushwa na Hamas hadi sasa.
  4. Hamas haitambui uwepo wa Israeli. Kwa maana nyingine, Hamas katika ILANI yao, wameapa kuwafurukusha Israel wasiwepo kabisa eneo lote la Mashariki ya Kati.
  5. Hamas wanahamasisha raia wa Gaza wasiondoke maeneo yale hatarishi ili watumike kama ngao ya kibinadamu (human shield) wakidhani Israeli itawaacha warushe tu roketi,
  6. Israeli inatumia njia za kisayansi kuwatumia watu wa Gaza meseji kwenye simu zao kuwatahadharisha wasiende maeneo yanayotarajiwa kupigwa mabomu. Hili ni jambo la kistaarabu sana, huwezi kulitarajia wakati wa vita. Ubishi wa tahadhari kama hizi ndio umepeleka raia wa Gaza kudhuriwa na mashambulizi ya Israeli.
Baada ya maelezo hapo juu, tujiulize kama Taifa, Je, Membe alitaka Israeli wakirushiwa maroketi na Hamas wakae kimya wasiyajibu? Membe ukiwa Waziri wa Mambo ya Nje, upo tayari kuona miji ya Dar es Salaam au Dodoma ikirushiwa maroketi na nchi jirani, na Tanzania tukaae kimya tu kwa sababu Tanzania ikijibu inaweza kuua raia wa hiyo nchi ya jirani chokozi?
Waziri Membe umeonesha udhaifu mkubwa ulio nao katika tasnia ya mambo ya nje kwa kutojua historia ya mgogoro huu, na kitendo chako cha kuegemea upande mmoja ni cha aibu na fedheha kwa wizara unayoongoza. Miaka ya nyuma uliwahi pia kunukuliwa ukilaani Israeli pale ulipoalikwa kama mgeni wa siku ya Palestina katika Ubalozi wao hapa Dar es Salaam.
Waziri Membe tunakuhakikishia kuwa, kiitendo chako cha kuilaani Israeli hakiwezi kupita kimya bila kupingwa na Watanzania. Umelaani Israeli lakini laana yako ikurudie wewe mwenye na familia yako. Ni aibu kubwa kwa mtu kama wewe unayetamani kuongoza ofisi kubwa kuliko zote hapa Tanzania (IKULU) unatamka maneno ya laana.
Imeandikwa, HESABU 23: 8 “Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani? Nimshutumuje, yeye ambaye Bwana hakumshutumu?” , Ni wazi kuwa Anayelaani ISRAELI naye ANALAANIWA. Anayebariki ISRAELI naye ANABARIKIWA. Tunamshukuru Mungu kwa kutuonesha Moyo ulio nao ili waakati wako wa kugombea urais ukifika tukuweke kwenye jalala la milele. Waziri Membe Umetegwa kwa maneno ya kinywa chako mwenyewe.
 
Huyu ridhiwani iko siku atakiona cha moyo , maana anafikiti hii nchi niya baba yake na familia yao...kwa hiyo anasema anachotaka.
 
Back
Top Bottom