Ridhiwani Kikwete apiga Marufuku Watumishi wa Umma kwenda Dodoma Kufuatilia Masuala Binafsi ya Kikazi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,064
49,749
Mawaziri dizaini ya Hawa wanakuwa wamevimbiwa madaraka,Kuna mtumishi wa Umma Huwa anaenda Dodoma kujifurahisha?

Ukiona hivyo ujue mambo ni pending na ya muda mrefu kiasi huyo Afisa Utumishi anakosa jawabu la Moja kwa Moja.

Kabla ya kutoa Kauli za ajabu ajabu muwe mnatafakari kwanza.
---

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amepiga marufuku tabia ya baadhi ya maofisa utumishi kutoa vibali vya safari kwa watumishi kwenda Dodoma, kufuatilia masuala binafsi ya kiutumishi.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, hiyo ni kazi ya maofisa utumishi hao, kwani wengi wa watumishi wanaokwenda Dodoma, hufuatilia masuala yahusuyo kupandishwa madaraja, kubadilishiwa miundo na kada, au kudai malimbikizo ya mshahara.

"Vitendo kama hivi, vinawanyima wananchi haki yao na fursa ya kuhudumiwa na watumishi hao ambao hulazimika kusafiri na hivyo kuwa nje ya vituo vyao vya kazi," amesema.

Ridhiwani ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, ikiwa ni siku yake ya tatu ya ziara anayoendelea kufanya mkoani Mara, ambapo amewataka maofisa hao kuleta matumaini kwa wenzao.

"Acheni ile tabia ya kuonekana miungu watu, tatueni matatizo ya watumishi," amesema.

Pia amewaagiza maofisa utumishi wa halmashauri zote nchini kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake watembelee ofisi zilizopo katika kata na vijiji ili kutatua changamoto za watumishi walioko huko.
 
mifumo ya kidigitali inatosha ulimwengu wa sasa
Swala sio kidijitali swala ni kutatua tatizo
Hadi Waziri wa Afya anaongea haya unadhani Hali ikoje?
---
Ummy: Watumishi wa Afya wanapaswa kulipwa stahiki zao kwa wakati

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael, kuwahimiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuwalipa watumishi wa Afya stahiki zao kwa wakati.

Waziri Ummy ameyasema hayo wakati akiongea na wajumbe wa Timu za Usimamizi na Uendeshaji wa huduma za Afya ngazi ya Mkoa (RHMT) na Halmashauri zote za Mkoa (CHMT) na Wajumbe wa Timu ya Uendeshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (RRHMT) wakati akihitimisha ziara yake katika Mkoa wa Songwe.

"Naomba sana Mkuu wa Mkoa kupitia kwako kuwahimiza Wakurugenzi kuwalipa watumishi wa Afya stahiki zao kwa wakati ili wapate moyo wa kuendelea kutoa huduma katika vituo vyetu vya Afya," amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema Wakurugenzi wengine waige mfano wa Mkurugenzi wa Momba ambaye amewagawia viwanja watumishi wa Afya. Hivyo, lazima kuwajengea motisha na kuwavutia watumishi hao wa Afya ili waendelee kufanya kazi katika Halmashauri za Mikoa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. Francis Michael, amemuomba Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kupeleka watumishi wa Afya hasa madaktari Bingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.
 
Back
Top Bottom