Ridhiwani Kikwete ang'aka tena

Ridhiwani Kikwete ang'aka tena

Red one

Member
Joined
Apr 22, 2011
Posts
99
Reaction score
26
Mtoto wa Rais Kikwete ang’aka

MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, amesema hataki kufuatiliwa maisha yake na wanasiasa hasa wanaomtuhumu kuwa ni bilionea huku akisisitiza kuwashughulikia waolimchafua.

Ridhiwani, alisema hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima akitakiwa kueleza hatua atakazochukua baada ya muda wa siku saba aliowapa Mwenyekiti wa Demokratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa kupita.

Awali, mtoto huyo wa Rais aliwataka wanasiasa hao wamwombe radhi katika kipindi cha siku saba vinginevyo angewapeleka mahakamani kwa kuwa wamemchafua pamoja na familia yake.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu, ili kujua lini angekwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka viongozi hao, alijibu kwa jazba kwamba jambo hilo linahusu maisha yake hivyo haoni sababu ya kufuatiliwa na vyombo vya habari.

“Jambo la kuwafikisha wanasiasa hao mahakamani si jambo lenu, hilo ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu hivyo nitachokifanya nakijua mwenyewe,” alisema Ridhiwani huku akisisitiza kwamba hata alipozungumza na waandishi wa habari juma lililopita alisema lengo lake ni kuueleza umma na sio kufuatiliwa maisha yake.

Kwa nyakati tofauti Mchungaji Mtikila na Dk. Slaa, walimtuhumu Ridhiwani kwa ukwasi huku wakiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumchunguza.
 
mtoto wa rais kikwete ang'aka

mtoto wa rais jakaya kikwete, ridhiwani, amesema hataki kufuatiliwa maisha yake na wanasiasa hasa wanaomtuhumu kuwa ni bilionea huku akisisitiza kuwashughulikia waolimchafua.

Ridhiwani, alisema hayo jana alipozungumza na tanzania daima akitakiwa kueleza hatua atakazochukua baada ya muda wa siku saba aliowapa mwenyekiti wa demokratic party (dp) mchungaji christopher mtikila na katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) dk. Willbrod slaa kupita.

Awali, mtoto huyo wa rais aliwataka wanasiasa hao wamwombe radhi katika kipindi cha siku saba vinginevyo angewapeleka mahakamani kwa kuwa wamemchafua pamoja na familia yake.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu, ili kujua lini angekwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka viongozi hao, alijibu kwa jazba kwamba jambo hilo linahusu maisha yake hivyo haoni sababu ya kufuatiliwa na vyombo vya habari.

"jambo la kuwafikisha wanasiasa hao mahakamani si jambo lenu, hilo ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu hivyo nitachokifanya nakijua mwenyewe," alisema ridhiwani huku akisisitiza kwamba hata alipozungumza na waandishi wa habari juma lililopita alisema lengo lake ni kuueleza umma na sio kufuatiliwa maisha yake.

Kwa nyakati tofauti mchungaji mtikila na dk. Slaa, walimtuhumu ridhiwani kwa ukwasi huku wakiitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) kumchunguza.

tzs : 3, 800, 00/=
shilingi: Shilingi milioni tatu na laki nane

$300, 000
usa dollars: Two hundred thousand
 
Anakula matapishi yake huyo mtoto. Alisema atawapeleka mahakamani Dr Slaa na Mtikila baada ya siku saba kupita kama hajaombwa msamaha, muda umefika na wananchi wanataka kuona ahadi aliyoitoa kama ataitimiza. Hiki kitoto kilikuwa kinatingisha kiberiti, sasa moto umeanza kumuunguza. Mahakamani atapelekwa yeye na lazima atueleze mabilioni hayo kayapata wapi, vinginevyo ni mwizi akanyee debe akakutane na akina papiii.
 
Mtoto wa Rais Kikwete ang'aka

MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, amesema hataki kufuatiliwa maisha yake na wanasiasa hasa wanaomtuhumu kuwa ni bilionea huku akisisitiza kuwashughulikia waolimchafua.

Ridhiwani, alisema hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima akitakiwa kueleza hatua atakazochukua baada ya muda wa siku saba aliowapa Mwenyekiti wa Demokratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa kupita.

Awali, mtoto huyo wa Rais aliwataka wanasiasa hao wamwombe radhi katika kipindi cha siku saba vinginevyo angewapeleka mahakamani kwa kuwa wamemchafua pamoja na familia yake.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu, ili kujua lini angekwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka viongozi hao, alijibu kwa jazba kwamba jambo hilo linahusu maisha yake hivyo haoni sababu ya kufuatiliwa na vyombo vya habari.

"Jambo la kuwafikisha wanasiasa hao mahakamani si jambo lenu, hilo ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu hivyo nitachokifanya nakijua mwenyewe," alisema Ridhiwani huku akisisitiza kwamba hata alipozungumza na waandishi wa habari juma lililopita alisema lengo lake ni kuueleza umma na sio kufuatiliwa maisha yake.

Kwa nyakati tofauti Mchungaji Mtikila na Dk. Slaa, walimtuhumu Ridhiwani kwa ukwasi huku wakiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumchunguza.
My hairs!
Hii ni kali!
Hapa hashitakiwi mtu hata ikiisha miaka 10!
Dogo keshastuka, hataki matatizo!
Kagundua kuwa kupima OIL kwa baadhi ya watu si jambo la mchezo!
 
My hairs!
Hii ni kali!
Hapa hashitakiwi mtu hata ikiisha miaka 10!
Dogo keshastuka, hataki matatizo!
swahiba... the only danger naiona hapa ni arrogance ya dogo while there are only 4 year left kwa baba kulinda familia, if it was me, i would be very careful with what i say to anyone

Tanzania iko kwenye mapito makali sana na kauli yoyote ile ni muhimu sana hasa ukiwa kwenye limelight

Nina story ya mtoto wa waziri wa siera leone ambaye ni rafiki yangu akisimulia yaliyomtokea, unaweza kupata kichaa... yeye amekimbilia UK

mlio karibu, mshaurini dogo akae kimya au hata asijibu chochote kwa waandishi, silence can be the best noise one can make
 
Alijibu kwa jazba kwamba jambo hilo linahusu maisha yake hivyo haoni sababu ya kufuatiliwa na vyombo vya habari.

“Jambo la kuwafikisha wanasiasa hao mahakamani si jambo lenu, hilo ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu hivyo nitachokifanya nakijua mwenyewe,”

Hapa ndipo anaponishangaza! Aliwaita waandishi kwa moyo safi nao wakaitikia wito. Akapiga mikwara mbuzi yake na ahadi zake, waandishi wanafanya follow up, kwa nini anawakasirikia? Kama ni jambo lake na hakutaka kushirikisha watu angewafuata Dr Slaa na Mtikila awaeleze kimya kimya? Maji ukiyavulia nguo....
 
Mtoto wa Rais Kikwete ang'aka

MTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, amesema hataki kufuatiliwa maisha yake na wanasiasa hasa wanaomtuhumu kuwa ni bilionea huku akisisitiza kuwashughulikia waolimchafua.

Ridhiwani, alisema hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima akitakiwa kueleza hatua atakazochukua baada ya muda wa siku saba aliowapa Mwenyekiti wa Demokratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa kupita.

Awali, mtoto huyo wa Rais aliwataka wanasiasa hao wamwombe radhi katika kipindi cha siku saba vinginevyo angewapeleka mahakamani kwa kuwa wamemchafua pamoja na familia yake.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu, ili kujua lini angekwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka viongozi hao, alijibu kwa jazba kwamba jambo hilo linahusu maisha yake hivyo haoni sababu ya kufuatiliwa na vyombo vya habari.

"Jambo la kuwafikisha wanasiasa hao mahakamani si jambo lenu, hilo ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu hivyo nitachokifanya nakijua mwenyewe," alisema Ridhiwani huku akisisitiza kwamba hata alipozungumza na waandishi wa habari juma lililopita alisema lengo lake ni kuueleza umma na sio kufuatiliwa maisha yake.

Kwa nyakati tofauti Mchungaji Mtikila na Dk. Slaa, walimtuhumu Ridhiwani kwa ukwasi huku wakiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumchunguza.

Hii kama ni kweli basi Ridhiwani kaogopa kwenda kuumbuka mahakamani, hivyo ni kweli yeye ni bilionea na wala si uongo
 
Ewe Dr Slaa na Mch Mtikila mnaongoza kundi la watz wenye uchungu na nchi hii tafadhari mfungulieni kesi huyu m.s.e.n.g.e R1 Kwani mali za watz zinaliwa na hii familia ya pale MSOGA BAGAMOYO huku baadhi ya watz wanaishi chini ya mstari wa kimataifa wa umasikini tsh 260!
 
swahiba... the only danger naiona hapa ni arrogance ya dogo while there are only 4 year left kwa baba kulinda familia, if it was me, i would be very careful with what i say to anyone

Tanzania iko kwenye mapito makali sana na kauli yoyote ile ni muhimu sana hasa ukiwa kwenye limelight

Nina story ya mtoto wa waziri wa siera leone ambaye ni rafiki yangu akisimulia yaliyomtokea, unaweza kupata kichaa... yeye amekimbilia UK

mlio karibu, mshaurini dogo akae kimya au hata asijibu chochote kwa waandishi, silence can be the best noise one can make
Kumbe sasa nimegundua kwa nini familia nzima ilichangamkia kampeni za "Urahisi" wa Mzee wa kuchakachua a.k.a. Dr. wa kubumba wa chama cha Magamba! Kumbe walikuwa wakiulinda ulaji wa familia na si uchungu wa nchi.
 
Hivi inakuwaje mtoto baba yao ni rais na wewe unataka kuwa front line kwenye siasa. Kwa nini usifaidi mambo nyuma ya pazia tu . Watu wengine sijui hawana washauri.

Sijui kwa nini huyu Riz alikimbilia kwenye mambo ya siasa. Anamuharibia baba yake na yeye mwenyewe.
Timig yake ya kuingia kwenye siasa tena front line ni mbaya

JK leo kawaambia mawaziri kuna mambo ukikubali kuwa waziri inabidi ukubali kuyakosa. Je hajamawambia rizwani na familia yake haya kama mtoto au familia ya wa rais kuna vitu vingine wavipotezee tu na waendele kufaidi mambo nyuma ya pazia
bila kuwa front line
 
mimi nilijua tu haya ndiyo yatatokea , siku saba ni kidogo sana kuchakachua mambo.
nadhani mganga wake alimdanganya----ohoo kawambie wakuombe radhi!!!
alikuwa naongea mpaka mate yanamtoka na misemo kibao ---makanjanja
sasa hasubiri moto wa mtikila---- atakwenda kujifunza huo u-lawyer kwa vitendo kwa kushinda mahakamani na mtikila.
yeye anajifnya rofa wakati hao wahandishi wa habari alikutana nao new africa hotel hiyo hela ya ukumbi nani alimlipia?
au kawakopa.
mwambie na mama hapo hela za hiyo saccos anayokwenda kuchangisha mabilioni USA na hatuone mahesabu yake sio muda naye hataanza kujikuna upupu
sijui naye mkwara wake utakuwa siku ngapi?
 
At least if he would have stayed quite it would have made more sense
 
Wacha1, lugha nyingine hizi, zinaishushia heshima jf yetu mbele ya jamii!.

Ni mtazamo wake lakini.
Ni sawa tu na Rz1 alipowaita waandishi na kuwaambia kuwa anatoa siku 7 kwa Dr. Slaa na Mtikila, waandishi wanafanya follow up anawajia juu; hiyo nayo si kujishushia heshima yeye na ikulu.
 
Alifanya kosa kubwa sana kuzungumza na wanahabari kuhusiana na swala hilo, sasa hana jinsi itabidi aende tu mahakamani na asipoenda swla hili litamtafuna yeye na familia yake.
 
Hapa ndipo anaponishangaza! Aliwaita waandishi kwa moyo safi nao wakaitikia wito. Akapiga mikwara mbuzi yake na ahadi zake, waandishi wanafanya follow up, kwa nini anawakasirikia? Kama ni jambo lake na hakutaka kushirikisha watu angewafuata Dr Slaa na Mtikila awaeleze kimya kimya? Maji ukiyavulia nguo....

Yote hiyo ni katika kuchanganyikiwa. Maji yamekuwa marefu. Like father like son....
 
Back
Top Bottom