Ridhiwani Kikwete akanusha tuhuma juu yake na kusema ni uhalifu wa mtandao!

Kuna utata gani kwenye tamko la Riz jamani kama si kumfanyia roho mbaya na wivu wa kike?. Kikwete anapokea watoto wa kambo nanyinyi mnaweza kuomba kuwa watoto wa kikwete ili muache wivu.

Hiyo singo ya 'wivu' tena 'wivu wa kike' imeishazoeleka sana katika masikio ya wabongo - magamba hayataki kukosolewa na hivyo kila anayejaribu kuwakosoa wanamchezea singo hiyo hiyo. Huyu kijana kama alivyo mzee wake wanapaswa kujitambua kuwa ni watu maarufu sana nchini, kwa hiyo hawana budi waache tabia za uswahili za kuzungumzia masuala mazito kwa kutumia mipasho. Tunawaheshimu sana na hivyo na wao wanahitajika kujiheshimu. Hili ni mojawapo ya fundisho - matumaini bwana mdogo ataanza kuwa mwangalifu kabla ya kufungua kinywa chake.
 
Kati ya Chadema na CCM ni chama kipi hakiko tayari kukoselewa mkuu?. Chadema hawako tayari kusikiliza na wala kukosolewa hata kabla hawajachukua madaraka. Wakichukua madaraka si itakuwa hatari hapa Tanzania?. Chadema ukiwakosoa kidogo unafukuzwa uanachama mara moja. lakini CCM kila siku watu wanaikosoa na inachukua yale yaliyo mema inayafanyia kazi na yale ya kipuuzi inayaacha. leo hii bila haya unasema CCM haitako tayari kukosolewa?.
 
Usiandike kitu usichokijua, toka lini huyu kilaza akawa na Masters degree? Alipokwenda kule Hull University alitunukiwa CERTIFICATE na sio degree!! Hana uwezo wa kupata shahada ya pili!!!!!!!
unajua mkuu Ndinani, sisi wengine huwa tukisikia maelezo ya awali tunajua yatafanana na mwisho (the beginning resembles the end). Mimi nilisikia anakwenda UK kufanya Masters na mara nyingi sijawahi kusikia mtu anaenda kusoma Ulaya akashindwa kupata alichofuata, hapo kwenye red sasa haya mapya!
 
Usilolijua ni usiku wa kiza!!! Soma thread aliyoandika akijitambulisha kuwa yeye ni partner wa law firm moja hapo Dar; mule umeandikwa wasifu wa huyo jamaa.
 
kweli hapo nashangaaa sana kila siku anajisafisha kuwa sio yake. au anapima joto la watu?
 
Habari wanaJF!

Ridhiwani Kikwete alikuwa akihojiwa na Star Tv amesema ahusiki kwa namna yeyote na yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusiana na suala la Absalom Kibanda.

Amesema kuna mtu aliingia na kuandika maneno yale ambayo yamesababisha atukanwe sana na watu,amesema kwamba ametoa taarifa polisi na uchunguzi unaendelea,

Vile vile amesema hata suala la John Mnyika ya kwamba alimkashifu kuwa hajasoma sio kweli,yeye hajawahi kuandika maneno hayo bali ni watu wanamchafua kwa kutumia ukurasa wake na amedai kwamba huo ni uhalifu wa mtandao na anaomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi!

UPDATE:
Wakuu sijui mimi ni uelewa wangu mdogo, hiyo taarifa iliandikwa Tar: 17th Mar 2013, ikapostiwa Tar: 15th Mar 2013 hapo kuna nini kama si umagumashi?????
 
Sijui kama nimekuelewa vizuri , hapa unazungumzia kinywa cha nani - mimi binafsi au victim wa scam za mtandaoni!! Mkuu niseme hivi - unaweza kufikili maneno mawili niliyo tumia hapo juu hayana maana yoyote, wewe ukahamua ku-stick 2 your GUNS for reasons best known 2 yourself and your like mind!!

Tangu lini siku za nyuma ukasikia kuna baadhi ya wasomaji wa magazeti ya Serikali au watu binafsi wamefanikiwa kuingilia printing press na ku-doctor makala za wahandishi wa habari bila hidhini ya mwendesha mitambo au mhariri mkuu, lini umesikia watu waliwahi kwenda posta kufungua masanduku ya barua za wateja na kuzifanyia usanii? Kwa kifupi nilipo kuwa nazungumzia SNAIL-MAIL nilikuwa nazungumzia mfumo huo wote wa stone age technology - hupo hapo mkuu.

Oh, karibu nisahau kitu cha muhimu!! Mara ngapi umesikia watu wana-wafanyia usanii picha za watu, kukutumia E-Mail wakati hajawapa hata E-Mail address zako, wakafungua address folder/book ulizoweka majina ya rafiki zako na wana uwezo wa kuwatumia E-Mail bila ya wewe kujua, wakajua website unazo tembelea mara kwa mara, wakajua speed unayotumia kuandika text au tuseme alphanumerical characters kweye keyboard yako, wakajua browser na operating system na aina ya microprocessor ndani ya system yako, wakaingilia mpaka wizara ya ulizi ya Merikani na Pentagon na nchi nyingine, simu za mikononi na ATM and what have you!

Nilipokuwa nazungumzia dot.com/E-Mail nilikuwa namaanisha tekinolojia ya kileo, ambayo hakuna mtu yeyote ambaye atakuwa salama akisha amua kufunga chombo chake kwenye INTERNET basi unajiweke tayari kujikuta amefungulia floodgate za kushambuliwa si virusi tu hata watu wabaya wanaweza kupitia loop hole hiyo kuwadhalilisha watu.

Sasa kama kuna watu weledi wenye uwezo wa kufanya maovu yote ya mtandaoni kama niliyoainisha katika paragraph yangu ya pili kutoka mwisho, kwa nini watu wanashindwa kukubali kwamba Ridhiwani anafanyiwa hujuma kweli na hii si mara yake ya kwanza kulalamikia watu kuingilia account yake ya facebook na kuweka madudu yao, dogo anajikuta anakuwa victim wa dot.com kwa sababu ambazo kwa akili za kawaida si rahisi kuzielewa.
Mkuu hatukatai ya Riz1 ila kama kweli unayosema ni haswaaa,mbona ya Lwakatare na VIDEO fake yanamuweka ndani, kwa nini Ritz1 asihojiwe pia??? Mbona mke wa Raisi Museven kahojiwa na vyombo vya dola????

Kati ya Chadema na CCM ni chama kipi hakiko tayari kukoselewa mkuu?. Chadema hawako tayari kusikiliza na wala kukosolewa hata kabla hawajachukua madaraka. Wakichukua madaraka si itakuwa hatari hapa Tanzania?. Chadema ukiwakosoa kidogo unafukuzwa uanachama mara moja. lakini CCM kila siku watu wanaikosoa na inachukua yale yaliyo mema inayafanyia kazi na yale ya kipuuzi inayaacha. leo hii bila haya unasema CCM haitako tayari kukosolewa?.
Mkuu na hao kina Kibanda kina Dr Ulimboka Kina Mwangosi kosa lao lilkuwa ni nini vile kuukosoa uongozi wa CCM au kuwaimbia mashahiri!!!!!

Mkuu hatukatai ya Riz1 ila kama kweli unayosema ni haswaaa,mbona ya Lwakatare na VIDEO fake yanamuweka ndani, kwa nini Ritz1 asihojiwe pia??? Mbona mke wa Raisi Museven kahojiwa na vyombo vya dola????

Mkulu M7 nazanisa Abaganda amagezi! i.e M7 ni msanii tu, hawezi kutoa amri ya dhati kwa vyombo vya dola kumkamata/ kumuhoji mkewe - kilicho fanyika ni kujidai mkewe kaitwa kituoni kuhojiwa na dola ili kutoa impression kwa wanachini wa Uganda kwamba hakuna mtu yeyote ambaye yuko juu ya sheria mkewe notwithstanding!! Kumbe Janet anapelekwa VIP lounge kwa masaa anangalia tamthilia kwenye luninga huku akiwa na glasi ya wine ya kienyeji (rubisi) - baadae wanaitwa wahandishi wa habari kushuhudia mkwe wa RAISI akitoka kituoni kuojiwa na dola - kumbe sakata zima ni usanii mtupu!

Mkuu hata Rais na wabunge ukatazwa kuzungumzia kesi iliyo mahakamani, hivyo siwezi ku-comment chochote kuhusu Ndugu Lwaka-lion!
 
Back
Top Bottom