Ridhiwani Kikwete akanusha tuhuma juu yake na kusema ni uhalifu wa mtandao!

Frank Sojo

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
343
95
Habari wanaJF!

Ridhiwani Kikwete alikuwa akihojiwa na Star Tv amesema ahusiki kwa namna yeyote na yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusiana na suala la Absalom Kibanda.

Amesema kuna mtu aliingia na kuandika maneno yale ambayo yamesababisha atukanwe sana na watu,amesema kwamba ametoa taarifa polisi na uchunguzi unaendelea,

Vile vile amesema hata suala la John Mnyika ya kwamba alimkashifu kuwa hajasoma sio kweli,yeye hajawahi kuandika maneno hayo bali ni watu wanamchafua kwa kutumia ukurasa wake na amedai kwamba huo ni uhalifu wa mtandao na anaomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi!

UPDATE:
Ndugu zangu, habari za wikiendi.

Yapo mambo machache ningependa kuwashirikisha ili kuweka kumbukumbu sawa na pia kuzuia upotoshaji ambao unaweza kujitokeza siku za usoni iwe kwangu, kwako au kwa mtu mwingine.

Mojawapo ya mambo makubwa ambayo yamejitokeza siku za karibuni hasa katika suala la Teknolojia na habari ni jambo la sheria za faragha (privacy and privacy lawas). Tumeshuhudia kufungwa kwa gazeti za News of The World, mali ya bilionea Rupert Murdoch wa Kimarekani baada ya kudhihirika alitumia wataalam wa teknolojia (hackers) kutafuta siri za watu mashuhuri kwa kuingia katika simu zao za mkononi kinyume cha utaratibu na sheria za faragha (Privacy Laws). Tumeshuhudia pia wahalifu hao hao wa mtandao wakifanya mengi kama kuvamia kwa mitandao ya makampuni makubwa kama Sony na mengineyo na hata katika mitandao hii ya kijamii upo wakati marafiki zako wanakwambia mbona umenitumia kitu kisichoeleweka, na baadaye kuja kugundua kwamba si wewe uliyefanya hivyo.

Tarehe 1, 8 na 9 mwezi huu wa Machi nilikuwa Dar es Salaam kwa shughuli zangu za kawaida kimaisha lakini ziko updates 5 zilifanyika hapa moja ikimhusu ndugu Absalom Kibanda. Ni ajabu kwamba baadhi ya waandishi tena waliojivika taji la usahihi katika uandishi waliiandika habari hiyo bila hata kuniuliza kwamba ni nini kinatokea. Tunajitahitahidi na kutamani kuwa na Taifa la waandishi makini na wenye kufuata maadili lakini wapo wanaoturudisha nyuma. Ni ajabu gazeti kuandika jambo lisilo la kweli huku wahusika wakiwa na kila uwezo wa kumfikia yule wanayedhani kwamba ameandika na kumhoji ili kuhakiki habari. Kazi ya uhariri ni kuhakiki. Ikiwa mtu atakimbilia kuandika jambo likuhusulo ambalo hana hakika nalo na alikuwa na kila uwezo wa kuwasiliana na wewe na kukuuliza lazima utajiuliza maswali mengi. Kwanza: Nini hasa lengo lake na pili ufahamu wake wa kile anachokifanya kwa maana ya taaluma yake katika kazi anayoifanya.

Napenda kuwaambia kwamba katika tarehe tarehe hizo mwezi huu wa Machi, wahalifu wa mtandao wakiwa eneo la Njiro na baadaye Kijenge mjini Arusha (Kila post ilionyesha eneo ilipotoka), (wakati huo mimi nikiwa Dar es Salaam) waliingia bila idhini kwa njia haramu (Hacking) katika anuani yangu ya Facebook na ku-post habari hizo tano. Sasa nimeliacha jambo hilo katika vyombo stahiki vya ulinzi na usalama ili kufuatiliwa kadiri ya taratibu zao.

Natoa wito kwa ndugu zangu waandishi kujitahidi kuhakiki habari kabla ya kuzipeleka katika vyombo vyao.

Hii itasaidia
1. Wao kujenga heshima mbele ya jamii
2. Kufikisha kile hasa ambacho ni habari
3. Kuzuia mikanganganyiko isiyo ya lazima.

Haya yakizingatiwa nadhani hata sintofahamu hizi za uandishi wa habari unaotokana na hisia na vyanzo vumbi na ufahamu mdogo wa jambo utaondoka na tutakuwa na jamii ambayo haki na uwajibikikaji wa wanahabari kwa jamii utaonekana kutendeka.

Niombe radhi kwa ndugu yangu, rafiki yangu na pia mwalimu wangu, Ndugu Absalom Kibanda kwa usumbufu wowote uliojitokeza ambao naamini watu wasio na nia njema walitaka kuutumia kuleta hisia tofauti katika jamii na pia kumpa pole kwa mara nyingine tena kwa maumivu yaliyosababishwa na ujangili huo. Namuombea kwa Mungu ampe unafuu mapema zaidi ili arudi katika meza yake kuendeleze harakati za kupambana na mchango wake katika kuleta maendeleo ya kweli kwa nchi yetu. Pili, pole pia kwa wote ambao kwa namna moja au nyengine walikwazwa na uzushi huo, kwa kuwa sina tatizo lolote na Bwana Kibanda na wala nisingependa lililomtokea limtokee yeye wala mtu mwengine yeyote.

Ni imani yangu ya dhati kwamba vyombo husika katika nchi yetu havitasita kulitalifanyia kazi jambo hili na ukweli juu ya nini kimemtokea Bwana Absalom Kibanda utajulikana na kuwekwa bayana.

Mwisho, shukrani kwa wote mlionipigia simu kuhusu hili, tuko pamoja na nawatakia kila la kheri katika shughuli za ujenzi wa Taifa letu hili la Tanzania ambalo msingi wake umejengwa katika haki, umoja, amani na kujali hali za watu wake.

Asanteni sana.

Ndugu yenu,
Ridhiwani Kikwete,
Jumapili Machi 17, 2013.
 
Habari wanaJF!

Ridhiwani Kikwete alikuwa akihojiwa na startv amesema ahusiki kwa namna yeyote na yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusiana na suala la Absalom Kibanda.

Amesema kuna mtu aliingia na kuandika maneno yale ambayo yamesababisha atukanwe sana na watu,amesema kwamba ametoa taarifa polisi na uchunguzi unaendelea,

Vile vile amesema hata suala la John Mnyika ya kwamba alimkashifu kuwa hajasoma sio kweli,yeye hajawahi kuandika maneno hayo bali ni watu wanamchafua kwa kutumia ukurasa wake na amedai kwamba huo ni uhalifu wa mtandao na anaomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi!

Uhalifu wa TEKNOLOJIA kama vile wa LWAKATARE. Mbona yeye hajakamatwa na Suleyman Kova japo kwa kuhojiwa tu?
 
Habari wanaJF!

Ridhiwani Kikwete alikuwa akihojiwa na startv amesema ahusiki kwa namna yeyote na yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusiana na suala la Absalom Kibanda.

Amesema kuna mtu aliingia na kuandika maneno yale ambayo yamesababisha atukanwe sana na watu,amesema kwamba ametoa taarifa polisi na uchunguzi unaendelea,

Vile vile amesema hata suala la John Mnyika ya kwamba alimkashifu kuwa hajasoma sio kweli,yeye hajawahi kuandika maneno hayo bali ni watu wanamchafua kwa kutumia ukurasa wake na amedai kwamba huo ni uhalifu wa mtandao na anaomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi!
Au amempa mtu kuendesha ukurasa wake halafu anamuwekea madudu yasiyoendana na fikra zake. Maana kuna password sasa hawa wahuni wakitembelea ukurasa inakuaje wanaweka madudu?! Hebu nielimisheni wakuu.
 
Habari wanaJF!

Ridhiwani Kikwete alikuwa akihojiwa na startv amesema ahusiki kwa namna yeyote na yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusiana na suala la Absalom Kibanda.

Amesema kuna mtu aliingia na kuandika maneno yale ambayo yamesababisha atukanwe sana na watu,amesema kwamba ametoa taarifa polisi na uchunguzi unaendelea,

Vile vile amesema hata suala la John Mnyika ya kwamba alimkashifu kuwa hajasoma sio kweli,yeye hajawahi kuandika maneno hayo bali ni watu wanamchafua kwa kutumia ukurasa wake na amedai kwamba huo ni uhalifu wa mtandao na anaomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi!

Damu ya kibanda inaanza kumuandama huyu bwana mdogo,mwanasheria gani hajui hata kujitetea.
 
Habari wanaJF!

Ridhiwani Kikwete alikuwa akihojiwa na startv amesema ahusiki kwa namna yeyote na yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusiana na suala la Absalom Kibanda.

Amesema kuna mtu aliingia na kuandika maneno yale ambayo yamesababisha atukanwe sana na watu,amesema kwamba ametoa taarifa polisi na uchunguzi unaendelea,

Vile vile amesema hata suala la John Mnyika ya kwamba alimkashifu kuwa hajasoma sio kweli,yeye hajawahi kuandika maneno hayo bali ni watu wanamchafua kwa kutumia ukurasa wake na amedai kwamba huo ni uhalifu wa mtandao na anaomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi!

Duh! kweli AKILi NDOGO kuongoza AKILI KUBWA.
HIvi si alikuja humu JF na kumpongeza MNYIKA kwa kujitokeza hadharani kutoa majibu kw amaswali amabyo yeye aliyauliza facebook?
kama hakuwa yeye kwanini alikuja humu kupongeza?
au na ile akaunti ya JF pia ilikuwa fake?

Kwlei polisi wetu hawana kazi, yani wmaekuw ani kichaka cha kusingizia kila kitu.
 
Kumbe wao wanajua kuna uhalifu wa kumitandao mbona filamu yao kuhusu Lwakatare wanaipa promo ya ajabu ili watuaminishe ni ya kweli?ushauri wangu kova na wenzake ongezeni bidii maana hautuingii akilin kamwe.
 
In riz1 i trust not Lwakatare,since many bad events concerns CHADEMA has occured like the muder of Chacha, Mwangosi, Mussa,and even the trial to kill Zitto.
CHADEMA hamsafishiki mmejaa damu za watu wasio na hatia na zitawatafuna mpaka mwisho wenu.
Mungu ibariki Tanzania, rest in piece Chacha Wangwe and the rest.
 
Habari wanaJF!

Ridhiwani Kikwete alikuwa akihojiwa na startv amesema ahusiki kwa namna yeyote na yaliyoandikwa kwenye ukurasa wake wa Facebook kuhusiana na suala la Absalom Kibanda.

Amesema kuna mtu aliingia na kuandika maneno yale ambayo yamesababisha atukanwe sana na watu,amesema kwamba ametoa taarifa polisi na uchunguzi unaendelea,

Vile vile amesema hata suala la John Mnyika ya kwamba alimkashifu kuwa hajasoma sio kweli,yeye hajawahi kuandika maneno hayo bali ni watu wanamchafua kwa kutumia ukurasa wake na amedai kwamba huo ni uhalifu wa mtandao na anaomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi!

Hii si mara ya kwanza Riz anakana yaliyo kwenye facebook page yake.
Lakini nadhani kukiri kwake kuwa hicho kilichokutwa kwenye fb page yaker si chake kunapaswa kuwashtua wanaopeleleza video ya Lwakatare kuwa kuna uwezekano pia kuwa sauti kwenye video hiyo nayo inaweza kuwa si ya Lwakatare

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hahahahaha kazi kweli kweli.. Ina maana hiyo account sio yake au??

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kwa hiyo anakubali kuwa hiyo account ni ya kwake ila kuna watu wameichakachua??
 
Back
Top Bottom