Ridhiwan Kikwete: Hoja za CAG zijibiwe kwa kufuata sheria na si kisiasa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,832
2,000
''Ni hatari kubwa kugeuza taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu (CAG) kuwa ya kisiasa. Sheria inataka kila Ofisi, Chama au Taasisi iliyotajwa kujibu hoja zake kisheria na katika taratibu zilizoelekezwa. Tuwajibike kwa kutoa majibu kwa njia sahihi. Tusiharibu kazi za kitaalamu" - Mbunge Ridhiwani Kikwete


 

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,689
2,000
Hawa watu wanaambiwa lakini hawataki kusikia kabisa,huyu Harrison naye ni mwanasheria mkubwa tu,tena wa kiwango cha PhD lakini anakwepeshakwepesha hoja ya msingi,kwamba wao sio maafisa masuhuli,hivyo hawapaswi kujibu,Naibu Spika naye sbb kawekwa pale na muhimili wa serikali,basi hasimamii misingi ya bunge lake,anatetea tu upande wa serikali.


Afisa Masuhuli ni afisa mwenye mamlaka ya juu na wajibu wa kusimamia na kutoa taarifa kuhusu matumizi ya fedha zilizotolewa kwa taasisi yake kutoka hazina baada ya kuidhinishwa na bunge. Kwa kiingereza wanaitwa "Accounting Officers".

Hili jina halimaanishi kuwa ni wahasibu, hapana.Linamaanisha kwamba wao ndiyo wawajibikaji wakuu katika taasisi- "they are accountable of every shilling".

Hata katika marejesho ya masurufu na maduhuli, ni afisa masuhuli ndio yuko accountable kwa CAG kuhusu matumizi mabaya ya masurufu na maduhuli.

Wengi wanafikiri mawaziri ndio "mabosi" kule mawizarani, kumbe wao ni mabosi kisiasa tu,nguvu ziko kwa Katibu Mkuu, ambapo waziri lazima amuone ili kujipatia fungu la ziada.
 

Mgeni wa Mungu

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
1,233
2,000
Magufuli asifikirie Kikwete amemsamehe kwa alivomdhalilisha. Kicheko chake anachomchekea kina maana kubwa. Watu wa pwani huwa wanamezea mambo meng
 

Ng'wale

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
2,964
2,000
Ridhiwani kwawambia chadema pia
Hakuna aliyehoji hilo. Ndiyo maana kasema taasisi yoyote. Lakini kuna taasisi ambazo zimekua mbele sana kujibu huo ukaguzi wa CAG. nadhani hizo ndo zimemfanya Riz aliongelee hili.
 

Kocrochi

Member
Jun 12, 2017
24
45
Bila shaka MwenyeziMungu anataka kuleta nusura, haya ni maandaliza ya ccm kuondoka madarakani maana kila bays walitendalo wao hujihebu wako sahihi. Allah ajalie waendelee hivyo hivyo
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,663
2,000
Ukisikiliza vyema maelezo ya Naibu Spika utagundua kabisa Mawaziri wanafanya nje ya utaratibu wa kisheria na kikanuni. Kama watajitafakari na kutumia busara wangekuwa waangalifu sana kufanya wanalolifanya.

Kwa maelezo ya Naibu Spika Mawaziri wanayoyatoa ni maoni yao binafsi kuhusu ukaguzi huo. Tatizo tu ni kuwa kauli ya Waziri ni kauli ya serikali. Taabu itakuwa pale kauli ya Waziri (maoni yake binafsi) yatakapotofautiana na majibunl rasmi ya hoja za CAG yatakayotolewa kwa utaratibu unaofahamika kupitia Afisa Masuhuli husika. Maoni binafsi yanaruhusiwa lakini kuna ngazi fulani serikalini maoni binafsi ni hatari kuyatoa horera horera.

Lakini pengine tujishangae wenyewe kwa kuyashangaa haya. Maana kwa sasa Mawaziri wanayoyafanya ni vigumu hata kutofautisha kati yao na maafisa wa Wuzarani. Maana wanafanya kaxi zote ambaxo hufanywa na hao maafisa. Pia ni kwamba Mawaziri bado wzkonkatika 'mode' ya kampeni. Hawajatoka huko tangu tumalize uchaguzi uliopita.

Utaratibu wa ukaguzi unafahamika.
 

Maharo

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
3,187
2,000
Wa
Magufuli asifikirie Kikwete amemsamehe kwa alivomdhalilisha. Kicheko chake anachomchekea kina maana kubwa. Watu wa pwani huwa wanamezea mambo meng
Wabongo wananifurahisha sana pale wanapogeuza watu kuwa miungu watu na kuwafanya wako special sana na kusahau kwamba Mungu yupo na nguvu yake hakuna kenge yeyote anaeiweza.TUPUNGUZE.
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
3,735
2,000
Awamu hii utawala bora na utawala wa sheria haupo. Badala ya kuwaachia wataalamu wazungumze kitaalamu eti mawaziri wanatoa maoni yao binafsi kuhusu hoja za CAG. Sasa wakija hao wataalamu wenyewe wakatoa majibu tofauti na mawaziri wao itakuwaje? Kwa nini maoni binafsi yatangulie mbele kuliko majibu ya kitaalamu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom