Richest 1% now owns half the world's wealth - CNBC.com

stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
6,379
3,492
1572608628669.png

baada ya kupata mda kidogo leo, nkaona nipitie taarifa kuhusu uchumi wa dunia unavoenenda kila siku na nkakutana na hii taarifa, hii imenipa hamasa ya kuja kuuliza apa forum:

Je ni kweli serikali ni ya kulaumiwa kwa sababu watu maisha yao ni duni? waliopata elimu mpaka vyuo vikuu, wengine wakaenda nje ya nchi kusoma wanakwama wap wanavojiunga na wengine amabo hawajasoma kutupia lawama serikali ilihali kuna watu wana uchumi mkubwa kuliko serikali?

1572609058864.png
 
Shughuli ambazo mtu/wananchi wanafanya katika kujiletea maendeleo zinategemea sana sera, sheria, miundombinu na uendeshaji na usimamizi wa jumla wa shughuli za kila siku za serikali.

Kwa mfano unaweza kujitutumua ukalima zao fulani, ghafla serikali ika weka zuio la kuuza zao hilo nje ya nchi, bei ikaporomoka ukapata hasara.

Lakini pia unaweza ukawa unataka kufanya jambo fulani, hasa jambo jipya unahitaji vibali vya serikali...serikali ikakuzungusha weee hadi mtaji au morali yako ya kufanya jambo hilo vukapotea.

Umasikini wa nchi yetu ni wa kihistoria na historia hiyo inatutafuna, hadi leo. Baadhi ya mambo ambayo yametusababishia umasikini ni haya yafuatayo:
1. Sera ya ujamaa ambayo ilikuja na mambo yafuatayo.
1.1. Utaifishaji wa mashirika na makampuni uliofanywa na Serikali ya awamu ya kwanza.
1.2. Uanzishwaji wa vijiji vya ujamaa mwaka 1977. Hapa watu wengi walirudishwa nyuma sana kimaendeleo.
1.3. Vita dhidi ya wahujumu uchumi.

Mambo haya yaliwaacha watanzania wengi wakiwa hoi. Wajasiriamali wa wakati huo walikatishwa tamaa. Nchi ikabaki ya wakulima na wafanyakazi. Mwamko wa ubunifu na uchakarikaji ukafa. Kila mtu akabaki kuiangalia tu serikali...umasikini ukatamalaki.

Baadhi ya mambo yanayoendelea sasa awamu ya tano ni mwendelezo wa mazoea na legacy mbaya iliyoachwa na sera za ujamaa.

Eneo lingine ambalo linasababisha umasikini ni kutokuwa na utamaduni au sera ya kuwezesha na kulinda biashara hasa za wazawa. Ukosefu wa mifumo thabiti ya kuunganisha mitaji na mlolongo mrefu wa maswala yanayohitaji uamuzi wa kisheria. Ukiwa na kesi inayohusu mambo ya biashara inaweza kuchukua hata miaka 10, na hata ukishinda hukumu hazitekelezwi.

Jambo jingine ni kutotumia wataalamu wa ndaji katika miradi mikubwa na hivyo kukuta kila kitu kinafanywa na kampuni kutoka nje.

Yapo mengi lakini niishie hapo.
 
uko smart katika kuelezea mada
 
Back
Top Bottom