Riba za bank za Tanzania ni kikwazo cha maendeleo

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Sababu mojawapo ya Tanzania kuwa na ajira ndogo ni riba kubwa za mikopo ya bank zetu. Imefika wakati hata Kimei ambaye alikuwa mkurugenzi wa CRDB kasema bungeni.
  1. Riba ikiwa kubwa biashara ndogo ndogo hazitaweza kukopa hivyo haziwezi kuwekeza kwenye ukuaji wa biashara. Hii inasababisha ajira ndogo na kodi ndogo
  2. Riba kubwa zinaongeza gharama za uzalishaji na uuzaji wa vitu. Mfanyabiashara inabidi aongezee gharama za bank kwenye maligafi anazotaka kuuza na kusababisha malighafi kuwa na gharama kubwa na kushidwa kabisa kushindana na malighafi za nchi ambazo wana riba ndogo
Nitoe tu mfano unaweza kupata mkopo wa gari 3% nchi nyingine kwa miaka mitano .Kwa gari hilo hilo Tanzania unapata mkopo wa asilimia 15% kwa miaka miwili tu. Hivyo mfanyabiashara pesa nyingi inaenda kwenye kulipa mkopo na habaki na pesa ya kukuza biashara yake. Bank kuu yetu itafute utaratibu wa kupunguza riba tukizingatia mfumuko wa bei umeshuka mpaka 4% tu kwa mwaka.

Niongezee tu

Nilikuwa naulizia mkopo kwenye bank inaitwa Equity Bank wakaniambia riba kwa diaspora ni 17% kwa Tsh na 9% kwa $$. Nimenunua gari mwaka jana nimepata riba ya 4.5% na wamenipa miaka 7. Kwasasa nilikuwa naulizia mkopo wa kujenga apartment.

Riba ni tatizo kubwa sana sitaweza kuchukuwa mkopo wa 17% au 9% kwa $$$ ni juu sana
 
Tuna sera ambazo bado zinamtazamo wa "siasa za ujamaa":
1.kuzuia mtu binafsi kumiliki na kutajirika
2.Riba na kodi ambazo zinazuia mtu binafsi kupata unafuu katika kumiliki na kuendesha maisha ya kuinuka kiuchumi na kiuwekezaji.

Tunaongea tu,bila kuweka katika vitendo:
a).Tunasema tunataka tuendelee kiviwanda,lakini hatupunguzi kodi,kuvutia wananchi kuagiza na kuwekeza mashine na mitambo ya viwanda.
b).Tunasema "kilimo ni uti wa mgongo";lakini mtu akilima mazao,akivuna Viongozi wa Serikali wanamzuia kuuza nje ya nchi "eti akiuza nje atapata njaa"(Wakati kiuhalisia ukiuza bidhaa nje unapata fedha nyingi).

Kwa ujumla bado tupo kinyume na mifumo ya kibishara ya kimataifa!(mfano ukinunua gari nje,mpaka linafika Tanzania utakuwa umelipa jumla ya fedha ambayo ni mara 2 hadi 3 ya fedha uliyonunulia),Lakini viongozi wanaona yote haya ni sawa tu.
 
Hii ndio michango niliyotegemea kutoka kwa Dr Kimei mchana kuna mtu alianzisha mada alichosikia yeye ni swala la kuiwajibisha serikali tu kutofikia malengo ya budget akaacha techinical issues za msingi alizoshauri za kiuchumi.

Ila Kimei inabidi ajifunze public speaking kwanza anaongea haraka sana, pili awe ana simplify arguments zake ili watu wakawaida waelewe unapopendekeza inflation iwe 3% na interest rate ni 5% not sure watu wengi wataelewa anaongelea future value ya thamani za mkopo na jinsi interest za mikopo zinavyofikiriwa ili mkopaji asipate hasara, wengi wanaweza zani anaongelea inflation rate ya uchumi.

Hoja zake kama hizi anapoongea lazima ajue anasikilizwa na wengi wasio na ufahamu wa finance, yeye anaongea as if yupo kwenye mkusanyiko wa bankers not sure many people grasped.

I always thought Kimei kama umri unamruhusu alitakiwa kuwa Governor wa BoT.

Nina uhakika angekuwa anapewa muda wa kutosha kuchangia bank kuu na Mwigulu wangejifunza kitu kwenye money circulation (monetary policies).
 
Kimei ni mchaga!
Na BOT Haina historia nzuri na wachaga!.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Bado na wewe umeongea kitu kigumu,kwa asiye na taaluma ya fedha bado haueleweki.
Hakuna njia rahisi ya kuongelea eneo hilo kwa mtu layman wa finance akaelewa,japo wenyewe kwa wenyewe wanaelewana.
Kikubwa ushauri wake ufanyiwe kazi ili riba zishuke,ili wakopaji waongezeke na waweze kumudu marejesho pamoja na kupata faida pia
 
Basically anachosema ukinikopa sh 2200 ambayo leo napata kilo ya sukari, mwakani ntakapolipa sh 2200 lazima na yenyewe inunue kilo ya sukari (sema yeye akuanzia hapo amezungumzia future value as if wote wanaelewa anaongelea nini).

In the real world bidhaa zinatabia ya kupanda walau in a market basket, considering inflation kuakikisha mwakani napata kilo ya sukari kwenye mkopo 2200 naweka interest ya 3% kwanza kwa sababu ya inflation risk factor, then nafikiria interest ya faida ambayo ni 5% jumla mkopo unakuwa na interest rate ya 8%.

Tatizo banks nyingi kwa sasa inflation rate zao za mikopo zipo juu wengine wanaweka mpaka 8% kama future value ya hela jumlisha na interest ya faida ndio maana mikopo inakuwa juu, that is kwa mujibu wa Kimei.

Kuendelea sijamuelewa vizuri analaumu bank kuu nayo inachangia kwa sababu ya coupon rates, mara akaongelea intrest rate za mikopo kuwa juu ambazo zinachangia na banks nao kuweka zao juu.

Labda wawe wanampa muda zaidi adadavue hoja zake polepole ili awe more clearly beside the analog is too simple uchumi ambao ufisadi umeshamiri inakuwa ngumu ku control inflation so banks might set higher risk rates.
 
Kimei ni mchaga!
Na BOT Haina historia nzuri na wachaga!.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Haya ndio matatizo ambayo sometimes watu wanapotoa positive critism tunaishiwa kutukanwa.

Kwa sababu mmeshajengeana hizi fikra na consistency ya michango kupitia ukabila, udini, ukanda and whatever nonsense zilizomo kwenye vichwa vyenu.

Unfortunately wengine tumelelewa mazingira tofauti hayo mambo ya division ni vitu vya mwisho kwenye ku judge watu.

Akikosolewa au kusifiwa Samia sio kwa sababu ya jinsia au dini, akikosolowa Kimei au kusifiwa sio sababu ya kabila lake or anything; wengine we are just objective kwenye hoja and conclude on merit walau kwa mtazamo wetu which is unbiased.
 
Sababu mojawapo ya Tanzania kuwa na ajira ndogo ni riba kubwa za mikopo ya bank zetu. Imefika wakati hata Kimei ambaye alikuwa mkurugenzi wa CRDB kasema bungeni.
  1. Riba ikiwa kubwa biashara ndogo ndogo hazitaweza kukopa hivyo haziwezi kuwekeza kwenye ukuaji wa biashara. Hii inasababisha ajira ndogo na kodi ndogo
  2. Riba kubwa zinaongeza gharama za uzalishaji na uuzaji wa vitu. Mfanyabiashara inabidi aongezee gharama za bank kwenye maligafi anazotaka kuuza na kusababisha malighafi kuwa na gharama kubwa na kushidwa kabisa kushindana na malighafi za nchi ambazo wana riba ndogo
Nitoe tu mfano unaweza kupata mkopo wa gari 3% nchi nyingine kwa miaka mitano .Kwa gari hilo hilo Tanzania unapata mkopo wa asilimia 15% kwa miaka miwili tu. Hivyo mfanyabiashara pesa nyingi inaenda kwenye kulipa mkopo na habaki na pesa ya kukuza biashara yake. Bank kuu yetu itafute utaratibu wa kupunguza riba tukizingatia mfumuko wa bei umeshuka mpaka 4% tu kwa mwaka.
Ccm inawajengea TANZANIA MPYA ionekane kama ULAYA RIBA inatakiwa IONGEZEKE
 
Riba ipungue sana Ili mtu akope amalize mkopo wake na aweze kukopa tena ila kwa wafanyakazi riba ipungue zaidi maana wao ni wateja wa bank wa kudumu kwa kupitisha mishahara na kukopa.
 
Haya ndio matatizo ambayo sometimes watu wanapotoa positive critism tunaishiwa kutukanwa.

Kwa sababu mmeshajengeana hizi fikra na consistency ya michango kupitia ukabila, udini, ukanda and whatever nonsense zilizomo kwenye vichwa vyenj.

Unfortunately wengine tumelelewa mazingira tofauti hayo mambo division ni vitu vya mwisho kwenye ku judge watu.

Akikosolewa au kusifiwa Samia sio kwa sababu ya jinsia au dini, akikosolowa Kimei au kusifia sio sababu Kabila lake or anything; wengine we are just objective kwenye hoja and conclude on merit walau kwa mtazamo wetu which is unbiased.
Siku nyingine usijaribu kukwepa kuzungumza jambo kwasababu ni baya wakati jambo hilo kipo.
 
Alisema Kikwete, Benki sio rafiki wa maskini.

Kiwango cha riba ni maswala ya kibiashara, kuyawekea sheria inaweza ikaleta hasara kuliko faida. Kenya walijaribu kufanya hili jambo, wakaweka ukomo wa riba, kilichofuatia ni mabenki kuongeza makali katika vigezo vya kuombea mikopo, kilichofuatia ni mikopo nafuu lakini haipatikani; wakaona it doesnt work wakaondoa hiyo sheria.

Risks na riba ni direct proportional, risks ya watu kutolipa inapokuwa kubwa, riba lazima nayo itakuwa kubwa ili wale wanaolipa in a way wazibe mapengo ya wanaokimbia.
 
Eti mfumuko wa bei umeshuka hadi asilimia 4 hii sio kweli ni zile takwimu feki zinazotolewa na serikali ili kukidhi malengo yao ya kisiasa.

Haiwezekani mfumuko wa bei ushuke huku bei za bidhaa ikizidi kupanda..!! Tuangalie kwa kipindi tu cha mwaka mmoja uliopita ni bidhaa gani ambayo haijapanda bei.

Hizi takwimu za kiuchumi zinazotolewa na serikali mara nyingi ni kinyume na hali ya mambo ilivyo, ni za kuhadaa watu kwenye majukwaa tu.
 
Tunashukuru tunaona Raisi Samia anaelewa tatizo kubwa la riba za bank.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mkuu hizo ni nchi nyingine, riba kuwa ndogo i ategemea how strong yhe economy is, kwa tanzania bado sana kwa sababu zifuatazo
1. Government borrowing bado ni kuanzia 12% to 14% so usitegemee commercial bank kuwa chin ya hapo.
2, high inflation rate, mtu anakukopesha pesa leo ambayo inflation kila mwaka ni 5% so in five years pesa imeloose value kwa 25%
3. High default rate ya borrowers, kushindwa kulipa kwa wakat pia kunafanya credit kuwa expensive
4. High credit administration cost, kuna mambo meng sana ya visit, collateral verification registration etc,
5. Poor liquidity, tukubali mabenk mengi hayana deposit ya kutosha, hii imepelekea ku atract deposit ambazo ni very expensive i.e. fixed deposit and bonds ambazo nying depositor qnqlipwa mpaka 15% so tusitegemee lending rate kuwa kidogo kuliko deposit rate
 
Nimesikia mama ameelekeza bank kuu ishughulikie kushuka kwa riba.

Mama amekiri kua riba Tanzania ziko juu sana, kuanzia 12% hadi 19% ila ukweli zinaenda hadi 25%.

Mama ameagiza ziwe 10% kushuka chini. Kwa kuliona hili nampongeza. Bank Tanzania zina riba kubwa sana.

Kuna wakati ofisini nilipewa kazi ya kufanya analysis kama tukope kwa shilingi ama tukope kwa dollar, ukweli ni kua kukopa kwa dollar ni way cheaper kuliko kukopa kwa shilingi.

Banks Tanzania zinakopa kwa riba ndogo sana, mathalani, zikikopa bank kuu riba haizidi 9% ila wao wanakuja kuwakopesha wananchi kwa 18%. Banks zimehamishia operational costs kwa wateja.

Banks hata zikikopa Dollar, mara nyingi ni LIBOR+1.5 ama LIBOR+2 ila wanakuja kucharge riba ya 18% kwa Watanzania.

Nchi nyingine watu wanakopa hadi kwa 5% ila Tanzania gharama za kukopa ziko juu sana.
 
Back
Top Bottom