Agresive
JF-Expert Member
- Feb 18, 2018
- 889
- 1,226
WanaJF habari ya leo na hongereni kwa kukumudu changamoto ya kukatikakatika kwa umeme.
Niende kwenye mada.
Leo nimepata sms kutoka company za ukopeshaji inayonihamasisha kuchukua mkopo kutoka company ya MABOTO.
SMS yao inasema karibu uckukue mkopo wenye riba nafuu CHUKUA LAKI 5 URUDISHE LAKI 6 KWA MIEZI 11 AU MILIONI 1 URUDISHE MILIONI NA LAKI 2 KWA MIEZI 11.
Namba ile ile iliyonisms nikaitumia sms kuwa riba hii ni kweli wakanipigia nakuniambia ni kweli.
Laki 5 makato ni 54545 kwa mwezi kwa muda wa miezi 11.
Sijawahi kukopa taasisi yoyote binafsi zaidi ya BANK NMB NA CRDB NA TPB (Bank ya posta.)
Company hii ya Maboto, Bayport, Faidika na nyingine za binafsi kwa historia najuwa ni zile kausha damu.
Riba hii haijanishawishi kukopa hapana ila tu nahisi inaweza kuwa ni janja janja za company hizi kulaghai watumishi wa umma.
MWISHO.
1. EPUKA KUKOPA BILA SABABU
2. USIKOPE TU KWA SABABU UNAKOPESHEKA KOSA KWA SABABU UNA SABABU YA KUKOPA.
3. Usikopee pesa yote unayoweza kukopeshwa isipokuwa kopa kwa sababu una uhitaji wa kukopa.
4. Usikope kabla ya kuandaa bajeti bali kopa kufuata bajeti uliyoandaa.
5. Usishawishiwe kukopa kamwe mkopo haushawishiwi ila shida ndiyo utakusababisha ukope.
6. Usikope kwa ajili ya ujenzi endapo unaweza kulipa kodi bila kuathiri kipato chako ripa kodi na jenga pole pole.
7. Kopa kwa ajili ya kuwekeza biashara zaidi usikope kununua vitu vya ndani au kwenda kuoa au kulipia mahali au kazi ya harusi, funga ndoa kulingana na kipato chako.
Kuwa na nidhamu ya pesa ili usiwe mtumwa wa madeni.