Rfa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rfa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kakuruvi, Jan 28, 2011.

 1. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Katika mambo mengi yanayozuia wachumba au marafiki wengi kutofikia adhma ya kufunga ndoa mojawapo ni DINI. Kuna wakati wapendanao wenyewe wanafikia kikomo kwa sababu ya dini au wakati mwingine wao wako radhi ila wakileta suala la ndoa kwa wazazi au walezi wanapigwa stop.

  Jana nilikuwa nasikiliza RFA usiku kuna kipindi cha nyimbo za zamani kila saa nne usiku alhamisi wimbo ulionivutia na kunikumbusha mbali ni ''Wazazi wake Jane - Msondo Ngoma''

  wazazi wake Jane,
  hawakupenda Jane aolewe nami na kipingamizi kwetu ni dini na kwamba sina pesa za kumtunza.

  Jane alipowaelewa,
  alijaribu kuwabembeleza na kwamba jambo la muhimu ni maelewano na hata hivyo hawakukubali.

  CHORUS:
  nilipokutana na Jane nilimshauri akubaliane na mawzo ya wazazi wake,
  ni wao walikulea wakakupeleka shule wakakupa matunzo ya kila aina kipenzi...............

  Narudi kwenu wana JF, Jambo kama hili lina suluhisho kweli? umewahi kukutwa na jambo kama hili? Nawatakia mwisho wa wiki mwema.
   
 2. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  kama hukusikia maneno ya wazee tutakosa radhi, hatuwezi kuishi kwa raha.......
   
 3. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Asiyefunzwa na wazazi ulimwengu utamuonyesha kazi
   
 4. kakuruvi

  kakuruvi JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 646
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  [WAZAZI HAWAKUBALI - Juwata Jazz Band] - Mtukwao

  Wazazi wake Jeni,
  Hawakupenda binti yao aolewe nami,
  Vipingamizi vyao vilizidi,
  Na kwamba sina pesa za kumtunza.

  Jane alipoelewa,
  Aliamua kuwabembeleza,
  Ili aolewe nami,
  Na kwamba jambo la muhimu ni maelewano,
  Hata hivyo hawakukubali,

  Kibwagizo:

  Nilipokutana na Jeni,
  Nilimshauri [nitampata wapi]
  Akubaliane na mawazo ya wazazi wake x2

  Kwani hao walikuleaaaaa,
  Wakakupeleka shuuuuule,
  Wakakupa mafunzo,
  Ya kila aina mama,

  Nilipokutana na Jeni,
  Nilimshauri,akubaliane na mawazo ya wazazi wake,
  [Msondo ngoma]

  Kama hukusikia,
  Maneno ya wazee,
  Utakosa radhi,
  Hatuwezi kuishi kwa rahaa aeeeh,

  Nilipokutana na Jeni,
  Nilimshauri, [nitampata wapi]
  Akubaliane na mawazo ya wazazi wake,

  Kwani wao walikuleaaaaa,
  Wakakupeleka shuleeeee,
  Wakakupa mafunzo ya kila aina kipenzi,

  Nilipokkutana na Jeni.....

   
Loading...