Kwanza kabisa mfumo wa awamu ya Kwanza wa kuwa na vyuo vya Ufundi na kilimo ndio tuufuate, elimu ya msingi iimarishwe kwa kuwa na waaalimu bora sio waalimu wa upe, jingine na kuna baadhi ya mitaala iimarishwe zaidi kuwa na practical zaidi kuliko theory, na tatizo jingine ni ya na la rushwa na kifamilia ambalo huwafanya vijana kutokujitambua,Mkuu umeibua hoja za msingi. Labda tukuulize wewe ushauri wako ni nini sasa? Je! unakubali kuna tatizo la ukosefu wa ajira na linaongeka? unakubali kuwa mfumo wa elimu hauwezeshi vijana kujiajiri na kuingiza elimu hiyo kwenye matendo labda waajiriwe na nafasi za kuajiriwa ni chache sana? unakubaliana kuwa wanaotakiwa wajiajiri hawana mtaji na hawawezi kupata mtaji mpaka pawe na 'external force'? tunafanyaje sasa? Unaamini maono ya kisiasa yanayotoa muelekeo wa kisera yanaweza kusaidia kitu?
Umetoa mfano wa udaktari na urubani. Kuna aina ya fani ni lazima kusoma darasani. kwa watakaochagua fani husuka watasoma darasani lakini kwa kuspecialize kutokea mapema kabisa kwa mfano udaktari. Lakini ushangae sasa, huo udaktari wenyewe mfano kwenye korona tumerudi kwenye tiba asili na zimesaidia kwa kiasi flani. Waliozibuni walisoma kwa utaratibu gani? Urubani kwa mfano uliousema, hivi unajua urubani ni kama udereva? unahitaji zaidi 'skills' na sio 'academics' yaani la saba anaweza kuwa dereva mzuri kuliko PhD holder?
Mwisho wa siku, ili tuweze kufanikiwa kama taifa, tunatakiwa kujifunza kufanya vitu vyetu sisi kama sisi na sio kuiga wengine. Hakuna namna tunaweza kufanikiwa kwa kufuata mkumbo, tujifunze kwa wengine lakini tufanye kivyetu na kwa ubunifu wetu wenyewe.
Na kufikiria misheni town ndio uvumbuzi wa Maisha na mahali pa familia ndio halali yake , matokeo yake Mzee wa miaka 60-70 bado analisha vijana wake badala ya wao kuwa wanamsaidia yeye au kumpisha Mzee apangishe baadhi ya vyumba walivyokuwa wanakaa walipokuwa wadogo.
Katika hali kama hii vijana kama hao kuwakopesha inakuwa ngumu , ingawa inaweza kuwa kikwazo kwa wanaojitambua kutoka na kujiajiri.
Ingawa hilo lina kuwa addressed kwa kuwaaambia vijana kujiunga ktk vikundi, kutumika kwa vitambulisho cha taifa kuweka taarifa za mtu n.a. ufuatiliaji.
Kwa ufupi rushwa na upendeleo ndio zilizoharibu maono ya wazazi na vijana kuhusu Maisha binafsi na maendeleo