Review: In the tall grass movie

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
9,110
27,048
Habari zenu wakuu, natumaini mko poa.

Kuna muvi nimeiona inaitwa IN THE TALL GRASSES ila imenichanganya sana tena sana. Haya ni baadhi ya mambo yaliyonichanganya

i)Je, yule mdada mwenye mimba aliekuwa kwenye gari na kakake wakienda kwa mchumba wa yule dada, je waliingia mle kwenye yale majani marefu au hawakuingia? 🤔

ii) Kama hawakuingia mbona gari yao ilionekana nje plate number zikiwa zimechafuka kuonesha lilikaa muda mrefu pale nje kanisani?

iii)Je, kati ya yule mdada mwenye mimba pamoja na kakake na yule mchumba wakealiekuja kuwatafuta, je nani alianza kuingia mle kwenye majani? 🤔

iv)Ni ipi hasa logic behind ya ile movie?

Karibuni sana waungwana kwa mawazo zaidi
 
Toka uanze kuangalia movie miaka mitano inafika ?

Tuanze hapo kwanza

Passion -common sense -silent-language
 
Hebu kuwa specific ili ueleweke, umeiona au umeitazama? Kuna tofauti kati ya kuona (to see) na kutazama (to watch). Kama umeishia kuiona ni kweli lazima ikuchanganye lakini kama ungeitazama usingejiuliza hayo maswali, kwani jibu ungekuwa nalo.

Hebu angalia hapa chini, huenda ukapata majibu ya maswali yako...

Ki ukweli hata na mimi ilinichanganya. Haijulikani mwanzo wala mwisho. Ila zipo movie za aina hivyo. Niliachana nayo tu
 
Kama hiyo umeshindwa elewa, THE TRIANGLE ndo' utaumiza kichwa kabisa. Mahadhi yake yanafanana ambapo kunakuwa na looping plot, the same na HAPPY DEATH DAY.

Hiyo movie ya IN THE TALL GRASS, kuna namna ambavyo wale waliozama ndani walipata nasibu ya kumwokoa yule mtoto ambaye ndo anafanya watu waingie humo kwa kuwaita akiwaomba msaada. Na kwakuwa mtoto yule alikuwa amemezwa na sacred stone ambayo hufanya plot iwe ya kujirudiarudia pasipo kukoma, ndipo wale waliozama ndani wakamsihi yule mtoto arekebishe makosa yao kwa kuwazuia wasiingie tena humo ndani ya Majani. Ndo unaona yule dogo karudi na kuwasihi wale watu wasiingie mule ndani ya majani pasipo kujali wanasikia mtu akiwaita humo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hiyo The Triangle ni movie nzuri ila ukiondoka kidogo tu ushapoteza mwelekeo, ilivyoisha yaani mwanzo ndio mwisho na mwisho ndio mwanzo...
 
In the tall grass ipo very direct. Mwanzo na mwisho wake unaonekana vizuri tu. Tulia uangalie tena.
Kama wadau walivyosema hapo juu movie ambayo haina mwanzo wala mwisho ni TRIANGLE pale Ndio utajua hujui ukiangalia ile movie Yani uanaangalia 20 minutes af unarewind uangalie tena Ndio uelewe Yani kama unasolve hesabu.
Happy death day to you kwangu Naona ipo straight.

Ila ukitaka kufurahisha ubongo chek the nun na curse of la ronna.
Usisahau the clown 🤡☠️

Happy death day to you all in the tall grass

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu nimeangalia hiyo Triangle sijaelewa kitu
Imekuwaje mwisho ndo mwanzo na mwanzo ndiyo mwisho??
In the tall grass ipo very direct. Mwanzo na mwisho wake unaonekana vizuri tu. Tulia uangalie tena.
Kama wadau walivyosema hapo juu movie ambayo haina mwanzo wala mwisho ni TRIANGLE pale Ndio utajua hujui ukiangalia ile movie Yani uanaangalia 20 minutes af unarewind uangalie tena Ndio uelewe Yani kama unasolve hesabu.
Happy death day to you kwangu Naona ipo straight.

Ila ukitaka kufurahisha ubongo chek the nun na curse of la ronna.
Usisahau the clown

Happy death day to you all in the tall grass

Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmenipa kila sababu ya kutafuta hizi movie...I like to crack my brains...

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom