REVEALED: Mgao wa umeme kuendelea mpaka mwaka 2013! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

REVEALED: Mgao wa umeme kuendelea mpaka mwaka 2013!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RICH-MONDULI, Jul 29, 2011.

 1. R

  RICH-MONDULI New Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maumivu ya mgao wa umeme yataendelea mpaka mwaka 2013 ambapo kampuni za Pan African Energy na Songas zitakapokuwa zimewekeza kwenye miundombinu ya kuzalisha na kusafirisha gesi ya ziada mpaka Dar itakayowezesha kuzalishwa kwa umeme zaidi. Cha ajabu na kusikitisha ni kuwa serikali imeagiza mitambo mipya ya kuzalisha umeme ya 100MW kutumia gesi huku kukiwa hakuna gesi hiyo ya kuzalisha umeme. Hata Symbion (a.k.a new Richmond/Dowans) inazalisha 60MW tu wakati ina uwezo wa kuzalisha 112MW kutokana na upungufu wa gesi.

  Huko Kenya wanajenga flyovers, Rwanda wanasonga mbele, Uganda wanaimarika na utajiri wa mafuta. Uchumi wa Tanzania kuendelea kudumaa kwa miaka ijayo kutokana na kukosa umeme. Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akiulizwa tatito ni nini anasema ni ukame, si kosa la mtu kutokuwepo kwa umeme. Nchi inakufa!

   
 2. W

  Warofo Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2006 Edward Lowassa angefanya maamuzi magumu na kukataa kupokea mlungula wa Rostam Aziz na kutoa tenda kwa Richmond, hii nchi isingekuwa kwenye matatizo haya sasa hivi. Lowassa alaaniwe kwa kuiletea maafa nchi hii, na wote wanaosema alikuwa kiongozi bora wapelekwe Mirembe kupimwa akili.

  Serikali iliyopo madarakani ni laana kubwa kwa Watanzania. Wananchi wanajuta kuzaliwa kwenye nchi hii.
   
 3. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  umeyasikia ya mahakamani kisutu jana,bado mnadhani mwakyembe na sitta team walimsaidia jk kumgombanisha na lowassa?
  Tuwe huru kifikra lakini wahenga walisema kuna wawinda ndege na wawinda tembo, hawa ni watu wawili tofauti ktk uwindaji.
   
 4. M

  Mojo Senior Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mahakama za Tanzania zinanuka rushwa, huwezi kutegemea kupata haki mahakani bali maamuzi ya mahakama hununuliwa kwa pesa. Huyo Lowassa wenu hawezi kukwepa ufisadi wa Richmond, angeacha tamaa zake za utajiri na kuwa mwadilifu bado angekuwa serikalini sasa hivi na kuwa na nafasi ya 2015. Sasa hivi hana nafasi tena, kwishnei!

  Lowassa pamoja na serikali nzima ya Kikwete wanastahili kubeba lawama kwa haya maumivu ya mgao wa umeme tunayopata sisi Watanzania
   
 5. Zagazaga

  Zagazaga JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 519
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  hebu msituzingue hapa matatizo ya umeme hayatokani na richmond pekeyake..... Lowasa alijitahidi kupush mambo yaende sawa watu wapate umeme wengine wakapata mahala pa kumtoa kafara.. si ndo hiyo mitambo ya dowans (symbion) inayozalisha umeme kwa sasa... mbona kina mwakyembe walisema haina uwezo wa kuzalisha umeme na isitoshe mkulu JK alisema hela ya richmond kaizuia? wakulaumiwa ni sita na mwakyembe wanafki wakubwa.
   
 6. M

  Mtanzania Huru Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe kweli akili zako Zagazaga, yaani unajaribu kufuta ukweli wa historia na kudai eti Lowassa hana kosa kwenye Richmond?! Pamoja na jitihada zenu, ukweli utabaki palepale daima. Lowassa hachomoki kwenye kashfa ya Richmond kwani yeye akiwa kama Waziri Mkuu ndiye aliye push tenda wapewe Richmond wakati wataalamu wa TANESCO walisema wazi kabisa tangu awali kuwa Richmond hawana uwezo wa kuzalisha umeme. Msalaba wa Richmond Lowassa ataubeba milele na stahili yake kutokana na kuhusika na kashfa hiyo. Hili wote mnaodhani atarejea tena kutawala nchi hii bora mrudi usingizini, kuna viongozi wengi wenye maadili safi ya uongozi na uchapakazi wanaoweza kazi hiyo, si mpenda mali na mwenye kuchafuka kama Lowassa wenu.

  Bottom line, matatizo ya umeme si Lowassa peke yake wala si Richmond tu, bali ni serikali nzima za Kikwete kutokuwa makini kukabiliana na tatizo hili. Ila ukweli utabaki palepale, Lowassa kuliingiza taifa mkenge na mkataba wa Richmond kumezidisha matatizo ya umeme nchini.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  wacha tuendelee kuwa wateja wa tochi. hapo ndipo wanapoirahisishia chadema kuchua nchi bila jasho
   
 8. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Richmond ni kichaka tu cha kujifichia, tatizo halikuanzia hapo.. Mbona hujiulizi mipango ya maendeleo ya umeme ni mw100 na si zaidi ya hapo? Kama tatizo lilikuwa ni EL basi sasa tungeona serikali ikija na miopango kama ya stiglers gorge, tusidanganyike na hiyo hadithi, tumeliwa richmond kwaajili ya ujinga wa kuwekeza kwenye miradi ya zimamoto na sio miradi ya muda mrefu yenye tija kwa taifa letu.

  Miaka mingapi tangu EL aondoke madarakani tatizo bado linaendelea... ilipaswa kama tatizo ni yeye lingeisha mara baada ya yeye kujiuzulu.. tatizo hapa ni mfumo mzima wa serikali yetu.
   
 9. T

  The Informer Senior Member

  #9
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Richmond ni muendelezo tu wa madudu ambayo serikali imekuwa ikifanya kwenye sekta ya umeme. Lowassa kweli alifeli mtihani wa uongozi pale swahiba wake Rostam Aziz alipomfuata na kumwambia apitishe mradi wa Richmond. Alishindwa kufanya maamuzi magumu na kumwambia Rostam "HAPANA!" maslahi ya nchi mbele. Badala yake alipush kampuni feki ipewe mkataba na matokeo yake sote tumeyaona.

  Lowassa anahusika katika matatizo yanayoendelea ya umeme kwani alikuwa Waziri Mkuu na akashindwa kupata ufumbuzi wakati mgao wa kwanza wa umeme ulipoanza mwaka 2006 na badala yake akaingia kwenye Richmond. Lakini lawama kubwa ziende kwa Rais Kikwete kwani tangu kuondoka kwa Lowassa mpaka leo nchi iko pale pale gizani. Kikwete aliporudi kutoka Spain mwaka 2006 huku mgao wa umeme mkubwa ukiitafuna nchi, kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari Ikulu neno la kwanza lilikuwa anafanya mpango Real Madrid waje kutalii Tanzania, badala ya kuzungumzia jinsi ya kukabiliana na mgao wa umeme.
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,058
  Likes Received: 3,085
  Trophy Points: 280
  "Corruption,poor planning and bad leadership"....natamani kumwaga chozi!

  Huyu ndo rais anayesema nje wanamsifia? hata mipango ya dhararu inawashinda? sasa wataweza nn make inaeleweka ya mda mrefu ni ndoto sasa kumbe hata ya dharura? JK ni hasara kwa taifa na yawezekana pia akawa ni mzigo ktk familia yake
   
 11. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,548
  Likes Received: 12,805
  Trophy Points: 280
  ILL BE IN HEAVEN BY THEN I MEAN 2013 so i better forget about power loool
   
 12. L

  Luiz JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni mfumo wa serikali ya magama full coruption frm top to ze bottom wajinemesha wao tu bila kuangalia wanainchi wanavyopata shida watu wengi hapa Tz wanategemea umeme kuendesha shughuli zao za kiuchumi ili wapate kula.
   
 13. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa, mwaka 2013 ndio mgao utaanza kuisha. Hii ni kwa sababu mkuu wa nchi ameanza kufanya biashara ya MAFUTA YA TAA baada ya mwanae kuhodhi soko la dizel. Ndio maana kwa sasa bei ya dizel ni sawa na mafuta ya taa. Mkuu katengeneza dili la kustafia. Umeme tusahau rangi yake. Sasa hivi mwenye vibatar vitatu ni sawa na mwenye gari la dizel.
   
Loading...